William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
bob, COMRADE44, Field Marshall ES, Hey, Kamuzu, Mwita Maranya nk . . . .
Mnasemaje Wakuu?
1. Mkuu Allien, nimejaribu sana kukusoma na pia mawazo ya wengine wengi hapa, binafsi ninasema hivi vyama vya siasa Tanzania ni vingi mno, vinahitaji kupunguzwa kwa sababu in the end vinaleta mzigo mkubwa sana wa ruzuku kwetu wananchi walipa kodi.
- Mawazo yako ni mazuri sana, ila ningekushauri uyaingize kwenye chama kimojawapo nchini, kwa mfano TAA waligundua kua hawana uwezo wa kukaa meza moja kuongea uhuru na Mkoloni, kwa hiyo wakam-recruit Makaputula-(Mwalimu) na akaweza kufanikisha waliyokuwa hawawezi on their own, ninaamini ukihamishia uchungu wako katika moja ya vyama vyetu vya siasa na kuki-reform utakuwa umelisaidia sana taifa letu, na utapokelewa vizuri sana huko hasa mawazo yako!
2. Maana think kwamba kwenye internent kuna forums ngapi? Sasa forums zote zikianzisha vyama vya siasa itakuwaje mkuu wangu? Litakuwa ni taifa gani hili? Wacha JF tuendele kuwa taasisi ya wananchi na viongozi kuja kutoa kiu hapa, na kuchota elimu bure in the process na sisi wengine wenye uchungu na taifa tunakula elimu nzito hapa ambayo pole pole tunaihaimisha kwenye vyama vyetu na eventually, with time tutaleta mabadiliko kwa taifa tena makubwa sana lakini chanzo kitakua ni hapa kwenye shule ya bure yaani JF.
3. Mkuu sijui wengine ila mimi siku zote hua ninachota sana hapa JF na kuhamishia kunakotakiwa, na hasa kwa viongozi wetu Richimonduli ilianzia hapa mkuu, nusu ya info za ile scandal zilitokea hapa JF na tukaweza kuliamsha taifa, ni vyema tukaendelea hivyo hivyo,
- Lakini pia ninaheshimu sana mawazo yako kwani ni ya kimaendeleo sana, kuliko majibu mengi ambayo nimeona ukipewa yaani yameacha ishu na kukimbilia shortcut za personal, it is about time wananchi hapa wakajua kwamba hakuna ndugu wa mtu hapa JF hili ni jungle na tumo wote kutoka njia mbali mbali za maisha na sio lazima kwamba tupo hapa kwa malengo yanayofanana, au ni lazima yafanane, au lazima tuaminiane na kupendana na si kweli kwamba kwa sababu una msimamo flani basi wewe ndiye mwanamapinduzi sana na wengine sio, lets get real wakuu mimi ninaheshimu sana kila mwananchi aliyeko hapa JF na hasa anayechagia hoja, Tanzania ni yetu wote na ni muhimu sana katika kila mwisho wa siku tukaendelea kuheshimiana kwa kuwa na mawazo tofauti maana ndio hasa sababu ya kuwepo hapa JF yaani mawazo mbadala.
Mkuu Allien, respect kwa hoja yako nzito sana, lakini JF tuendelee kuwa taasisi ya kuelimisha taifa bure kama tulivyo sasa!