JF yawaponza wakurugenzi, tuwasaidie!

Kihwele na Salala picha haziendi kwa muda mrefu sana.

I hope kupelekwa kwake (Salala) likizo ya lazima isn't a personal vendetta.
 
Je, waliosimamishwa wameweza kuwasiliana nani ili tuweze kuwasaidia, au kama mnanipa ruksa nifanye jitihada za binafsi kuwapata na kuwaleta hapa?

Mwenye mawazo tafadhali anitumie PM.
 
Je, waliosimamishwa wameweza kuwasiliana nani ili tuweze kuwasaidia, au kama mnanipa ruksa nifanye jitihada za binafsi kuwapata na kuwaleta hapa?

Mwenye mawazo tafadhali anitumie PM.

Wasiliana na Invisible kwa kumtumia PM anaweza kukusaidia kuhusu hawa waungwana. Kama utalishughulikia tafadhali tupe taarifa ya kinachoendelea. Kila la heri.
 
Haya mapambano ya kifikra yanazidi kupata majeruhi...hii inanikumbusha ule waraka wa mafisadi; mwanzoni walianza kutafuta umetoka wapi badala ya kuangalia kilichomo. Nadhani wakati umefika waandishi wapige kambi kule Posta na kuwabana kwa maswali wahusika wote..

Kwa kuwa benki hii ni ya umma, ni vyema suala hili pia likatinga bungeni. Kama kuna mwenye maswali mahususi au amefanya uchambuzi wa kina kuhusu suala hili anitumie kwenye mnyika@yahoo.com; nataka niwapatie baadhi ya wabunge Dodoma

JJ
 
Wakurugenzi waliofukuzwa sio wafanyakazi wasi wasi waende kufungua mashitaka watarudishwa na kulipwa fidia kubwa tu . No issue here,
 
Nikirejea maelezo ya GAZETI LA TANZANIA DAIMA kuhusu Ufisadi Benki ya posta kuna sehemu iliyoonesha kwamba walifanya mahojiano na mtendaji mkuu wa benki ya posta na kwamba aliwaahidi kuwasiliana nao IJUMAA kwa ufafanuzi zaidi,lakini tangu ijumaa nimejaribu kufuatilia habari kwenye GAZETI sijaona chochote kuhusu yaliyojiri kati yao na mtendaji mkuu wa Benki ya POSTA.........KULIKONI TANZANIA DAIMA au mmekamata BINGO.
Katika tuhuma zote zilizotajwa ukiacha zile za ubadhirifu wa fedha nafikiri hii ya KUGHUSHI ni nzito na ni ya wazi zaidi cha ajabu sioni kama kuna jitihada zozote za kutolea ufafanuzi toka BODI ya WAKURUGENZI au hata wizara yenyewe.....KUNANI ????
Habari nilizofanikiwa kuzinasa ni kwamba BOT imetuma maafisa wawili kufuatilia mambo ndani ya bENKI YA POSTA media tusaidieni kuchimbua ili tuweze kujua UONGO au UKWELI wa yaliyosemwa.........NAPATA SHAKA NA JINSI HII VITA YA UFISADI INAVYOPIGANWA NAFIKIRI MAJESHI YANACHAGUA AINA YA MAFISADI WA KUWAANGAMIZI NA WENGINE WAKIPEPEWA PEPEWA..........
NAOMBA WANA JF WALE WALIO NA TAARIFA SAHAIHI ZIFUATAZO
-KAMA NI KWELI BOT IMETUMA MAAFISA KUCHUNGUZA
-WANAFUATILIA NINI NA NINI MATARAJIO KAMA IKITHIBITIKA UKWELI WA YALE YALIYOSEMWA ?
-WANAWEZAJE KUFANYA UCHUNGUZI DHIDI YA MAFISADI HUKU WAKIWA WAMESHIKILIA OFISI..?
 
Kuna Taarifa Ambazo Binafsi Sijazithibitisha Lakini Nazifanyia Kazi.....
Kwamba Ndugu Benedict Kapelega Anayetuhumiwa Kushiriki Kashfa Ya Kughushi Benki Ya Posta Ana Soo La Kuagiza Used Car Za Shirika La Posta Na Kughushi Nyaraka Kuonyesha Kuwa Magari Aliyoagiza Ni Bland New.............kwa Mwenye Taarifa Zaidi Jf Tuelezane Ili Tupambane Na Ufisadi Katika Taasisi Za Umma.
Shirika La Posta Inasemekana Liko Taabani Kifedha Litawezaje Kuwa Na Afya Kifedha Kama Watendaji Wake Ni Hawa Mafisadi Kina Kapelekga
 
Wakulu,
Hawa jamaa wawili wamerudishwa kazini lakini hawana kazi yoyote, wamewekwa kijiweni wanapewa magazeti yote hadi ya udaku wasome na chai kwa wingi. Nafasi zao wamepewa jamaa zake huyo Kihwele ambao hawajasomea taaluma hiyo. Yule wa tatu amefukuzwa kazi kwa sababu alikataa kufuta kesi mahakamani, yeye ndiye mwanasheria wa benki hiyo. Kihwele anafanya mambo yaleyale. Hebu wanahabari rudini muulizeni majibu ya maswali yenu.

BoT walikwenda lakini kama kawaida ya TZ hakuna lolote hadi sasa maana nao wamekamatishwa BINGO na Kihwele wakaishia. Kuhusu barua aliyoghushi ndiyo imefanya awape bingo maana alishindwa kuwaoonyesha barua iliyoidhinisha aongezewe mkataba sasa hata leo haipo.

Ukweli ni kuwa alipewa mkataba wa mwaka mmoja lakini yeye na Kapelega wakaidanganya Bodi kuwa ni ya miaka mitatu akapewa tena. Kama ni ubishi basi atoe hiyo barua wazi sote tuikodolee mimacho yetu hadharani. MWONGO kama nini sijui, huyo mzee Kihwele halafu fuska ajabu kwa vimwana utadhani Liyumba. Sasa ivi yuko Nairobi na kimwana mmoja. heheeeeee Tz tumekwisha
 
Jamani;

JF ina wananchama ambao ni wengi na hawajuani. Sasa mnaanza vipi kuwaandikia barua?

Mtu yeyote anaweza kupost chochote humu bila ridhaa ya uongozi wa JF.

Kwahiyo HONGERA ZIENDE KWA WANACHAMA na si uongozi wa JF!
 
Jamani;

JF ina wananchama ambao ni wengi na hawajuani. Sasa mnaanza vipi kuwaandikia barua?

Mtu yeyote anaweza kupost chochote humu bila ridhaa ya uongozi wa JF.

Kwahiyo HONGERA ZIENDE KWA WANACHAMA na si uongozi wa JF!
Aprili mwaka jana kwa ushirikiano na wanachama watatu, uongozi wa JF uliiandikia Bodi barua ya kutaka waliokuwa wamesimamishwa kazi kurejeshwa haraka:

Mkurugenzi Mkuu
Benki ya Posta Tanzania
Dar es Salaam.

YAH: TUHUMA ZA UBADHIRIFU KATIKA BENKI YA POSTA

Katika gazeti la Tanzania Daima la Jumatano ya tarehe 16 Aprili 2008, pamoja na habari nyingine, kulikuwa na taarifa ya kupewa likizo ya lazima wafanyakazi watano wa benki yako kwa kile kilichodaiwa kupisha uchunguzi unaofanywa katika kuwatambua watu waliosambaza taarifa kuhusu ubadhirifu katika Benki ya Posta katika mtandao wa internet wa Jambo Forums. Tunapenda kuamini kwamba taarifa hizi ni za kweli kwa kuwa hazijakanushwa na ofisi yako hadi tunapoandika barua hii.

Sisi wanachama wa Jambo Forums na Menejimenti nzima tumesikitishwa sana na uamuzi wako wa kuwapa kile kinachodaiwa kuwa ni likizo ya lazima wafanyakazi watano wa Benki ya Posta. Tukiamini kwamba Benki ya Posta inaendeshwa kwa misingi ya uwazi na kwa kuheshimu haki za wafanyakazi na binadamu kwa ujumla, tulitarajia kwamba uongozi wa benki yetu hii baada ya kupata taarifa za ubadhirifu ungeanzisha mchakato wa kujua ukweli kuhusu taarifa hizi ili kuchukua hatua stahiki. Hatuoni ni kwa namna gani uamuzi wako wa kuwapa likizo wafanyakazi hawa watano kutakomesha vitendo vya ubadhirifu ambavyo, kwa taarifa ambazo mtandao wetu wa Jambo Forums unazo, vimekithiri katika Benki ya Posta.

Pamoja na kwamba hatupendi kuingilia utendaji wako wa kazi, hatukubaliani na uamuzi wako wa kuwapa likizo wafanyakazi watano wa Benki ya Posta kwa kuwahusisha na taarifa zilizopatikana katika mtandao wetu wa Jambo Forums. Tunapenda kukuhakikishia kuwa habari za ubadhirifu katika Benki ya Posta zilizopatikana katika mtandao wa Internet wa Jambo Forums [hazikutolewa na mfanyakazi yeyote wa benki hiyo]. Zaidi ya yote, tunapinga kwa nguvu zetu zote vitendo vyovyote vya kudhoofisha mapambano dhidi ya ufisadi na udhaifu wa kiutendaji kwa viongozi wa mashirika ya umma, kama kilichoonyeshwa na Benki ya Posta, kwa kuwatia hofu watu wenye nia njema ya kufichua vitendo hivyo vya ufisadi hapa nchini.

Kwa barua hii tunakushauri uondoshe adhabu uliyowapa wafanyakazi wako kwa kuwa hawahusiki kwa namna yeyote ile na taarifa za ubadhirifu wa Benki ya Posta kama zilivyoandikwa katika mtandao wa Jambo Forums.

Tuhuma zilizoandikwa JamboForums ni kidogo kulinganisha na kile tulichopewa kuhusiana na Benki ya Posta na wanasiasa wa Tanzania. Tulichofanya ni kutoa kwa ufupi tu nini kinaendelea ndani ya Benki yetu ya Posta, kwa nia ya kuwazindua na kuepuka kuibua "EPA" nyingine inayoweza kuendelea kuchafua ‘hali ya hewa' ya kisiasa nchini.

Wako katika ujenzi wa Tanzania bila ubadhirifu,

Invisible,
k.n.y Jambo Forums.


CC.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (Tuma watu makini kuchunguza)
Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo (Safisha kumbukumbu zako TPB)
Gavana Benki Kuu ya Tanzania
Kamishna Financial Intelligence Unit (FIU)
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
Vyombo vya Habari
 
Barua nzuri sana Mkuu Invisible. Nadhani ndio chimbuko la mafanikio yaliyojitokeza (wafanyakazi wawili kurudi kazini). Je kuna taarifa zozote za uchunguzi uliofanyika kuweza kujua ukweli wa ufisadi huo?
 
Kuna namna inaandaliwa namna ya kuidhoofisha benki ya posta ili wajigawie.
Katika tuhuma za awali kubwa ilikuwa ni kughushi ambayo ilikuwa haihitaji gharama kubwa wala muda mrefu wa uchunguzi, Pamoja na akaguzi si tu kushindwa kuona minutes za board hata barua iliyotoka hadhina kumpa mkataba mwingine hawakuonyeshwa na mpaka leo Bado anaendelea kuendesha benki bila mandate.Inasemekana swala zima linatokana na Ikulu kuamua kuziba masikio na kufunika kombe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom