Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,667
- 40,546
Kuna mambo yametokea hapa JF katika wiki hizi chache ambayo yamewafanya watawala washtuke kidogo. Ndio wamekuwa wakishtushwa na yanayoendelea lakini haya makubwa matatu yamefanya kutoa ushauri wa kuitaka JF ipunguze mwendo kidogo na kuwapa nafasi ya kupumua.
- Kuibuliwa kwa kashfa Shirika la Posta ambapo baadaye wafanyakazi watano walijikuta wakiwekwa pembeni kwa hatua za kinidhamu. Mambo hayo yalitakiwa yamalizike ndani "kwa ndani" na kutolewa hadharani jinsi ile hakikuwafurahisha watu wengi. Wanasema wenye manung'uniko wangefuata taratibu.
- Ukodishaji wa Airbus (dege letu kubwa kabisa) na jinsi ambavyo mambo yaliendeshwa. Uvujaji wa habari za ATC licha ya kutofanyiwa kazi na wakubwa kufuatia agizo la "mkulu" mmoja mwenye maslahi ya kibinafsi kuliwaudhi wahusika wengi kwani lolote walilokuwa wanapanga kufanya liliibuliwa hadharani. Watu wengine wasiopungua watano wakapoteza kazi zao kwa kudhaniwa kwa namna moja au nyingine wanahusika na uvujaji huo.
- Kuibuliwa kwa barua ya Jim Sinclair ambayo ilichambuliwa na kufanya ionekane kuwa jamaa ana ubia na kumlazimisha kuandika barua ya kujieleza kwa wadau imemsumbua mmoja wa wakulu kwani imemfanya aonekane kama poodle wa Jim. Hakufurahishwa na jinsi watu walimshambulia mwekezaji na kukawa na hofu kuwa tunaweza kusababisha wawekezaji waanze kukimbia.
- Kuibuliwa kwa deni la Mkullo masaa machache kabla ya yeye kusoma bajeti kulionekana ni mbinu ya aina fulani kumchafulia. Siku chache baada ya statement ile kuanza kusambazwa mtandaoni Bw. Mkullo ameanza haraka ya kulipa deni lake na hivyo kushughulikia jambo hilo ambalo anaamini lingemletea picha mbaya hasa kwenye mjadala ujao wa wizara yake.
- Kilele cha kukerwa huko nako kumetokea masaa machache yaliyopita ambapo Bajeti ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania ilipatikana hapa kwanza kabla ya kupatiwa Wabunge! Hiki inadaiwa kimemuudhi hata JK kwani amshangazwa inakuwaje bajeti yetu jinsi ilivyo inasomwa karibu masaa ishirini na nne kabla ya ile ya Wakenya, Waganda, Rwanda na Burundi! Hili la kuvuja kwa bajeti limeanza kuwasumbua watu fulani fulani kwa kuonesha uzembe au kutowajibika.
- Lakini kilichowaudhi baadhi ya watu ni jinsi habari za "sanaa ya jadi/kisasa" kuonekana kutumika Bungeni na habari hizo kufika JF kabla ya vyombo vya usalama na hivyo kuharibu jitihada za uchunguzi. Inadaiwa kitendo cha kuweka habari za "mbunge" huyo hapa na kile kilichojiri inadaiwa iliwapa nafasi wahusika kuanza kujaribu kupoteza ushahidi hasa baada ya habari kuonesha kuwa tukio lilikuwa ni Jumanne kumbe ni la Jumatatu na haikuwa kwenye mkutano wa wabunge wa CCM bali baada ya briefing ya wabunge wote. Hili la habari hizi ambazo wabunge walitaka zimalizike kimya kimya kwani zinaweza kumuabisha mtu zimewafanya wawe waangalifu sana na vyombo vinavyochunguza vimesikitika kuwa wao wamepata habari toka kwa waandishi waliopitia kwenye mtandao na baadaye kuthibitishiwa na uongozi wa Bunge.
Mambo hayo na mengine madogo madogo ambayo yanajulikana JF kama "datas" yamesababisha ujumbe utumwe japo si kwa maneno kamili kuwa JF katika jitihada za kumwaga data yawezekana wakawa wanaharibu mambo mengi ya uchunguzi, upelelezi n.k Ujumbe huo unaashiria kuwa kama kuna mtu anaona kitu chochote serikalini hakiendi sawa afuate taratibu za malalamiko na kama ni suala la uhalifu afuate vyombo vya kisheria badala ya kuweka taarifa kwenye mtandao ambako hajulikani ni nani na ni vigumu kufuatilia. Zaidi ya yote, inashauriwa tuwe tunasubiri taarifa rasmi ili kuwe na uhakika wa kinachosemwa badala ya kueneza tetesi, uvumi, propaganda na "vijimaneno" ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama, amani, mshikimano na utulivu wa nchi yetu.
Swali kwenu: Je JF na wale watoa data watangaze unilateral ceasefire? Tuendelee kuwa mahali pa kujadiliana mambo mengine lakini mambo ya kuleta habari nyeti tuyaweke pembeni hadi tupate taarifa, ushahidi na vielelezo kamili?