Jicho la Tatu: Kuporomoka kwa elimu kanda ya kusini

Andrew Jr

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
330
117
Wana Jf nawasalimu,

Suala la elimu hasa kusini mwa Tanzania linazidi kuleta matokeo yasiyotarajiwa, hapa namaanisha elimu ya msingi na sekondari.
Matokeo ya mitihani ya kitaifa yanaonesha shule za kusini mwa Tanzania ( Lindi, Mtwara) yanashuka kila kukicha. Kwa tathmini ndogo nikabaini:

- Wasimamia elimu, namanisha wakuu wa idara, wakuu wa shule wengi ni wazawa. Inakuwa ni vigumu kutambua umuhimu wa kuhimiza elimu, izingatiwe jamii nyingi za kusini shule kwao si jambo la lazima. Kama mkuu wa shule akiwa mzawa hatoweza kunyooshea kidole jamii yake maana watamwambia wewe nawe ni walewale.

- Athari za tamaduni, imezoeleka kila mwaka kuanzia mwezi wa Tano hadi wa saba watoto (asilimia kubwa chini ya miaka 7) hupelekwa porini kwaajili ya jando na unyago. Kwahyo mzazi nguvu kubwa huielekeza huko.

- Ndoa za utotoni, wanafunzi wengi huacha shule kukimbilia kuolewa. Niliobahatika kuongea nao hueleza ya kuwa hutekeleza yale waliyofundishwa jandoni.

-Nature vs Nature, si la kushangaa wazazi wa mwanafunzi hawajui kusoma wala kuandika..unategemea nini kwa mwanafunzi?
Yapo mengi sana ambayo yanaimaliza kusini kielimu. Serikali ya awamu ya Tano na Sera yake ya elimu bure huku imeshatafsiriwa tofauti, imesababisha wazazi kugombana na wakuu wa shule wakidai serikali inaleta hela nyingi za kumfanyia kila kitu mwanafunzi.

Naipongeza NECTA kuchukua mitihani yote mana mtu asipofikisha wastani wa 20 kwa kidato cha pili utaskia hata akiwa na 18 ruksa kuendlea.
Wadau ruksa kushauri ili kuinua elimu ya kusini mwa Tanzania.
Nawasilisha.
 
Mna wengi wa kulibeba na kulimaliza tatizo la elimu huko kusini kama Majaliwa, Mkapa, Kingunge na Nape. Hawa ni wepesi na wapo kwenye nafasi nzuri sana ya kuifanya Mtwara corridor ulaya ndogo.
 
Back
Top Bottom