Jicho la siasa: Hayati John Pombe Magufuli ndiye aliyerithi mafuriko ya Edward Lowassa. Nani tena kuyarithi mafuriko hayo!?

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
JICHO LA SIASA:DAKTARI JOHN POMBE MAGUFULI NDIYE ALIYERITHI MAFURIKO YA MH EDWARD LOWASSA,NANI TENA KUYARITHI MAFURIKO HAYO!?

Leo 13:45hrs 25/04/2021

Muonekano,maamuzi yao,mitazamo yao kwa taifa la Tanzania,na sampuli ya utofauti kabisa katika siasa na uongozi ndivyo vilivyowainua watu na kufanya mafuriko barabarani hadi kwenye viwanja vya mikutano ya kampeni na popote walipokuwa kuwasikiliza Daktari John Pombe Magufuli na Mh Edward Lowassa katika kuwania Urais katika uchaguzi wa mwaka 2015,watu hawakuangalia tena vyama CCM au Chadema bali Wananchi waliwaangalia watu wawili John Pombe Magufuli na Edward Ngoyai Lowassa,hili ndilo jambo kubwa lililoleta utofauti katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Mh Edward Lowassa ambaye alianza kuonekana kuwavutia watu wengi kwa nafasi ya urais kabla ya kufarakana na CCM,akaendelea hivyo hata alipohamia Chadema,kwani umaarufu wake kwa nchi nzima haukufifia na Watanzania wengi walielekea kumkubali kwamba ndiye mtu awezaye kuleta mabadiliko yanayotakiwa katika Tanzania ambayo kwa wakati huo ilionekana kama shamba la bibi,baada ya kuhamia Chadema,Mh Edward Lowassa akapata dhamana ya kuwa mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema),Mh. Edward Lowassa aliungwa mkono na Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Fredrick Sumaye.

Tuliona pia "toroka uje" ikiondoka na Wenyeviti wa CCM na Mawaziri wa Serikali ya CCM ya awamu ya nne kuja Chadema kumuunga mkono Mh Edward Ngoyai Lowassa,tulimuona Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Lawrance Masha akimnadi Mh Edward Lowassa kwa Maelfu ya wananchi,tulimuona Mh Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mikoa wa CCM akimnadi Edward Lowassa kupitia Chadema,tulimuona pia aliyekuwa Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), Mh. Tundu Lissu akibeba funguo ya mlango wa Ikulu na kumnadi Mh. Edward Lowassa,kuwa ndiye Rais wa matarajio ya Wananchi Wanyonge na Walalahoi.

Kwa upande wake Daktari John Pombe Magufuli alisaidiwa kwa kiasi fulani kujulikana kupitia vyombo vya habari kama mtendaji wa maamuzi magumu ya serikali toka akiwa waziri katika wizara mbalimbali alizowahi kuziongoza katika awamu tofauti za CCM Madarakani,ingawa wakosoaji wa mambo wanadai kwamba vigogo wa CCM wangeweza kumdhibiti pindi atwaapo madaraka ya Urais,lakini bado aliweza kuonyesha kuwa sampuli tofauti na viongozi waliozoeleka katika utawala wa CCM.

Wakati Daktari John Pombe Magufuli akitetea rikodi ya zaidi ya miaka 50 na sera za chama tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM),mpinzani wake mkubwa ambaye ni mshika bendera wa chama cha upinzani cha Chadema chini ya mwamvuli wa umoja wa upinzani (ukawa),Mh Edward Ngoyai Lowassa, alisisitiza kuwa sasa ni "wakati wa kuweka mtazamo mpya kwa taifa kubwa la Afrika Mashariki,Taifa la Tanzania ambalo daima limekuwa likionewa kwa wizi,ufisadi ambao kamwe haujalisaidia Taifa la Tanzania.

Wakati fulani mambo yalivyokuwa magumu kwa CCM,ilibidi ibadilishwe style ya kunadi mgombea,badala ya kuitaja CCM sasa ilipendekezwa kutaja jina tu la John Pombe Magufuli,na mara moja ikaanza kuonekana kama mgombea wa CCM,Daktari John Magufuli alionekana kujikwaa kwa makusudi kwa kutumia alama ya chama kikuu cha upinzani cha Chadema ya M4C (Movement for Change) na sasa ikaanza kutamkwa "Magufuli 4 Change" M4C ili kusukuma mbele kampeni za CCM ambazo kwa hakika maji yalifika shingoni.

Mafuriko ya watu wenye furaha na vikundi vya wasanii vilijitokeza kupata ujumbe wa uchaguzi mahali popote wawania hao wawili wa urais walipokwenda,kwa kifupi,na kwa kutumia alama ya M4C yaani "Magufuli 4 Change" Daktari John Pombe Magufuli alitoa ahadi za kwenda “kusafisha nyumba” ndani ya Serikali na ndani ya CCM ambayo ilionekana kulaumiwa kwa mambo mengi kama ufusadi mkubwa wa Epa, Richmond na Escrow na kwa upande wa Mgombea wa Chadema,Mh Edward Lowassa,yeye alisimama kwa umaarufu wake na kwa mitazamo yake na kuahidi kuwatoa mamilioni ya watu katika umaskini na kutoa elimu bila malipo kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu,kitu ambacho kilikuja kutekelezwa na Hayati Rais John Pombe Magufuli mara tu baada ya kushinda Uchaguzi na kuingia Madarakani.

-Nikukumbushe Mafuriko ya Augustino Lyatonga Mrema.

Nakumbuka ilikuwa mwaka 1995. ambako Mzee Augustino Lyatonga Mrema alitikisa Tanzania hii katika Uchaguzi wa Urais wa mwaka 1995,Mgombea Urais wa CCM wakati huo alikuwa ni Hayati Benjamin William Mkapa,na Mh Augustino Lyatonga Mrema akitokea CCM alipata dhamana ya kugombea Urais na kubeba bendera ya Nccr Mageuzi,kwa hakika historia inamkumbuka Mh Augustino Lyatonga Mrema kama mpinzani wa kweli na wa kwanza kukonga nyoyo za Watanzania hata kufanya mafuriko kila mahali alipopita huku gari lake likizimwa na kusukumwa na Wananchi Wanyonge waliokuwa na matarajio makubwa juu yake,

Miaka hiyo ya 1995 hakukuwa na wasanii kuja kuimba ili watu wajae,hakukuwa na kuhonga watu na kuwasomba kwa malori kutengeneza mafuriko feki,Mafuriko ya Augustino Lyatonga Mrema yalikuwa mafuriko halisi,Gari lake lilisukumwa km 23 tokea Bukoba mjini kuelekea sehemu moja inaitwa katano Ishozi,Gari lake lilisukumwa toka njia panda ya Mwanga hadi Moshi,gari lake lilisukumwa toka Msamvu apaka katikati ya viunga vya mji wa Morogoro,gari lake lilisukumwa toka Ubungo hadi Jangwani alipokwenda kuhutubia bila kumuhonga kijana yeyote,aliweza kuteka hata hisia za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuingilia kati kwenye kampeni na kusema polisi wawaache watu wamsukume maana ndiye aliyebeba hoja za wanyonge na kwa hakika ilikuwa taa nyekundu kwa CCM,

Augustino Lyatonga Mrema alipata umaarufu bila hata kuwa na chawa ama kuwanunua waandishi wa habari na magazeti,Augustino Lyatonga Mrema hakuwa supported na walanguzi ili akiingia madaraki aje kuiuza Ikulu,tetesi zilisema Augustino Lyatonga Mrema aliogopwa na CCM mpaka baadhi ya vituo masanduku ya kupigia kura hayakupelekwa, Augustino Lyatonga Mrema alizunguka Tanzania karibia robo tatu kwa gari na alikuwa na nguvu sana,style hii pia ilifanywa na Hayati Rais John Pombe Magufuli kuzunguka Tanzania nzima kwa kutumia gari,Augustino Lyatonga Mrema hakutoka CCM kwa kashfa za rushwa, Augustino Lyatonga Mrema hakuwahi kujiuzuru au kutuhumiwa rushwa na hapendi rushwa.

Uchaguzi wa 2015 ulikuwa Uchaguzi wenye mchuano mkali kuwahi kutokea Tanzania,hii ilitoka na Tanzania kukabiliwa na changamoto nyingi na kuzitaja zote katika muda mfupi wa kampeni za uchaguzi ni jambo ambalo halikuwezekana,Wananchi walikuwa wameshachoka na tuhuma za ufisadi uliokithiri kila kukicha na watu wengi walihitaji mabadiliko na ndio maana sehemu nyingine vijijini watu walichagua walevi vilabu walijitokeza kugombea kupitia Chadema,lakini ni jambo la faraja kuwa wagombea wote John Pombe Magufuli na Edward Ngoyai Lowassa

Walionekana kuwa makini kuhusu mateso na matarajio ya wananchi wanyonge na masikini waliokuwa na yao mengi moyoni,hofu ya wapigakura kwa CCM ilikuwa kwamba ahadi za kampeni huenda zisitimizwe,kwa sababu Awamu zilizopita za utawala wa CCM zinakumbukwa kwa ahadi ambazo hazikutekelezwa na visingizio vya kushindwa kuzitekeleza, Shukrani kwa Hayati Rais John Pombe Magufuli ambaye kufikia Mwaka 2020 alikuwa ameitekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 100% hivyo basi alikwenda kwenye uchaguzi wa 2020 akiwa ametimiza ahadi zake kwa Wananchi kwa asilimia 100% na kwa hakika Wananchi walimlipa kwa kumpigia kura kwa asilimia 84%

-Kwa nini Rais John Pombe Magufuli aliingia kwa ukali baada ya kushinda Uchaguzi wa 2015?

Kwa hakika Mwaka 2015 maji yalimfikia shingoni na aliona kwa macho yake malalamiko ya Watanzania na nini wanataka wafanyike ikiwa mabadiliko ndio wimbo uliokuwa mioyoni mwa Watanzania na katika akili zao,daima usingeweza kufanikiwa kuongoza kwa kwenda kinyume na Watanzania waliokuwa wanadai mabadiliko, Watanzania hawakuhitaji blah blah tena bali walihitaji mabadiliko kwa vitendo ambavyo vingegusa maisha yao, Watanzania hawakutaka kusikia tena kuwa Tanzania masikini lakini kuna watu wapo Tanzania ni matajiri kuliko Taifa la Tanzania,

Watanzania walihitaji kuiona Tanzania kuwa kubwa kuliko mwananchi mmoja mmoja,hivi ndivyo Wananchi walitaka kusikia na kuiona Tanzania ikiwa nchi kubwa kutokana na rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu ameibariki nchi ya Tanzania,katika Uchaguzi wa 2015 ilikuwa Mgombea aliyewavutia Watanzania ilikuwa lazima aongee kwa ufasaha kuhusu masuala yanayowahusu katika maisha yao ya leo,hali bora ya maisha,kijamii na kiuchumi, Watanzania walipenda kuona mabiliono yatikanayo na madini yakijenga Zahanati kila Kijiji kuliko mabilioni hayo kuliwa na mtu mmoja halafu baadae waje wasikie fusadi fulani kala mabilioni na dhahabu,almasi na Tanzanite, Watanzania walitaka kuona ustawi wa kiuchumi kwa pato la Taifa kuwanufaisha Wananchi pasipo kufujwa na mafisadi wachache waishie kujenga mighorofa wakati mwananchi wa kawaida hawezi kumudu milo miwili kwa siku,

Nimalizie kwa kushukuru maisha ya Hayati Rais John Pombe Magufuli katika ardhi ya Tanzania,tumeona Mafuriko makubwa ya watu wakienda kumzika kila mahali jeneza lake lilipopita,hii nayo ni neema ya Mungu kwa mwana wake,Mwaka 2015 Wahubiri watatu mmoja ninayemkumbuka ni PhD Chris Oyakilome,wote walisema tunawaona malaika wakielekea upande wa Tanzania na tunaiona Tanzania ikipaa kimaendeleo, ikipata mabadiliko makubwa,Mwaka 2020 Rais John Pombe Magufuli aliingiza Tanzania katika nchi za uchumi wa kati kabla ya muda uliopangwa 2025,hii ni kazi ya Mungu na utimilifu wa viongozi hao wa dini kwa kile walichokiongea 2015,

Hii ilitokana na nia za dhati za kuwatumikia Watanzania zilizoonekana kwa wagombea wakubwa wawili Daktari John Pombe Magufuli na Mh Edward Ngoyai Lowassa,hii naiweka kama performance appraisal ya wagombea wawili wa Urais Mwaka 2015,Daktari John Pombe Magufuli na Mh Edward Ngoyai Lowassa,ahsante kwa ajili ya baraka zao katika taifa la Tanzania,tunapokwenda na Rais Mama Samia Suluhi Hassan tumwombee baraka nae akatende sawa sawa na mapenzi ya Mungu.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
1619353046999.png

Edward Sokoine alipofariki hakuna aliyezuiwa kuchinja mbuzi au kuwekwa ndani kwa kushangilia msiba.
 
Kwahiyo lowassa alishinda kwa 80%+ Kama jiwe alivyocopy and paste kwa msaada was sirro na mahera?
 
Hakuna kama jpm hatatokea asilani
na hakuna mpuuzi atakayejenga Hospital kwao bila kupitia Bunge aende akafie Dispensary km ya Mzena
sasa hivi tupo macho km kwenu hakuna kitu hatukupi Uongozi, siamini Mama yangu km atajenga hata Jengo la Benki kwao sembuse uwanja wa ndege kwani ni Tajiri wa roho
UMASIKINI ni mbaya
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom