JF Scheduled Maintenance: June 13, 2020

Wakuu,

Leo usiku wa manane, kati ya saa 8 na saa 10, tutakuwa na marekebisho kadha wa kadha katika miundombinu yetu yanayoweza kupelekea kusimama kwa baadhi ya huduma (na wakati flani huduma zote kusimama).

Hii ni katika kuimarisha zaidi miundombinu yetu na kuongeza uwezo wa kuhimili mikikimikiki yoyote inayoweza kutokea. Zoezi hili liliwahi kufanywa miaka 2 iliyopita lakini safari hii linatarajiwa kuchukua takribani dakika 30 hadi saa 1.

Tunapenda kutoa taarifa hii mapema ili mtu akiona kuna vitu haviko sawa muda huo asishtuke; ajue tupo kazini.

Endapo kutatokea lolote linalohitaji kushirikishana, tunaomba fuatilia kurasa zetu za Telegram - JamiiForums na Twitter - https://twitter.com/JamiiForums

Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu katika kufanikisha zoezi hili.

/ Jamii Forums
Ahsante kwa taarifa mkuu. Ngoja niingie PM fasta nikamate namba za wachuchu wa MMU kwa ajili ya ukaguzi wa weekend...
 
Dakika chache zijazo, itabidi kufunga tovuti kwa muda ili process ichukue muda mchache zaidi.

Asante
 
Ilikuwa effective , kwa muda kama ilivyosemwa katika taarifa

Imesaidia, zama ni tofauti. Mara paap unakutana na ''Telegram” bila taarifa hapo unatupa kifaa ulichotumia
 
Ilikuwa effective , kwa muda kama ilivyosemwa katika taarifa

Imesaidia, zama ni tofauti. Mara paap unakutana na ''Telegram” bila taarifa hapo unatupa kifaa ulichotumia
Hahaha, asante mkuu wangu.

Naamini katika kutoa taarifa mapema kwa wadau ili wasishtuke nini kimetokea. Landa iwe emergency ambayo hakuna jinsi zaidi ya kufanya haraka sana
 
Naamini katika kutoa taarifa mapema kwa wadau ili wasishtuke nini kimetokea.
Imesaidia sana mkuu. Mara tufuatilie Telegram na Tweeter, hapo hakuna muda wa kupoteza, tosa kifaaa mto Ruvu, kikisombwa na maji ni ngumu ku trace. Baharini kinaweza kuvuliwa. Halafu toa taarifa simu imeibiwa, unguza vidole hasa gumba na mafuta ya mawese, alizeti hapana DNA haifutiki.
 
Hahaha, asante mkuu wangu.

Naamini katika kutoa taarifa mapema kwa wadau ili wasishtuke nini kimetokea. Landa iwe emergency ambayo hakuna jinsi zaidi ya kufanya haraka sana
Mkuu mara ya Kwanza mtu aki ni QUOTE au aki ni LIKE nilikua napata taarifa hata Kama nipo nje ya JF siku hizi kimya Nini tatizo au Nifanyeji iwe Kama mwanzo?
 
Back
Top Bottom