JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,689
2,000
Dumila na Dakawa kuna umbali wa maili kama 22 ukiangalia google maps. Wami Sokoine ni jina jipya kutokana na ajali ile. My recollection ndio hizo na wakati ule hakukuwa na lami. Barabara ya lami haikupita baadhi ya sehemu kwa hiyo siwezi kubishana kwa hilo. Kwa hiyo alipata ajali Wami Sokoine.

Ndiyo

Dumila ni eneo jingine na Dakawa ni eneo jingine kabisa kama ilivyo Kibaha na Mlandizi au Chalinze na Bwawani
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,326
2,000
there is no such thing as public documents for public events

Paskali, ukibeba kakamera kako ka gulioni, ukaenda kwenye mkutano wa wazi wa Chama Cha TADEA ukawapiga video ukaondoka, hiyo ni mali yako milele!

Na kama kamera ilikuwa ni ya TBC, footage ni mali ya TBC milele!

Na kama ulikuwa uko kwenye masaa ya kazi ya Clouds Media lakini umebeba kamera mbili, yako na yao, hiyo ni mali ya Clouds Media milele, they don't care which camera you used!

You should know this better than anybody...

Ndio maana walikuwa wanamlaani Issa Michuzi, wakati ule wa shamba la bibi, awamu ya Kikwete, anachukua archive picha za kazini Daily News na Maelezo anapeleka Michuzi Blog, mali binafsi, sidhani kama bado anafanya vile vi ujanja ujanja any more... angeshafungwa Segerea

Hivi vitu vina haki miliki! Huwezi kuvikuta youtube bure bure!
Sijui mwenzetu unaishi dunia gani kwenye ulimwengu huu wa kidigitali. TV karibu zote zinarusha live streaming zao kwenye YouTube, hakuna copy rights restrictions zozote, kwa yoyote. Public events zinazorushwa live uajipakulia tuu na kujilia bila restrictions zozote.

Naendelea kusisitiza public events video hazina any restrictions duniani kote.

Usichangaye public events, copyright na mambo ya terms of services za waandishi na wapiga picha. Video yoyote kwenye public domain haina copyright, ila pia kuna copyright restrictions kwenye public domain mfano picha za Getty Images au National Geographic. Hata wewe, mimi, naweza kuweka restrictions kwenye video zangu la VOD zote ni free na hazina copyright restrictions.

P
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,037
2,000
Tunaposema elimu tuna maana gani? Isije ikawa ni lugha ya kiingereza.
Hapana, sina maana hiyo. Naelewa sana ninapozungumzia elimu kwa sababu mimi ni muumini mkubwa katika hilo.

Nikisema elimu kwa Kenya kuwa vizuri zaidi, nina maana ya hatua waliyopiga katika kutoa elimu kwa wananchi wao kiujumla. Sina maana ya kuwa wote wameelimika, hapana, wapo wengi ambao hawana elimu bado, hasa katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo kama Turkana na kwingineko. Lakini hata huko hatua zinazochukuliwa ni za kutia moyo sana.

Hiyo ni elimu kwa ujumla.

Hawa waliobahatika kupata elimu ya juu, kama vyuo vikuu, wana mwamko zaidi. Nadhani ushindani unawafanya kila mtu ajitutumue zaidi kuonyesha uwezo wao.
Katika ngazi hii pia, usidhani kuwa sijui ubabaishaji mwingi na utapeli walio nao baadhi ya hao wasomi. Lakini kwa ujumla wao, wengi ni watu wenye uelewa wa mambo kiasi cha kutosha. Hawa wakiajiriwa, wanao uwezo wa kujifunza haraka na kumudu matakwa ya mwajiri katika kazi zao.

Wasomi ngazi za juu, hawa hasa ndio msingi wa elimu ninayoizungumzia na kipimo ninachokitumia mimi ni kuangalia machapisho mbalimbali yanayofanyika katika majarada yanayochapisha tafiti katika nyanja mbalimbali. Hizi naziona mara kwa mara na habari zao kimataifa zinaonekana kwa hiyo sio jambo la kudhania tu.

Hapa kwetu namsoma mara kwa mara Mh Zitto, kwa makala zake zilizonyooka hata kama yaliyomo kwenye makala hizo siyo mawazo ninayokubaliana nayo. Tundu Lissu nimemsoma mara kwa mara, kwa maandiko usiyoweza kuyatilia shaka katika elimu yake. Bila shaka wapo na wengine ambao sijabahatika kuwasoma hata magazetini. Sijaona makala hata moja ya waziri yeyote. Ma-Profesa wetu huko kwenye vyuo vikuu, hata kwenye magazeti yetu tu wananchi wasome na kujua wasomi wetu wanayoyashughulikia.

