JF's Impact on Tanzanian Politic (Part 2)

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Wandugu,

sifahamu hasa wamiliki wa JF na kwamba waliazisha wakikusudia nini.

Kwangu mimi ni dhairi kwamba JF imechangia sana katika kukuza demokrasia katika siasa na sera za Tz. Pia katika mapambano dhidi ya ufisadi.

Siku chache kabla ya Uchaguzi mkuu wa Octoba 2010, MM aliazisha thread ambayo alidai angejiuzulu kuandikia humu JF kwa kuwa alihisi impact ya nguvu zake haikuwanufaisha wananchi wa vijijini. Patten ya idadi ya kura na ushindi katika Uchaguzi uliopita pengine ilithibitisha hilo

Kwa kuwa naamini kwamba bado tunahitaji JF kuelekea 2015, ingekuwa vema JF ikafanya impact assessment kuona achievment na changamoto ili kuboresha zaidi

Wandugu,

nashukuru sana kwa michango yenu kwenye Part one ya thread hiyo hapo juu na link yake hii. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/92335-jfs-impact-on-tanzanian-politicts-4.html

1. Kwa ufupi mchango wa kwanza uliibuka kulalamikia Mods lakini kadri mjadala ulivyoendelea ilikuwa wazi kwamba Mods wanafanya kazi nzuri sana na kwamba hata kama kuna kasoro chache zinatokana na ubinadamu pamoja na ufinyu wa rasilimali walizonazo.

2. Wazo la pili lilikuwa kwamba JF ni muhimu sana kwa kuchochea mjadala na kushirikishana taarifa muhimu. Hapa changamoto imetajwa kuwa ni wale mavuvuzela wasio na ufahamu wa kujadili hoja kwa kutumia sayansi ya mantiki. Kwamba wanapotezea wenzao muda na kukera

3. Wachangiaji pia walikiri kwamba JF ilikuwa burudani zaidi kabla ya kampeni za uchaguzi wa 2010 kwani kipindi cha uchaguzi waliingia watu waliokuwa na kazi ya kutetea na kusifu vyama vyao na itikadi zake.

4. Kwa ujumla wachangiaji wengi wamekiri kwamba access ya JF ni kwa wateule wachache. Hasa wenye fursa ya internet ofisini kwao, wanaoishi mijini, na hasa wanaume.

5. Mtazamo ulikuwa ni kuelekea 2015, hivyo mapendekezo machache yalitolewa.

6. Kwamba ili kufikia watu wa vijijini, wachangiaji wengi wa JF waandike makala za uchambuzi wachape kwenye magazeti yasambazwe. Pia radio ilionekana ni mojawapo ya njia kuu ya kuweza kuwafikia watu wa vijijini na hasa wale wasio na access na internet. Tv nayo ilitajwa.

7. Lengo ni kusambaza hizi fikra zinazopatika hapa kwenye kisima JF kuamsha uelewa na ari ya wananchi wengi katika kuleta mabadiliko ya kisiasa na kisera.

8. Kuna magazeti ambayo kuchukua mijadala iliyojiri humu JF na kuandika. Nimefurahi kwamba Star TV nao wameanza kutumia JF kama njia ya kuzalisha fikra ambazo wanazitumia kuendesha mijadala ya kitaifa ambayo watazamaji na wasikilizaji ni wengi zaidi kuliko wanaotembelea hapa JF.

9. Je, kuna jitihada za kuanzisha JF radio ambazo zitakuwa zinatumia mijadala hii hapa kuendesha live discussion na wananchi hasa katika yale maeneo ya nchi hii ambayo mwamko wa elimu ya uraia umedhihirika kwamba ni mdogo? Awamu hii tuna kazi kubwa na ngumu ya kudai katiba mpya, tume ya uchaguzi huru, na sheria ya uhuru wa habari. haya ni majukumu makubwa ambayo yanahitaji mjadala mijadala mipana katika ngazi zote za jamii yetu. Ni vizuri kufanyia kazi hili
 
Yaani watu ndio wamesusa au yaliyojadiliwa yatatekelezwa kimya-kimya?

Nimegundua ukiandika post inayohitaji watu kufikiri hupati wachangiaji isipokuwa watazamaj (viewers). Lakini ukiweka post ya udaku inashambuliwa kama mchwa!
 
Not sure if it was discussed here but you can post it as new thread. I liked the thing about structural repitition of 2005 voting and position switching!
 
utamu wa JF ni anonymity ....sasa ukiweka radio na tv nani atachangia waziwazi?
 
utamu wa JF ni anonymity ....sasa ukiweka radio na tv nani atachangia waziwazi?

Kwanza, unachukua mawazo kutoka JF kwa kutumia majina hayo hayo bandia, unayasoma hewani live kisha wasikilizaji wasio na previlage ya ku-access JF wanachangia. Wakati mwingine hata wanachama wa JF wanachangia pia, kama ilivyofanyika last Sunday na Star tv.

Pili, kwenye part 1 ya hii thread kulitokea swali kwamba mabadiliko yataletwaje na watu walio mafichoni (JF)? Kwamba aina na scope ya mabadiliko yanayokusudiwa awamu hii yanahitaji kuongea wazi bila kuogopa kujulikana. Angalia kwa mfano B. Mkapa amesema tz inahitaji katiba mpya. S. 6 naye kasema kulipa Dowans ni kuhujumu uchumi wakati yuko kwenye baraza la mawaziri na akijua kwamba aliyemteua anahusishwa na Richmd.

Tatu, mkuu mwanakijiji tayari amevua mask na ameitisha mkutano j2 ijayo kujadili madai ya katiba mpya. Wapo wengine pia hawatumii mask hapa JF au wana identity 2.

Hivyo utaona huu unafiki wa kujificha kwenye majina bandia hautatufikisha. Hata serikali haitaweza kujibu hoja zinazojadiliwa hapa kwa sababu hawajui wanamjibu nani. Hii pia ilikuwa ni moja ya observation kwenye part 1 ya hii thread. Kwamba serkali haijawahi kujibu hoja hapa ingawa nyingi ni nzito na zina ushahidi wa kufa mtu.

Should we then continue enjoying JF facility as a venting room? Chumba ambacho watu waoga, wambea, wazushi, na wanafiki wanakutana wakiwa wamefungwa vitambaa vyeusi vichwani kisha kila mmoja anapiga kelele kwa sauti na hasira zote?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom