JF Foundation: Let's start giving | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF Foundation: Let's start giving

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TANMO, Sep 9, 2012.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Wapendwa Wanajamii,


  Naomba nilete kwenu wazo la kuanzisha mfuko wa Jamii Forums (JF Foundation) ambao lengo lake kuu itakuwa ni kushiriki katika kusaidia watanzania wenzetu walio katika hali ngumu kimaisha kama Watoto Yatima, Akina mama wajawazito, na wale watoto wanaoomba omba mitaani.


  Napendekeza huu Mfuko uwe unashiriki aidha kusaidia kituo Fulani cha kulelea watoto Yatima ama tuwe tunapeleka misaada mbalimbali Mahospitalini kwa lengo la kuwafariji ndugu zetu wenye shida na mahitaji ambayo hawana uwezo wa kuyapata.


  Hivyo basi, napendekeza wanajamii wenzangu tuwe tunachangia chochote tulicho nacho (k.m pesa, mavazi, vyakula n.k) kisha vitu hivyo tuwe tunavipeleka kwa wahitaji. Napendekeza tufanye uteuzi wa wanajamii kadhaa ambao watakuwa wana organize hiyo michango na kisha kuiwasilisha kwa wahitaji kwa niaba ya Wanajamii forums. Pia wanajamii wote kwa ujumla, tuwe tunashauri ni sehemu gani tupeleke msaada ambao tutakuwa nao kwa wakati husika.


  Wakuu wangu naomba kutoa wito wa kushiriki katika kuleta mabadiliko japo kwa kile kidogo tunachoweza kujitolea.


  Naomba kutoa wazo.
  Mapendo,
  TANMO.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  wazo zuri.....wacha tusubiri mawazo zaidi........
   
 3. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja 100%
   
 4. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,857
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  naunga mikono na miguu hoja kwa 150%
   
 5. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ni hoja nzuri.. lakini kwa wanachama wa JF walivyotapakaa huku duniani sidhani kama 'management' itakuwa rahisi!
  Inaweza kuwa rahisi kama itaundwa kwa locations..let say walioko sehemu flani wajiorganize na kufanya hizi shughuli kwenye locality yao...Nina uzoefu flani..somewhere kwenye hizi forums tulishawahi jaribu kufanya hizi habari but ilishindikana cuz watu walichukulia kutofahamiana 'physically' kama advantage wakatafuna mpunga hatimaye idea ikafa.
   
 6. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeona mbali,
  ni vema kujiweka vikundi mahala ulipo ili kupunguza uwezekano wa mvurugano kati ya location moja na nyingine.
  Ila kama itajumuisha wana Jf popote pale walipo Duniani,basi wawepo watu maalum wa kupokea na kufanya shughuli ktk hyo Foundation.
   
 7. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wazo zuri
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  management ya fedha za michango itakuaje? Maswala ya fedha huwa mmmmh
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Kwenye jamii halisi tunazoishi ndiko kunakofaa kufanya vitu kama hivi, humu sidhani sana; wengi wetu hatupendi IR zetu zitambulike so hata kuifuatilia hii kitu inaweza kuwa ngumu!

  Kuna nafasi kubwa sana ya kufanya charity work hata individually!
   
 10. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Wakuu wangu kwa namna moja ama nyingine nakubaliana na mawazo yenu.
  Ni kweli penye wengi hapakosi mengi. Binafsi nilifikiria kuwa humu ndani wapo watu wanaojuana vyema na ni mambo mengi yamekuwa yakifanywa na hao watu na hakujawahi kutokea kudhulumiana.
  Pia nilifikiria kuwa Kama Bwana Max akikubali kuwa msimamizi mkuu wa foundation, kwa maana ya kuwa mpokeaji wa michango itaweza kujenga trust kubwa as (kuanzisha Jamiiforums pekee ni charity kubwa), hivyo uhakika wa lengo la foundation kufanikiwa utakuwa mkubwa.. Na wale watakaopewa jukumu la kusimamia shughuli zote za foundation watakuwa wana report kwa Max.

  Pia hilo la ku organize kikanda ni wazo zuri, na kama tukikubaliana kwa pamoja tunaweza kuitengeneza Foundation kikanda kisha wanakanda wawe wanapewa jukumu la kuripoti kuhusu wahitaji waliomo kwenye kanda yao na tukawa tunawasilisha michango kadri mahitaji yatakavyokuwa.

  Kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko tunayotaka.
   
 11. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  TANMO kumpa Max mzigo huu wa kusimamia hiki chombo inaweza kuwa big task..kwa sababu kama umemsoma kwenye mahojiano yake inaonyesha ana majukumu mengi sana..Ofcourse anaweza kusema mwenyewe pia. Lakini kumbuka issue kubwa ni anonymities..yaani wanachama wengi wa Jamii Forums hatufahamiani in physical. Na kitu kama Charity Organisation mnatakiwa mkae muunde Utaratibu na aina ya uendeshaji..sasa kama hamjuani hii kitu mnaifanyaje??

  Binafsi nadhani wanachama wenyewe wa JF kwenye sehemu husika wanaweza kukutana kama wakiamua na kukubaliana kuunda hizi foundations kwa kila sehemu walioko..Ili kupata authenticity ya JF wanaweza kuchagua Viongozi ambao wanaweza kuwasiliana na Utawala kwa ajili ya kutumia label pamoja na brands za JF. Kwa hiyo kina Max et al wanaweza kuwa facilitators tu lakini mipango ikawa inaamuliwa na JF members wenyewe kwenye locations zao!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  TANMO
  Ni wazo zuri. Na pia utaoata watu wengi sana watakaochangia na kusema ni wazo zuri ila utekelezaji wake utakuwa hafifu sana.

  Asilimia kubwa ya Watu hawawezi kuchangia uendeshaji wa JF wa maswala ya kila siku wa kufanikisha JF kuwa hewani, am abit persmistic kama watachangia hii foundation.
   
 13. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu, ni kweli unaoyasema na iwapo itaundwa kikanda angalau uwezekano wa kuiendesha kiufanisi utakuwa mkubwa zaidi as ni rahisi kwa wanachama kushikana mashati pale ndivyo sivyo inapojitokeza, manake ni rahisi kutafutana. Lengo hasa la kuwa na JF Foundation iwe ni kusaidia jamii, na sioni ubaya wowote iwapo itakuwa chini ya JF Management kiujumla, hata kama Max atakuwa bize si vibaya iwapo ata delegate majukumu kwa wengine.
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  hivi wajawazito nao wanahitahi msaada?

  Na hiyo foundation itasaidia eneo gani maana jf watu wamesambaa sehemu tofauti tofauti.
   
 15. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mike, nashukuru kwa hii changamoto, tusubiri maoni ya wadau tuone nini tunaweza kufanya.. Ni matumaini yangu kuwa iwapo tutafanikiwa angalau katika hili basi Jamii Forums itaweza kujipambanua zaidi kwa jamii kuwa siyo tu kijiwe cha porojo bali kijiwe cha wanamabadiliko.

  Lets anticipate for positivity....
   
 16. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Samahani nimetumia neno wajawazito kiujumla sana..
  Ila nilikusudia wale wajawazito ama wodi za akina mama wazazi wenye uhitaji wa misaada..
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Ni wazo zuri lakini napata wasiwasi na utekelezaji wake.
   
 18. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Katavi, ni nini hasa kinakufanya uwe na wasiwasi?
  Na kwa kuwa unaona ni wazo zuri, ni nini hasa kifanyike ili utekelezaji wake ufanikiwe?
   
 19. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni wazo zuri, suala kubwa is just walking our talks!!!!!!
   
 20. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  hongera kwa wazo lenye kuleta manufaa kwa jamii na TAIFA kwa ujumla.nasubiri maelekezo
   
Loading...