JF Unilateral Ceasefire...?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Kuna mambo yametokea hapa JF katika wiki hizi chache ambayo yamewafanya watawala washtuke kidogo. Ndio wamekuwa wakishtushwa na yanayoendelea lakini haya makubwa matatu yamefanya kutoa ushauri wa kuitaka JF ipunguze mwendo kidogo na kuwapa nafasi ya kupumua.

- Kuibuliwa kwa kashfa Shirika la Posta ambapo baadaye wafanyakazi watano walijikuta wakiwekwa pembeni kwa hatua za kinidhamu. Mambo hayo yalitakiwa yamalizike ndani "kwa ndani" na kutolewa hadharani jinsi ile hakikuwafurahisha watu wengi. Wanasema wenye manung'uniko wangefuata taratibu.

- Ukodishaji wa Airbus (dege letu kubwa kabisa) na jinsi ambavyo mambo yaliendeshwa. Uvujaji wa habari za ATC licha ya kutofanyiwa kazi na wakubwa kufuatia agizo la "mkulu" mmoja mwenye maslahi ya kibinafsi kuliwaudhi wahusika wengi kwani lolote walilokuwa wanapanga kufanya liliibuliwa hadharani. Watu wengine wasiopungua watano wakapoteza kazi zao kwa kudhaniwa kwa namna moja au nyingine wanahusika na uvujaji huo.

- Kuibuliwa kwa barua ya Jim Sinclair ambayo ilichambuliwa na kufanya ionekane kuwa jamaa ana ubia na kumlazimisha kuandika barua ya kujieleza kwa wadau imemsumbua mmoja wa wakulu kwani imemfanya aonekane kama poodle wa Jim. Hakufurahishwa na jinsi watu walimshambulia mwekezaji na kukawa na hofu kuwa tunaweza kusababisha wawekezaji waanze kukimbia.

- Kuibuliwa kwa deni la Mkullo masaa machache kabla ya yeye kusoma bajeti kulionekana ni mbinu ya aina fulani kumchafulia. Siku chache baada ya statement ile kuanza kusambazwa mtandaoni Bw. Mkullo ameanza haraka ya kulipa deni lake na hivyo kushughulikia jambo hilo ambalo anaamini lingemletea picha mbaya hasa kwenye mjadala ujao wa wizara yake.

- Kilele cha kukerwa huko nako kumetokea masaa machache yaliyopita ambapo Bajeti ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania ilipatikana hapa kwanza kabla ya kupatiwa Wabunge! Hiki inadaiwa kimemuudhi hata JK kwani amshangazwa inakuwaje bajeti yetu jinsi ilivyo inasomwa karibu masaa ishirini na nne kabla ya ile ya Wakenya, Waganda, Rwanda na Burundi! Hili la kuvuja kwa bajeti limeanza kuwasumbua watu fulani fulani kwa kuonesha uzembe au kutowajibika.


- Lakini kilichowaudhi baadhi ya watu ni jinsi habari za "sanaa ya jadi/kisasa" kuonekana kutumika Bungeni na habari hizo kufika JF kabla ya vyombo vya usalama na hivyo kuharibu jitihada za uchunguzi. Inadaiwa kitendo cha kuweka habari za "mbunge" huyo hapa na kile kilichojiri inadaiwa iliwapa nafasi wahusika kuanza kujaribu kupoteza ushahidi hasa baada ya habari kuonesha kuwa tukio lilikuwa ni Jumanne kumbe ni la Jumatatu na haikuwa kwenye mkutano wa wabunge wa CCM bali baada ya briefing ya wabunge wote. Hili la habari hizi ambazo wabunge walitaka zimalizike kimya kimya kwani zinaweza kumuabisha mtu zimewafanya wawe waangalifu sana na vyombo vinavyochunguza vimesikitika kuwa wao wamepata habari toka kwa waandishi waliopitia kwenye mtandao na baadaye kuthibitishiwa na uongozi wa Bunge.

Mambo hayo na mengine madogo madogo ambayo yanajulikana JF kama "datas" yamesababisha ujumbe utumwe japo si kwa maneno kamili kuwa JF katika jitihada za kumwaga data yawezekana wakawa wanaharibu mambo mengi ya uchunguzi, upelelezi n.k Ujumbe huo unaashiria kuwa kama kuna mtu anaona kitu chochote serikalini hakiendi sawa afuate taratibu za malalamiko na kama ni suala la uhalifu afuate vyombo vya kisheria badala ya kuweka taarifa kwenye mtandao ambako hajulikani ni nani na ni vigumu kufuatilia. Zaidi ya yote, inashauriwa tuwe tunasubiri taarifa rasmi ili kuwe na uhakika wa kinachosemwa badala ya kueneza tetesi, uvumi, propaganda na "vijimaneno" ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama, amani, mshikimano na utulivu wa nchi yetu.

Swali kwenu: Je JF na wale watoa data watangaze unilateral ceasefire? Tuendelee kuwa mahali pa kujadiliana mambo mengine lakini mambo ya kuleta habari nyeti tuyaweke pembeni hadi tupate taarifa, ushahidi na vielelezo kamili?
 
Either JF is doing the right thing, the right way and wrong time (to them) or JF is doing the wrong thing completely.

The question I have is why is Serikali and Usalama (Polisi, PCCB, TISS, AG) always 10 steps behind JF in uncovering, investigating and providing prognosis (analytical assesment) on everything that involves Corruption, Economic Sabotage and white colar crime?

If they can answer that, then we could make pact with them and dance to the same tune. Otherwise, their lack of responsiveness is prompting everyone kumwaga Dataz!
 
Hapa ni kupeana habari tena zikiwa za moto tusubiri watuambie kile wao wanataka tusikie ? sisi tunawataka wawe wa kwanza kusema na sio vinginevyo.

Pia kubwa ni kuwekwa kwa Ripoti ya EPA humu imewasumbua sana sana na hili limekuwa na mtikisiko mkubwa kwenye gov.circles.
 
Mwendo mdundo kama dataz zinakuja na mtu anazo azimwage tu hapa tunataka hao mafisadi wakose usingizi
 
From the lack of faith on the part of JF, any such request becomes suspect.

Ni kama vile polisi wanaojulikana kuwa wala rushwa wawaambie wananchi "msiwaripoti wala rushwa kwa PCCB (if PCCB was credible) na tuachieni tutawashughulikia na kufanya upelelezi.

Sababu inayoifanya JF kupata umaarufu na kupewa documents zote hizi ni ukweli kwamba wananchi wamekuwa frustrated na the available conventional means.

Once they restore the public's trust in investigation and the legal framework, automatically watu watatumia the conventional means (mahakama za kazi, etc etc)
 
Mkuu Wangu MMJ,

Heshima mbele mkuu, kama kawaida hizi nimezisikia kutoka another angle, na ninashukuru kuwa wewe umekuwa wa kwanza kuzileta maana nilikuwa mbioni,

Binafsi, nipo speechless lakini nitazi-diggest na kurudi na jibu, ila ahsante kwa ujumbe huu mzito!
 
Hapana Mkjj, HAKUNA Ceasefire unilateral, bilateral, multilateral, or vertically. Hapa ni Horizontal tu yaani sambamba.

Waambie hao wakulu, all they have to do is follow the law of the land, and JF will die a natural death kwa kukosa cha kudiscuss. As long as injustice continue in our motherland, JF will gain traction and continue to prosper.

Kwa wapenda haki serikalini, JF ni sehemu ambayo inawasaidia hata wao kufanya kazi vizuri, kwani mabomu mengine wanayagundua mapema, kwa hiyo ikifika sehemu wanatakiwa kufanya ujinga wanakuwa na info za kutosha.

VIVA JF, ALUTA CONTINUA!!!
 
Ni vizuri wakajua na sisi wana JF tuna nia njema sana. Na katika hii dunia ya ushindani dawa ya kuwashinda JF ni kutoa habari in 'realtime'. Ni lini PCCB walitoa breaking news! Uchunguzi unaendelea milele!

Mimi nasema watupishe, tuendelee kusafisha nchi yetu kwa namna hii kutokea upande huu na wenyewe kama wanataka waanzie upande wa pili tukutane katikati, nchi yetu ikiwa inang'aa (kwa transparency na ufanisi)! Huwezi kuwa best student darasani kwa kuwaua/kuwahujumu (au hata kunegotiate na) wanaokuzidi - dawa ni kukaza msuli, ili upate sifa unayo deserve. Watu wamepoteza imani na vyombo vya usalama/serikali.

Kama wako serious basi watuonyeshe kwa kuwashikati wa EPA, Mkapa, Vijisenti, akina Richmund nk!

Kwa ujumla waambie hivi, safari hii wamelamba galasa kwa sababu JF ni umma na wao ni watawala! Nao waanzishe tovuti ya kwao (labda waiite WF), kama hao mamluki waliowaweka hapa JF wameona hawako effective!

Kama moshi umezidi sana jikoni watoke!!!
 
Kumbe wanasikia! Kukaa kwao kiomya nilidhani ujumbe haufiki! Sasa wametutHibitishia kuwa hatutWangi maji kwenye kinu. Ninataka kuwapa onyo kuwa chochote watakachokifikiria, wasifanye lolote linalolenga kuidhibiti jf kwa hakika nawaambia wakinyamaza hawa, hata mawe yatapiga kelele
 
Maneno yote anayo yasema Mzee wa Kijijini ni mazito na yana make sense sana lakini wao kwa kudhani kwamba tu haribu watupe rajha kidogo kwa kuchukua action against the criminals ambao wako nao pamoja .Wanashangaa sisi kujua ya Chenge na uchawi wake mbona wasishangae Sinclair kuwa na ripoti ya madini kabla ya watanzania hawajaambiwa lolote .Kwa kuwa wao huwa hawasemi hadi waweke mbinu za kutudanganya kwa maslahi ya kisiasa sisi hatuna siasa tutasema kwa maslahi ya Watanzania .

Watuache tuendelee wakitaka kama wengi walivyo sema ni kutenda haki pekee .
 
No surrender no retreat. Hivi wanapoiba huwa wanawaonea huruma waliolipa kodi? Wao ni kula tu tena bila kunawa mikono. Hatuwezi kuendelea na tabia kama hii ambayo Serikali ya CCM inajiona imepewa ufalme wa kufanya watakalo kwa WTZ. Hivi ni aibu ya namna gani kudhalilishwa na wageni kutoka nje?

No way! Waanze kuwawajibisha waliojiuzulu na kuwafilisi wote waliotafuna pesa ya walipa kodi na kulihujumu taifa. Vitendo madhubuti vya kuwashikisha adabu MAFISADI ndio vitaleta maisha bora kwa kila MTZ na JF inaweza kuongelea ceasefire then only then.

Mzee Mwanakijiji – Hatulali hapa wala hatuchezi upatu kwenye maswala ya Tanzania. The game is on.
 
Kushaa kwao kuwa dataz zinafika hapa kbla wao hawajaamka kunadhihirisha kuwa wameshindwa kufanya kazi. Tuwape adhabu gani?
 
still, mpakakieleweke...mmoja yapoints zako mwanakjj, wanasema "mbunge" alionekana kwenyecameras onthe wrong day...sawa,swali lilelile alikuwa anatafuta nini kwenye viti vya wenzio? aliangusha mawani kwenye kiti cha spika? No ceasefire! - mpaka kieleweke.
 
Mimi nashauri tuwabane mbavu na kujiweka sawa kuwa na massive campaign against wao na Chama chao mwaka 2010 .We can do it kama Sinclair kalazimika kuandika barua kuomba msaha sabau ya JF na yeye ndiye ana ubia na Rais na Urais kwa nini tusiwashinde ? Tujiandae tumechoshwa na longo longo.
 
Mimi nashauri tuwabane mbavu na kujiweka sawa kuwa na massive campaign against wao na Chama chao mwaka 2010 .We can do it kama Sinclair kalazimika kuandika barua kuomba msaha sabau ya JF na yeye ndiye ana ubia na Rais na Urais kwa nini tusiwashinde ? Tujiandae tumechoshwa na longo longo.

wewe unachangia nini humu zaidi ya hizo habari zako za kucopy and paste ?
 
wewe unachangia nini humu zaidi ya hizo habari zako za kucopy and paste ?

Kada mara moja moja uwe unaacha mambo yanakupita kama ni maji marefu kwako .Yaani leo unasemaje ? Mimi si mtu wa ku copy na ku paste kila mara ni mara moja moja sana .Lakin hata hivyo ukitaka kujibizana nami tafadhali fungua thread mpya hapa tuna ongelea kazi nzuri ya JF kwamba hatuwezi iibodi pembeni ni kuwabana tu .Changia katika hili na ukitaka kuni hoji tafadhali unaruhusiwa kufungua mada pale watachangia watu .
 
Kada mara moja moja uwe unaacha mambo yanakupita kama ni maji marefu kwako .Yaani leo unasemaje ? Mimi si mtu wa ku copy na ku paste kila mara ni mara moja moja sana .Lakin hata hivyo ukitaka kujibizana nami tafadhali fungua thread mpya hapa tuna ongelea kazi nzuri ya JF kwamba hatuwezi iibodi pembeni ni kuwabana tu .Changia katika hili na ukitaka kuni hoji tafadhali unaruhusiwa kufungua mada pale watachangia watu .

huyoooooooo ! basi usilie..haya tuendelee na mada !
 
Serikali, ingawa bado iko usingizini, imeisaidiwa sana na JF katika kuongeza umakini katika utekelezaji wa shughuli zake. Bila ya JF, watawala wangekuwa wakiendelea kulala na huku watawala wengine wakiendelea kuhujumu uchumi wa nchi yetu kwa kasi kubwa bila ya yeyote kujitokeza kufichua dili zao zote chafu.

I think it makes more sense kwa watawala kutoa official statement kuishukuru JF kwa kuwafanya wawe makini zaidi katika utekelezaji wa shughuli zao, badala ya kuitaka JF i-declare ceasefire.

Tunapaswa kuongeza juhudi na maarifa zaidi katika kuendeleza haya mapambano. Hakuna kurudi nyuma.
 
Back
Top Bottom