Ji ukweli kuwa kuna Viumbe wa Ajabu wataiangamiza Dunia?

Kulama

Member
Jul 30, 2015
37
25
Katika riwaya hii ya kusisimua ya THE DOOMSDAY CONSPIRACY, mwandishi Sidney Sheldon anatujuza kuwa Shirika la Ushushushu linalohusika kunasa mawasiliano la Marekani(NSA) linahaha kuhakikisha linawafahamu na kuwaangamiza watu wote walioshuhudia viumbe vya ajabu(aliens) au ( Unidentified Flying saucers(UFOs).

Viumbe hivyo vinaaminika kuanguka katika eneo la Uetendorf nchini Uswizi na watu waliyovishuhudia ambao walikuwa watalii inasemekana baadhi yao walitapika, wengine kupata kizunguzungu na taharuki za kila aina.

Lengo la NSA ni kuhakikisha watu hao walioshuhudia hawaenezi hizo habari za viumbe hao na kuzua taharuki kwa umma(Public panic), kwa kuwa viumbe hao wanasemekana kuwa wanatisha na inaaminika kuwa ipo siku wataivamia dunia na kuiangamiza.

Kwa wale wafuatiliaji wa movies watakuwa wamewahi kuona Alliens and Predators, Star Wars, Predator, Men in Black nakadhalika .

Lakini pia katika baadhi ya maandiko ya kidini nimesikia kuna kitu kinaitwa Armageddon, ikiamanisha kuwa vita kubwa itakayotokea baina ya waovu na watu wema na kuashiria mwisho wa dunia. Waovu ikisemekana ndio hao UFOs au Alliens(Utafiti zaidi unahitajika).
Stori za viumbe hawa zipo nyingi tu na inasemekana viumbe hawa wana nguvu za ajabu na wanaishi nje ya sayari yetu ya dunia(Extraterrestrial beings).

Tuendelee, Wakati Maafisa wa NSA wanahaha kuwadhiti watalii hao, yanaibuka maswali magumu kwao. Mosi, hao watalii walisafiri na basi la kampuni gani? Je majina yao ni kina nani? Walitokea nchi gani?

Hata hivyo maswali hayo hayawakatishi tamaa, hivyo wanaaamua kuanzisha Operesheni maalumu ya kijasusi iitwayo “Operation Doomsday”.

Katika kuendesha Operesheni hiyo anateuliwa Kamanda Robert Bellamy kutoka idara ya Intellijensia ya Jeshi la majini la Marekani(ONI).

Jukumu kubwa la Kamanda Bellamy ni kuhakikisha watalii wote hao wanajulikana na kisha kutuma taarifa kwa mabosi wake.

Hata hivyo, wakati Kamanda Bellamy anapewa jukumu hilo alidanganywa na mabosi wake kuwa watalii hao walishuhudia kifaa kilichokuwa kimebeba taarifa za siri za kijeshi(Weather Balloon) ambacho kilikuwa kimeanguka huko Uswizi.

Alikuja kubaini ukweli baadae alipoambiwa na mmoja wa mashuhuda kuwa ni UFOs, jambo ambalo lilimuogopesha Kamanda na kuanza kuwagombeza mabosi wake kwanini walimdanganya.

Kwa kuwa tayari alishakabidhiwa jukumu, Kamanda Bellamy hakuwa na la kufanya zaidi ya kuendelea na Operesheni.

Akitumia mbinu mbalimbali za kijasusi kama kujifanya mwandishi wa habari, Kamanda Bellamy aliweza kuwatambua washuhuda wote katika nchi tofauti tofauti.

Mashuhuda hao walikuwa 10 na aliweza kuwafahamu kupitia maelezo(clues) ya kila mmoja wao na alikuwa akituma majina yao kwa mabosi wake.

Jambo alilokuwa halifahamu Kamanda Bellamy ni kuwa kila jina la shuhuda alilokuwa akilituma kwa mabosi wake, walikuwa wakitumwa watu maalumu(wasiojulikana) na kummaliza huyo shuhuda.

Wapo waliouawa kwa ajali, wapo waliotupwa shimoni, wapo waliochomwa sindano za sumu, yupo aliyeuawa na kisha kuwekewa silaha na maandiko eti alijiua na yupo aliyeuawa kwa kubakwa.

Kamanda Bellamy alikuja kutambua kuwa mashuhuda wote waliuawa baada ya kuanza kuwapigia simu tena ili kuhakiki kama walikuwa 10 tu kwani awali aliambiwa walikuwa saba tu.

Mauaji hayo yalimkera sana Kamanda Bellamy na kushangaa kwanini mashuhuda hao waliuawa ilihali haikuwa kusudi yao kuona viumbe hao waajabu.

Muindaji anawindwa(The hunter is hunted)
Baada ya Kamanda Bellamy kumaliza kazi yake, sasa ni zamu yake kuuawa. Kamanda Bellamy anatambua jambo hilo baada ya mtu kumpenyezea taarifa. Yeye anashangaa kwanini anatakiwa auawe tena na maswahiba wake.

Kwenye vyombo vya habari taarifa zikasema kuwa Kamanda Bellamy anatafutwa kwa kosa la kujihusisha na biashara haramu ya magendo na dawa za kulevya.

Hivyo nusu ya Serikali duniani zinamsaka na donge nono la zawadi limetolewa kwa atakaetoa taarifa za mahali alipo.

Kwa kuwa kamanda Bellamy nae ni mtaalum wa sanaa za giza(Dark arts) anaanza kucheza nao ngoma. Anatumia mbinu mbalimbali kuwachanganya wanaomfuatili akimtumia binti anaejiuza nchinini Italia aitwae Pier.

Kamanda Bellamy anamwambia huyo binti kila kitu na kwa kuwa Pier anawachukia sana Polisi ambao huwasumbua sana kwenye biashara yao ya ukahaba na waliwahi kumbaka, anaamua kumsaidia Bellamy.

Hata hivyo wanawake ni wakuishi nao kwa akili, kwani baada ya kusikia kuwa kamanda Bellamy anatafutwa na zawadi nono itatolewa kwa atakaetoa taarifa, Pier anaamua kuwapigia simu Polisi kuwa yupo na kamanda nyumbani kwao.Lengo ni kupata pesa.

Polisi wanafika nyumbani kwao hata hivyo Bellamy hakuwepo. Kamanda akiwa anarejea kwa akina Pier anahisi jambo ndani ya nyumba anaamua kukimbia.

Baada ya kusumbuana kwa muda mrefu, ndipo Kamanda Bellamy akaamua kuwapigia simu wabaya wake akiwaambia kuwa amempata shuhuda wa 11.

Wanakubaliana wakutane Uswizi wazungumze na awaoneshe huyo shuhuda. Siku ya tukio inafika, wanafika eneo la tukio.

Mara inatokea Helkopta ambapo ndani yake anatokea mwanamke mwenye nguo nyeupe aitwae Suzan. Bellamy anawaambia wabaya wake kuwa Suzan ndio shahidi wa 11.
Pia Kamanda Bellamy anawaambia wabaya wake kuwa Suzan ni kiumbe cha ajabu(Allien), nae Suzan anaanza kuonesha miujiza yake.

Hatimaye Suzan anafanikiwa kumuokoa Kamanda Bellamy asiuawe. Mwisho!
Ni kweli kuna UFOs?

Mwishoni mwa kitabu, Mwandishi kaweka baadhi ya taarifa mbalimbali zinazoonesha uwezekano wa uwepo kweli wa viumbe hao wa ajabu ila hata hivyo taarifa hizo inadaiwa zimekuwa zikifichwa.

Mfano anasema mwaka 1947 Rais wa Marekani Harry Truman aliunda jopo maalumu lililoitwa Majestic 12 au MJ-12 ili kuchunguza uwepo wa UFOs.
Matokeo ya uchunguzi huo yaliyotolewa mwaka 1952 yalionesha uwepo wa viumbe hao wa ajabu hata hivyo suala hili lilifanywa kuwa siri.

NI MIMI YUSUFU LULUNGU!
dcdeccc0fa80d63c6ed4256de8ab61e9.jpg
 
Hicho Kitabu kina flaws nyingi sana kama mwandishi ndio kaandika uliyoleta wewe!..

Halafu kumbe ni Riwaya mie nilikiweka kama research!
 
Hicho Kitabu kina flaws nyingi sana kama mwandishi ndio kaandika uliyoleta wewe!..

Halafu kumbe ni Riwaya mie nilikiweka kama research!

Mwandishi wa hiki kitabu aliombwa aandike riwaya kuhusu UFO kwa kutumia research reports mbalimbali zizowahi kuchapishwa (anazionesha mwishoni) lakini kwa mfumo ambao utawafanya watu wavutiwe kusoma lakini pia waelewe.

Kuna kitabu chake kingine kinaitwa Tell me your dreams ambacho kinaelezea tatizo la kiafya linaitwa Multiple Personality Disorder (MPD) ambalo tunaweza kulinganisha na mapepo kwa huku kwetu. Lakini alikiweka in a way unaenjoy hadithi huku unaelewa somo


Sent using Jamii Forums for Iphone App
 
Back
Top Bottom