Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,958
- 718
Sina budi kutoa hongera kwa wana JF wote ambao wamekuwa wakichangia hoja hapa. Siku za karibuni nilisoma thread moja hapa kuhusu Mh. SU-PIKA ooh samahani, I meant SPIKA Sitta jinsi na yeye anavyoendesha UFISADI wake kwa kutumia nafasi yake. Katika hiyo thread mtoa hoja alidokeza kuwa kuna kamati mojawapo ya Bunge iligundua huo uchafu lakini wakanyamazishwa kwa kutishiwa kukatiwa unono wa posho pamoja na trip za nje.
Jambo Forums wakaikalia hiyo ishu kidedea, watu wakatoa data n.k
Sasa nimesoma katika gazeti moja Bongo kuwa ofisi ya Katibu wa Bunge wameanzisha uchunguzi kuhusu hizo tuhuma. Ingawa sina uhakika kama hiyo ofisi itakuwa huru kumchunguza SPIKA lakini hii inaonyesha kuwa JF ni BALAA kwa Serikali yetu maana inafichua uchafu wanaofanya hao WAHESHIMIWA.
Kama kweli hizo tuhuma zitakuwa za kweli na wakam-muadhibu Spika kwa mujibu wa Katiba, nilikuwa nina dokezo dogo ambalo ni la kupiga kampeni ya kumuondoa John Cheyo kwenye huo Uenyekiti wa hiyo kamati ya Bunge kwa kufumbia macho huo uchafu wa Spika. Naamimi kutakuwa na wabunge wengine kutoka Upinzani wanaweza kufanya hiyo shughuli. Sitapenda kumuhukumu kabla hizo tuhuma hazijathibitishwa. Ila kama zitakuwa za kweli itabidi Cheyo aachie ngazi kwenye hiyo nafasi.
Again napenda kuipongeza JF na wanachama wake wote kwa kazi nzuri mnayofanya kwa faida ya Taifa letu tukufu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI JAMBO FORUMS.