JF Female Politician Of The Year 2011

Je, Ni Nani Unampigia Kura Kuwa "JF Female Politician Of The Year 2011"?

  • Faiza Foxy

    Votes: 31 46.3%
  • Josephine

    Votes: 36 53.7%

  • Total voters
    67
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Mie huwa simkubali faiza lakini kwa hili anampita josephina kwa mbali kwa michango hapa jf faiza yuko juu.
 
Hebu kuisaidia tume basi wekeni sababu zenu zote hapa badala ya kuambiwa tu hastaili wakati kura zenu zimestahilisha.
Ukweli ni kwamba hajakidhi(hana sifa) vigezo vitatu ambavyo kwa mujibu wa Tume ni hivi vifuatavyo:

3. Anayependekezwa lazima kuwe na ushahidi unaoonyesha kuwa ni Mwana JF aliyebobea hasa kutokana na Threads alizozianzisha na pia post anazobandika. Vyote lazima viwe na impact chanya kwa wasomaji wa JF.

4. Awe ni mwenye uwezo wa kusimamia hoja zake na kuzijibu kikamilifu bila jazba na kwa umahiri wa hali ya juu pale ambapo anapata challenge toka kwa wachangiaji.

5. Awe ni mwenye ushawishi wa hali ya juu katika mabandiko anyochangia walau kwa muonekano wa wachangiaji kuunga mkono hoja zake.
 
Pole sana kwa usumbufu mheshimiwa Mwenyekiti.....

Kiukweli Josephine hajakidhi vigezo namba 3, 4 na 5.....Nadhani Ashadii(naye alipata kura 2 kama Josephine angefit hapa.....Hata Gaijin ama Regia(R.I.P) wangepewa tu nafasi ya kushiriki japo walikuwa ni washindi wa mwaka jana.....)

Kamanda Wangu

Shida ya zoezi kama hili ni kuwa hakuna anayezingatia vigezo. Hata ukimwambia member anominate jina moja ananominate zaidi ya moja nk.

Bado kuna mwingine atasema FF amepigwa BAN atolewe nk nk. nadhani challenge hizi zinatufanya tujipange vema siku za mbeleni ambazo nitakuomba uwe Mwanakamati alongside TANMO na Maxe kama mshauri.

Uliowataja:

AshaDii aliomba asishirikishwe zaidi kutoa nafasi kwa wengine
Gaijin haamini katika mashindano haya kabisa both last year na this year bado msimamo wake ni huo na hatuwezi kulazimisha.
Regia - alikuwa mshindi wa last Year. Kama ilivyokuwa kwa NN naye pia tumempa heshima ya kutokushiriki
Hata Mwanakijiji pia ameshinda kwa kura nyingi lakini toka last year aliomba wengine wapewe nafasi akiamini yeye mchango wake unatosha.

Sasa mawazo yenu kwa Kamati ni yapi? Tumwengue Josephine? Au Tusitishe kupiga kura na kufuta shindano? Au kuna maoni gani?
 
Bila chuki wala wivu naomba kusema wazi kabisa kwamba Dada yetu Josephine hajakidhi vigezo vya kuwa mwanasiasa bora hapa JF, inawezekana kwenye majukwaa huko mitaani anafanya vizuri.

Kiukweli kabisa nadhani AshaDii na Gaijin walistahili kuingia fainali. Sidhani kama FF alistahili pamoja na kuwa imara muda wote kutetea hoja zake lakini hana nidhamu na ndio sababu ya kupigwa ban za mara kwa mara.

Mkuu mheshimiwa mwenyekigoda wa 'NEC' ya Jf tafadhali liangalie upya hili, si suala la watu kutaja tu, bali pia tume ijiridhishe kama kweli anayetajwa anakidhi vigezo tajwa.
 
Kwa mara nyingine tena umefunguka na kusema unachokiamini. Muraaaa Big Up.
 
Kamanda Wangu

Shida ya zoezi kama hili ni kuwa hakuna anayezingatia vigezo. Hata ukimwambia member anominate jina moja ananominate zaidi ya moja nk.

Bado kuna mwingine atasema FF amepigwa BAN atolewe nk nk. nadhani challenge hizi zinatufanya tujipange vema siku za mbeleni ambazo nitakuomba uwe Mwanakamati alongside TANMO na Maxe kama mshauri.

Uliowataja:

AshaDii aliomba asishirikishwe zaidi kutoa nafasi kwa wengine
Gaijin haamini katika mashindano haya kabisa both last year na this year bado msimamo wake ni huo na hatuwezi kulazimisha.
Regia - alikuwa mshindi wa last Year. Kama ilivyokuwa kwa NN naye pia tumempa heshima ya kutokushiriki
Hata Mwanakijiji pia ameshinda kwa kura nyingi lakini toka last year aliomba wengine wapewe nafasi akiamini yeye mchango wake unatosha.

Sasa mawazo yenu kwa Kamati ni yapi? Tumwengue Josephine? Au Tusitishe kupiga kura na kufuta shindano? Au kuna maoni gani?
Tumwengue tuweke mwingine. Sijui hili la Ban kwa FF nalo litakuwaje manake naona Mwita Maranya amekuja nalo. Pia nakumbuka lilikuwa kwenye vigezo. Tukajaribu kulitetea lakini tukashindwa na kama ilivyo demokrasia basi washindi huchukua kila kitu; hivyo basi suala la Ban likawa ni kigezo cha kumwengua mtu.
 
Sasa mawazo yenu kwa Kamati ni yapi? Tumwengue Josephine? Au Tusitishe kupiga kura na kufuta shindano? Au kuna maoni gani?
Nimekuelewa Mheshimiwa Mwenyekiti.....

Ningekuwa mimi ningemuweka FaizaFoxy peke yake then ipigwe kura ya NDIYO au HAPANA kama ilivyofanyika kwenye category ya Kongosho......

FaizaFoxy ni zaidi ya Mwanasiasa......Anajenga na kutetea Hoja na anasimamia anachokiamini...

Pitia thread na post za Josephine hapa chini utakubaliana nami kwamba HASTAHILI KABISA kuwa JF-FPoY......J

https://www.jamiiforums.com/search.php?searchid=8031062

https://www.jamiiforums.com/search.php?searchid=8031074

Ni mtazamo tu ndugu Mwenyekiti....

Kazi njema

Bala.
 
Waliomnominate mpaka akawaacha wengine wengi unawaambiaje?
 
Ni wangapi wamemnominate?.....

Mkuu hivi unavijua vigezo vilivyotumika kumtangaza Baba wa Taifa kwa Mwanasiasa wa karne(ya 20)?....

Achana na Habari ya waliomnominate,Josephine HANA SIFA ya kuwa Mwanasiasa (wa kike) wa mwaka 2012..Sidhani kama Hiyo Tume yenu inamptisha yeyote aliyependekezwa bila kujiridhisha na vigezo mlivyoviweka pamoja na kupitia thread na post za nominees.....Nina uhakika Josephine amkuwa nominated kwa ushabiki/mahaba na si kwa vigezo tajwa hapo juu na katika hili hata wewe umekiri kwamba mmemuweka kwa sababu tu amepata kura 2 baada ya Ashadii na Gaijin kujitoa na baada ya kuonekana kwamba mpendwa wetu Regia alishinda mwaka jana......

Sidhani kama kulikuwa na haja ya kulazimisha kumuweka Josephine hata kama hana sifa/hakidhi vigezo.....Ni bora mngemuweka hata Binti Sayuni(Zion Daughter) aliyepata kura 1.....Huyu pamoja na kupata kura 1 anakidhi vigezo,ana sifa ya kushiriki katika category husika.......

JF siku zote ni Home of Great Thinkers....Ni sehemu ya watu makini ambao kwayo HOJA ni sehemu ya maisha yao ndani ya JF...Na kwa kiasi kikubwa kitu kinachoifanya JF iwe ni ya watu makini/Great Thinkers ni Jukwaa la Siasa...Hapa kila mtu anategemea kwamba JF Female/Male Politician Of The Year atakuwa ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa kujenga HOJA,kutetea HOJA zake na kuzichambua.....Anao uwezo wa kujibu HOJA kwa HOJA na si VIROJA.....

Kwangu mimi AWARD hizi za JF Male/Female Politician Of The Year ni kubwa na ya muhimu kuliko Award zote zinazotolea na JEC hapa JF so nategemea hata nominees na washindi watakuwa ni watu wa aina ya Mchambuzi, EMT, FJM, Mwita Maranya, Mzee Mwanakijiji, Gaijin, Regia, Ashadii na members wengine wote ambao ni mabingwa wa kujenga HOJA ndani ya Jukwaa la Siasa na majukwaa mengine ambayo huzungumzia siasa(Siasa ipo kila sehemu)......

Mheshimiwa Mwenyekiti Lengo langu hasa ni kuzifanya Tuzo hizi ziwe na HESHIMA inayostahili na si kingine.....

Pole sana kwa majukumu na Mungu akuzidishie nguvu maana kwa hakika kazi hii unaifanya kwa kujitolea tu na si vinginevyo.....

Tuko pamoja sana...Tunasubiri na Nominees wa kule kwenye Jukwaa muhimu la Michezo......Kazi na dawa

Bala.
 
Superman nakusalimu.
Nimesoma poster ya 24 kama ulivyosema.
Kwa kweli Gaijin ungemuweka tu .
Akikataa mwaka huu basi tungemchukua mshindi wa pili
Anapendwa na wengi na ni mwanasiasa mzuri kwenye mijadala yake.
 
mkuu hapa hakuna jema watu wanataka mtumie u-great thinker wenu wakati mliwapa nafasi ya kuchagua wakaoneakana wnaomtaka ni wengi zaidi, ingekuwa hivyo mngetuchagulia mshindi moja kwa moja ila mkaona umuhimu wetu sisi kama wadau, wanataka mfanye kama nec_ccm kumtangaza mshindi wanaomtaka wao badala ya aliyechaguliwa na wananchi, hili c vyema, kwa sasa mshindi apatikane tu ila wakati ujao watu watoe maoni tu kwamba tufanyeje,
ndo hivyo hivyo hata kwenye uchaguzi wa nchi watu hawapigi kura wansubiri wenzao wawachagulie baadae wanalalamika amepitaje pitaje huyu?, wakati wanaomhitaji ni wengi.
tuache unafki, tuheshimu mawazo ya wengi.
tukisema watu maarufu wasichaguliwe basi mzee mwanakijiji na regia hawakustahili, pia itawafanya watu wengine pia washindwe kujiunga na id zao za ukweli na hii itapunguza mvuto hp jf kwan tunahitaji sana waheshimiwa watupatie majibu ya maswali yetu wakati mwingine.
zoezi liendelee kama lilivyopangwa wakati tukiambiwa kupendekeze majina tujitokeze kwa wingi ili tuwachague tunaowataka
 
Superman nakusalimu.
Nimesoma poster ya 24 kama ulivyosema.
Kwa kweli Gaijin ungemuweka tu .
Akikataa mwaka huu basi tungemchukua mshindi wa pili
Anapendwa na wengi na ni mwanasiasa mzuri kwenye mijadala yake.

Tafuta post zake za 2010 na 2011 uone msimamo wake na aliyoandika . . . . .
 
Ni wangapi wamemnominate?.....

Mkuu hivi unavijua vigezo vilivyotumika kumtangaza Baba wa Taifa kwa Mwanasiasa wa karne(ya 20)?....

Achana na Habari ya waliomnominate,Josephine HANA SIFA ya kuwa Mwanasiasa (wa kike) wa mwaka 2012..Sidhani kama Hiyo Tume yenu inamptisha yeyote aliyependekezwa bila kujiridhisha na vigezo mlivyoviweka pamoja na kupitia thread na post za nominees.....Nina uhakika Josephine amkuwa nominated kwa ushabiki/mahaba na si kwa vigezo tajwa hapo juu na katika hili hata wewe umekiri kwamba mmemuweka kwa sababu tu amepata kura 2 baada ya Ashadii na Gaijin kujitoa na baada ya kuonekana kwamba mpendwa wetu Regia alishinda mwaka jana......

Sidhani kama kulikuwa na haja ya kulazimisha kumuweka Josephine hata kama hana sifa/hakidhi vigezo.....Ni bora mngemuweka hata Binti Sayuni(Zion Daughter) aliyepata kura 1.....Huyu pamoja na kupata kura 1 anakidhi vigezo,ana sifa ya kushiriki katika category husika.......

JF siku zote ni Home of Great Thinkers....Ni sehemu ya watu makini ambao kwayo HOJA ni sehemu ya maisha yao ndani ya JF...Na kwa kiasi kikubwa kitu kinachoifanya JF iwe ni ya watu makini/Great Thinkers ni Jukwaa la Siasa...Hapa kila mtu anategemea kwamba JF Female/Male Politician Of The Year atakuwa ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa kujenga HOJA,kutetea HOJA zake na kuzichambua.....Anao uwezo wa kujibu HOJA kwa HOJA na si VIROJA.....

Kwangu mimi AWARD hizi za JF Male/Female Politician Of The Year ni kubwa na ya muhimu kuliko Award zote zinazotolea na JEC hapa JF so nategemea hata nominees na washindi watakuwa ni watu wa aina ya Mchambuzi, EMT, FJM, Mwita Maranya, Mzee Mwanakijiji, Gaijin, Regia, Ashadii na members wengine wote ambao ni mabingwa wa kujenga HOJA ndani ya Jukwaa la Siasa na majukwaa mengine ambayo huzungumzia siasa(Siasa ipo kila sehemu)......

Mheshimiwa Mwenyekiti Lengo langu hasa ni kuzifanya Tuzo hizi ziwe na HESHIMA inayostahili na si kingine.....

Pole sana kwa majukumu na Mungu akuzidishie nguvu maana kwa hakika kazi hii unaifanya kwa kujitolea tu na si vinginevyo.....

Tuko pamoja sana...Tunasubiri na Nominees wa kule kwenye Jukwaa muhimu la Michezo......Kazi na dawa

Bala.

Mkuu Bala nakubaliana kwa sehemu kubwa sana na maelezo yako.

Kitu kimoja ninachokipingana nawe ni kuhusu FF.

Kimsingi FF alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja na kuzisimamia mwanzo mwisho. Tatizo lake ni moja tena kubwa sana, yule mama alikuwa hajiheshimu wala kuheshimu watu wengine, nidhamu yake ilikuwa mbovu sana hadi kupelekea kulambwa ban za mara kwa mara. Kwahiyo tukiruhusu watu wasiokuwa na nidhamu kupewa tuzo ni kama tutakuwa tunahamasisha watu wengine kutukana na kukashifu wenzio ili tu wajikusanyie ufuasi usiokuwa na faida kwetu kama jamii. JF lazima ionekane kuzingatia uadilifu wa washindi wake, hapo ndipo thamani ya tuzo hii itakapoonekana, vinginevyo itakuwa ni kupoteza muda na kushusha hadhi ya JF na tuzo yenyewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom