JF: Happy ending-Wanaharakati waitetea Jambo Forums!

Status
Not open for further replies.

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,354
1,943
Najua jinsi ambavyo hawa wenzetu serikalini wameziba mishipa ya kufikiri watakuwa hawakutarajia kuwa kwa kuitikisa JF walikuwa wanaifanya iwe rasmi. Kwa kifupi, kwa kitendo chao hiki wameitaaisisha JF bila wao kupanga wala kujua. Sasa ukiona tunaanza kutetewa na vyombo vikali kama LHRC ujue basi tena JF tena sio tu ni forum kama forum zingine; hiki sasa ni chombo muhimu kwa maendeleo ya ya Taifa letu kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nami natoa wito kuwa wale wenzetu katika forum ambao bado wanafikiri hiki ni chombo cha "ku-buzi" time waone sasa kwamba hapa sio mahala tena pakupitisha muda. Hapa sasa ni mahala hasa pa kumkoma nyani gladi tena mchana na usiku-yaani 7/24. Na kuthibitisha jinsi JF ilivyorasmishwa na kutaaisishwa na msukomsuko uliotokea, soma habari hii hapa chini kutoka kwenye gazeti la Tanzania Daima. Nawatakia michango miema, niliwa-miss sana wandugu. Nice to see you all back.***************************************************************


Wanaharakati waitetea Jambo Forums

(Tanzania Daima, 23-02-2008)

na George Maziku

WANAHARAKATI wa haki za binadamu nchini, wamesema kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata vijana wanaoendesha mtandao wa Jambo Forums kinakiuka katiba ya nchi na misingi ya haki za binadamu.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Helen Kijo Bisimba, alisema katiba ya nchi inatoa hakikisho la kila mtu kuwa na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, na uhuru wa kupokea habari.

“Nimesoma habari za kukamatwa kwa vijana wa Jambo Forums katika magazeti, lakini kituo chetu hakioni kosa lolote la jinai walilotenda kama polisi wanavyodai.

“Kitendo cha kuwakamata ni kuingilia uhuru wao wa kujieleza na uhuru wa habari bila sababu za msingi, kinyume cha katiba ya nchi na haki za binadamu,” alisema Bisimba.

Alisema kuwa kituo chake kinaiona hatua hiyo ya polisi kuwa jaribio la kuwatisha na kuwashona midomo Watanzania ili waogope kuhoji mambo mbalimbali yanayohusu nchi yao, kisiasa, kiuchumi na kijamii.

“Mtandao wa Jambo Forums umesaidia Watanzania wengi sana kujua mambo mengi kuhusu nchi yao. Hata kashfa za Richmond na BoT kwa mara ya kwanza zilichapishwa kwenye mtandao huu,” alisema mtendaji huyo wa LHRC.

Alisema kituo chake kinalifuatilia kwa karibu tukio hilo, na kwamba kipo tayari kutoa msaada wa kisheria kwa wahusika ili kuhakikisha haki inatendeka.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha Wanahabari wa Haki za Binadamu nchini (Journalists for Human Rights-JournoRights), Christopher Kidanka, alilaani kitendo cha polisi kuwakamata wanahabari wa Jambo Forums na kukielezea kuwa ukandamizaji wa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza.

“Tunalaani kukamatwa na kuzuiliwa kwa saa 14 kinyume cha sheria, kwa wanamtandao wa Jambo Forums na tunatoa wito wa kufutwa mara moja mashitaka dhidi yao,” alisema Kidanka katika taarifa yake ya ukurasa mmoja kwa vyombo vya habari.

Kidanka alisema kuwa kitendo hicho cha polisi kinathibitisha kuwa, watawala wamejiandaa kuuminya kwa haraka uhuru wa kujieleza unaoanza kuchanua miongoni mwa Watanzania.

Alisema kuwa mtandao wa Jambo Forums umekuwa mstari wa mbele kutangaza maoni ya watu na kufichua uozo unaoikabili nchi, hivyo kuwakamata wanamtandao hao kwa tuhuma za uchochezi, ni kuifutilia mbali heshima ya Tanzania kama nchi ya kidemokrasia.

Jumatano wiki hii, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema alizungumza na wanahabari, ambapo pamoja na mambo mengine, aliwapa taarifa kuwa jeshi lake lilikuwa limewakamata na kuwazuia wanamtandao wa Jambo Forums kwa tuhuma za kutenda uhalifu kwa kutumia mtandao wao huo.

Hata hivyo, si Kamanda Mwema mwenyewe wala taarifa yake kwa vyombo vya habari, aliyefafanua uhalifu uliotendwa na vijana hao, zaidi ya kauli za jumla kuwa wanatangaza taarifa za kihalifu.

Wakati huo huo, habari zilizotufikia zinasema kuwa Jeshi la Polisi nchini limewaachia kwa dhamana wanamtandao wa Jambo Forums na watu wengine tisa waliokuwa wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za ugaidi.
 
“Mtandao wa Jambo Forums umesaidia Watanzania wengi sana kujua mambo mengi kuhusu nchi yao. Hata kashfa za Richmond na BoT kwa mara ya kwanza zilichapishwa kwenye mtandao huu,” alisema mtendaji huyo wa LHRC.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha Wanahabari wa Haki za Binadamu nchini (Journalists for Human Rights-JournoRights), Christopher Kidanka, alilaani kitendo cha polisi kuwakamata wanahabari wa Jambo Forums na kukielezea kuwa ukandamizaji wa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza.

“Tunalaani kukamatwa na kuzuiliwa kwa saa 14 kinyume cha sheria, kwa wanamtandao wa Jambo Forums na tunatoa wito wa kufutwa mara moja mashitaka dhidi yao,” alisema Kidanka katika taarifa yake ya ukurasa mmoja kwa vyombo vya habari.

Kidanka alisema kuwa kitendo hicho cha polisi kinathibitisha kuwa, watawala wamejiandaa kuuminya kwa haraka uhuru wa kujieleza unaoanza kuchanua miongoni mwa Watanzania.

Alisema kuwa mtandao wa Jambo Forums umekuwa mstari wa mbele kutangaza maoni ya watu na kufichua uozo unaoikabili nchi, hivyo kuwakamata wanamtandao hao kwa tuhuma za uchochezi, ni kuifutilia mbali heshima ya Tanzania kama nchi ya kidemokrasia.

Baaab kubwa!
 
Ndugu zangu wana-JF,

1. Heshima mbele kwa Invisible, Mike, na Max, mashujaa wa JF kwa kazi nzito mliyoifanya ya kutubeba sisi wote wana-JF mbele ya pilato, Mungu awabariki, na hatuna cha kuwalipa ila kumkoma nyani tena mchana kweupeee!

2. Mkuu Halisi, respect mkuu kwa kazi nzito ya ku-cordinate the ordeal, you are a true JF-hero!

3. Brother Mwanakijiji, wewe ni mwamba na the heart and soul wa hii JF, uliyoyafanya katika kipindi cha majaribio, hayana mfano ni Mungu ndiye atakulipa.

4. Wakuu Steve D, Mtanzania, Rev Kishoka, Bob Mkandara, Mtanganyika, Azimio Jipya, Morani, Kitila, heshima mbele kwa kazi bubu na muhimu sana kwa JF, underground na behind the scene katika kipindi hiki kizima cha the ordeal, ilikuwa ni muhimu sana kwetu kusimama pamoja kwa nyuma katika hiki kipindi kigumu.

5. Salaam kwa wana-JF wote popote mlipo, kwa kusimama imara kulilia chombo kirudi, sasa kimerudi tuanze tena mawe.

6. Salaam kwa wa-Tanzania wote kwa kazi nzito ya kuivumilia mpaka JF imerudi, karibuni tena na wale wapya hapa hatuna peremende kwa waovu na wafisadi, tuna mawe na fimbo tu.

Mungu Aibariki JF, na Tanzania na hasa Wanyonge!
 
aaah, kwa hiyo munamaana kwenye JF, fursa kwa yule ambaye anatuhumiwa, kuja kuregister, kujibu hoja inaruhisiwa eeeh!!! kwa hiyo kwa maana nyingine... JF inatoa ruhusa mshutumiwa kusikilizwa, hivyo haivunji katiba bali inatekeleza katiba na natural sijui nini tena...!!! ama kweli JF ninyi mnajua kutenda haki...
 
For the record.

Like any true Tanzanian patriot and without the slightest disregard to the importance of all aspects of law and order, the cyberspace aspect being no exception, I wish to register my disgust and dissapointment with the obvious, deliberate and totalitarian muffling of our recently acquired freedom of speech.

The ignominious and cooked up charges against two members of JamboForums.com cannot go without the strongest condemnation from all peace and freedom loving Tanzanians.The charges exhibits some "US Patriot Act inspired" fearmongering at a time when some of us were just beginning to restore our faith in the uniqueness of Tanzania's relative freedom of speech. The fearmongering currently prevalent was made clear by our Inspector General of Police as documented by IPPMedia ( Police chief links use of internet to crime wave
http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2008/02/21/108832.html.)

It has been said that African governments not only engage in gross mismanagement and abuses, but also our rulers even go the extra mile by doing bad things badly.In this unfortunate instance the government unleashed a non objective state arm to sustain a police state, terrorizing patriotic dissent and meaningful discussion by using cheap and false pretenses.To achieve the feat of silencing a formidable agent of change that is Jambo Forums, if at all possible, will take much more than "state terrorism" disguised as "the state fighting terrorism".

The outrage is not only that these clouded false accusations legitimized by generalized half truths, manipulations and fabrications of terrorism and cybercrime propagated by the IGP at this most opportune moment are not only forcefully and manipulatively silencing the voice of reason and meaningful debate, but also squandering taxpayers resources at the whims of our mis-leaders.

The IPPMedia article, probably unintentionaly, potrays an IGP that generalizes and lumps together some ramshackle press release in the tradition of an inefficient police with no specific leads, who still wants to appear on top of his game in an effort to appease his masters and manipulate the public.

Let's face it, neither the Tanzanian government nor the law enforcement agencies are prepared to deal with the rigors of an online campaign.To careful observers,the government by using its law enforcement agencies to infringe upon Tanzanians constitutional right of association and expression, is not only making a laughingstock of itself, but also validating Jambo Forum's importance and resolute stance. Instead of trying to contain the jinn that is already out of the bottle, the powers that be should take a leaf out of Gorbachev's book and do away with tyrannical,unspecified, unjustified and shameful Gestapo like charges.


The Tanzanian people, most without internet access, do not see cybercrime (especially from discussion boards) as a top priority.The law enforcement bodies should concentrate on fighting grand corruption, beginning with processing procedures to prosecute the mis-leaders who took Kiwira Coal Mine illegally, all who are responsible in the Richmond saga some in peaceful taxpayers funded retirement, not to mention a total review of all major contracts from the container terminal (TICTS) to IPTL.

There is a prudent way of owning up past mistakes and starting restoring Tanzanin's confidence afresh,unfortunately, judging by using this incident as a barometer, the government and its agents did not choose to start by pursuing this prudent way.

The government had better seize the moment to come clean while there is still some semblance of confidence in it, before even the proverbial "kipofu" sees the hand that takes a bigger chunk from the plate.The new generation of Tanzanians will not take these dirty tricks, power abuses and totalitarian tendencies laying down.
 
Sasa ningewaomba wamiliki wa JF, wakae chini na kujaribu kuangalia tena the rules na sheria ndani ya JF, kwa sababu pamoja na ukiukaji wa haki wa polisi kwa kuwakamata wana-JF bila makosa, lakini pia na sisi JF huu ni wakati wa kujiangalia kwenye kioo, serikali imethibitisha one thing, kwamba hapa JF tunazo habari amabzo ni the right stuff kwa taifa,

Lakini at the same token pia kuna sometimes tunapitiliza kipimo, I mean ninaelewa hasira zeti dhidi ya mafisadi, lakini pia hapa kwenye elimu, tujaribu ku-stick na ishus ndugu zangu, sasa tukae chini tuangaliane usoni, wasioweza wakae pembeni wasome ya wengine wanaoweza, tuandike ishus na dataz, na ikibidi hata ushahidi, lakini matusi tuache maana sio lazima kwenye kufikisha ujumbe kwa mafisadi.

Invisible, na wenzio sheria iwe msumeno, kusiwe na zile bias tena atakayevunja sheria afukuzwe, tena isemwe wazi hadahrani bila kufichwa, na akiomba radhi kurudishwa iwekwe hapa wazi na kura ipigwe ili arudi au asirudi, maana sasa hatutaki mchezo tena, katika hiki kipindi kigumu binafsi nimepokea karibu ujumbe 1500 kutoka kwa wananchi mbali mbali, wakiwemo wananchi, viongozi wetu, mpaka mafisadi kuhusiana na mwenendo wetu hapa JF, nitajaribu ku-diggest na kuyafikisha mapendekezo kwa Invisible, lakini ninaomba tuheshimu sheria zetu, na ikiwezekana ziwekwe hadharani wote tuzisome tena, ni a serious system yetu wenyewe ya regulation na moderation ndiyo inayoweza kutuokoa na majanga ya sheria wakuu, na kutunza heshima kati yetu wananchi hapa!

Wakuu nitarudi karibuni ninahitaji muda kidogo ku-absorb yaliyojiri maana niko overwhelmed na recent events kidogo, na tuendelee kumkoma nyani giladi tena mchana kweupeee, lakini ninaomba wananchi tuelewe kuwa sasa we are a new JF sio ile tena ya zamani, sasa tumekubalika na taifa zima kuwa we are for real, na number one na sisi sasa tubadilike tuwe for real zaidi!
 
ES
na wengine wote Kishoka. MKJJ,Robot mkuu , na wale ambao tumegongana angani na wale ambao wametoa michango na sala .Nasema JF idumu.Nilitegemea IGP angalikuja hapa akasema samahani .Ametufanya tumepoteza kuwapa watanzania habari za Kiteto, tumechelewa kuichambua safari ya Bush , bado hatujua nani anaunda kamani ya waziri Mkuu ili tujue kama Hosea na Mwanasheria Mkuu wanatimua.Pia hatujui kwa nini kule Kiteto Komba alaimua kulala kwenye jukwaa ama eneno la Chadema ambapo walitakiwa kufananya mkutano na hawajachukuliwa hatua .IGP na Serikali ya JK kwa Ujumla wana jambo la kutueleza.

Kwa sasa nasema Asanteni sana .Niko Arusha Naeleke Kiteto sasa ila usafiri ni mgumu . Natoa wito wa kuzidi kumwaga mawe mazito na ya uhakika sasa maadamu wamesha tupa utambulisho mkubwa .
 
Tunashukuru kwamba Serikali nayo imekuwa mbele Kuipigia debe JF kwani sio wengi kule tunduru walikuwa wanaiyelewa na kuwaambia Wapi Kunapatika ukweli na HAKI basi ingia jf utazikuta haki zako zoote mwanawa nchi hii, thanks
 
Kwa kweli wadau hatuna budi kufurahi kwani wengine tulishakuwa tumeandika makala mbalimbali kuhusu hawa jamaa na kuzisambaza kwa magazeti ya bongo na bbc ili zitoke hewani.Kwa wale ambao watapenda kuziona mojawapo ya reaction ilikuwa ni kama hivi.

JAMBO FORUMS ITENDEWE HAKI.

Na augustoons[1].

Hivi karibuni kumekuwapo taarifa juu ya kukamatwa vijana wawili wakihusishwa na mtandao maarufu wa tovuti uitwao jambo forums. Mtandao ambao ulikuwa ukipatikana kwa anuani hii www.jamboforums.com popote duniani. Vijana hawa walishikiliwa na polisi kwa zaidi ya saa 24 wakihojiwa na baadaye kuachiliwa kwa dhamana. Baadaye ilifuatiwa taarifa ya mwanachama mwandamizi wa jambo forums katika BBC akieleza kusikitishwa kwake na kukamatwa kwa wanachama hao,ambapo maelezo yake yalijibiwa kwa maelezo toka kwa msemaji wa jeshi la polisi kuwa mtandao huu unatoa habari za uongo,ni wa kichochezi na unahusishwa na ugaidi.

Mbali ya kuzungumzia mambo ya cyber crimes, mkuu huyo toka polisi aliuhusisha moja kwa moja mtandao huu na ugaidi ikiwa ni pamoja na kusema kuna watu wamelalamikia mtandao huu kuwa unawachafua majina yao. Mwandishi wetu katika makala haya anajaribu kuchambua kauli hizo kwa kulinganisha na kile kinachofanyika jambo forum na sheria zetu zilizopo.

Labda tuanze kuangalia jambo forum ni nini na inafanya nini.

Kwa watu wachache ambao wamepata kuuona mtandao huu kwenye internet (kwani internet sio siri) mimi nikiwa mmojawapo, watakubaliana na mimi kuwa ni vigumu kuamini kuwa mtandao huu ni wa kigaidi kutokana na mambo yaliyomo mule labda kama polisi wana vigezo vingine na maana nyingine ya ugaidi tofauti na ile iliyopo kwenye sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2002 yaani Prevention of Terrorism Act. Jambo forum ni mtandao ambao unaitwa jukwaa la majadiliano ambapo watu wa kada mbalimbali huruhusiwa kutoa maoni yao kuhusu mada yoyote iliyowekwa humo. Aidha watu huruhusiwa kuuliza maswali na kujibizana ikiwa hata kukanushana wenyewe kwa wenyewe.Mtandao huu hautofautiani kabisa na unapowakuta watu pale Manzese, kariakoo,au Nkurumah chuo kikuu cha Dar-es-salaam wakijadiliana jambo, hivyo daima kutakuwa na pande mbili zinazopingana,wale wanaokubali hoja na wale wanaopinga hoja. Haya ndiyo yanayofanyika jambo forum.

Tena mtu akiandika kitu ambacho hana uhakika nacho wachangiaji watamshambulia sana hadi kupelekea mada hiyo kufungwa. Suala la kujiuliza hapa je hizo mada zinatoka wapi? Mada hizi,hutokana na mambo ya kila siku yanyoibuka na kuendelea Tanzania na duniani pote na hasa yale yaliyoandikwa kwenye magazeti ya kila siku. Mada nyingine ni kweli huwa za kutungwa hasa zile zilizo mfano wa maswali. Hapa nitatoa mfano kidogo. Hivi karibuni nchini Tanzania kulikuwa na matukio ya kufukuzwa kwa Gavana wa benki kuu, ripoti ya richmondi na ujio wa Rais Bush wa marekani,mada zilizotawala mtandao huu toka wakati wa sakata la BOT zilikuwa,je,Balali ashtakiwe? Je, Ziara ya Bush nchini Tanzania haina faida yoyote kama baadhi ya watu wanavyosema? Je, Hosea atakwepa dhambi ya kujiuzulu kwa mujibu wa ripoti ya mwakyembe na suala la hotuba ya Rais Kikwete na Bush wakiwa ikulu darn a jinsi vyombo vya magharibi vilivyoiandika.Hivyo kwa ufupi jambo forums ni jukwaa la majadiliano.

Tofauti na lilivyo gazeti ambapo habari hutolea na mhariri na msomaji hana nafasi ya kuidadisi habari hiyo au kuuliza maswali au kuchangia jambo;Jambo forum msomaji wa mada(tena sio habari) mada hupata nafasi ya kuchangia, kuuliza maswali, hata kutofautiana kabisa na mwandishi kwa kuja na hoja tofauti yenye ushahidi na vigezo mahiri. Aidha pamoja na mada kama hizi zinazohusu siasa kuna sehemu ya mtandao huu ambayo hujadili habari kuhusu Afrika mashariki, uchumi, elimu, sheria, maswali, afya, burudani na michezo, dini, pamoja na lugha. Katika hizi mada nyingine utakutana na majadiliano kuhusu sayansi ya teknolojia, utakutana na masuala ya uchaguzi wa marekani,utakutana na maneno mbalimbali ya Kiswahili jnsi yanavyotumika na kukosolewa na vilevile masuala ya dini. Katika kuchangia mada hizi wachangiaji ambao idadi yao ni zaidi ya elfu nne wenye elimu na nyadhifa mbalimbali serikalini na nje ya serikali,na waliotawanyika popote duniani na ambao ni watanzania,huchangia mada hizi kutokana na uelewa wao wa mada hizo na wasipoelewa huomba nafasi ya kuuliza toka kwa wale wanaoelewa na hata wakipewa majibu basi wao huyachallenji.Hata baadhi ya waheshimiwa muhimu wa hapa Tanzania hutoa mada kwenye mtandao huu. Na kizuri zaidi katika mtandao huu, mada yoyoyote inayojadiliwa mara nyingi huwa haina hitimisho zaidi ya kukosa wachangiaji na matokeo yake kufungwa, katu hata siku moja watu hawatoki na azimio Fulani au kupanga namna ya kutekeleza majadiliano haya. Na kila siku huibuka mijadala mipya na mingine kufa. Sasa sijui suala la ugaidi linatoka wapi? Je,mtu anayechangia misamiati ya Kiswahili ili kukuza lugha ugaidi wake unatoka wapi? Mtu anayechangia mada kuhusu ugonjwa wa malaria, teknolojia, mauaji ya Kenya na kuomba watu waishi kwa amani anatoa habari zipi za uongo au ugaidi?

Ni ukweli usiofichika kuwa katika jukwaa la siasa, jambo forum au jf kama wao wanavyoiita,imekuwa ikiibua mambo mazito katika jamii yakiwemo masuala ya buzwagi, richmondi, EPA,TICTS na mengineyo mengi ambayo yamepelekea habari nyingi kwenye vyombo vya habari hadi bungeni na hata kuundwa kamti ya mwakyembe ambayo sote matokeo yake tumeyaona.Habari hizi wakati mwingine zimekuwa zikigusa idara muhimu za serikali, maafisa wake na hata chama tawala kama vile This day, kulikoni na mwanahalisi zinavyofanya. Aidha katika siku za karibuni jambo forum imekuwa mstari wa mbele kusisitiza kufanyiwa kazi kwa ripoti ya mwakyembe ikiwa ni pamoja na kuchambua uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja kwenye ile ripoti,jambo ambalo sidhani kama ni kosa.Kwani hata hukumu iliyotolewa na mahakama watu wanahaki ya kuichambua.Inawezekana kabisa,ni kwa sababu hizi labda ndio maana jf inatajwa kama mtandao wa kigaidi kutokana na kufukua maovu mengi katika jamii na kuyaweka hadharani watu wachangie na mwishowe wajibu ni wao kuchukua ama kutochukua hatua.

Matumizi ya majina
Katika kujadili mada mbalimbali kwenye tovuti hiyo watu hutumia majina mbalimbali, bandia na yasiyo bandia, kwa maana ya kwamba baadhi hutumia majina yao halisi, anuani za barua pepe, na wengine hutumia majina ya kubuni. Hii haina maana kwamba wanaotumia majina bandia ni wahalifu. Kwani wakati wa kutoa maoni hakuna sheria yoyote inayomtaka mtu ataje jina lake kwanza ndipo atoe maoni. Hata wao Polisi mara nyingi wamekuwa wakituomba wananchi kuwapa habari kuhusu vitendo vya uhalifu bila kutaja majina yetu au hata kama tukitaja kwa maelezo kwamba watatuhifadhi. Sasa je,kuna ubaya wowote wa mtu kutotaja jina lake? Nchi zilizoendelea kama Uingereza,ipo sheria kuhusu uhifadhi wa habari za mtu(Data protection Act) ambapo kwa mujibu wa sheria hii mtu anayo haki ya kutotaja jina lake. Aidha majina mengi yanayotumika kwenye forum ni ya kisanii zaidi kuliko kuwa bandia mathalani mtu anajiita mwanakijiji, maskini jeuri, mtanzani halisi n.k. hayana uhusiano wowote na jinai.

Hivyo kuufungia mtandao huo kwa mada moja tu ya kisiasa bila kuangalia content zake nyingine ni kukiuka uhuru wa watu kutoa maoni kwani si kweli kuwa habari zilizo katika mtandao huo zote ni za uongo. Hivi watu wanapojadiliana, nani anamdanganya nani?Isitoshe wachangiaji mada katika mtandao ule wana elimu zinazolala kati ya darasa la saba na phd,na asilimia 60 ya wachangiaji wanaonekana kuwa na elimu kati ya form six na chuo kikuu. Aidha wachangiaji wa jf wana itikadi tofauti wapo wa chama tawala na wa vyama vya upinzani, webye dini na wasio na dini,wanaoguswa na habari hizo na wasioguswa moja kwa moja.

Jaji mmoja wa mahakama kuu ya Tanzania katika kesi ya TAKRIMA[2] aliwahi kusema (wakati akijibu hoja ya serikali kuwa sheria ya takrima ililetwa ili kuondoa matumizi mabaya ya haki ya kushtaki katika mahakama kuhusu makosa ya uchaguzi)kwamba,ukweli kwamba haki au uhuru Fulani unatumika vibaya si sababu ya kuufuta au kuizui haki hiyo,kinachotakiwa ni kutafuta mbinu za kuboresha kwa kuondoa matumizi mabaya. Sote tunafahamu kwamba kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba yetu,aidha sheri haisemi ni maoni gani,au yatoleweje.

Japokuwa kimsingi hakuna haki bila wajibu,au hakuna haki isiyo na mipaka,bado mipaka hiyo isitumike vibaya. Twafahamu kuwa haki yako inapoishi ndipo ya mwingine inapoanza. Hivyo mtu yeyote angtegemea kwamba,mtu au watu waliokashfiwa kwenye mtandao huo waende mahakamani kwani tayari hiyo ni defamation sio criminal case. Na suala kwamba mtandao huo umesababisha watu wapigane au ugomvi wa baba na mwana,halina msingi kwani ni habari ngapi zinazoandikwa magazetini na watu kuishia kushikana mashati huko mtaani?Je,tunadhani habari zote zinazoandikwa kwenye magazeti watu wanazifurahia?vikatuni je? Naam hii ya jeshi la polisi kukemea mitandao kama jambo forum inanikumbusha miaka ya tisini ambapo aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo Ernest Nyanda alipiga marufuku vikatuni. Watu kama kina kipanya walipata shida sana wakati ule.Lakini je,vikatuni vimeondoka Tanzania? Tujiulize,hivi ni gaidi gani mjinga anayeweza kujadili mambo kwenye internet ambako hakuna usiri wowote? Kama ni hiyo cyber crime polisi wanayosema, sijui wanaielewaje? Nadhani vitivo vyetu vya sheria vinapaswa kuanza kufundisha somo la cyber crimes. Kwani kwa jinsi navyoelewa cyber crimes hazitokani na majadiliano.

Cyber crime[3] inahusu vitendo vya jinai vinavyohusu matumizi ya kompyuta na netiweki yaani kwa kiingereza "hacking" mfano kuiba website ya mtu na kubadilisha matumizi yake, kuharibu data,wizi wa kutumia internet,matangazo ya biashara feki,udanganyifu wenye lengo la kujipatia pesa au mali(fraud),wizi wa utambulisho wa mtu na kutumia visivyo(identity theft) na kutengeneza akaunti za credit card bandia.Pia inahusu picha za ngono za watoto,vitisho kwa kutumia barua pepe, maelezo ya matusi yanayohusu ngono na utupu na usambazaji wa habari chafu. Sasa je,katika hayo hapo juu, jf imefanya lipi?

Kama ni maelezo ya Uongo au habari za uzushi ziko tovuti nyingi kwenye ambazo zimekuwa zikionesha barai za ngono,na zisizo za kweli na pia yapo hata magazeti Tanzania tunayaita ya udaku ambayo habari zake nyingi zimekuwa za kutungwa ama ukweli wake unasuasua. Ikumbukwe kuwa Tanzania tofauti na nchi zilizoendelea hatuna sheria zinazotawala internet. Na hili ni tatizo kubwa ambalo mimi na wadau wengine tulidhani wakati umefika kwa polisi na wizara husika kufikiria kuwa na sheria hizi. Zaidi ya kanuni ya adhabu(pena code),sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai,(Criminal procedure Act)hatuna sheria ya msingi kabisa inayogusa cyber crime. Mbona mwaka Fulani hapa tovuti ya serikali iliibwa na bwana mmoja na ikatumika kuoneshea picha za ngono,Yule bwana tulishindwa kumfanya chochote? Nadhani umefika wakati Tanzania kuwa na sheria kama vile Data Protection Act, Fraud Act, Computer Misuse Act na Information and communications Act ambazo labda ndizo zitawawezesha polisi kudhibiti matumizi ya internet. Kutokuwa na sheria hizi polisi watajikuta wakilazimisha makosa kuingia katika sheria ambazo haziyataji makosa hayo. Na kesi zinazohusiana na internet si rahisi kama wao wanavyofikiri.Nje ya sheria hizi polisi watajikuta wanavunja sana haki za binadamu. Na ndio maana tunasema kwamba jambo forum watendewe haki,polisi waseme ukweli,je,sababu walizozitoa ni za kweli au kuna jambo jingine lililojificha?.

Mtakumbuka kuwa mwaka 2007 kulikuwa na habari kwenye internet kuhusu ubadhirifu wa pesa za BOT na wabadhirifu hao kutajwa.Pamoja na wananchi kutaka hatua zichukuliwe juu ya watu hao,na polisi kufanya uchunguzi.Polisi hao hao na baadhi ya wanasiasa walitoa majibu kuwa hawawezi kufanyia kazi habari za internet,kwani nyingi ni za uzushi na wala hawajui nani mwandishi.Tukasema sawa, lakini jeshi la polisi hilohilo leo limegeuka na kuanza kufanyia kazi habari za internet. Ndio kusemaje hapa,au kwakuwa zile za awali ziliwagusa baadhi ya watu ndani ya jeshi la polisi? Na hizi za sasa haziwagusi? Hebu tuwe consistent. Tuache watu watoe maoni.Tuache watu wajadiliane,hivi ukiwakuta watu wanajadiliana jambo Fulani pale kariakoo utawakamata eti kwa kuwa tu wanamjadili waziri mkuu aliyeondoka? Uhuru wa vyombo vya habari utainua taifa. Wenzetu katika nchi zilizoendelea mtu anaweza hata akasimama barabarani na bango kubwa ukasema "simtaki Gordon Brown kwa kuwa amefanya a,b,c." Polisi hawatamfanya kitu maadamu haathiri haki za watu wengine. Wapo watakaokuunga mkono na pia wapo watakaomdharau tu. Ifike wakati tuache kufanya mambo kisiasa, tushughulike mamilioni ya EPA,TICTS,BUZWAGI n.k kuliko kushughulikia majadlianoya watu yasiyo na kichwa wala miguu.Mtu ambaye amekwazwa na jambo forums aende mahakamani,polisi wamsaidie tu kujua nani mmiliki wake ili aweze kumpelekea summons kwa urahisi.Sheria za madhara(torts) zipo zitumike.

Aidha, Ikumbukwe kuwa ni vigumu kudhibiti matumizi ya internet hasa bila kuwa na sheria pia ushirikiano wa wadau na nchi nyingine za afrika au duniani. Leo utawakamta hao vijana wawili kuwa ndio wanaohusika,lakini bila kujua hasa nani anamiliki hiyo server,utawafunga na kuwafanya lolote uwezalo,lakini kama server iko uingereza au marekani bado internet itaendelea kuwa hewani,na watu wataendelea kuandika na hapa ndio linakuja suala la jurisdiction. Je,unayo-jurisdiction ya kuzuia flow ya internet? Nadhani polisi walikurupuka,wajipange na waliangalie upya jambo hili na wakati mwingine kabla ya kuchukua hatua wawe wanaomba ushauri kwa wanazuoni wengine. Tunaliamini sana jeshi letu na tunajua kuna wasomi wengi lakini,kusoma hakuishi na mtu huwezi kuwa mtaalamu kwenye fani zote na ndio maana kuna mashauriano(consultation). Hili likifanyika tunadhani jeshi letu la polisi litaweza kufanya kazi vizuri zaidi kwa faida yetu sote.

Mwisho,natoa mwito kwa jeshi letu la polisi kujipanga na kufnya kazi kisayansi, kuwa na uchunguzi makini ili kutoathiri haki za watu. Na sio lazima kila wakati mtu akiripoti jambo kuhusu mtu Fulani umkamate hapohapo huyo mtu,upo uwezekano wa kufanya uchunguzi bila mtu huyo kujua halafu ndio unamkamata.Mmetuambia mnachunguza suala hili,tunashukuru lakini hata kama hili suala linachunguzwa,basi lisiathiri uhuru wa watu na haki zao kikatiba, ili wananchi tujue habari za uongo katika mtandao huo ni zipi? Nani aliathirika nazo na hatimaye haki iweze kutendeka.Kwa upande mwingine mwito ni kwamba polisi waache kujumuisha mambo(generalisation) kwamba mtandao huu ni wa hivi na vile,kabla ya kuongea wafanye utafiti,kwani kauli wanazozitoa wkwa umma ni kauli nzito na zinawakilisha msimamo wa serikali.Hivyo ni vema zikatolewa baada ya kufanya utafiti wa kina na sio wa kuambiwa.Pia ni vema polisi nao wakaingia kwenye mtandao huo wakaona kinachofanyika na kwa sasa wawaruhusu wanaouendesha mtandao huo wauweke hewani ili wananchi wajue ukweli na waweze kuisaidia polisi katika uchunguzi wake.


--------------------------------------------------------------------------------

[1] Mwandishi wa makala hii ni Mwanasheria binafsi na anayebobea katika masuala ya sheria za kimataifa za biashara, internet na jinai zake.Anapatikana kwa barua pepe augustoons@gmail.com
[2] Legal and Human Rights Centre and others v. AG [2005] HCT-DSM(Haijaripotiwa)
[3] http://www.naavi.org/pati/pati_cybercrimes_dec03.htm
 
Sasa ningewaomba wamiliki wa JF, wakae chini na kujaribu kuangalia tena the rules na sheria ndani ya JF, kwa sababu pamoja na ukiukaji wa haki wa polisi kwa kuwakamata wana-JF bila makosa, lakini pia na sisi JF huu ni wakati wa kujiangalia kwenye kioo, serikali imethibitisha one thing, kwamba hapa JF tunazo habari amabzo ni the right stuff kwa taifa,

Lakini at the same token pia kuna sometimes tunapitiliza kipimo, I mean ninaelewa hasira zeti dhidi ya mafisadi, lakini pia hapa kwenye elimu, tujaribu ku-stick na ishus ndugu zangu, sasa tukae chini tuangaliane usoni, wasioweza wakae pembeni wasome ya wengine wanaoweza, tuandike ishus na dataz, na ikibidi hata ushahidi, lakini matusi tuache maana sio lazima kwenye kufikisha ujumbe kwa mafisadi.

Invisible, na wenzio sheria iwe msumeno, kusiwe na zile bias tena atakayevunja sheria afukuzwe, tena isemwe wazi hadahrani bila kufichwa, na akiomba radhi kurudishwa iwekwe hapa wazi na kura ipigwe ili arudi au asirudi, maana sasa hatutaki mchezo tena, katika hiki kipindi kigumu binafsi nimepokea karibu ujumbe 1500 kutoka kwa wananchi mbali mbali, wakiwemo wananchi, viongozi wetu, mpaka mafisadi kuhusiana na mwenendo wetu hapa JF, nitajaribu ku-diggest na kuyafikisha mapendekezo kwa Invisible, lakini ninaomba tuheshimu sheria zetu, na ikiwezekana ziwekwe hadharani wote tuzisome tena, ni a serious system yetu wenyewe ya regulation na moderation ndiyo inayoweza kutuokoa na majanga ya sheria wakuu, na kutunza heshima kati yetu wananchi hapa!

Wakuu nitarudi karibuni ninahitaji muda kidogo ku-absorb yaliyojiri maana niko overwhelmed na recent events kidogo, na tuendelee kumkoma nyani giladi tena mchana kweupeee, lakini ninaomba wananchi tuelewe kuwa sasa we are a new JF sio ile tena ya zamani, sasa tumekubalika na taifa zima kuwa we are for real, na number one na sisi sasa tubadilike tuwe for real zaidi!


Mkuu FMES,

Sina la kuongeza, you have said all, tuache kuweko bumba hapa tunatumia muda mwingi kuchambua na kupata ukweli... tulete mambo ambayo hayapo too biased!!!
 
Bandugu

Nina imani wale wote waliokuwa wanatumia lugha za matusi Mods wetu walikuwa macho either kuwapa warning na kuondoa immediately posts zao, sheria zetu ziko makini katika hilo na ziko wazi kuwa watu watoe inf wakiw ana uhakika na wanachokisema, na mara nyingi hapa mwenye kuleta data feki watu walio na adata za uhakika waliweza kukanusha

tatizo ni kuwa Mafisadi walizidiwa/wamezidiwa na information za uhakika zinazotoka hapa na wameanza kulia lia

Mkuu FMES
Ni kweli ndg yangu ni vyema kujiangalia.....where did we go wrong.......have we (JF)overlooked the term CYBERCRIME?......Nafikir Invisible amekuwa mstari wa mbele kukemea hoja zenye kujenga chuki sio baina yetu hapa JF tu bali hata huko Uswazi na Serikalini pia.

Ninaendelea kusoma elimu mbali mbali kuhusu cybercrime ili kujua ni nini kinaendelea, kw amfani wa-Canada wanasema hivi
Cyber crime consists of specific crimes dealing with computers and networks (such as hacking) and the facilitation of traditional crime through the use of computers (child pornography, hate crimes, telemarketing /Internet fraud). In addition to cyber crime, there is also “computer-supported crime” which covers the use of computers by criminals for communication and document or data storage. While these activities might not be illegal in and of themselves, they are often invaluable in the investigation of actual crimes. Computer technology presents many new challenges to social policy regarding issues such as privacy, as it relates to data mining and criminal investigations. (Canada Foreign Affairs)

Mwema anajua alichokuwa anakifanya kwani ni mmoja wa wazoefu sana wa Interpol, lakini pia akumbuke hapa JF tumejiwekea sheria zetu na ziko wazi kabisa. Akina Mwema na wezake watueleze....tena ikiwezekana waje hapa (wanakaribishwa) ni kw amisingi ipi waliwashikilia wenzetu.................kusema JF SAMAHANI KWA USUMBUFU PEKEE HAITOSHI....je hao wenzetu wamekuwa CLEARED OUT OF CYBERCRIME????

Afande Mwema vipi Matumizi ya Simu huoni kuwa huko MKO HOI na MNAO UDHAIFU WA HALI YA JUU!!!

Mwema.......ungejua ni jinsii gani JF imekuwa mstari wa mbele sio tu kufichua maovu bali hata KUISHAURI Serikali kwa mema (though wengi wenu mumeweka pamba masikioni)wala usingethubutu kuingia MTEGO wa MAFISADI waliokuwekea...........You got to be extremely careful na watu waliokuja kukulalamikia kwa kisingizio cha CYBERCRIME
 
Field Marshall Es,

Mimi nafikiri kuwa jambo moja tu ndilo zito zaidi.. MATUSI!
Matusi ya nguoni kwa kiongozi ama mtu yeyote ni nje ya haki hiyo tuliyopewa.
Hao wote wanaoshindwa kujadili vitu kwa hoja kisha wakazua vioja wakidhani wao ndio pekee wenye uchungu basi hawa hawafai kabisa kutoa michango yao humu. Personal attack bila hoja ya msingi inayomhusu mhusika ni pumba tupu.

Matusi kama yalivyo matusi ni swala la wahusika tena wakiafikia wote (laa sivyo ni rape), kujifungia chumbani wakakahakikisha madirisha na milango yote imefungwa, sio kuwa hadharani kama wanyama....

Mwenye issue na kiongozi ama mtu yeyote kufikia point ya kutoleana matusi basi bila shaka atumie private message - PM au hata e-mail, kwani vimewekwa kwa malengo kama hayo. Jifungieni huko hakuna mtu anayetaka kusikia upuuzi kama huo.
 
Naam wakuu mie nawaunga mkono wote manaake kitu chochote bila kuwa na kanuni zinazotekelezeka ndio mwanzo wa kuwapa loophole maaduni zetu kutukoma mchana kweupeeeeeeeeee manaake tunawakusanyia evidence.Nafahamu sote tunamachungu na ufisadi lakini ni vema kuangalia approach zetu na kudhibiti moods na emotions zetu kwa sheria.Siku zote ukiwa unargue-au kutoa hoja kwa emotions hoja yako inaonekana pumba lakini ukicontrol emotion unaweza kuongea vizuri na kueleweka.Kitu kingine tudumishe uvumilivu wa maoni ya wengine.yapo maoni ambayo yanauma sana lakini ikiwa yana ukweli basi tuongeze uvumilivu ndio demokrasia.Tukianza kutukanana wenyewe na kutumia lugha za matusi,hapo ndio wenyewe tutakuwa tunajichomeka kwenye definition ya cyber crimes.
 
Field Marshall Es,
Matusi kama yalivyo matusi ni swala la wahusika tena wakiafikia wote (laa sivyo ni rape), kujifungia chumbani wakakahakikisha madirisha na milango yote imefungwa, sio kuwa hadharani kama wanyama....

Mwenye issue na kiongozi ama mtu yeyote kufikia point ya kutoleana matusi basi bila shaka atumie private message - PM au hata e-mail, kwani vimewekwa kwa malengo kama hayo. Jifungieni huko hakuna mtu anayetaka kusikia upuuzi kama huo.

Mkandara;

You said it all!

Niongezee kidigo. Ni kweli kuna wakati mtiririko wa hoja na mchakato wa issue humu JF unakuwa mkali ambavyo sio jambo baya. na kuna wakati mchakato unakwenda mpaka unapitiliza from mental level to emotional state! ikifikia hapa... mtu ana_loose control...!! Lakini kitaalamu kabisa..inafahamika kuwa in this particular state ndipo panapoamua ni nani atashinda na kufikia lengo lake. Hapo ndipo inapobidi Utu uzidi Hisia zetu kama tunataka kutakata na kushinda jambo au hoja.

Kweli kuna wakati bado mambo yanakuwa mazito..NA HAPO ndipo tunarejea wazo la makandara kuwa there is PM.

Kipidi tulichopo we need sharp and bright intelligent kwenda foward. Emtional activities zinaturudisha upande wa mafisadi. Ni kweli wao katika nafasi zao and in Private times waliaaza kushindwa kujimiliki kihisia na taratibu wakaanza kuepress externaly what they are inside..Ufisadi. We dont want to go into that line. Ni tofauti yetu ya dhati nao ndio itakuwa Nuru na njia ya kwenda mbele!

Ni kweli kabisa sometimes mwingine atahitaji ku_joke....etc na kila mtu has his/her own way of achieving that..mwingine..unachokita tusi kwake..ni sentsi ya kawaida mdomoni kwake....inatoka tu..wala haina maana inayokusudiwa na mlengwa au mtu mwingine..

BUT..and BUT

Adui wa ukweli, adui wa harakati za kutetea utu na haki ya ubinadamu.., anaweza akaichukua the same sentence akaitumia to his advantage. Na kuna wakati hatuhitaji kumpa such a cheep starting. We know whatever protective measure we take..mtu akikutafuta atakupata....Tu, Lakini asiwe na vianzio rahisi na bure kabisa.
 
Mkuu FMES,

Sina la kuongeza, you have said all, tuache kuweko bumba hapa tunatumia muda mwingi kuchambua na kupata ukweli... tulete mambo ambayo hayapo too biased!!!

Unazoziita 'pumba' wewe, mwenzako anaziona pointi muhimu. Ukweli kwako si lazima uwe ukweli kwa kila mtu.
That is why JF is thriving. The diversity and divergence of points of views.
 
Mkandara;

You said it all!

Niongezee kidigo. Ni kweli kuna wakati mtiririko wa hoja na mchakato wa issue humu JF unakuwa mkali ambavyo sio jambo baya. na kuna wakati mchakato unakwenda mpaka unapitiliza from mental level to emotional state! ikifikia hapa... mtu ana_loose control...!! Lakini kitaalamu kabisa..inafahamika kuwa in this particular state ndipo panapoamua ni nani atashinda na kufikia lengo lake. Hapo ndipo inapobidi Utu uzidi Hisia zetu kama tunataka kutakata na kushinda jambo au hoja.

Kweli kuna wakati bado mambo yanakuwa mazito..NA HAPO ndipo tunarejea wazo la makandara kuwa there is PM.

Kipidi tulichopo we need sharp and bright intelligent kwenda foward. Emtional activities zinaturudisha upande wa mafisadi. Ni kweli wao katika nafasi zao and in Private times waliaaza kushindwa kujimiliki kihisia na taratibu wakaanza kuepress externaly what they are inside..Ufisadi. We dont want to go into that line. Ni tofauti yetu ya dhati nao ndio itakuwa Nuru na njia ya kwenda mbele!

Ni kweli kabisa sometimes mwingine atahitaji ku_joke....etc na kila mtu has his/her own way of achieving that..mwingine..unachokita tusi kwake..ni sentsi ya kawaida mdomoni kwake....inatoka tu..wala haina maana inayokusudiwa na mlengwa au mtu mwingine..

BUT..and BUT

Adui wa ukweli, adui wa harakati za kutetea utu na haki ya ubinadamu.., anaweza akaichukua the same sentence akaitumia to his advantage. Na kuna wakati hatuhitaji kumpa such a cheep starting. We know whatever protective measure we take..mtu akikutafuta atakupata....Tu, Lakini asiwe na vianzio rahisi na bure kabisa.

Ni furaha iliyoje kuona JF imerudi tena hewani. Tutaendelea na harakati za kuhakikisha mafisadi wote waliohusika na kusaini mikataba mibovu, kashfa ya Richmond, kashfa ya TICTS, kashfa ya ununuzi wa rada, ndege za jeshi na helikopta, kashfa ya kujipatia KCM katika mazingira yasiyojulikana, kashfa ya EPA wanafikishwa mahakamani na kufilisiwa pindi itakapoonekana kuna ushahidi wa kutosha dhidi yao.

Idumu JF.
Mungu ibariki Tanzania
 
Wakuu,

Hii ya JF kurudi na publicity ambayo JF imepata, mimi mpaka nimetishika. Nimetishika kwasababu naona huenda tumepewa sifa na heshima kubwa kuliko tunayoweza kuibeba.

Naona ni kama tumepata green light ya kuendesha mambo yetu. Huenda tusiguswe tena au kufungiwa siku za karibuni. Wasiwasi wangu ni kwamba kuanguka kwa JF kunaweza sababishwa na sisi wenyewe.

Nakubaliana kabisa na FMES kwamba tutumie muda huu kujiangalia vizuri kwenye kioo na kugundua wapi tunakosea ili tujirekebishe.

Mategemeo ya Watanzania wengi na hasa hao watakaojiunga sasa ni kwamba kuna chombo hiki JF ambacho ni jawabu na ngao kubwa dhidi ya vita na mafisadi na uongozi mbaya. Ni kweli, lakini pia sisi wenyewe bado tuna mapungufu mengi ambayo yanaweza kuathiri uimara wa hiki chombo.

Labda tutumie umaarufu mpya tuliopata ili kuijenga JF iwe tayari kuwapokea hata Watanzania laki moja bila matatizo na pia kwamba pawe pa watu wa kila aina kuanzia vijana mpaka wazee. Matusi ndio linaweza kuwa tatizo kubwa ambalo lisipo tatuliwa baadhi ya watu wanaweza kuona JF hapawafai. Pia mafisadi wanaweza kuivamia JF na kutumia matusi kama njia ya kuwafanya watu wengi wasione tena umuhimu wa JF. Kuna haja ya kuwa na utaratibu wa kuzuia lugha ya matusi kutumika hapa JF. labda moderators wanaweza kuja na utaratibu mzuri, lakini njia iliyo nzuri ni kwa sisi wanachama kujitahidi
kuepuka matusi.

Naomba tusilewe na huu umaarufu mpya tulioupata na badala yake tukae chini na kuimarisha JF kifedha, kimaadili na kimapambano ili kiwe chombo ambacho kinaendana na matakwa ya Watanzania mbalimbali.
 
Sasa ili tuonekane sisi ni kweli wazalendo wa nchi hii na watu makini, naomba Mwanakijiji atuongoze tena kutoa tamko kwamba... sisi wanaJF tunashukuru kwa kurudi hewani lakini pia kwamba tunatambua kwamba wakati mwingine kwa uchungu wa hoja, tunafika kujadili hoja kwa hali ya emotions, hivyo basi member watakuwa wakizuiana kuhakikisha chombo hiki/taasisi hii inaendelea kuheshimika kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu...
 
Sasa ili tuonekane sisi ni kweli wazalendo wa nchi hii na watu makini, naomba Mwanakijiji atuongoze tena kutoa tamko kwamba... sisi wanaJF tunashukuru kwa kurudi hewani lakini pia kwamba tunatambua kwamba wakati mwingine kwa uchungu wa hoja, tunafika kujadili hoja kwa hali ya emotions, hivyo basi member watakuwa wakizuiana kuhakikisha chombo hiki/taasisi hii inaendelea kuheshimika kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu...

Nakupinga Kasheshe no need to do so . Kuwa hewani is our right ila wao kuanza kutubughudhi ndiyo dhahma inapo anza . Lakini sisi tuko sahihi na wao wana kiwewe .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom