Jibwa la kizungu kwa wazenji noma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jibwa la kizungu kwa wazenji noma!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngekewa, Mar 17, 2009.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mbwa aliyezua tafrani Z`bar apelekwa NY

  2009-03-15 14:07:06
  Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
  Hatimaye mbwa aliyedaiwa kuwa kero kubwa kwa wafanyakazi wa hoteli ya Kimataifa ya Zamani Zanzibar Kempinski ameondolewa nchini na kurejeshwa New York, Marekani.

  Mbwa huyo anayeitwa Lucky, alidaiwa kusababisha baadhi ya wafanyakazi wa hoteli hiyo kutakiwa wamuombe radhi pale walipompiga au kutishiwa kufukuzwa kazi.

  Akizungumza na Nipashe, Meneja Mkuu wa hoteli hiyo, Silke Macke alisema amelazimika kumuondoa nchini ili kulinda heshima ya hoteli hiyo baada ya kujitokeza taarifa kwamba mbwa huyo analeta kero.

  Alisema kwamba pamoja na yeye binafsi kuwa haamini mbwa huyo alikuwa kero, ameamua kuchukua uamuzi huo ili kuondoa mtazamo ulioanza kujitokeza kuhusina na mnyama huyo.

  ``Mimi na familia yangu tunampenda sana mbwa huyu, na ili abaki katika hali ya usalama nimeamua kumrejesha New York ili akakae kwa utulivu hivi tunapozungumza yupo njiani kuelekea huko,`` alisema Meneja huyo wa hoteli.

  Alisema madai yaliyotolewa na baadhi ya wafanyakazi wa hoteli hiyo, kuwa Meneja wa Vyakula na Vinywaji hotelini hapo alikuwa akiwalazimisha wafanyakazi wanaompiga mbwa wa bosi wake kumuomba radhi mbwa huyo hayakuwa ya kweli.

  Silke alisema hadi sasa hafahamu wafanyakazi hao walikimbilia kwenye vyombo vya habari kutoa malalamiko hayo kwa misingi gani, hasa kwa kuzingatia mbwa hapa Zanzibar ni jambo la kawaida.

  Alisema kwamba wapo mbwa wengi tu Zanzibar na wengine wanazurura ovyo, hivyo haikuwa jambo la ajabu hotelini hapo kuwepo mbwa.

  ``Nayajua mazingira ya Zanzibar pamoja na mila na utamaduni wa watu wake, lakini suala la mbwa si kitu cha ajabu kwa sababu wapo mbwa wengi wanafugwa na wengine wanazurura ovyo,`` alisema alipokuwa akizungumza na Nipashe.

  Hivi karibuni baadhi ya wafanyakazi katika hoteli hiyo walisema walikuwa wakifanya kazi katika mazingira ya wasiwasi kutokana na kero za mbwa huyo dume ambaye alikuwa na kawaida ya kuwanusa na kuwarukia rukia kati ya miguu na pale wanapompiga walikumbana na adhabu hizo.

  Walisema kuwa mbwa huyo pia alikuwa akiambatana na mmiliki wake katika vikao na kuleta kero kubwa kwa baadhi ya wajumbe wanaohudhuria kwenye vikao hivyo na wakati mwengine mbwa huyo kutumia vyombo wanavyootumia wafanyakazi.

  Kuhusu malalamiko kwa baadhi ya wafanyakazi kuwa wamekuwa wakizuiwa kuvaa `kanzu za kiislamu` na viatu vya utamaduni vya makubadhi na Afisa Ulinzi mmoja mwenye asili ya Kenya, Meneja huyo alisema madai hayo hayana msingi.

  Alisema kwamba utaratibu uliowekwa hotelini hapo haukatazi kuja na vazi aina yoyote, lakini mfanyakazi anapoingia eneo la hoteli hutakiwa kubadilisha nguo zake na kuvaa sare ya hoteli, iwe mwanamke au mwanaume.

  Kufuatia malalamiko ya wafanyakazi hao kuchapishwa na gazeti hili, Makamu wa Rais wa hoteli za Kempinski Afrika Mshariki, Malhotra alitembelea Zanzibar kuzungumza na uongozi wa hoteli hiyo juu ya suala hilo.

  Aidha, Malhotra aliahidi kurejea tena Zanzibar na kuahidi kuzungumza na gazeti hili juu ya ukweli wa suala hilo, ambalo limegusa hisia za wananchi visiwani.
  • SOURCE: NIPASHE
   
Loading...