JF Investigates: Zakaria ni nani huyu Tarime? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF Investigates: Zakaria ni nani huyu Tarime?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Oct 13, 2008.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Tumekuwa tukifuatilia kampeni na Uchaguzi wa Tarime ambapo Mtu mzima pwaa! LAkini matukio yaliyoendela wakati wa Kampeni yalimuhusisha sana mtu aitwaye Peter Zakaria kwa mambo yafuatayo:

  1. Kuwalisha Polisi waliopelekwa Tarime chini ya Kamanda wa Operation Venance Tossi. Hii ni fedheha kubwa kwa nchi na jeshi letu la Polisi kwani ilismekana hawakuwa hata na posho na hata chakula kilikuwa cha shida kwa Askari hawa na hivyo kupelekea Zacharia kuwalisha Askari wetu ili wapate nguvu ya kuwanyamazisha Wana TArime.

  2. Katika tukio la kujeruhiwa kwa Wafuasi 4 wa CHADEMA kwa kukatwa mapanga na Wana CCM, ni gari la ZAcharia ambalo nilo lililokamatwa kwa kuwa liliwabeba Wakereketwa hawa waliokuwa na silaha aina ya mapanga.

  Nataka kujua Wajameni, huyu mtu ni nani na ana nguvu na jeuri gani ya kufanya haya? Anajiamini kitu gani kuweza kuwatendea hivi wana TArime kwa kufadhili ugaidi na ujambazi huu? Polisi wameshthibitisha kuwa ni gari lake ndilo liliwabeba wale jamaa waliowakata mapanga Wanachadema waliokuwa wakisubiri helkopta ya Chama chao kutelemka na kwa nini hatujasikia amekamatwa na kufikishwa mahakamani? Au ndo Polisi wanaogopa wakimkamata basi hakuna chakula Tarime na watakufa njaa?

  Hivi ni kweli Jeshi la Polisi lilikuwa halina pesa za kuwahudumia askari wake hata kwa Chakula jamani? Habari nilizonazo hapa Arusha ni kuwa Askari wengi waligwaya na kutoa vizingizio kibao ili kuepuka kupelekwa TArime kwenye Operation hiyo Maalumu ya kuwasaidia CCM na Watu wao.
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  Oct 13, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Ni muda wa kumfuatilia na kumchukulia hatua kali sasa
   
 3. M

  Mtu Kwao JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2008
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 258
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwa uhakika huyu Peter Zakaria ni mfanya magendo mkubwa huko mwanza na tarime,na kuna wakati alimwagia mtu tindikali .jambazi mkubwa huyo mungu kamweleleze
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sasa Inazidi kuwa wazi kwamba

  Fisadist kwao CCM
  Wakolimbaji na Ipyanaling kwao CCM
  Jujuling ndani ya bunge kwao -//-
  Majambazi kwao CCM

  No wonder bado tuko masikini kiasi hiki chini ya utawala wa CCM takribani nusu karne kwa sasa!


  Ee Maulana tunusuru na zahma hii.
   
 5. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2008
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  kidogo ninayofahamu kuhusu peter zakaria
  1. wajihi: mfupi mweusi,well built,anaonekana kama mtu wa ibada usoni(lakini sura yake imeficha mengi)
  2.Mfanyabiashara mmiliki wa mabasi ya zakaria trans,kituo cha mafuta n.k
  3.awali alikataa kusaidia kampeni za CCM,hadi siku moja 'alipotekwa' kwa staili ya Kijasusi,na tangia aliporejesha kutka huko alikopelekwa ametekea kuwa mfadhili mkubwa waCCM akishirikia na na C.M.Gachuma(CMG) (aliwahi kuonekana kwenye picha ya gazeti moja akiwa viwanja vya bunge akitambulishwa na CMG kwa F.T SUMAYE)
  4.Ana rekodi ya ubabe inayohusisha tukio la kummwagiwa tindikali usoni dereva wa bus la Tanganyika bus, kutoa bastola kwenye ibada ya mazishi kumtishia padre liyetoa mahubiri yaliyomgusa,kucharaza bakora wapiga debe wa stend nk
  5.Tarime he is above the law,kwa kauli tu ana uwezo wa kumtoa mtu rumande.
  6.anatajwa kuwa na urafiki mkubwa sana na Rtd. IGP mahita
  7. Ziko habari zisizothibitishwa amewahi kuchapwa bakora LUGALO na MP kufuatia yeye peter kuwachapa bakora abiria wa basi lake aliowalazimisha kushuka ili katishe ruti,miongoni mwao alikuwapo mwanajeshi.

  I'll try to gather more info
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Zakaria alishawahi kuua huko Tarime na mabasi yake yanasifiwa kwa kutembea kasi na polisi hawamfanyi lolote... Inasemekana pia alishawahi kuwa jambazi..
   
 7. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu poa kabisa hii.
  8.Pia alikuwa na ki depot cha bia hapo nyuma ya stend ya mabasi Tarime kuna wakati kilivamiwa na majambazi mchana mchana.
  9.Mshauri wake na mshirika wa karibu ni huyo NEC-Mara
   
 8. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #8
  Oct 13, 2008
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sio alishawahi kuwa jambazi, bado ni jambazi hadi kesho, ni bingwa wa kuuza mafuta ya magendo toka kenya, ni bingwa wa kuteka magari ya mafuta toka kenya kwenda migodini na huuza hayo mafuta vituoni kwake, pale mpakani sirari ana kituo cha mafuta kwa ajili ya kuuza mafuta ya wizi tu toka Kenya, na hayalipiwi ushuru.

  Ni bingwa wa kuteka meli za mafuta toka pipe-line kisumu na na kuyashusha mafuta visiwani huko Mwanza, mara nyingi kwenye wizi huu hutumia meli ya mv. Munanka ambayo ni ya rafiki yake jambazi wa mwingine wa Mwanza, huyu wa Mwanza anaitwa Chacha Gitano.

  Hapa Tarime ana jeshi lake binafsi pia ana selo zake, kwa mfano wapiga debe wakipuuza mabasi yake huweza kupelekwa kwenye hayo magereza yake na kupewa adhabu ngumu ya viboko pamoja na kusafisha gereji yake, inasemekana pia kwenye mradi wa mabasi IGP mstaafu , jambazi mahita ana shea kubwa, mabasi mengi ni ya wizi toka Kenya.

  Kwa sababu raia wa Tarime wanamuona kama pirate, zamani halmashauri ikiongozwa na ccm walimpa vituo vya mafuta vya halmashauri bure bila malipo hadi leo, kikiwemo cha mugumu wilayani Serengeti.

  Aliwahi kumwagia dereva wa basi la Bunda Bus tindikali pia, live stand, na sheria haikumgusa, hadi leo huyo jamaa ni kilema. Mara nyingi amekuwa na tabia ya kuwakoromea madereva wa kampuni nyingine kama Tanganyika Bus kwa kuwatishia bastola, tena mbele ya abiria.

  Peter Zacharia ni Mungu mtu hapa Tarime, Gachuma ndo God father wake.
   
 9. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Hebu fikiria serikali inapowapeleka askari polisi kwenda kulinda usalama mahala fulani bila posho ya kutosha kujikimu. Halafu wanafadhiliwa na mtuhumiwa wa ubabe na uhalifu unategemea nini hapo?

  Inasemekana hao matajiri wa kanda ya ziwa huwa wanawaweka ma RCO kwenye payroll zao pamoja na kuwajazia pesa kwenye simu zao za mkononi kila mwezi!
   
 10. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama yote yanayoongelewa humu juu ya huyu mtu ni kweli .....inaelekea basi hata kodi halipi huyu au analipa anapojisikia.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Elimu yake?
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani mtu kama huyo akakumbatiwa na chama tawala, nadhani mnamsingizia na kumuonea wivu. Vinginevyo mtakifanya CCM kionekane kama Chama cha Majambazi hivi...
   
 13. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mbona wanakumbatiwa majambazi makubwa kuliko huyo ...yaani ile "mibaka uchumi"
   
 14. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Hivi Mwanakijiji unadhani CCM bado ni chama cha wanyonge? Ni chama cha wababe na wenye pesa! Haijalishi kama pesa hizo umeiba serikalini au kwa wananchi! Ili mradi uwe nazo nyingi na uwe tayari kuwasaidia kwenye kampeni zao! Ndio maana walifikia mahali wakahalalisha rushwa kwenye uchaguzi kwa kuuita TAKRIMA!

  Hao matajiri wa kanda ya Ziwa "miungu watu". Yaani anaweza kumpigia simu mkuu wa polisi muda wowote anaotaka yeye na akafanya kile anachokitaka yeye! RUSHWA!!
   
 15. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Elimu ya nini tena wakati umeshaambiwa jamaa ni "mjasiriamari".
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kuna "mjasiriamali" mkuu walio na vyeti vyao, CPA, MBA or something......ama unataka kusema Zacharia anatumia uzoefu?
   
 17. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Ndio maana hilo neno "mjasiriamali" nimelifungia kwenye funga na fungua semi. Nikimaanisha kwamba kazi yake haihitaji kwenda shule....Si umeona sifa zake zilizotajwa hapo juu, je kuwa mtu wa namna hiyo unahitaji kwenda shule?
   
 18. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa kadri nijuavyo mimi (i might be wrong), Zakaria huyu elimu yake ni darasa la pili au zaidi ni la nne. Alishindwa shule na akafanya magendo mpakani kule ndio akajikusanyia utajiri wote huo alionao.
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Thanks !!! CCM bwana ndo walitaka awe diwani huyuuuuu ama kweli hawanazo!
   
 20. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Mkubwa,
  Neno "mjasiriamali" nimelifungia kwenye funga na fungua semi. Nikimaanisha kwamba kazi yake haihitaji kwenda shule....Si umeona sifa zake zilizotajwa hapo juu, je kuwa mtu wa namna hiyo unahitaji kwenda shule?
   
Loading...