JF yapata ushindi mwingine dhidi ya ufisadi

Hivi kuna ushahidi kuwa hili ni matokeo ya kazi ya JF, au tunataka kudandia sifa za wengine?

Tusiwe tunajisifu kwa sifa tusizostahili, badala yake tujikosoe pale tunapoteleza.
 
Tanzania 1 Re: JF yapata ushindi mwingine dhidi ya ufisadi

Hivi kuna ushahidi kuwa hili ni matokeo ya kazi ya JF, au tunataka kudandia sifa za wengine? Tusiwe tunajisifu kwa sifa tusizostahili, badala yake tujikosoe pale tunapoteleza.

Kuna mambo tulijifunza tuliposhughulikia suala la vijana wa Ukraine, mpambanaji asiyeadjust mbinu zake hafai kupambana. JF (na hapa tuna maana wanachama.. and believe me wapo wenye ujiko wao..) wameshiriki kwa namna ya ajabu na majina yao yatabakia nameless. Sasa, mna uamuzi wa kukubali au kukataa it doesn't matter kilichotakiwa kufanyika kimefanyika.

Mkuu MMJ,

Maneno yako ni very loud and clear, maswali zaidi hakuna!
 
Hivi kuna ushahidi kuwa hili ni matokeo ya kazi ya JF, au tunataka kudandia sifa za wengine?

Tusiwe tunajisifu kwa sifa tusizostahili...

Ahsante Tanzania 1 kwa uzalendo wako wa dhati na kwa kuinua gravitas ya mdahalo.

Bahati mbaya wanasema mambo mengine tuyaache kama yalivyo. Tupunguze jazba na malumbano. Tukitaka tuwasiliane nao pembeni pembeni watuambie ni kiongozi gani waliongea nae na ilikuwaje wanafunzi wakarudishwa.

Lakini viongozi wengi tunao wasulubu hapa nao wanaona ni jazba na malumbano, na kufuaitilia vitu vidogo vidogo. Kwa mfano, kutoka kwenye thread moja ya leo, Mtanzania wa kawaida anaweza asione ubaya wa kampuni ya Maji kutangaza jina la mkwepa bili. Lakini sisi tumekemea hili kama ni kuingilia mambo binafsi.

Hatuwezi kufuatilia vitu vidogo vidogo kwa wengine halafu sisi tukataka simile katika kutakana ukweli. Tutakosa uaminifu. Sio kwamba tunasaliti misheni yetu dhidi ya uozo wa Serikali na Mafisadi, isipokuwa tunataka baraza liwe na gravitas. Tunaposema, ngoja kidogo, hiyo sifa sio yetu, tunaonyesha objectivity. Objectivity itakayotusaidia siku tukisema 'Lodi Lofa jiuzulu,' kwamba haitaonekana kama ni 'jazba na malumbano ya kufuatilia vitu vidogo.'

Uwajibikaji unaanzia kwetu wenyewe, na kidogo kuliko vyote tunacho weza kufanya sisi 'arm-chair critics' ni pamoja na kuwa wakweli. Vinginevyo tutaonekana tunakaa nyuma ya vioo vya Komputa kubwabwaja tu, kama alivyo tuasa Mama Mwanaidi Maajar, ubalozi wa London. Sio kwamba ni malumbano na jazba na kufuatilia vitu vidogo, ila ni kutaka kujipima wenyewe katika viwango vile vile tunavyo wapima wengine.

Tanzania 1 ahsante tena kwa uzalendo wako.
 
Ukisema mkitaka kuwasiliana nao ili kujua ilifanyika vipi hadi wakarudi na "wao wakakataa" sio sababu ya kukataaa kuwa JF haikuhusika. Kitu kimoja labda unasahau hapa ni kuwa JF ni members wake.

Wewe sasa hivi ukiwasiliana na member wa JF na mkasaidia kuchangia maji kijijini kwenu ila mkataka majina yenu yasitajwe, mnaweza kabisa kusema kuwa JF imechangia maji kwa vile nyie ni JF.

Lakini viongozi wengi tunao wasulubu hapa nao wanaona ni jazba na malumbano, na kufuaitilia vitu vidogo vidogo. Kwa mfano, kutoka kwenye thread moja ya leo, Mtanzania wa kawaida anaweza asione ubaya wa kampuni ya Maji kutangaza jina la mkwepa bili. Lakini sisi tumekemea hili kama ni kuingilia mambo binafsi.

Hii haiusiani na kilichofanyika hapa. Mkuu hivi kinakuuma sana kuona JF ikipata credit? Ulitaka isemwe kuwa kuhani mkuu naye amesaidia kurudisha wanafunzi chuoni ndio usikie vizuri?

Hatuwezi kufuatilia vitu vidogo vidogo kwa wengine halafu sisi tukataka simile katika kutakana ukweli. Tutakosa uaminifu. Sio kwamba tunasaliti misheni yetu dhidi ya uozo wa Serikali na Mafisadi, isipokuwa tunataka baraza liwe na gravitas. Tunaposema, ngoja kidogo, hiyo sifa sio yetu, tunaonyesha objectivity. Objectivity itakayotusaidia siku tukisema 'Lodi Lofa jiuzulu,' kwamba haitaonekana kama ni 'jazba na malumbano ya kufuatilia vitu vidogo.'

Ukweli gani unaoutaka zaidi ya kuwa wana JF wasiotaka kutajwa majina wameshughulikia wanafunzi wa UD. Mbona leo hii bado hujataka kujua mwana JF aliyevujisha barua ya Balali ya kujiuzulu au yule aliyevujisha mkataba wa Buzwagi?

Uwajibikaji unaanzia kwetu wenyewe, na kidogo kuliko vyote tunacho weza kufanya sisi 'arm-chair critics' ni pamoja na kuwa wakweli. Vinginevyo tutaonekana tunakaa nyuma ya vioo vya Komputa kubwabwaja tu, kama alivyo tuasa Mama Mwanaidi Maajar, ubalozi wa London. Sio kwamba ni malumbano na jazba na kufuatilia vitu vidogo, ila ni kutaka kujipima wenyewe katika viwango vile vile tunavyo wapima wengine.

Tanzania 1 ahsante tena kwa uzalendo wako.

Wewe inaonekana unasikia vibaya sana JF ikipata sifa na credits hapa. Sasa endelea kutafuta ili ujue aliyevujisha muziki wa bank ya posta juzi. So far kumbuka imetajwa JF na hakuna aliyetajwa na namna ilivyotoka huko kwenye management.

Kumbuka kuwa JF ina wanachama kuanzia ikulu hadi kwenye kata.
 
Vijana wamerudishwa chuoni kufuatia maombi ya uongozi wa DARUSO kukubaliwa na Prof. Maghembe, kumekuwa pia na majadiliano kati ya uongozi wa Chuo na DARUSO kuhusu huu mgogoro. Kwanini tusimpongeze waziri, viongozi wa DARUSO au hata viongozi wa Chuo? But instead, all the credit goes to JF! Excellent job! Kuna mambo mengi tunayostahili kujifagilia but am afraid this isnt one of them.
 
Una hakika kuwa viongozi wa Daruso sio members wa JF? Wewe kwa mawazo yako unadhani JF ni nani?
 
I can understand now! Kwa mtaji huo basi hata mtoto akifaulu mtihani wa darasa la saba au mgonjwa akipona kuhara- credits tupewe JF kwa kuwa kuna walimu na madaktari ambao ni members hapa.
 
Hivi mnafikiri vijana wa UDSM walikuwa wajinga kuja hapa kuomba msaada wa JF..........

Kilichofanyika...watu walio serious waliwauliza wanafunzi maswali ya msingi ili kuona watasaidiwa vipi......then serious people of JF took it from there.......trust me kuna wabunge humu ni member ndani ya CCM na upinzani, kuna walimu maprof wa UDSM wenyewe ni member hapa......hata Mukandala mwenyewe ananusa nusa humu........na hoja za hapa anazifahamu na anazipata kuanzia REDET yake mpaka tukio hili la sasa.......

......so guys sio kwamba JF hapa tunatafuta sifa NO.......tulishaweka misimamo yetu hapa na tukaisimamia na baadhi yetu hapa tukawashukia huko huko waliko............

msisahau pia kuwa JF tulialaani vitendo viovu vya wanafunzi vya kuvunja vitu visivyowaletea faida ktk kudai yanayowastahili.......na pia tulilaani vitendo vya serikali kutumia nguvu za dola kupiga wanafunzi wasio na hatia na akina mama wajawazito

.....kama hamuijui JF muulizeni Manumba, Mwema na RO walivyo na wanavyo haha na members wetu.......and i know is not overt yet because they still feel the JF pressure.......kutoka katka kila angle from Top to bottom and from everywhere in the world
 
Naona watu mnajitafutia ujiko msiokuwa nao. Wenzenu siku hizi JF wameamua kuipuuzia; mmeshazua matatizo yanayotosha kwa viongozi.

asante.
 
Ina matatizo gani wakati wakati hamna cha maaana mnachokifanya, zaidi ya mtu mmoja asiye na kazi alifanywa mtumwa na Mbowe kushinda humu na majina mia moja. mwenzake Mbowe anakuraha raha na mvuta bangi wake yeye anakesha humu kwa dola elfu mbili za website kawa kama mfanya kazi wa ndani ambaye hajui anaanza kazi saa ngapi na kumaliza saa ngapi.kaka kasome utapata kazi wenzako kina Masha Lawrance walitumia nafasi hizo kwa kusoma sio kuchambisha wazungu na kushinda JF.
 
Pole pole mkuu Ogah, usije ukaishia kumwaga yote, maneno mazito sana hayo makuu!
 
Ogah, kwa wengine JF ni kijiwe tu cha kupoteza muda; wakati kwa wengine ni chachu ya mabadiliko ya kifikra.
 
Ina matatizo gani wakati wakati hamna cha maaana mnachokifanya, zaidi ya mtu mmoja asiye na kazi alifanywa mtumwa na Mbowe kushinda humu na majina mia moja. mwenzake Mbowe anakuraha raha na mvuta bangi wake yeye anakesha humu kwa dola elfu mbili za website kawa kama mfanya kazi wa ndani ambaye hajui anaanza kazi saa ngapi na kumaliza saa ngapi.kaka kasome utapata kazi wenzako kina Masha Lawrance walitumia nafasi hizo kwa kusoma sio kuchambisha wazungu na kushinda JF.

ntakuona wa maana kweli kama ukiniletea ushahidi uliojitosheleza kuwa kuna mtu anatumikishwa na mbowe juu ya hii website.
 
Naona watu mnajitafutia ujiko msiokuwa nao. Wenzenu siku hizi JF wameamua kuipuuzia; mmeshazua matatizo yanayotosha kwa viongozi.

asante.

kama utumbo ni nyumba ya mavi, buchani unaufuatia nini?
kama JF mmeamua kuipuuza sasa mbona mnaingia na kuchangia mada?
 
'Hivi mnafikiri vijana wa UDSM walikuwa wajinga kuja hapa kuomba msaada wa JF..........'
hivi waliokuja kuomba msaada ni members wa Jf na waliotoa msaada ni members pia, kwa hio?........
Mi naona hii ni forum, inapanua tu watu mawazo na kutupa moyo kila mti akafanye wajibu wake kwa ubora zaidi, kwa hio asante JF kwa kuwapa moyo na ujasiri members wakaenda kutekeleza wajibu wao wa kawaida.
Kutoa haki kama kiongozi ndio kazi yako, ukuterereka iwe bahati mbaya, na kama JF au vikundi vingine, maandamano, Swala/maombi vimesiadia ukaitoa hiyo haki then thank to all of the parties.
 
Yap,huo ni ushindi kwa JF na wapenda haki wote,kwani vijana walipoomba ushauri na watu wakajitokeza kuchangia pamoja na kunyesha nini kifanyike si ndio hiyo namna mojawapo ya mapambano?Hongera wale walioenda extra mile na kulishughulikia hili swala,sio lazima kutaja ushiriki wako katika hili ulikuwa vp cha msingi tumefika hapo tulipo,sasa tuendelee kuimba nyimbo za Balali,Richmond, Chenge,Mkapa &co. Mpaka kieleweke tusisahau hii vita dhidi ya ufisadi ni vita endelevu haitakuwa na mwisho!
 
Naona watu mnajitafutia ujiko msiokuwa nao. Wenzenu siku hizi JF wameamua kuipuuzia; mmeshazua matatizo yanayotosha kwa viongozi.

asante.

Bi senti,

Nyie muendelee tu kuipuuzia JF lakini hapa halali mtu hapa kieleweke. Mukandala anajua amekosea kuingilia chaguzi huru za vijana wa mlimani na kisha kuleta FFU na kupiga wanafunzi bila hatia yoyote. Katika hili ameingia kwenye list of mafisadi na madikiteta ambao JF inapigana nao kila siku.

Kama anataka kuijaribu nguvu ya JF, basi aendelee kuipuuzia kama Mkapa alivyopuuzia kwa miaka miwili kabla mambo hayajamwakia kila anakoenda.
 
Katika vitu ambavyo Prof. Mkandara aliwahi kuchemka nafikiri hili linaongoza, hivi hakujua kuwa kuna University bylaws za kuwashughulikia hawa vijana badala ya kuwapeleka mahakamani na kumdhalilisha waziri wake kwa kulitngazia bunge kuwa wamefukuza wanafunzi na kuwarudisha kesho yake?

Hili limewapa credit vingozi wa DARUSO waliopo madarakani kwa kuonekana wanajua wanachofanya zaidi ya mkandara na serikali walikurupuka na kufukuza wanafunzi.

Mungu ibariki tanzania tutaona mengi mwaka huu, ni mwaka wa kuonyesha uozo wa viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom