Jiandalie mazingira ya kujiajiri ukiwa chuo ama ukiwa unaendelea na masomo yako

miamiatz

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
504
927
Haijalishi unasomea masomo gani. Iwe uhandisi, iwe unajimu, iwe biashara, iwe ualimu, etc. Unapaswa kuandaa mazingira ya kujiajiri kwa kufanya mambo yafuatayo.

1. Jifunze public speaking (kuzungumza katika hadhara). Hakikisha kila ikijitokeza fursa ya kuongea mbele ya watu basi wewe simama uongee. Hata kama sio mzuri katika kuongea kadri unavyojitahidi utamudu zaidi na kujisahihisha.

Uwezo wa kuzungumza huleta fursa nyingi sana. Hata kuwa MC ni kazi yenye tija sana. Hata udalali ni kazi yenye tija. Kuna makampuni ya udalali. Kuna makampuni ya minada. Yote haya hutumia vyema uwezo wa watu wao kuzungumza.

2. Jifunze uandishi. Unajifunzaje uandishi? Andaa blog yako na uwe unaandika yale unayoyasoma darasani ukijaribu kuyachambua vile ulivyoyaelewa. Andika kwenye facebook, jamiiforums, quora blog na mitandao mingine ya kijamii.

3. Jifunze kukusanya taarifa za watu na taasisi. Kumbuka maisha huwa bora zaidi kadri network yako inavyozidi kupanuka. Usibeze mtu. Usiache fursa ya kupata mawasiliano ya mtu ama taasisi ikupite.

Kuna tovuti kibao kama zoomtanzania ambazo zina taarifa za taasisi kibao. Kusanya taarifa hizo. Ukiwa na namba za simu, emails, na other details za taasisi nyingi itakusaidia sana.

4. Jifunze kuuza na kuandaa proposal ya kuuza. Hata uwe na ujuzi gani kama hujui jinsi ya kuuza ujuzi wako ni kazi bure. Unajifunzaje kuuza ujuzi wako? Jaribu kutafuta watu wa kukulipa kwa wewe kuwafanyia huduma ihusianayo na ujuzi wako.

Kumbuka kuna watu wengi huku mitaani wameshafungua biashara zao. Kazi kubwa inayowashinda ni kupata wateja. Hivyo basi uwezo wa kuuza kwa aliye nao ni fura kubwa sana tena sana kwa sasa.

Na uwezo wa kuuza huja kwa kukuza uwezo wako wa kushawishi. Anza sasa ili uwezo huo ukue pole pole. Mpaka umalizapo masomo utakuwa ushakuwa mjuzi zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom