JF ..Msaada wenu mkubwa kimawazo unahitajika....

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,374
Good day to you all.. i salute

nimewaza na kuwazua hili naona ili nifanikiwe peke yangu siwezi
Nimechoka sana habari za kuajiriwa kuamka asubuhi na mapema kutoka nimechelewa nimefanya hivi kwa muda sasa ktk sekta fulani
Nataka kuacha kazi ndani ya miezi 6 au Mwaka ili niweze kujikita katika swala zima la biashara

Nisaidieni ni biashara gani nifanye ili niweze kufanikiwa pia faida na hasara zake nipeni mbinu wapendwa

i am totally feed up

FL1
 
Samahani FL1,

kwa sasa unaprofessional gani?ukishanijibu nitakwambia nini cha kufanya.

Pia kama unafikiria kufanya biashara mtaji wako uliopo tayari mpaka hapo ni kiasi gani kwa makadirio tu.

Najua wengine watakuja na mengi yangu ni hayo tu ndugu yangu.
 
Utaweza Biashara wewe?
Fungua kituo cha ushauri nasaha wa Mapenzi mm nitakusaidia capital.
 
Purchassing Officer sehemu
Kuhusu mtaji ninao kiasi nitakopa hata Bank kuongezea mpendwa ...na ndani ya matazamio yangu nitakuwa na mtaji wa kueleweka i hope so
 
Good day to you all.. i salute

nimewaza na kuwazua hili naona ili nifanikiwe peke yangu siwezi
Nimechoka sana habari za kuajiriwa kuamka asubuhi na mapema kutoka nimechelewa nimefanya hivi kwa muda sasa ktk sekta fulani
Nataka kuacha kazi ndani ya miezi 6 au Mwaka ili niweze kujikita katika swala zima la biashara

Nisaidieni ni biashara gani nifanye ili niweze kufanikiwa pia faida na hasara zake nipeni mbinu wapendwa

i am totally feed up

FL1

Hiyo red nimeipenda sana. Mi nakushauri uendelee na ufisadi wako kwenye purchasing. Biashara lazima itakushinda. By the way ile ya mama ntilie imekufa? Kama bado kaza buti mpaka ufungue hoteli.
 
Fanya biashara ya kilimo tafuta eneo la kufaa fanya biashara ya kilimo cha mboga mboga
 
Kama unahitaji nakushauri fungua duka la spare za pikipiki za Kichina unaona mahitaji ya vipuri vya tuktuk yanaongezeka kila kukicha hii biashara ukifungua utanipa miezi 6 wewe utakuwa mbaaaaaaaali kama hujanunu kiwanja k/koo basi umejenga kwenu Gorofa.
 
Kwa kuwa una ujuzi wa mambo ya purchasing, labda unaweza kuanzisha ofisi yako ya kununua, kuuza, kushauri na kufundisha makampuni au watu jinsi ya ku order, kununua na ku negotiate bei kwa kutumia njia/systems unazozijua.
 
Hiyo red nimeipenda sana. Mi nakushauri uendelee na ufisadi wako kwenye purchasing. Biashara lazima itakushinda. By the way ile ya mama ntilie imekufa? Kama bado kaza buti mpaka ufungue hoteli.

Chrispin
tuache basi utani ..inawezekana una mawazo mazuri yi unaweza kunishauri
pls pls
 
Kama unahitaji nakushauri fungua duka la spare za pikipiki za Kichina unaona mahitaji ya vipuri vya tuktuk yanaongezeka kila kukicha hii biashara ukifungua utanipa miezi 6 wewe utakuwa mbaaaaaaaali kama hujanunu kiwanja k/koo basi umejenga kwenu Gorofa.

mmh huu ushauri thanks naufanyia uchunguzi kwanza
 
Kwanza hongera fl1...
Sio wanawake wengi wana mawazo kama yako...
Pili usiache kazi ili uende kuanza biashara....
Fanya biashara wakati wa free mpaka ikichanganya ndo uache kazi...
Halafu chagua biashara zenye risk kidogo...
Nakushauri angalia uwezekani wa kujenga guest.....au
fuga kuku..........
 
mmh huu ushauri thanks naufanyia uchunguzi kwanza

Shauri yako watu tunapiga bao k/koo hapo wewe utakapo kuja kujua sisi tunahamia kwenye biashara zingine kwenye matractor si umesikia nayo yanakuja kwenye Kilimo Kwanza.
 
Nakushauri angalia uwezekani wa kujenga guest.....au.......

Yeah kweli kabisa hii biashara nayo inalipa sana endapo utaruhu maswala ya lipia kwa sekunde aaah utakula vichwa balaa kuanzia j3-j2 yaani wewe full kukusanya inabidi uweke msimamizi mnoko.
 
Ndugu yangu pole kwa l=kuchoka kazi,kumbuka pia biashara nazo lazima utaaangaika sana kupita kiasi hata hutaweza kulala.biashara ni nzuri ila unatakiwa kujua ni biashara gani unaihitaji kufanya,kiasi gani cha pesa inacho,wateja wako wapi an washindani ni kina nani.

Gift of life is life itself.
 
Mpendwa kwanza jitizame wewe mwenyewe ni kitu gani unakipenda na una uwezo nacho. Ukifanya biashara ili mradi biashara nayo utaichoka kama ulivyochoka kazi.

Plus usiache kazi mpaka uone biashara inachanganya labda kama una kitu ambacho kina kuingizia pesa hata kama ufanyi kazi
 
Back
Top Bottom