Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,592
- 11,831
Tumia jicho lako la tatu kutueleza utofauti wa hawa viongozi wawili wenye ushawishi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.
Baada ya kumalizika kwa kampeni za leo kwa wagombea wote wawili mmoja akiwa Dodoma na mmoja akiwa Dar es salaam wote waliandike jumbe kwenye kurasa zao za Twitter.
Kwa kauli hizi inatupa picha namna wagombea hawa wanavyo tofautiana katika mambo mengi.
Lissu
Hili ndilo jibu letu kwa waliokuwa wanadai kwamba hatuna sera!!Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu! Njia ya kupata maendeleo sio lazima iwe iliyojaa damu, mateso na vilio. Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu ndio njia bora zaidi.
Magufuli
Nawashukuru wana CCM wote na Watanzania wa vyama vyote kwa kujitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM 2020 Jijini Dodoma. Pia nawashukuru wasanii, waandishi wa habari, viongozi wa Dini, n.k waliojitokeza kuniunga mkono katika uzinduzi huu. Maendeleo hayana chama. Tanzania Hoyee

- Kwa upande wangu naona Kuna mmoja amejawa Chuki na visasi n.k alafu Kuna mmoja yuko na moyo mweupe wenye furaha bila vinyongo, chuki, visasi n.k
- Kuna mmoja anapangilia sana maneno kuepuka kuropoka ovyo, alafu Kuna mmoja huongea tu kile kinachomjia kichwani kwa wakati huo.
- Kuna mmoja anapenda Sana utani unao tokana na utamaduni wa kitanzania, alafu Kuna mmoja yeye kwake kila kitu ni nongwa kwakifupi hana jema kwake kila kitu ni kibaya.
- Kuna mmoja ana siasa za asili ya kiuhuni uhuni yani haziko ki presidential alafu Kuna mwingine ni mtulivu sana.
- Mmoja anaweka sana utaifa mbele alafu mwingine ni mwanaharakati zaidi yupo tayari kwa chochote ikiwa tu kinamletea political popularity.