JF Members,Wasomi,Watanzania:Vishoka tunaopepetwa Kama Mpunga na Serikali ya Kikwete?

INFORMANT

Member
Dec 9, 2010
26
0
Kitila Mkumbo, amesema jambo, nimemsikia, amenigusa. Amesema ukweli, ukweli ambao hatujauona, na kamwe hatutauona.

Kuna maswala muhimu ya msingi, mjadala wake umeishia hewani, na yalikuwa agenda ya watu, agenda iliyotishia uhai wa serikali iliyoko madarakani, agenda yenye kubeba hisia za wengi, agenda kuu yenye kugusa maisha ya walio wengi.

Gharama ya umeme, tumepiga kelele-hatujafikia muafaka, likaja la Dowans, halijaisha, tumepigwa ganzi la mabomu, na jinsi watanzania walivyokuwa vishoka, propaganda yenye kuipa salama serikali dhidi ya haya manyanyaso inafanya kazi kwa nguvu ya ajabu.

JF, tumetekwa kirahisi, tumeshindwa kuwa nuru na taa kwa watanzania na kuongoza na kuendeleza mijadala ya msingi.Tunapepetwa kama mpunga, kwa raha zao, wanapata pumziko!

Kikwete ana akili sana, amejenga technique zake kwenye hisia za watanzania. Yumkini matukio haya yawezekana siyo ya bahati mbaya, ninahisi ni matukio ya kupangwa ili kuweza kuondoa attention toka maswala ya muhimu na kujadili matukio, na hivyo ndiyo saa, siku, wiki miaka inapoenda na muda wa serikali hii utaisha kwa raha mustarehe kabisa.

Hakika, hakuna atakayewajibika, wanawafahamu vizuri watanzania, hamwezi kufanya chochote.

Tutafakari;

Mijadala ya hoja zifuatazo za msingi mustakabali wake ukoje sasahivi?

1.Mauaji ya Arusha
2.Kupanda kwa bei ya umeme
3.Kupanda kwa bei za bidhaa
4.Mfumuko wa bei
5.Wizi wa fedha mpya uwanja wa ndege
6.Dowans
7.
8.
.
.
.
.
.
.
Tuamke usingizini...

 
Watanzania wote sisi ni jamii ya watu majinga wapumbavu na mapunguani,(YES I SAID IT)na me nikiwa mmoja wapo. Yan hapa tukubali hakuna cha magreat thinker wala wapagazi wala wakulima kijijini wote akili zetu fupi tu. Natoa mifano hai kidogo

CCM wametutawala miaka na miaka hakuna maendeleo hakuna atua tunayochukua zaidi ya kuwarudisha madarakani au kungoja eti uchaguzi ujao tutawatoa.

Sisi ni watu tusiojua kujifunza utakuta ttz limetokea tutalalama pale zen tunakaa kimya na kujifunga mkanda kuyakabili hayo mttz,mfn nauli ya mabasi ikipanda utaona watu wanapiga kelele na kugoma kwa kutembea na miguu halaf mda kidogo wanakaa kimya,mfn ni kupanda kwa umeme mpk tuliandamana kupitia cuf,kiko wapi saiv?si tunalipa hizo hela kwa kujifunga mkanda...

Watanzania ni watu wa porojo na maneno mengi kuliko vitendo utasikia ohh lzm tuandamane watoke lkn hakuna linalofanyika zaidi ya maneno,ndo mana hta me siwashangai wana siasa wa kitz mana wao ni wenzetu ndo mana wanatoa ahadi nyingi hakuna utekelezaji.

Mimi jaman yangu ndo hayo sisi ni wapumbavu tu,na wa humu ndani soo called great thinker,they r just that,great thinkers nt action oriented nor risk taker,so wacha watuburuze tu mana tumewapa wenyewe uwezo wa kutubutuza
 
7. Gongo la Mboto ni janga
8. Katiba Mpya ni msingi kuyaondoa yote hapo Juu.
9. SPIKA WA HOVYO

NINACHOAMINI MIMI NI KWAMBA KAZI KUBWA ALIYONAYO DR SLAA NA AMBAYO NINAAMINI ANAIFANYA KWA MOYO WAKE MMOJA NA KWA UMAKINI NI KUWAFANYA WASOMI WAJIPAMBANUE. KAMA SIO DR SLAA NA CHADEMA TUSINGEMFAHAM DR KITILA MKUMBO, NINAAMNI MUNGU AKIENDELEA KUMTUNZA KIONGOZI WETU DR SLAA NCHI HII SI MDA MREFU TUTAPATA MABADILIKO YA KWELI MANAKE UKIPATA AKINA KITILA 100,000. KAZI IMEISHA. MIMI NAAMINI DR SLAA ATATELEKELEZA HILO MANAKE HIYO NDIO ITAKUWA MAJIBU YA KUCHACHULIWA KWENDA IKULU. KITILA NI MOTO, DEUS NI MOTO, LUGEMELEZI NI MOTO, WAPO WENGI NA WANAZIDI KUJIPAMBANUA. UKIWASIKIA WABUNGE WENGI WA CHADEMA WANAFUATA NJIA YA SLAA -SASA SIJUI KAMA CCM WATAPONA.

MIMI NAAMINI HAYA YALIYOORODHESHWA HAPA JUU WATANZANIA TUTAYASHUGULIKIA KWA UMOJA WETU BILA KUSAHAU -TUKUMBUKE MBUNGE MMOJA WA CHADEMA -MFANO MNYIKA, MDEE, SILINDE, SUGU, REGIA, MDEE, ZITO, TUNDU, BABA KIONGOZI WA ANGA MBOWE, WENJE, NYERERE, NA WENGINE SAWA NA WABUNGE 15 WA CCM. KILA MMOJA ATAKAMATA MOJA HAPO NA KUFA NALO, TUMEONA JINSI LEMA ALIVYOMGALAGAZA PINDA BUNGENI NA BAADO. KITILA ASIHOFU AZIDI KUONGEA WANACHI WANAAMKA TENA KWA KASI YA AJABU.
 
Ilikuwa ni vyema kama mimi na wewe na yule tunaojua haya nini tufanye tuwafikie walengwa. Wenzetu Egypt na kwingineko walifanya maandamano kilio chao kikasikika sasa sisi tufanye nini na tuanzie wapi labda hili litakuwa la msingi zaidi. Sipingani na mawazo yako kwamba JF tumekuwa watu wa kuandika tuuuuuuuuuuuu lakini hakuna matendo. Tukumbuke kwamba sio wengi wana access ya mtandao kwa hivi tushauriane nini tufanye kulikomboa taifa letu. Tunashukuru kwa mada maana ni ukweli mtupu tutaishia kuandika mpaka kristo atakaporudi mara ya pili ooops sorry mpaka labda mzimu wa baba wa Taifa ututokezee labda ndio tutaamka usingizini.
 
(1) JF mnaotaka watende wengi wao hawako Tanzania. Watatendaje?

(2) Matendo yanatakiwa yawe na viongozi. Kwetu sisi CHADEMA ndio kiongozi. Siku wakisema Watanzania tuandamane kudai hiki au kile basi utashangaa watakavyotoka wengi.

(3) Kuuana sio vizuri. Kama kukiweko maandamano basi yawe ya amani. Iwe ni kudai kuzuia malipo ya Dowans au kudai viongozi wabovu wajiuzulu, lazima tufanye hivyo kwa amani. Ni haki ya wananchi kunadamana kwa amani.
 
Kuwa na majibu ya hovyo hovyo si kitu cha bahati mbaya.Ukiangalia vizuri, from Dowans mpaka mabomu ya Gongolamboto, utasikia majibu au kauli za hovyo hovyo tu kutoka kwa Rais au viongozi wengine.Si bahati mbaya, bila shaka ni mpango kabambe (propaganda to divert attention, and it is very unfortunate we got drugged into it.

We have demanded Dr.Mwinyi to resign, haikuhitaji busara ya ziada kwa yeye kuwajibuka if this was unexpected, but you heard it all loud and clear that he will not....chukua hatua!
 
hivi kwan tumeshindwa kabisa kumshinikiza dr. Mwinyi kujiuzulu? coz lazima awajibike this is 2nd time yeye akiwa same office, hata kama ni kubebana JK sio kihivyo wote waziri, mkuu wa majeshi, mnadhimu mkuu wanatakiwa kujiuzulu hiyo ni dalili wameshindwa kuimplement changes ktk jeshi watoke wapishe new ideas and challenges thats all
 
Wana JF wenzangu tunatumia mbinu dhaifu na uoga uliopitiliza kujaribu kupata mambo makubwa kama yalivyo orodheshwa kwenye hii thread.it will never work this way.haki inashinikizwa na kupiganiwa live na sio kupitia kwenye keyboard.
 
(1) JF mnaotaka watende wengi wao hawako Tanzania. Watatendaje?

Wadhalimu wanaonyonya hii nchi wa advantage ya kupanga madili ya Dowans kujikwapulia mahela na kutumia serikali na facilities zake kuendeleza maovu yao. Vyama vya siasa na NGOs zinazowabana mafisadi na serikali yao wanahitaji sana resources. Nyie mlioko nje mnatakiwa mji group halafu muwasiliane na wapambanaji Tanzania muone mtakavyoweza kuwasaidia in terms of resources (pesa, vitendea kazi, mbinu, contacts za marafiki, kutangaza maovu ya tz huko nje etc etc).

(3) Kuuana sio vizuri. Kama kukiweko maandamano basi yawe ya amani. Iwe ni kudai kuzuia malipo ya Dowans au kudai viongozi wabovu wajiuzulu, lazima tufanye hivyo kwa amani. Ni haki ya wananchi kunadamana kwa amani.

Ndugu yangu Moshi maandamano yote hapa Tanzania huwa ni ya amani mpaka pale polisi wanapoamua kuivunja hiyo amani. Hili somo wanatakiwa wapewa ndugu zetu wa jeshi la polisi. Waelewe kwanza wao hawako juu ya sheria. Na pili ccm haiko juu ya sheria na waache kuchukua maagizo kutoka kwao. Tatu wafanye kazi kwa uweledi na sio kukipendelea chama kilichopo madarakani. Na nne wanayoipinga serikali wana haki ya kusema watakalo hata kama litamkera nani ili mradi hawamvunji haki yake wanaomsema.
 
Mimi nafikiri ku organize kitu chochote kinahitaji viongozi ambao watasimamia na kuhahikisha mpango unafanikiwa, Mwl nyerere na viongozi wenzake walisimama kidete mpaka uhuru ukapatikana, walipita huko na huko, walicheza bao na kunywa kahawa vijiweni ili mradi waweze kueleza mipango kwa wananchi wawe tayari, kwa kipindi hiki naona ni rahisi kwa sababu means za mawasiliano ni nyingi, ni viongozi tu.
 
Usomi ni kuwa na weledi wa kuchambua mambo na kufanya maamuzi kwa kuwa na taarifa sahihi (informed decision) sio kusukumwa na utashi wa kisiasa na kucheza zumari wanayopiga wengine. Mitandao kama JamiiForum inapoteza muelekeo kama malengo yake ni kuleta yaliyoleteleza ya Tunisia, Misri na yanayoendelea Nchi za Kiarabu-Electronic Media kujenga Uadui na Kutokuamini Serikali zilizo Madarakani. Hivyo Msomi anaependekeza CDF na MDNS wajiuzuru au kutaka umma ushinikize pasipo kubainisha katika tukio la GLM kulikuwa na Omissions, Neglegence na Misdids zipi Miongoni mwa Watendaji wao wa chini kama Kanuni za Political Resposibility zitakazo ni Msomi ambae Jamii imtegemee au ni Msomi Mpotoshaji. Wapo wengi wa aina hii Wanavaa Miwani za Giza. Tukio la GLB ni Disaster kama Disaster nyingine-Hazard-Armoury Explosions ; Probability of Occurence-Rare; Impact- Severe; Mitigation Measures-Inspection and disposal of obselete explosives plus other specialised military measures and separation of civilians dwellings; response measures-quick detonations of remaining explosives in the vicinity and evacuations. Haya yote yamefanyika kwa mujibu wa kanuni za Disaster Risk Management. Ukitaka kuwajibika kwa suala hili sio CDF na MDNS pekee yao hata Tibaijuka (Nyumba na Makazi-makazi kuwa karibu na kambi), Ngeleja (Nishati na Madini-umeme kuenezwa makazi ya uvamizi) etc . JamiiForum iwe kweli kwa Critical Thinkers. Jana kwenye Kipima Joto ITV niliona Tz kuna Wasomi wa kikwelii kama Dr. Peter Mateso ambao Wanaongozwa na Critical Analytical Thinking na sio ushabiki wa kisiasa wa wengine wengi-Baregu; Lwaitama;Shivji ect Waliotukuka Usomi wao umegubikwa na Polaroid Lenses za Itikadi zao.
 
hivi kwan tumeshindwa kabisa kumshinikiza dr. Mwinyi kujiuzulu? coz lazima awajibike this is 2nd time yeye akiwa same office, hata kama ni kubebana JK sio kihivyo wote waziri, mkuu wa majeshi, mnadhimu mkuu wanatakiwa kujiuzulu hiyo ni dalili wameshindwa kuimplement changes ktk jeshi watoke wapishe new ideas and challenges thats all

Kwa sababu sisi ni waoga!!! Watu tusiowajibika kwa mustakabali wa taifa letu!!! Watu tusiotayari kujitoa kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo!!! Wote tumekua kama zombies tu!!! Hivi ni nani aliyetuloga???? Na kwa mtaji huu tutaburuzwa mpaka mitume walioahidi kurudi warudi!!! Sisi ni kama watu wanaopenda kwenda peponi lakini hawataki kufa??? No pain... no gain!!!
 
7. Gongo la Mboto ni janga
8. Katiba Mpya ni msingi kuyaondoa yote hapo Juu.
9. SPIKA WA HOVYO

NINACHOAMINI MIMI NI KWAMBA KAZI KUBWA ALIYONAYO DR SLAA NA AMBAYO NINAAMINI ANAIFANYA KWA MOYO WAKE MMOJA NA KWA UMAKINI NI KUWAFANYA WASOMI WAJIPAMBANUE. KAMA SIO DR SLAA NA CHADEMA TUSINGEMFAHAM DR KITILA MKUMBO, NINAAMNI MUNGU AKIENDELEA KUMTUNZA KIONGOZI WETU DR SLAA NCHI HII SI MDA MREFU TUTAPATA MABADILIKO YA KWELI MANAKE UKIPATA AKINA KITILA 100,000. KAZI IMEISHA. MIMI NAAMINI DR SLAA ATATELEKELEZA HILO MANAKE HIYO NDIO ITAKUWA MAJIBU YA KUCHACHULIWA KWENDA IKULU. KITILA NI MOTO, DEUS NI MOTO, LUGEMELEZI NI MOTO, WAPO WENGI NA WANAZIDI KUJIPAMBANUA. UKIWASIKIA WABUNGE WENGI WA CHADEMA WANAFUATA NJIA YA SLAA -SASA SIJUI KAMA CCM WATAPONA.

MIMI NAAMINI HAYA YALIYOORODHESHWA HAPA JUU WATANZANIA TUTAYASHUGULIKIA KWA UMOJA WETU BILA KUSAHAU -TUKUMBUKE MBUNGE MMOJA WA CHADEMA -MFANO MNYIKA, MDEE, SILINDE, SUGU, REGIA, MDEE, ZITO, TUNDU, BABA KIONGOZI WA ANGA MBOWE, WENJE, NYERERE, NA WENGINE SAWA NA WABUNGE 15 WA CCM. KILA MMOJA ATAKAMATA MOJA HAPO NA KUFA NALO, TUMEONA JINSI LEMA ALIVYOMGALAGAZA PINDA BUNGENI NA BAADO. KITILA ASIHOFU AZIDI KUONGEA WANACHI WANAAMKA TENA KWA KASI YA AJABU.

Hii nchi haitakombolewa kwa kazi ya mtu mmoja au wakina Mkumbo peke yao. Hawa, serikali inaweza kuwafuatilia mmoja mmoja na kuwabana. WanaJF na watanzania wote lazima tuungane. Kila mmoja aone anahusika, tusidhani fulani atafanya. Dr Slaa katufumbua macho, tuamke tujadili mstakabali wa nchi yetu. Tuache kuchukuliwa na upepo wa hoja zisizo na uzito, zinazoletwa na wafuasi wa watawala.
Tutasubiri mpaka lini kuona umaskini huu unaendelea?
Tena unasababishwa na serikali!
Tutasubiri hata lini kuona rasilimali zetu zinakombwa?
Tena nasikia waarabu sasa wanakuja rasmi kununua ardhi yetu kwa bei ya madafu.
Tutasubiri hata lini tukiangalia haki zetu zinadhulumiwa?
Tena sasa hata kupigwa mabomu ni kama halali kwetu!
Tutasubiri lini tukiendelea kuwa wajinga?
Tena sasa elimu si haki ya kila mtu bali wachache!
Tutasubiri hadi lini?
 
Junazungumzia mustakabari wa Nchi au ya Chadema. Wengine wanaonyesha hata Uhitler wao kama David Cameroon wa UK na falsafa yake ya Multiculturism has Failed & Lets Guard European Values. Uchumi wa Dunia unapita wakati mgumu hata huko Ulaya kupanda kwa gharama za maisha haswa Uingereza -Umeme,Gas, Fuel, Matibabu,Ada za Chuo,Nyumba na Chakula imepanda na wananchi wanalalamika. Obama ametangaza kukata matumizi ya Serikali hivyo nako wataenda huko huko sembuse sisi tena ambao tulikuwa katika Socialist Camp iliyosambaratishwa. Tusivae miwani za giza katika kuangalia mustakabari wa Nchi. Tuone sasa kama Wabunge wa Chadema watarudisha Hundi za Tsh 90m za Mkopo wa Magari kwa dhana kuwa Wananchi Wengi ni Maskini hawawezi kuendeleza matumizi hayo. Pia kumbukeni riwaya ya 'The Animal Farm' hakuna uhakika kama Chadema watakwepa dhambi hiyo-Mapinduzi yote yamekumbwa nayo si ya Kijamaa, Kikomunist au Kijeshi siku zilivyoenda zikaishia kwenye The Animal Farm' kwa mshangao na dhahama ya Wananchi wengi. Jengeni na toeni hoja pasipo kutukana na kubeza Serikali iliyopo Madarakani na Viongozi Wake kwani navyo kuna wanaoithamini.
 
Kaka! maneno yako makali lakini yana ukweli saaana!!! Ujinga wa Mtanzania umeanzia kwa Wanachuo ambao wana jiita wasomi, tena mimi wananichefua sana, maandamano yao nikutaka kuongezewa pesa ya kujikimu, lini walisha wahi kutoa mapendekezo ya jambo gani lifanyike katika kusaidia hawa viongozi wetu ambao wamesha ota kutu?? ni ubinafsi, ubinafsi, ubinafsi, elimu ya juu ina uwanja na attention kubwa sana si kwa wananchi tu, bali hata kwa jamii pia, lkn hakuna hata siku moja wametoa mapendekezo kama wasomi ya kusaidia taifa letu, sana sana ni UPUMBAVU MTUPU, UTADHANI WAMELOGWA, Wana andaa maandamano ya kudai nongeza ya 5000/- mi nina hakika kama wanapata walau dk5 za kutafakari wanayo yafanya hata kama serikali inawasikiliza basi lazima hawata thubutu kujiita wasomi NEVER!!! hawa ndo watu walio kuwa na less thinking capacity ever on earth, UJINGA WA MTANZANIA UNA ANZIA KWA MWANA CHUO, UHSUSANI MLIMANI UDSM!!!
 
Back
Top Bottom