Jicho la kisheria kuhusu uhalali wa barua ya Spika Ndugai kujiuzulu

Hii siyo mimi. Ni katiba ya Tanzania. Speaker hajajiuzulu
Screenshot_20220107-091233_WhatsApp.jpg

MODS. TAGADHALI MSIUNGANISHE.
 
Nikiri wazi kuwa nami, nikiwa mtanzania wa kawaida na mfuatiliaji mzuri wa mambo ya kisiasa na kijamii, nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sakata lililopelekea Spika Job Yustino Ndugai kuandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Spika. Nimefuatilia pia mjadala ulioibuka kuhusu uhalali wa barua yake ya kujiuzulu Uspika. Kama Msomi wa sheria (neno lililokuwa likimkwaza Mjiuzulu) nawiwa kuchangia katika hoja hii.

Nimepata fursa, ingawa si kubwa sana, kupitia Ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sura Nambari 2 ya Sheria za Nchi yetu (Katiba) na Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2016) ili kuona utaratibu wa kufuatwa pale Spika anapotaka kujiuzulu. Nimepitia nyaraka hizi kwakuwa ndizo hasa zinazounda na kuendesha Bunge kwa kiwango kikubwa. Kanuni tajwa za Bunge zimetungwa chini ya Ibara ya 89 ya Katiba.

Nilianza na Kanuni za Kudumu za Bunge. Neno 'kujiuzulu' limetajwa mara sita kwenye Kanuni husika. Ni kuhusu maazimio ya kuwaondoa madarakani Rais, Makamu wa Rais, Spika na Naibu Spika. Kuhusiana na Spika, kujiuzulu kwake kunaelezwa kwenye Kanuni ya 137 Fasili ya 6. Ni pale ambapo Spika anajiuzulu kabla ya uamuzi wa hoja ya Bunge ya kumuondoa madarakani. Namna ya kujiuzulu huku, kwa mujibu wa Kanuni na Fasili tajwa ni kutoa maelezo yake Bungeni. Kimsingi, ni wakati wa kikao cha Bunge. Kwa Ndugai hakukuwa na hoja ya aina hiyo.

Kanuni za Bunge hazisemi wala hazitoi utaratibu wowote wa namna ya kujiuzulu kwa Spika pale ambapo hakuna hoja ya kumuondoa madarakani ndani ya Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 137 nzima. Lakini, Katiba inatoa majibu. Ibara ya 149, Ibara Ndogo ya 1 kifungu (c) inamtaka Spika anayetaka kujiuzulu kuwasilisha taarifa yake ya maandishi aliyoitia saini yake kwenye Bunge. Kwangu mimi, 'kwenye Bunge' kunamaanisha kwa Mtendaji Mkuu katika Ofisi ya Bunge ambaye ni Katibu wa Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 87, Ibara ndogo ya 2.

Kwakuwa Kanuni za Bunge ziko kimya kuhusu utaratibu wa Spika kujiuzulu bila ya uwepo wa hoja ya kumuondoa madarakani Bungeni, matakwa ya Katiba LAZIMA yatimizwe. Ndiyo kusema, taarifa ya kujiuzulu kwa Spika LAZIMA iwasilishwe kwa Katibu wa Bunge na si vinginevyo. Si sawa wala sahihi kwa Spika kuwasilisha taarifa ya kujiuzulu kwake kwa Katibu Mkuu wa CCM badala ya Katibu wa Bunge. Haikuwa sahihi pia Katibu wa Bunge kunakiliwa TU barua husika.

Hivyobasi, nakubaliana na wote wanaotoa maoni ya kisheria kuwa barua/taarifa ya Spika Job Yustino Ndugai ya kujiuzulu kwake haikuwa halali. Anapaswa kuandika, kusaini na kuwasilisha taarifa yake kwa mujibu wa Katiba. Katibu Mkuu wa CCM, namshauri, kujiweka mbali na mtego huu wa kikatiba. Ingekuwa sahihi kuandikiwa Katibu Mkuu wa CCM kama Ndugai angetaka kuachia uanachama wake wa CCM.
Kazi siyo utumwa. Nionyeshe sehemu yoyote ya katiba au sheria inayomlazimu mtu kufanya kazi asiyoitaka, yaani awe mtumwa wa kazi hiyo. Spika au mtu mwingine, akiona hataki kazi hiyo, au kazi ingine yoyote ile, anaweza kijiuzulu chooni au maktaba au barabarani au ITV, popote pale kwa njia yoyote ile mradi wahusika wamesikia. Mdau mkubwa hapa ni CCM, chama tawala, kikishasikia wadau wote wamesikia.Kufanya handing over ni kitu ingine, tena privare. Mbatiya hana akili.
 
Hizo ni technicalities ambazo can be cured by refiling the same letter to the correct authority.

Emphasis should be taken that, such an error is not fatal and doesn't negate the whole process to the extent that the petitioner rights are infringed or the process leads to abuse of powers stipulated in the Constitution.

I therefore find that any application to negate the resignation of his Honorable Speaker being plausible for academic purposes rather than justice for that cause.

However one cannot deny the fact that adherence to the Constitution is a matter of Law since it is a "grund norm".
 
Nauliza tuu.. Hivi kipindi cha Ndugai kulikuwa na bunge linalo fuata sheria? Au ilikuwa kama klabu ya ulanzi? Sasa muuza ulanzi kafunga banda lake. Hiyo sheria mnaitakia wapi?
 
Nikiri wazi kuwa nami, nikiwa mtanzania wa kawaida na mfuatiliaji mzuri wa mambo ya kisiasa na kijamii, nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sakata lililopelekea Spika Job Yustino Ndugai kuandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Spika. Nimefuatilia pia mjadala ulioibuka kuhusu uhalali wa barua yake ya kujiuzulu Uspika. Kama Msomi wa sheria (neno lililokuwa likimkwaza Mjiuzulu) nawiwa kuchangia katika hoja hii.

Nimepata fursa, ingawa si kubwa sana, kupitia Ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sura Nambari 2 ya Sheria za Nchi yetu (Katiba) na Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2016) ili kuona utaratibu wa kufuatwa pale Spika anapotaka kujiuzulu. Nimepitia nyaraka hizi kwakuwa ndizo hasa zinazounda na kuendesha Bunge kwa kiwango kikubwa. Kanuni tajwa za Bunge zimetungwa chini ya Ibara ya 89 ya Katiba.

Nilianza na Kanuni za Kudumu za Bunge. Neno 'kujiuzulu' limetajwa mara sita kwenye Kanuni husika. Ni kuhusu maazimio ya kuwaondoa madarakani Rais, Makamu wa Rais, Spika na Naibu Spika. Kuhusiana na Spika, kujiuzulu kwake kunaelezwa kwenye Kanuni ya 137 Fasili ya 6. Ni pale ambapo Spika anajiuzulu kabla ya uamuzi wa hoja ya Bunge ya kumuondoa madarakani. Namna ya kujiuzulu huku, kwa mujibu wa Kanuni na Fasili tajwa ni kutoa maelezo yake Bungeni. Kimsingi, ni wakati wa kikao cha Bunge. Kwa Ndugai hakukuwa na hoja ya aina hiyo.

Kanuni za Bunge hazisemi wala hazitoi utaratibu wowote wa namna ya kujiuzulu kwa Spika pale ambapo hakuna hoja ya kumuondoa madarakani ndani ya Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 137 nzima. Lakini, Katiba inatoa majibu. Ibara ya 149, Ibara Ndogo ya 1 kifungu (c) inamtaka Spika anayetaka kujiuzulu kuwasilisha taarifa yake ya maandishi aliyoitia saini yake kwenye Bunge. Kwangu mimi, 'kwenye Bunge' kunamaanisha kwa Mtendaji Mkuu katika Ofisi ya Bunge ambaye ni Katibu wa Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 87, Ibara ndogo ya 2.

Kwakuwa Kanuni za Bunge ziko kimya kuhusu utaratibu wa Spika kujiuzulu bila ya uwepo wa hoja ya kumuondoa madarakani Bungeni, matakwa ya Katiba LAZIMA yatimizwe. Ndiyo kusema, taarifa ya kujiuzulu kwa Spika LAZIMA iwasilishwe kwa Katibu wa Bunge na si vinginevyo. Si sawa wala sahihi kwa Spika kuwasilisha taarifa ya kujiuzulu kwake kwa Katibu Mkuu wa CCM badala ya Katibu wa Bunge. Haikuwa sahihi pia Katibu wa Bunge kunakiliwa TU barua husika.

Hivyobasi, nakubaliana na wote wanaotoa maoni ya kisheria kuwa barua/taarifa ya Spika Job Yustino Ndugai ya kujiuzulu kwake haikuwa halali. Anapaswa kuandika, kusaini na kuwasilisha taarifa yake kwa mujibu wa Katiba. Katibu Mkuu wa CCM, namshauri, kujiweka mbali na mtego huu wa kikatiba. Ingekuwa sahihi kuandikiwa Katibu Mkuu wa CCM kama Ndugai angetaka kuachia uanachama wake wa CCM.

sasa kama yeye alipitisha uviko 19 bado unataka kuja kuchambua barua !.
badilika kwa kuachana na ccm
 
Aibu kwa cc mabush lawyer, Mhimili unaotunga sheria haujui uadresi wapi barua.
Bunge halina washauri kitaaluma kwa sheria?
Bunge halina maofisa waliosomea elimu ya siasa?
Bunge halina maofisa wakushauriana na mihimili mingine?
Aibu!Aibu!
 
Nashauri serikali isije kukosea ikamlipa mafao ya u-spika.
Huyu mtu ameondoka kwa kashfa na hajamaliza muda wake!
Tusitumie vby fedha za walipa kodi jamani, ale vihela vya ubunge vinamtosha!
ACHA WIVU, ROHO MBAYA NA AKILI MBOVU
 
Nikiri wazi kuwa nami, nikiwa mtanzania wa kawaida na mfuatiliaji mzuri wa mambo ya kisiasa na kijamii, nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sakata lililopelekea Spika Job Yustino Ndugai kuandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Spika. Nimefuatilia pia mjadala ulioibuka kuhusu uhalali wa barua yake ya kujiuzulu Uspika. Kama Msomi wa sheria (neno lililokuwa likimkwaza Mjiuzulu) nawiwa kuchangia katika hoja hii.

Nimepata fursa, ingawa si kubwa sana, kupitia Ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sura Nambari 2 ya Sheria za Nchi yetu (Katiba) na Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2016) ili kuona utaratibu wa kufuatwa pale Spika anapotaka kujiuzulu. Nimepitia nyaraka hizi kwakuwa ndizo hasa zinazounda na kuendesha Bunge kwa kiwango kikubwa. Kanuni tajwa za Bunge zimetungwa chini ya Ibara ya 89 ya Katiba.

Nilianza na Kanuni za Kudumu za Bunge. Neno 'kujiuzulu' limetajwa mara sita kwenye Kanuni husika. Ni kuhusu maazimio ya kuwaondoa madarakani Rais, Makamu wa Rais, Spika na Naibu Spika. Kuhusiana na Spika, kujiuzulu kwake kunaelezwa kwenye Kanuni ya 137 Fasili ya 6. Ni pale ambapo Spika anajiuzulu kabla ya uamuzi wa hoja ya Bunge ya kumuondoa madarakani. Namna ya kujiuzulu huku, kwa mujibu wa Kanuni na Fasili tajwa ni kutoa maelezo yake Bungeni. Kimsingi, ni wakati wa kikao cha Bunge. Kwa Ndugai hakukuwa na hoja ya aina hiyo.

Kanuni za Bunge hazisemi wala hazitoi utaratibu wowote wa namna ya kujiuzulu kwa Spika pale ambapo hakuna hoja ya kumuondoa madarakani ndani ya Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 137 nzima. Lakini, Katiba inatoa majibu. Ibara ya 149, Ibara Ndogo ya 1 kifungu (c) inamtaka Spika anayetaka kujiuzulu kuwasilisha taarifa yake ya maandishi aliyoitia saini yake kwenye Bunge. Kwangu mimi, 'kwenye Bunge' kunamaanisha kwa Mtendaji Mkuu katika Ofisi ya Bunge ambaye ni Katibu wa Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 87, Ibara ndogo ya 2.

Kwakuwa Kanuni za Bunge ziko kimya kuhusu utaratibu wa Spika kujiuzulu bila ya uwepo wa hoja ya kumuondoa madarakani Bungeni, matakwa ya Katiba LAZIMA yatimizwe. Ndiyo kusema, taarifa ya kujiuzulu kwa Spika LAZIMA iwasilishwe kwa Katibu wa Bunge na si vinginevyo. Si sawa wala sahihi kwa Spika kuwasilisha taarifa ya kujiuzulu kwake kwa Katibu Mkuu wa CCM badala ya Katibu wa Bunge. Haikuwa sahihi pia Katibu wa Bunge kunakiliwa TU barua husika.

Hivyobasi, nakubaliana na wote wanaotoa maoni ya kisheria kuwa barua/taarifa ya Spika Job Yustino Ndugai ya kujiuzulu kwake haikuwa halali. Anapaswa kuandika, kusaini na kuwasilisha taarifa yake kwa mujibu wa Katiba. Katibu Mkuu wa CCM, namshauri, kujiweka mbali na mtego huu wa kikatiba. Ingekuwa sahihi kuandikiwa Katibu Mkuu wa CCM kama Ndugai angetaka kuachia uanachama wake wa CCM.
Mkuu waliomzonga ni chama chake cha kijani na kwakuwa yeye pia ni mwananchama na jina lake lilipendekezwa kupitia chama chake na kwakuwa wao ndio walioshinikiza kujiuzulu amewapelekea barua waliyotaka kisha kuondoka kwenye hiyo ofisiambayo wao wanahisi ni kikwazo kwao imetosha amewaachia mengine mtajua wenyewe.

Hamuwezi kumlazimisha kubadili barua aliyoandika nmwisho wa siku lazima aliyesimama hadharani kumtisha kwamba ni adui yake ataibeba lawama yote pamoja na laana zote kwa kile kilichotokea.

Usijadili kilichofanyika na spika tu, jadili pia kitendo cha mhimili tendaji ambao ndio heshima ya nchi ukisema hadharani maneno ya vitisho dhidi ya mwenye dhamana ya mhimili jamii hapo wote walikosea na watailipa gharama yake.

You are a seasoned lawyer, do not analyze issues by choosing a position to stake, it is absolutely double standards
 
Majivuno ndio yamemuangusha. Huwezi kusema " mama yenu juzi hapa kaenda kukopa" wakati huo mkopo ulipitia kwenye kamati ya bunge. Ndugai anatafuta maslahi ya kisiasa Kama angekuwa mkweli asingekubali pesa za walipa Kodi ziwalipe wabunge wasiokuwa na sifa.
Punguani tu yule,kajidhalilisha sana kwa wale uviko19
 
Back
Top Bottom