JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

Hahaa. Sikumbuki vizuri mazee. Inawezekana Sokoine.

Sokoine alikuwa anasifiwa eti Waziri Mkuu mwenye suti tatu, anarudia hizo hizo kila siku.

Hilo nalo tuliona hambo la kusifia.

..Dah!!

..kazi kweli.

..kwa hiyo mtu mtanashati alikuwa hafai kuongoza?
 
Kiranga, Jamaa mmoja alinisimulia, watu wenye maduka walikuwa wanatupa bidhaa kwenye mito kwa kuogopa kukamatwa.

Kama ni kweli, it is better he died early.
 
Hii ni kumbukumbu nzuri sana maana vijana wa siku hizi sijui hata kama wanafatilia mambo haya ya akina Sokoine au Abeid Karume.
 
Nakumbuka sana pale kanisani St Joseph akiwa amekaa katikati ya walinzi wawili benchi la pili kutokea mbele.

Akipenda kuvaa kaunda suit, alikuwa mtu mmoja mpole kwa muonekano wa nje.

Siku anafariki April 11 1984 nimetoka shule Forodhani nikaanza kusikia nyimbo za maombolezo, ilikuwa siku ya huzuni.

Naomba nikusahihishe kidg..Sokoine kafariki 12.04!hii ni siku muhimu kwangu!
 
Upanga kuna mtu aliokota boksi la dawa za kupigia mswaki jalalani, wahindi walitupa kwa kuhofia kuitwa walanguzi.
But kuna kitu kimoja huwa najiuliza.Ukiangalia Tanzania ya leo, Watanzania wenye asili ya Asia ndio wafanyabiashara wakubwa. Sababu huwa nadhani ni kwa sababu wao ni wafanyabiashara tokea miaka mingi hata kabla ya uhuru.

Sina tatizo na wao kuwa wafanyabiashara wakubwa.Ila huwa najiuliza

Kwa nini legacy hii imebaki pamoja na vita hiyo waliyodai ni dhidi ya "wahujumu uchumi".Je ni kweli walifanikiwa kuzuia biashara binafsi kama watu walewale bado ndio wafanyabiashara wakubwa?

Mliokuwepo enzi hizo mnaweza kutupa picha.
 
Idiot Embicile,

..kwanza MKOLONI alikuwa akiwapiga vita Waafrika / "natives" wasijiingize ktk biashara.

..kwa mfano, kulikuwa na SHERIA ya Kikoloni iliyokuwa ina-discourage mabenki au mtu yeyote kumkopesha Mwafrika au " native. "

..Kwa hiyo Wazungu walitengewa nafasi za Utawala. Waasia wakatengewa nafasi za biashara. Waafrika / Natives wakatengewa nafasi za kuwa watumishi au manamba wa matabaka hayo mawili.

..Baada ya Uhuru mwaka 1961 ilitegemewa kwamba milango ya fursa itafunguliwa kwa Waafrika kuingia ktk nafasi za utawala, na biashara.

..Sasa kabla milango ya Waafrika kuingia ktk biashara haijafunguka vizuri, mwaka 1967 Mwalimu Nyerere akaleta AZIMIO LA ARUSHA na SIASA ZA UJAMAA.

..Kuanzia hapo kukawa na propaganda na vita kali kwamba shughuli za kiuchumi zifanyike kwa njia ya USHIRIKA / UJAMAA.

..Mtu aliyekuwa na shamba kubwa aliitwa KABAILA na kutuhumiwa kuwa ni MNYONYAJI na anayedhulumu waTz wenzake.

..Mwenye kiwanda au kampuni kubwa alitaifishwa mali zake maana huo ulikuwa ni UBEBARI. Kulikuwa hata na msemo kuwa " UBEPARI NI UNYAMA. "

..Mazingira hayo yalimuweka Mtanzania / native aliyekuwa na nia ya kufanya biashara at a disadvantage au yalim-discourage kwani serikali, chama, na jamii, ingemuangalia kwa jicho la mashaka-mashaka.

..Kwa wenzetu Waasia pamoja na kwamba walitaifishwa mali na majumba yao baada ya Azimio la Arusha, bado waliendelea kuwa na mitaji midogo na ya kati.

..Pia Waasia wengi familia zao zimekuwa ktk biashara for at least two generations. Kwa hiyo wao kuwa na ujuzi wa biashara ni sawa na sisi Waafrika kuwa na ujuzi wa kilimo au ufugaji shughuli ambazo tumezaliwa tumezikuta zikifanywa na babu, bibi, baba na mama, zetu.

..Mzee Mwinyi alipofungua milango ya biashara wenzetu Waasia tayari walikuwa na msingi wa mitaji, ujuzi, na maarifa ya kufanya biashara. Waafrika walioingia ktk biashara wengi walikuwa wanafanya hivyo kwa mara ya kwanza wakiwa hawana mitaji ya kutosha na maarifa au uzoefu.
 
JokaKuu, Nimekuelewa vizuri.

Nilichojifunza zaidi Kwenye comment yako ni kwamba, hiyo Vita dhidi ya wahujumu uchumi kama walivyodai haikufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

I think I'm right kufikiri hivyo.
 
Jamaa mmoja alinisimulia, watu wenye maduka walikuwa wanatupa bidhaa kwenye mito kwa kuogopa kukamatwa.

Kama ni kweli, it is better he died early.
NI wazi kuwa wapo watu wanaoishi kwa masimulizi ya mitaani. Bahati mbaya sana hatuna kada nzuri ya wanahistoria ambayo ingeweza kuangalia mambo ya kihistoria kwa mwanga wa historia. Kauli yako kuwa ni "it is better he died early" inaonesha siyo tu hujui historia lakini hujatumia muda kuchunguza kwanini aliliwa na watu wengi. Leo hii Magufuli anapewa ulinzi mkubwa sana na watu wengine hawaelewi kwanini..

Inshallah wiki ijayo ningependa nilete mjadala wa kuangalia kipindi kile cha 1980-1985 na kuwaonesha watu ni kwanini Tanzania ilipata bahati ya kuwa na Waziri Mkuu kama Edward Sokoine. Mambo mengi unayosimuliwa kuhusu Operesheni dhidi ya Wahujumu Uchumi na Walanguzi mengi yana chumvi nyingi lakini mengi pia yanatolewa bila muktadha mzuri wa kihistoria. Kuna mtu hapo nyuma amegusia kidogo. Nitajaribu kwenda ndani kidogo kuhusu hayo na labda utaappreciate nafasi ya Sokoine katika historia ya nchi yetu.
 
Nimekuelewa vizuri.

Nilichojifunza zaidi Kwenye comment yako ni kwamba, hiyo Vita dhidi ya wahujumu uchumi kama walivyodai haikufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

I think I'm right kufikiri hivyo.
Ilifanikiwa kupitiliza; tatizo kubwa ni kuwa wakati haya yanatokea Tanzania haikuwa na legal regime ya kushughulikia mambo haya. Hili ndilo lilikuwa tatizo kubwa zaidi. Hatukuwa tumewahi kupitia hali kama hiyo na complexities zake. Nchi nyingi (ikiwemo Marekani kwa mfano) zimewahi kupitia ugumu kama ule na wameshajifunza kiasi kwamba wana sheria nzito sana za kushughulikia walanguzi na wahujumu uchumi.
 
Ilifanikiwa kupitiliza; tatizo kubwa ni kuwa wakati haya yanatokea Tanzania haikuwa na legal regime ya kushughulikia mambo haya. Hili ndilo lilikuwa tatizo kubwa zaidi. Hatukuwa tumewahi kupitia hali kama hiyo na complexities zake. Nchi nyingi (ikiwemo Marekani kwa mfano) zimewahi kupitia ugumu kama ule na wameshajifunza kiasi kwamba wana sheria nzito sana za kushughulikia walanguzi na wahujumu uchumi.

