Jicho la kisheria kuhusu uhalali wa barua ya Spika Ndugai kujiuzulu

Nikiri wazi kuwa nami, nikiwa mtanzania wa kawaida na mfuatiliaji mzuri wa mambo ya kisiasa na kijamii, nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sakata lililopelekea Spika Job Yustino Ndugai kuandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Spika. Nimefuatilia pia mjadala ulioibuka kuhusu uhalali wa barua yake ya kujiuzulu Uspika. Kama Msomi wa sheria (neno lililokuwa likimkwaza Mjiuzulu) nawiwa kuchangia katika hoja hii.

Nimepata fursa, ingawa si kubwa sana, kupitia Ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sura Nambari 2 ya Sheria za Nchi yetu (Katiba) na Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2016) ili kuona utaratibu wa kufuatwa pale Spika anapotaka kujiuzulu. Nimepitia nyaraka hizi kwakuwa ndizo hasa zinazounda na kuendesha Bunge kwa kiwango kikubwa. Kanuni tajwa za Bunge zimetungwa chini ya Ibara ya 89 ya Katiba.

Nilianza na Kanuni za Kudumu za Bunge. Neno 'kujiuzulu' limetajwa mara sita kwenye Kanuni husika. Ni kuhusu maazimio ya kuwaondoa madarakani Rais, Makamu wa Rais, Spika na Naibu Spika. Kuhusiana na Spika, kujiuzulu kwake kunaelezwa kwenye Kanuni ya 137 Fasili ya 6. Ni pale ambapo Spika anajiuzulu kabla ya uamuzi wa hoja ya Bunge ya kumuondoa madarakani. Namna ya kujiuzulu huku, kwa mujibu wa Kanuni na Fasili tajwa ni kutoa maelezo yake Bungeni. Kimsingi, ni wakati wa kikao cha Bunge. Kwa Ndugai hakukuwa na hoja ya aina hiyo.

Kanuni za Bunge hazisemi wala hazitoi utaratibu wowote wa namna ya kujiuzulu kwa Spika pale ambapo hakuna hoja ya kumuondoa madarakani ndani ya Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 137 nzima. Lakini, Katiba inatoa majibu. Ibara ya 149, Ibara Ndogo ya 1 kifungu (c) inamtaka Spika anayetaka kujiuzulu kuwasilisha taarifa yake ya maandishi aliyoitia saini yake kwenye Bunge. Kwangu mimi, 'kwenye Bunge' kunamaanisha kwa Mtendaji Mkuu katika Ofisi ya Bunge ambaye ni Katibu wa Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 87, Ibara ndogo ya 2.

Kwakuwa Kanuni za Bunge ziko kimya kuhusu utaratibu wa Spika kujiuzulu bila ya uwepo wa hoja ya kumuondoa madarakani Bungeni, matakwa ya Katiba LAZIMA yatimizwe. Ndiyo kusema, taarifa ya kujiuzulu kwa Spika LAZIMA iwasilishwe kwa Katibu wa Bunge na si vinginevyo. Si sawa wala sahihi kwa Spika kuwasilisha taarifa ya kujiuzulu kwake kwa Katibu Mkuu wa CCM badala ya Katibu wa Bunge. Haikuwa sahihi pia Katibu wa Bunge kunakiliwa TU barua husika.

Hivyobasi, nakubaliana na wote wanaotoa maoni ya kisheria kuwa barua/taarifa ya Spika Job Yustino Ndugai ya kujiuzulu kwake haikuwa halali. Anapaswa kuandika, kusaini na kuwasilisha taarifa yake kwa mujibu wa Katiba. Katibu Mkuu wa CCM, namshauri, kujiweka mbali na mtego huu wa kikatiba. Ingekuwa sahihi kuandikiwa Katibu Mkuu wa CCM kama Ndugai angetaka kuachia uanachama wake wa CCM.
Good brain barkiwa sana
 
Watanzania na dunia mzima inajua kwamba Ndugai kajiuzulu uspika. Hiyo ndo fact. We ukatae ni shauri yako na hakuna kitacho badilika. Huo ndo ukweli. Lakini kama ni school/academic discussion haya!
kama hujui kitu bora ufunge tu domo sio kila kitu unarukia tu
 
Katibu wa bunge ameshatangaza kiti kipo wazi na uchaguzi wa spika mpya ni tarehe 1 February.

Hizi nyingine ni porojo tu, wale wadada 19 wapo bungeni kwa katiba ipi?
nyammmbafff unakubali nini unakataa nini. ungefunga tu hilo domo
 
Back
Top Bottom