Invisible
Robot
- Feb 11, 2006
- 9,075
- 7,878
Not at all...
Kuna topic iliwahi kuanzishwa hapa na mwanachama akilalamika kuwa JF haiko salama na iko uchi, sikujibu kitu nikaacha wadau wamjibu ili kuona wangapi wanaelewa kinachoendelea.
Kwa manufaa ya wengi naomba nijaribu kuweka bayana mambo yafuatayo:
Kuna aina mbalimbali za mawasiliano ndani ya JF. Si rahisi na naomba kusisitiza si rahisi kuwa na upenyo wa mtu kusoma ujumbe wa mtu bila hiari ya mtu mwenyewe.
Namaanisha kuwa, ukitumiwa Private Message ukii-forward kwa mtu basi umeyataka mwenyewe hukulazimishwa! That's not a breach. Kwa wale wanaodhani wanaweza kuona Private messages za wengine basi wajaribu na wakifanikisha watufahamishe ili tufanye marekebisho ya haraka sana...
Private messages can be read thru Private Messages
Kwa ambaye hajajisajili hawezi kuona kitu hapo, labda aliyejisajili ndiye anaweza kuona na kujikuta badala ya kwenda kwenye Private Messages za mwenzake anadondokea kwake!
Kuna kitu kipya ambacho kilipowasili ndani ya JF tulikitambulisha kwenu na kuwambia kinaitwa Profile Visitor Messages. Hiki kinawachanganya wengi na wengine wakikiona wanadhani ndio wameona Private Messages za mtu.
Mfano: Ukitembelea Profile ya Invisible hapa: JamiiForums.com - View Profile: Invisible utakutana na baadhi ya jumbe zikiwa zimelenga mambo mbalimbali ambayo ni kwa ajili yangu kubadilishana na wanachama na ziko wazi kwa yeyote ili ajue nikiongea pembeni na watu huwa naongea nao nini na kivipi. Nimeziacha wazi kwa mapenzi yangu!
TAHADHARI: Ukiwa na ujumbe binafsi (ambao hutaki uonekane kwa wengine) usiandike kwenye Profile ya mwanchama yeyote kwani unaonekana kwa kila mtu. Ukiandika huko ni kumsalimia kwa kawaida na huoni kuna cha kuficha. Kama unajua wengi huwa wanakosea na kuandika vitu personal kwenye profile yako tafadhali nenda kwenye User CP na ondoa option ya kupokea Visitor Messages ili waache kumwaga mchele katika kuku wengi kwani ziko wazi kwa kila mtu hata ambaye hajajisajili.
Heri nimewafahamisha...