On that note, I believe majority of forumers wamesimuliwa tu. Tanzania ile ya wakati huo hawaifahamu kabisa hata wakijaribu kuifikiria hawawezi kufahamu. Hivi wanafikiria ni kwa nini hadi leo hii wengi Afrika bado wanaongelea mafanikio ya baba wa Taifa mwl J K Nyerere? Wanafikiria vipi hadi leo hii kwa nini Moringe Sokoine anapewa heshima ya kuwa waziri Mkuu Bora ambaye hadi leo hakuna wa kulinganisha nae.

For their information Tanzania tumekuwa na mawaziri wakuu kama vile Kawawa, Msuya, Salim A Salim, Sumaye nk kwa nini Moringe? Je, uchumi wa Tanzania kwa nini hasa ulishindwa ku-take off wakati viongozi kama Mwalimu, Sokoine etc walikuwepo? Je, hawa Watanzania wa leo wanafahamu kweli maana ya kauli wanazoziandika kwenye mitandao? Je, ni kweli vijana wanaoandika kwenye mitandao ndio werevu wa kuivusha hii nchi kwenye next level?

Wale ambao hawakuona hata chembe wakati wa uongozi wa Nyerere wanatakiwa wajifunze vitu vitatu: 1. Tanzania tulikotoka 2. Tanzania tulipokuwa na kufikia, 3. Tanzania ya sasa, 4. Tanzania tunakoelekea au tunakotaka kwenda.
 
Mzee Mwanakijiji, Nakubaliana na wewe kwamba wanahistoria hawajaliweka vizuri hili suala.

Kuliliwa na watu sio shida, hata watu wabaya wauaji kuna watu huwa wanawalilia.

Anyway nasubiri huo uzi utakaouleta. Ninaomba katika huo uzi unisaidie kunijibu haya maswali huenda nikapata mwanga.

1. Kuna uhusiano gani Kati ya watu kumiliki mali halali na uhujumu uchumi?

2. Je serikali iliwahusisha vipi wananchi kuielewa na wakaikubali sera hiyo ya ujamaa?. Maana huwa naona kama ilikuwa imejaa ubabe ubabe tu na uvunjanji wa haki za binadamu.

3.Je Watanzania wa kawaida waliukubali ujamaa au walilazimishwa tu?
 
Ilifanikiwa kupitiliza; tatizo kubwa ni kuwa wakati haya yanatokea Tanzania haikuwa na legal regime ya kushughulikia mambo haya. Hili ndilo lilikuwa tatizo kubwa zaidi. Hatukuwa tumewahi kupitia hali kama hiyo na complexities zake. Nchi nyingi (ikiwemo Marekani kwa mfano) zimewahi kupitia ugumu kama ule na wameshajifunza kiasi kwamba wana sheria nzito sana za kushughulikia walanguzi na wahujumu uchumi.
Marekani ukizingua unafungwa pasipo kuangalia pato au jina lako.

R Kelly kakalia kaa la moto licha ya kipaji chake.

Wesley Snipes alishafungwa miaka ya nyuma.

Marafiki wa karibu wa Trump wapo jela muda huu.
 
..Nyerere alikuwa akimpenda nani zaidi kati ya Sokoine na Salim Salim?

..Mzee Kawawa hakuwa anautamani Uraisi.


..Kawawa alibebeshwa misalaba ya watu wengine na hakuwa na kinyongo.
Kawawa alimpenda na kumuamini Nyerere, Nyerere alimpenda na kumlinda sana Kawawa sababu ya ukaribu waliokuwa nao. Nyerere toka enzi hakuruhusu Kambona wala yoyote awaye amsumbue Kawawa, alimuita binadamu wa aina yake na duniani hapa watu wachache wanazaliwa na roho aliyokuwa nayo Kawawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom