JF Get Together Party kufanyika Kebby’s Hotel Jumamosi 25 Januari 2014, michango imeanza kupokelewa…

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,111
http://1.bp.blogspot.com/-3n9zUDPKyT...ty-massage.gif

Haya tena wadau wa JF.

Baada ya kufanya utafiti wanakamati tumeona kwamba Kebby”s Hotel ndio kuna gharama nafuu na masharti yao sio magumu ukilinganisha na kumbi nyingine.
Baadhi ya kumbi tulizopitia wanataka tulipie ukumbi kiasi cha kati ya 200,000 mpaka 250,000 na bei ya chakula na vinywaji ni ghali lakini pia hawaruhusu kuingia na vinywaji kutoka nje hususan Sprit, hivyo basi tumeona kwa mara nyingine hafla hii ifanyike katika hoteli hiyo ya Kebby’s.

Kwa mujibu wa makubaliano ya awali, Management imekubali kutupa ukumbi bure na chakula tutalipa kiasi cha shilingi 15,000 kwa menu ya Bites kwa kila mtu. Bei ya vinywaji ni ya kawaida sana na wataturuhusu kuingia na vinywaji vikali kama chupa tatu.

Kwa wale watakaopenda kulala hapo wametupa bei vyumba ya shilingi 100,000 kwa mtu mmoja na kama ni watu wawili yaani mtu na mpenzi wake au mke wake watalazimika kulipa shilingi 120,000.

Tumekadiria idadi ya chini ya watu 40 lakini kama idadi hiyo itaongezeka itakuwa vizuri.

Hapa chini nitaweka mchanganuo wa bajeti inayohitajika ili kufanikisha hafla hii:

Cocktail Menu kwa makadirio ya watu 40 watakaohudhuria.

MahitajiIdadiGharama Jumla
Ukumbi100
BitesKwa watu 40@15,000/=600,000/=
VinywajiKwa watu 40Beer 4 @3,000/=480,000/=
Mziki1@150,000/=150,000/=
Corkage kwa vinywaji vikaliChupa 3@15,000/=45,000/=
Jumla1,275,000/=


Kwa hiyo kwa makadirio ya bajeti hiyo kila mdau anatakiwa kuchanga kiasi cha shilingi 30,000/=

Michango inakusanywa na Mtambuzi na inaweza kutumwa kwa M-Pesa na Tigo Pesa kwa namba zifuatazo:

+255 752 729292 au +255 715 729292

Mpaka sasa tumeshapokea michango ya wana JF wafuatao:

1. Jiwe Linaloishi
2. Jeska
3. Mtambuzi
4. jouneGwalu
5. ladyfurahia
6. cacico
7. lara 1
8. Vin Diesel
9. Mwita Maranya
 
Last edited by a moderator:
lara 1 kuna ambao hatunywi byere,so ninaimani tutakuwa na "free zone" kwenye soft drinks.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nitume mchango wangu haraka. Ngoja kwanza nimtafute Charity. Shughuli uwe na unaye ongea naye.
 
Last edited by a moderator:
lara 1 kuna ambao hatunywi byere,so ninaimani tutakuwa na "free zone" kwenye soft drinks.

Huwa kuna juice. Mnakunywa hadi mnavimbiwa. Halafu amesahau kuwaambia kwamba kule juu gorofani kunakua na disco la kufa mtu.
 
Last edited by a moderator:
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom