Elections 2010 JF ni kwa Watanzania wote

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
814
380
JF na wote,

Nimekuwa tafuatilia kwa makini sana mambo yanayojitokeza ktk JF. Ukweli kabisa ni mambo ambayo Watanzania wote, bila kujali chama, dini, kabila au rangi, waweze kufahamu.

Tatizo kubwa ninaloliona ni suala zima la mawasiliano kwa mamilioni ya watanzania walioko vijijini. Je Kama wana JF, hatuwezi kutengeneza mpango mkakati ambao utahakikisha kuwa by 2015 at least 85% ya watanzania wote wawe wanaelewa haya yanayo semwa humu?

Nina ukahika, ikiwa kama hili litafanikiwa, then uchaguzi wa 2015 utakuwa uchaguzi wa aina yake na tutapata Bunge kama tuonavyo yaona mabunge ya wenzetu huko Abroad.

Natoa hoja.
 
Je Kama wana JF, hatuwezi kutengeneza mpango mkakati ambao utahakikisha kuwa by 2015 at least 85% ya watanzania wote wawe wanaelewa haya yanayo semwa humu?

LABDA KWA KUANZA NA WEWE, ulikuwa unasuggest kifanyike nini!,

Maana isije ikawa ndo zilezile lugha za kibongo za "MPANGO ENDELEVU, MKAKATI, MCHAKATO, MPANGO-MKAKATI(kama wako) na vitu kibao vya aina hiyo, ambavyo mwisho wa siku havina productivity yoyote!

Lakini, kimsingi kuna taste fulani katika concept yako!
 
Nashukuru kwa kuona kuwa kuna taste ktk concept yangu.

Labda kwa kuanza ni kama nilivyoanza kuwashirikisha hiyo concept, na nimeileta hapo baada ya kuona kuwa JF kuna watu wana mawazo mazuri, ambayo kama yanawezakuwekwa vizuri ktk muelekeo mzuri, basi yanaweza kuwa na maana kwa Taifa lote na si wana JF pekee, na approach yangu ikawa ni kuanza na watu wa vijijini.

Hapo ndio nashauri kuanzia.
 
LABDA KWA KUANZA NA WEWE, ulikuwa unasuggest kifanyike nini!,

Maana isije ikawa ndo zilezile lugha za kibongo za "MPANGO ENDELEVU, MKAKATI, MCHAKATO, MPANGO-MKAKATI(kama wako) na vitu kibao vya aina hiyo, ambavyo mwisho wa siku havina productivity yoyote!

Lakini, kimsingi kuna taste fulani katika concept yako!

mimi napendekeza tutafute watu watakaojitokeza kwa mfano kutoka kila wilaya (kama mawakala) ile waweze kutawanya ujumbe kwa watu wenye uelewa na ushawishi katika jamii katika eneo husika ili hao nao wafikishe ujumbe kwa watu. Vile vile kuwepo kubadilishana mawazo kati ya hao mawakala ni kupeana mikakati ya kufikisha ujumbe kwa jamii.
 
Tatizo kubwa nalo liona ni suala zima la mawasiliano kwa mamilioni ya watanzania walioko vijijini. J
Kila kitu kina mipango yake na malengo yake mambo huanza taratibu hata redio tanzania toka ianzishwe miaka ya 60 hadi leo si sehemu zote inasikika, JF has done something imetuunganisha mimi na wewe, play your part mfano unaweza kuanzisha NGO au redio jamii ukaikaribisha JF, maana hata JF itanuke namna gani haiwezi kutegemea internet kuwafikia wanavijiji wote lazima iji modify ama iwe Radio/TV au NGO au iwe chama cha siasa ingawa sijui kama hayo ndiyo malengo ya JF.
 
Back
Top Bottom