JF inavyo set the AGENDA na JK anavyofuata

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,545
825
Ama kweli sasa JF tunaset the agenda. Baada ya kumcriticise JK na slow response yake kuhusu JANGA LA KITAIFA amefanya kama nilivyomwambia:

1) Avae parka jaket -TIK

2) Aongozane na mkewe- 0

3) Jamaa wa Emergency response wapeleke misaada -o

So far kama kawaida yake COMMANDER IN CHIEF wetu inaonekana harespond kitu mpaka tumsukume humu. Janga tangu limetokea imemchukua RAIS more than 72 hours kwenda Mererani

So far tumemwona waziri wake akiwa site anwaapa instructions madereva badala kuwaachia hao wenye kazi zao waendelee

sasa basi baada ya Janga hili tunaomba :

1) WAZIRI HUSIKA asubmit resignation yake

2) TUELEZWE KWA NINI IMEMCHUKUA JK muda wote huko kufika Mererani

3) TUAMBIWE kama vikao vya CCM ni bora kuliko janga la kitaifa

Once again wana JF hongereni na sie wengine tunarudi kule kwenye issue ya Comoro ambayo as days go by JK na timu yake wanaonekana ni ma-incompetents at best!

Tukimaliza hiyo tunaingia kwenye ya Waziri wa Fedha (MUSTAFA MKULLO) na vyeti vyake feki
 
Jf Babkubwa Wako Juu,sio Kwahii Tu Bali Mambo Mengi Yanaenda Sawa Kwasababu Ya Jf So Hii Chama Kubwa Mno.
 
Jf Babkubwa Wako Juu,sio Kwahii Tu Bali Mambo Mengi Yanaenda Sawa Kwasababu Ya Jf So Hii Chama Kubwa Mno.

Hakika kwa Tanzania mpaka jambo liwe jambo ndipo muongozo wa tahadhari hutolewa, nani hajui kwamba Watanzania bado wanakufa kwa ajali na bado sheria zinapambwa bila kutekelezwa? Huko Mererani hii ni mara ya kwanza au ya tatu kwa janga kubwa kama hili kutokea na serikali inazidi kutoa ahadi, tatizo kubwa hapa ni mawaziri husika kubaki ofisini wakifanya mchakato wa namna ya kujichotea chao badala ya ku-deal na masuala muhimu yahusuyo objectives zao. Mara nyingi wimbo wa wakubwa hawa ni "nitayafanyia kazi mapendekezo yenu" lakini kamwe hutaona dalili yoyote ya madai ya wananchi yakifanyiwa kazi kwa wakati muafaka kama si siku chache kabla ya uchaguzi. Jana katika hotuba ya Mh. rais aligusia mengi sana ambayo JF imekuwa ikitoa kama mapendekezo, kasoro, n.k. Nashukuru sana kuwa mwana JF kwani ninaona naanza kuiva katika nyanja ya uongozi. Lakini pia nampongeza sana Mh. JK kwa kuwa mwana JF mwenzetu kwani amekuwa akijibu hoja nyingi sana zinazotolewa hapa JF. SASA ningependa bila kuwa semina elekezi kama ile ya Ngurdoto iliyotumia mamilioni ya pesa za wananchi kuwasuka MAFISADI awatumie wasaidizi wake kuwakumbusha wajibu mawaziri hawa wachache kuhusu mambo ya msingi ya kiusalama kwa wizara husika katika kuhakikisha tahadhari za msingi zinachukuliwa ili kupunguza idadi hii ya matukio ya ajali yakiwemo ajali za barabarani n.k. Kuna mantiki kwamba kuna sababu nyingine ya vifo vya Watanzania wenzetu ni kazi ya Mungu, lakini tusifanye Mungu huyu akachukiwa bure katika masuala ambayo yalikuwa ndani ya uwezo wetu kuweza kuyazuia. KUNA AJALI NYINGINE ZINAZUILIKA-TUCHUNGUZE CHANZO KABLA YA KUMPELEKEA "LAWAMA" MUNGU. INGAWA MUNGU ANAWEZA KUFANYA LOLOTE ATAKALO.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom