Jf: Tuanzishe ukurasa wa saini kudai katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jf: Tuanzishe ukurasa wa saini kudai katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by MAMMAMIA, Dec 16, 2010.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mengi tumeshasema kuhusu umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya, lakini mawazo yetu ni ya mtu mmoja mmoja ingawa tunakuwa wengi pale tuanpochangia hoja.

  Ninachopendekeza kwa "Experts" wa mtandao huu, watuanzishie ukurasa ambao tutaorodhesha majina na kusaini ili kufikia watu milioni moja na zaidi ili yapelekwe bungeni ikiwa kama ni mchango wetu katika hoja na haja ya kudai Katiba Mpya.
   
 2. D

  DENYO JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kusaini haisaidii tunao great thinkers humu jamvin wanaoweza kutengeneza rasimu ya katiba mpya inayoweza kuonesha ni vipengele gani tuvibadili ili kuitwa katiba mpyaaa kabisa na ili kupambana na hoja kama za akina kombani, mwinyi na wengineo ambao wanajua kwa kuundwa katiba mpya kuna hatari ya ICC kuja Tanzania.
  Kuna watu katiba imewaruhusu kugeuza nchi hii ya kwao na wanaweza kufanya watakavyo kuanzia rasimali za nchi hii na uongozi-yaaani wameamua kuwa wanarithishana.
  CCM wana kundi la watawala na wapiga makofi lakini ccm ina members 5 miliion wakati watanania tupo 42 miliion -sasa lazima tuje na mawazo ya kimkakati sio kusaini haitoshi tuanze na msingi kuainisha mapungufu ya katiba ya sasa ili kushinkiza katiba mpya.

  LAZIMA WAJITOLEE WANAJF AU CHADEMA MANAKE IKO KWENYE ILANI YA CHAMA WATENGENEZE RASIMU YA KATIBA MPYA INAYOPAMBANUA KILA OUZO WA KATIBA YA SASA HALAFU TUISAMBAZE. TUPO TEYARI KUTEMBEA KWA MIGUU MTAA HADI MTAA NYUMBA KWA NYUMBA TANZANIA NZIMA KUELEZA KWANINI TUNAHITAJI KATIBA MPYA.
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ni wazo zuri, la muhimu ni Watanzania wenye uchungu na nchi hii tujitolee kusafisha uoza huu uliodumu miaka 49 sasa.
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Come on guy ukurasa huo upo mkuu fuata link hii usaini: TUNAHITAJI KATIBA MPYA Petition
  Na kama una jamaa zako ambao hawawezi kufikia internet download hii pdf View attachment katiba_mpya.pdf kisha tengeneza fomu hiyo watumie nao wajiorodheshe wakutumie kisha uitume kama ilivyoelekezwa kwa: katibatanzania@gmail.com
  Nadhani kila kitu kiko clear mzee. Wasaidie na wengine.
   
Loading...