Salamuni wapendwa,
Nafikiri muda umefika kwa sisi ambao wazalendo wa kweli kuonyesha uwepo wetu katika kuamua mustakabali wa nchi yetu. Ni wazi kuwa a group of Mediocres walioji organize tokea mwanzo wameteka chama alichokiasisi Mwlm Nyerere na sasa wamefikia kuiweka nchi katika hatari. Naamini kabisa sio wote ni waovu kwenye hiki chama ila wanaokishikilia wengi ni Mediocres na hawamuachii yeyote mwenye nia safi kufanya mazuri kwenye hii nchi. Huu ni ukweli ambao mimi na wewe na wao wanaufahamu.
Sisi tumekuwa tukizungumza sana, we are opportunists, lakini naamini ipo njia tunayoweza kuitumia kwa ustaarabu kabisa. Tuanzishe movement, sio chama cha kisiasa, hapana, ni vuguvugu la madai ya katiba mpya na uwajibikaji katika taasisi za umma. Tuitishe mkutano tualike mabalozi, wahadhiri, wanasiasa, vyombo vya kimataifa vya nje na vya ndani, tuutangaze mkutano huu kwa kila namna. Mimi najua humu tunao wasomi wa kila idara, wanasheria tutawahitaji sana sana. Hii nchi inakwenda kubaya jamani, natamani kama wote tungaliiona hali hii. Uungwaji mkono utakuwa ni mkubwa wa movement ya namna hii kama itapelekwa kisomi na kwa njia nzuri za amani. Tafadhalini sana wenzangu tufikirie jambo hili, tushiriki moja kwa moja tofauti na sasa tunawasubiria wenzetu wafanye kazi sisi tunajadili tu. Hii nchi imetekwa na lazima ikombolewe, hakuna jambo lolote chini ya hapo. Wanafanya umafya wa kila namna wamekamata madaraka sasa wanaanza kuhubiri Amani na mshikamano, udini na ukabila, uvumilivu na mustakabali wa nchi huku wakijua fika wao ndio wanaohujumu mustakabali wa hili taifa. Serikali inajua fika nani aliyesambaza sms za kidini lakini imefumba macho maana wanajua ilikua kwa manufaa yao.
Nchi yetu ipo kwenye majonzi makubwa, watu wengi wana huzuni na hawaridhiki na mambo yanavyokwenda. Takriban watu million 5 ndio waliomchagua raisi aliyetangazwa (Takwimu za NEC), millioni 14 waliobakia walipinga aidha kwa kutokwenda kupiga kura ama kuchagua wengine. CCM watu wa ajabu sana, hii asilimia 61 wanayoitangaza ingekuwa na maana kama ingekuwa inatokana na kura za watu million 19, less than that ni ujinga kujidai. Na hii ndiyo nayowaambia ni Mediocres, huwezi kusema ushindi wa kishindo huku robo tatu ya watu hawako upande wako. Kibaya zaidi hawaonyeshi kushtushwa na hali hii na kuchukua tahadhari mapema, watu wanasema waziwazi hawapigi kura maana wanaowachagua wawaongoze sio wanaoshinda. Hii ni hatari kwa wote wenye mapenzi mema na Tanzania, hima tuamke, kwa amani tupiganie mabadiliko yatakayofaidisha taifa letu.
Nawasilisha.