JF Our Country Needs Us...

Pax

JF-Expert Member
May 3, 2009
268
87
Salamuni wapendwa,
Nafikiri muda umefika kwa sisi ambao wazalendo wa kweli kuonyesha uwepo wetu katika kuamua mustakabali wa nchi yetu. Ni wazi kuwa a group of Mediocres walioji organize tokea mwanzo wameteka chama alichokiasisi Mwlm Nyerere na sasa wamefikia kuiweka nchi katika hatari. Naamini kabisa sio wote ni waovu kwenye hiki chama ila wanaokishikilia wengi ni Mediocres na hawamuachii yeyote mwenye nia safi kufanya mazuri kwenye hii nchi. Huu ni ukweli ambao mimi na wewe na wao wanaufahamu.

Sisi tumekuwa tukizungumza sana, we are opportunists, lakini naamini ipo njia tunayoweza kuitumia kwa ustaarabu kabisa. Tuanzishe movement, sio chama cha kisiasa, hapana, ni vuguvugu la madai ya katiba mpya na uwajibikaji katika taasisi za umma. Tuitishe mkutano tualike mabalozi, wahadhiri, wanasiasa, vyombo vya kimataifa vya nje na vya ndani, tuutangaze mkutano huu kwa kila namna. Mimi najua humu tunao wasomi wa kila idara, wanasheria tutawahitaji sana sana. Hii nchi inakwenda kubaya jamani, natamani kama wote tungaliiona hali hii. Uungwaji mkono utakuwa ni mkubwa wa movement ya namna hii kama itapelekwa kisomi na kwa njia nzuri za amani. Tafadhalini sana wenzangu tufikirie jambo hili, tushiriki moja kwa moja tofauti na sasa tunawasubiria wenzetu wafanye kazi sisi tunajadili tu. Hii nchi imetekwa na lazima ikombolewe, hakuna jambo lolote chini ya hapo. Wanafanya umafya wa kila namna wamekamata madaraka sasa wanaanza kuhubiri Amani na mshikamano, udini na ukabila, uvumilivu na mustakabali wa nchi huku wakijua fika wao ndio wanaohujumu mustakabali wa hili taifa. Serikali inajua fika nani aliyesambaza sms za kidini lakini imefumba macho maana wanajua ilikua kwa manufaa yao.

Nchi yetu ipo kwenye majonzi makubwa, watu wengi wana huzuni na hawaridhiki na mambo yanavyokwenda. Takriban watu million 5 ndio waliomchagua raisi aliyetangazwa (Takwimu za NEC), millioni 14 waliobakia walipinga aidha kwa kutokwenda kupiga kura ama kuchagua wengine. CCM watu wa ajabu sana, hii asilimia 61 wanayoitangaza ingekuwa na maana kama ingekuwa inatokana na kura za watu million 19, less than that ni ujinga kujidai. Na hii ndiyo nayowaambia ni Mediocres, huwezi kusema ushindi wa kishindo huku robo tatu ya watu hawako upande wako. Kibaya zaidi hawaonyeshi kushtushwa na hali hii na kuchukua tahadhari mapema, watu wanasema waziwazi hawapigi kura maana wanaowachagua wawaongoze sio wanaoshinda. Hii ni hatari kwa wote wenye mapenzi mema na Tanzania, hima tuamke, kwa amani tupiganie mabadiliko yatakayofaidisha taifa letu.

Nawasilisha.
 
Averos

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
899
570
Have you mada critical analysis or you just move to the conclution?
 
nchasi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
562
180
Katiba ndio kilio cha wengi na ni wa Tz wote wenye dira tunataka katiba ibadilike. Ili tumpate mkombozi wa kweli sio ving'ang'anizi wa madaraka.
 
Pax

JF-Expert Member
May 3, 2009
268
87
you sound like a leader.itisha mkutano wa maandalizi i will b there!

Naangalia namna ya sisi kuweza kukutana. Naomba tuanzie humu humu kuwashawishi watu wana jf wote tukae pamoja tuzungumze, katiba inaruhusu watu kukutana so haina shida. Hapo ndio tutaweka mikakati yetu kwa uzuri zaidi
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,332
Kwenye maisha yangu mafupi hapa Jamvini nimegundua kuwa kuna watu wa aina tofauti, (waandishi wa habari, wanasheria, wabunge, mafisadi n.k.) ambao wote wanaweza wakawa na mchango mkubwa katika jamii yetu, Bila kujali tofauti ya Vyama Vyetu Vya Siasa. Sababu maisha magumu hayajali kama wewe ni Chadema, CUF au CCM.

Binafsi Jambo ambalo ninalichukia ni ufujaji wa mali ya taifa na matumizi yasiyo na Tija. Ndugu zangu naomba tujiulize kuwa Mpaka sasa tumeifanyia nini Nchi yetu...... Au tunaweza kufanya nini ili tulete mabadiliko. Najua penye wengi hakiharibiki kitu kwahiyo naomba ushauri na mawazo yenu tunaweza kufanya nini ili kuokoa nchi yetu. Binafsi nilishajaribu mambo matatu ambayo nilidhani yanaweza kuleta mabadiliko positive....
  • Kutumia wasanii kwa njia ya nyimbo ili kuweza kufikisha elimu ya uraia kwa jamii (pse sugu tusaidie kwa hilo)
  • Nilijaribu kuitisha petition ili watu wasign kuwashinikiza wabunge, mawaziri kupunguziwa mishahara hence kuondokana na haya matumizi ya kipuuzi (wabunge wa jamvini tusaidieni kwa hilo)
Naomba tushauliane Jinsi ya kufanya wanajamvi mwenye wazo anakaribishwa.

"Its better to lose some of the battles in the struggles for your dreams than to be defeated without ever knowing what you're fighting for.”
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
13,236
14,331

Hoja yako ya kuwataka wabunge kupunguza mishahara yao ilikuwa ni nzuri sana, ila wasi wasi wangu ni kutokana na watu wetu kujazwa kasumba ya kuamini kuwa Tanzania ni nchi ya amani hivyo hatutaki kukwaruzana na kuvunja amani hata katika jambo la wazi la kuibiwa kura. Sioni njia yoyote ya maana ya amani itakayolazimisha wabunge wapunguze mishahara yao bila kukwaruzana na kuvunjiana amani kidogo. Wenye mabavu wenzetu huko Kenya tunajua jinsi katiba yao ilivyogeuka kuwa ya kisasa, na hakuna wasiwasi kuwa watakuwa superpower wetu muda mfupi sana ujao. Sisi tutabaki kuibeba CCM na kujivunia amani huku watu wetu wakizidi kuwa maskini kwa faida ya kikundi kidogo cha viongozi. Amani bila haki siyo amani hata siku moja.
 
Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
Binafsi Jambo ambalo ninalichukia ni ufujaji wa mali ya taifa na matumizi yasiyo na Tija. Ndugu zangu naomba tujiulize kuwa Mpaka sasa tumeifanyia nini Nchi yetu...... Au tunaweza kufanya nini ili tulete mabadiliko.

Japo hukuweka alama za viulizo, nadhani hilo ni swali.

Nadhani katika nchi ya utawala wa rushwa kama Tanzania, ni ngumu sana raia kufanya jambo fulani kwa ajili ya nchi yao.

Mahali ambapo elimu inatolewa kwa matabaka. Mahali ambapo madaraka makubwa kwenye mashirika ya umma yanashikwa na watoto wa matajiri tu. Mahali ambapo vijana wengi masikini hawana ajira. Ni vigumu sana kufanya jambo fulani kwa ajili ya nchi yako.
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,332
Lakini lazima kuna Jambo ambalo tunaweza kufanya kama GROUP (Wananchi Majority) ili kubadilisha hali ya sasa "Alijisemea Shida, 'Yanamwisho hayo'
Japo hukuweka alama za viulizo, nadhani hilo ni swali.

Nadhani katika nchi ya utawala wa rushwa kama Tanzania, ni ngumu sana raia kufanya jambo fulani kwa ajili ya nchi yao.

Mahali ambapo elimu inatolewa kwa matabaka. Mahali ambapo madaraka makubwa kwenye mashirika ya umma yanashikwa na watoto wa matajiri tu. Mahali ambapo vijana wengi masikini hawana ajira. Ni vigumu sana kufanya jambo fulani kwa ajili ya nchi yako.
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,213
22,992
Hoja yako ya kuwataka wabunge kupunguza mishahara yao ilikuwa ni nzuri sana, ila wasi wasi wangu ni kutokana na watu wetu kujazwa kasumba ya kuamini kuwa Tanzania ni nchi ya amani hivyo hatutaki kukwaruzana na kuvunja amani hata katika jambo la wazi la kuibiwa kura. Sioni njia yoyote ya maana ya amani itakayolazimisha wabunge wapunguze mishahara yao bila kukwaruzana na kuvunjiana amani kidogo. Wenye mabavu wenzetu huko Kenya tunajua jinsi katiba yao ilivyogeuka kuwa ya kisasa, na hakuna wasiwasi kuwa watakuwa superpower wetu muda mfupi sana ujao. Sisi tutabaki kuibeba CCM na kujivunia amani huku watu wetu wakizidi kuwa maskini kwa faida ya kikundi kidogo cha viongozi. Amani bila haki siyo amani hata siku moja.
......amani ni neno lenye maana pana sana ingawa watawala wanataka kutuaminisha maana moja tu ya kutokuwepo kwa mapigano/ghasia.
Wanasahau kuwa tulicho nacho TZ kwa sasa ni UTULIVU tu (kwani AMANI yetu ilizikwa na Mwalimu JKN - RIP).
Utulivu nao nadhani utatoweka siku si nyingi kwani mtu wa kuu-revive (Mwalimu) hayupo!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom