JF Scheduled Maintenance: June 13, 2020

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
Wakuu,

Leo usiku wa manane, kati ya saa 8 na saa 10, tutakuwa na marekebisho kadha wa kadha katika miundombinu yetu yanayoweza kupelekea kusimama kwa baadhi ya huduma (na wakati flani huduma zote kusimama).

Hii ni katika kuimarisha zaidi miundombinu yetu na kuongeza uwezo wa kuhimili mikikimikiki yoyote inayoweza kutokea. Zoezi hili liliwahi kufanywa miaka 2 iliyopita lakini safari hii linatarajiwa kuchukua takribani dakika 30 hadi saa 1.

Tunapenda kutoa taarifa hii mapema ili mtu akiona kuna vitu haviko sawa muda huo asishtuke; ajue tupo kazini.

Endapo kutatokea lolote linalohitaji kushirikishana, tunaomba fuatilia kurasa zetu za Telegram - JamiiForums na Twitter - https://twitter.com/JamiiForums

Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu katika kufanikisha zoezi hili.

/ Jamii Forums

=====
UPDATE:

Huduma zimerejea sawa baada ya kutoweka kwa takribani dakika 55.

Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu
 
Back
Top Bottom