Haya nayaona mara kwa mara katika magazeti ya majirani zetu. Hata kama huu sio ushahidi wa kuwa na elimu nzuri; lakini ina maana gani kama waliopata nafasi hiyo wasiitumie ipasavyo?

Hatuwezi kukataa lugha ya kiingereza kuwa kichocheo cha elimu, hata kama sio msingi wa elimu yenyewe.

Bila kukuchosha ngoja nikupe mfano unaoweza kukufikirisha katika hili swala la elimu, bila kujali lugha.

Ingia kwenye hii mitandao ya kijamii inayoruhusu watu kujieleza kwa ufasaha na kueleweka. Moja wapo ni hii yetu JF. Kule kwao, sijui ni mtandao gani, lakini nitoe tu mfano ingia kwenye gazeti lao la "The Star" ambapo wanatoa mawazo yao juu ya makala zilizoandikwa humo.
Wao wanaandika kwa Kiingereza, sisi kwetu tunaandika kwa lugha yetu adhimu. Bila kujali unyoofu wa lugha hizo mbili, soma tu maoni ya wachangiaji kuona uelewa wa wanayoyachangia na jinsi wanavyojieleza.

Haya mambo nimeyatazama kwa muda. Si utafiti wa hakika ninaoweza kufikia hitimisho la, lakini ni 'observation' inayonifanya niamini kwamba Kenya wanapiga hatua nzuri katika elimu. Hata ukiangalia bajeti yao tu ya elimu, inatosha kukuonyesha kwamba wapo makini na elimu yao.

Umenichokoza kwa mstari mmoja, nami nikaamua kukuandikia gazeti. Samahani sana.
 
Bu'yaka

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
1,471
2,000
Inawezekana huyajui sana mambo ya hakimiliki au hakiakili.

Naendelea kusisitiza public events video hazina any restrictions duniani kote.

Video yoyote kwenye public domain haina copyright

Okay, let me re-work my argument please, sorry for being fuzzy.

Zao la kazi, work product, ya mwanahabari au publisher au mmiliki wa chombo, ni mali yake anayoweza kwa utashi kuzuia isitumike na mwingine yeyote, popote kwa teknolijia yoyote.

Kwa hiyo raia huna haki kudai au kutegemea kupewa bure bure na Radio Tumaini au TBC au RTD archive ya clip ya hotuba ya mwisho ya Edward Sokoine kwenye uwanja wa wazi mjini Dodoma mwaka 1984 kabla hajafa, hata kama ilirushwa mubashara, bure bure, siku ya tukio .

Mnapinga?
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,326
2,000
Nakusaidia kuweka usahihi; nikwamba utingo/makonda walipokuwa wakiwaita abiria walikuwa wanatamka 'panda gari dola dola moja' matokeo yake neno doladola likaanza kupata hathari za kimatamshi nakuzaa daladala.
Neno Dala Dala limetokana na shilingi 5 iliyokuwa ikiitwa Dala baada ya noti ya shilingi 5 kuondolewa kwenye mzunguko ikaletwa coin ya pembe 5 ya dala.

Enzi hizo nauli ya UDA ilikuwa senti 60, ikapanda ikawa Shilingi 1, ndipo mabasi binafsi yakaanza kwa Chai Maharage. Nauli ikapanda kuwa Shilingi 250, nauli ya wanafunzi ikabaki 100. Ndipo kikaundwa chama cha wenye mabasi kikiongozwa na David Mwaibula na Muungano wa wenye dala dala Muwada kikiongozwa na George Ndaombwa wakafanya mgomo, ndipo nauli zikapandishwa kuwa shilingi 5, nauli ya wanafunzi ikabaki 100.

Huo ndio ukawa mwanzo wa mabasi kuitwa dala dala kufuatia wapiga debe kupiga debe la dala dala.
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,326
2,000
Okay, let me re-work my argument please, sorry for being fuzzy.

Zao la kazi, work product, ya mwanahabari au publisher au mmiliki wa chombo, ni mali yake anayoweza kwa utashi kuzuia isitumike na mwingine yeyote.

Kwa hiyo raia huna haki kudai au kutegemea kupewa bure bure na Radio Tumaini au TBC au RTD archive ya clip ya hotuba ya mwisho ya Edward Sokoine kwenye uwanja wa wazi mjini Dodoma mwaka 1984 kabla hajafa, hata kama ilirushwa mubashara, bure bure, siku ya tukio .

Mnapinga?
Hakuna mtu yoyote anatoa kitu chochote cha Bure kwa yeyote. Hoja ya Mzee Mwakijiji ni kwa vile enzi zile tulikuwa kwenye analojia na sasa tuko digitali, TBC ndio national achieve ya Audio Visual, akauliza kwanini hawajaamua ku digitize collections zao?.

Ukiisha digitize unaweza kutosha. Kwa taarifa yako TV zote ambazo zinarusha FTA, (Free To Air), content zao zote ni bure, hazina copyright for personal use, ila ukiomba video yoyote unaweza usipewe bure sio kwa sababu ya copyright but duplicating cost ndio maana uki digitize anybody can access freely.
P
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,037
2,000
Kimakusanyo kimapato Kenya wako juu zaidi yetu yanawasaidia angalau kupunguza utegemezi Wa bajeti yao hata ukitazama deni la taifa letu ni kubwa kuliko wao,Pesa yao inathamani,mauzo ya nje wako juu.Viwango vya uelewa angalau wako juu
...deni la taifa?
...mauzo ya nje?

Bajeti yao ni 'inflated' kwa sababu wanazozifahamu wao. Nusu ya bajeti hiyo inatumika kulipa madeni. Makusanyo ya mapato hayafikii lengo..., inalazimu wakakope kujazia

Hayo mawili ya mwanzo uliyoandika hapo juu hujui ulichoandika. Katafute takwimu uje hapa usahihishe upotoshaji wako..., hapo nitakuona wewe ni muungwana.
 
Ole

JF-Expert Member
Dec 16, 2006
2,159
2,000
Hapana, sina maana hiyo. Naelewa sana ninapozungumzia elimu kwa sababu mimi ni muumini mkubwa katika hilo.

Nikisema elimu kwa Kenya kuwa vizuri zaidi, nina maana ya hatua waliyopiga katika kutoa elimu kwa wananchi wao kiujumla. Sina maana ya kuwa wote wameelimika, hapana, wapo wengi ambao hawana elimu bado, hasa katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo kama Turkana na kwingineko. Lakini hata huko hatua zinazochukuliwa ni za kutia moyo sana.

Hiyo ni elimu kwa ujumla.

Hawa waliobahatika kupata elimu ya juu, kama vyuo vikuu, wana mwamko zaidi. Nadhani ushindani unawafanya kila mtu ajitutumue zaidi kuonyesha uwezo wao.
Katika ngazi hii pia, usidhani kuwa sijui ubabaishaji mwingi na utapeli walio nao baadhi ya hao wasomi. Lakini kwa ujumla wao, wengi ni watu wenye uelewa wa mambo kiasi cha kutosha. Hawa wakiajiriwa, wanao uwezo wa kujifunza haraka na kumudu matakwa ya mwajiri katika kazi zao.

Wasomi ngazi za juu, hawa hasa ndio msingi wa elimu ninayoizungumzia na kipimo ninachokitumia mimi ni kuangalia machapisho mbalimbali yanayofanyika katika majarada yanayochapisha tafiti katika nyanja mbalimbali. Hizi naziona mara kwa mara na habari zao kimataifa zinaonekana kwa hiyo sio jambo la kudhania tu.

Hatuwezi kukataa lugha ya kiingereza kuwa kichocheo cha elimu, hata kama sio msingi wa elimu yenyewe.

Bila kukuchosha ngoja nikupe mfano unaoweza kukufikirisha katika hili swala la elimu, bila kujali lugha.

Ingia kwenye hii mitandao ya kijamii inayoruhusu watu kujieleza kwa ufasaha na kueleweka. Moja wapo ni hii yetu JF. Kule kwao, sijui ni mtandao gani, lakini nitoe tu mfano ingia kwenye gazeti lao la "The Star" ambapo wanatoa mawazo yao juu ya makala zilizoandikwa humo.
Wao wanaandika kwa Kiingereza, sisi kwetu tunaandika kwa lugha yetu adhimu. Bila kujali unyoofu wa lugha hizo mbili, soma tu maoni ya wachangiaji kuona uelewa wa wanayoyachangia na jinsi wanavyojieleza.

Haya mambo nimeyatazama kwa muda. Si utafiti wa hakika ninaoweza kufikia hitimisho la, lakini ni 'observation' inayonifanya niamini kwamba Kenya wanapiga hatua nzuri katika elimu. Hata ukiangalia bajeti yao tu ya elimu, inatosha kukuonyesha kwamba wapo makini na elimu yao.

Umenichokoza kwa mstari mmoja, nami nikaamua kukuandikia gazeti. Samahani sana.

Tanzania tupo vizuri ki-elimu hilo nakuhakikishia. Watanzania wengi wamekuwa na kasumba tu kwamba ukiongea kiingereza vizuri basi wewe ni Gwiji, natolea mfano hili ambalo wewe umelikwepa kwenye ufafanuzi wako. Utendaji wa kazi nakuhakikishia leo hii hata nchi kama UK wanafunzi wengi sio vipanga jinsi unavyofikiria walivyokua shuleni, nashangaa Mbowe alikwenda kujaribu kusoma kule hakumaliza. Nimebahatika kusoma Tanzania na UK kwa hiyo basi nafahamu ninachokiongelea sio habari au porojo za kuambiwa.

Mfano UK wengi wanapomaliza masomo yao ambao ni native British sio wote ni vipanga. Ni wachache tu wanapoajiriwa hujituma na kuelewa kazi wanayoifanya na baada ya miaka miwili mitatu wanapata ile experience na kuwa wazuri na kujiendeleza kielimu sio ile ya darasani tu. Wanasema elimu haina mwisho. Kwenye kazi popote UK kwa mfano kuna training at least mara mbili kwa mwezi kutokana na kubadilika kwa sera na kuwaweka wafanyakazi kuzimudu kazi zao bila usumbufu. Yaani kwa mwaka at least unakuwa na training kama 5 zinazohusu mambo tofauti tofauti na kazi unazofanya. Hii inanikumbusha training wakati wa uchaguzi unaokuja, CCM walifanya training kwa makada wake lakini vyama vya upinzani hawakufanya kwa hiyo basi sio darasa la ndani tu linalo matter all kinds of training are required for you to be able to deliver the tangibles. Matokeo yake makosa mengi yametokea kwa wale ambao hawakufanya training.

Serikali hii kwa mfano sifahamu budget yake kwa sababu sijaangalia lakini kwenye awamu hii umeona kwanza wanatokomeza kukaa chini ya miti na kuwa na madawati nk na watoto wote ambao wanatakiwa kusoma wanasoma, kwa hiyo sina shaka hapo tunakwenda vizuri. Nilisoma zamani kidogo Tanzania lakini nakuhakikishia nilisoma shule za msingi kama 5 hivi kwa sababu ya kuhama na hata shule zote hizo za msingi nilizosoma sikukaa chini au kwenye mwembe hivyo nilishangaa sana kwenye you Tube kuonyeshwa kwamba kuna shule walikuwa wanakaa chini au kwenye mwembe (Hilo tuliache). Secondari nilisoma shule nzuri sana ambayo ilikuwa na hadhi lakini sio Dar.

Nafahamu wengi Watanzania hawana uwezo wa kulinganisha mataifa mbali mbali na jinsi wanavyojifunza nk lakini mfumo wetu wa elimu ni ule ambao tuliiga kutoka kwa Waingereza kwa maana hiyo hauna tofauti sana na Kenya , Uganda naweza kuthubutu hata kusema Zimbabwe na South Afrika. Cha msingi labda kinachokosekana Tanzania ni kuwapa waalimu training za mara kwa mara ili waendane na wakati. Vile vile lazima kujifunza kwa nchi nyingine kwa mfano kwa nini wanafanikiwa katika sekta flani flani nk. Kwa maoni yangu hakuna gap kubwa sana kati ya nchi hizo ambazo nimezitaja. Sikatai kuna improvements ambazo zinaweza kufanyika kwa sababu improvements ndizo zitatufanya tuwe perfect.

I hope my one liner did not infringe some hidden agenda.
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
16,478
2,000
Ni kweli yawezekana zoezi la kushughulikia wahujumu uchumi la kina Sokoine walengwa hawakuhujumu hata uchumi bali lilulenga kusimika mfumo wa kijama is nguvu za dola.
Nafikiri ni vizuri kwanza watu waelewe maana ya kuhujumu uchumi. Kuwa na pesa nyingi sio msingi wa wewe kuwa muhujumu uchumi. Mfano huyu raia wa Somalia aliyekiri kwamba aliikoseshea TRA 8 billion na amekubali kuilipa pamoja na kuwataja washirika wake.

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,037
2,000
Tanzania tupo vizuri ki-elimu hilo nakuhakikishia. Watanzania wengi wamekuwa na kasumba tu kwamba ukiongea kiingereza vizuri basi wewe ni Gwiji, natolea mfano hili ambalo wewe umelikwepa kwenye ufafanuzi wako. Utendaji wa kazi nakuhakikishia leo hii hata nchi kama UK wanafunzi wengi sio vipanga jinsi unavyofikiria walivyokua shuleni, nashangaa Mbowe alikwenda kujaribu kusoma kule hakumaliza. Nimebahatika kusoma Tanzania na UK kwa hiyo basi nafahamu ninachokiongelea sio habari au porojo za kuambiwa.

Mfano UK wengi wanapomaliza masomo yao ambao ni native British sio wote ni vipanga. Ni wachache tu wanapoajiriwa hujituma na kuelewa kazi wanayoifanya na baada ya miaka miwili mitatu wanapata ile experience na kuwa wazuri na kujiendeleza kielimu sio ile ya darasani tu. Wanasema elimu haina mwisho. Kwenye kazi popote UK kwa mfano kuna training at least mara mbili kwa mwezi kutokana na kubadilika kwa sera na kuwaweka wafanyakazi kuzimudu kazi zao bila usumbufu. Yaani kwa mwaka at least unakuwa na training kama 5 zinazohusu mambo tofauti tofauti na kazi unazofanya. Hii inanikumbusha training wakati wa uchaguzi unaokuja, CCM walifanya training kwa makada wake lakini vyama vya upinzani hawakufanya kwa hiyo basi sio darasa la ndani tu linalo matter all kinds of training are required for you to be able to deliver the tangibles. Matokeo yake makosa mengi yametokea kwa wale ambao hawakufanya training.

Serikali hii kwa mfano sifahamu budget yake kwa sababu sijaangalia lakini kwenye awamu hii umeona kwanza wanatokomeza kukaa chini ya miti na kuwa na madawati nk na watoto wote ambao wanatakiwa kusoma wanasoma, kwa hiyo sina shaka hapo tunakwenda vizuri. Nilisoma zamani kidogo Tanzania lakini nakuhakikishia nilisoma shule za msingi kama 5 hivi kwa sababu ya kuhama na hata shule zote hizo za msingi nilizosoma sikukaa chini au kwenye mwembe hivyo nilishangaa sana kwenye you Tube kuonyeshwa kwamba kuna shule walikuwa wanakaa chini au kwenye mwembe (Hilo tuliache). Secondari nilisoma shule nzuri sana ambayo ilikuwa na hadhi lakini sio Dar.

Nafahamu wengi Watanzania hawana uwezo wa kulinganisha mataifa mbali mbali na jinsi wanavyojifunza nk lakini mfumo wetu wa elimu ni ule ambao tuliiga kutoka kwa Waingereza kwa maana hiyo hauna tofauti sana na Kenya , Uganda naweza kuthubutu hata kusema Zimbabwe na South Afrika. Cha msingi labda kinachokosekana Tanzania ni kuwapa waalimu training za mara kwa mara ili waendane na wakati. Vile vile lazima kujifunza kwa nchi nyingine kwa mfano kwa nini wanafanikiwa katika sekta flani flani nk. Kwa maoni yangu hakuna gap kubwa sana kati ya nchi hizo ambazo nimezitaja. Sikatai kuna improvements ambazo zinaweza kufanyika kwa sababu improvements ndizo zitatufanya tuwe perfect.

I hope my one liner did not infringe some hidden agenda.
Eeenh, umesoma UK? Hongera zako mkuu!

Nakiri, nimekusoma na kuona jinsi uwasirishi wa hoja zako ulivyo makini vile vile.

Sawa, haya tuendelee na mengine, mkuu wangu.
 
  • Thanks
Reactions: Ole

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,991
2,000
Hakuna mtu yoyote anatoa kitu chochote cha Bure kwa yeyote. Hoja ya Mzee Mwakijiji ni kwa vile enzi zile tulikuwa kwenye analojia na sasa tuko digitali, TBC ndio national achieve ya Audio Visual, akauliza kwanini hawajaamua ku digitize collections zao?.

Ukiisha digitize unaweza kutosha. Kwa taarifa yako TV zote ambazo zinarusha FTA, (Free To Air), content zao zote ni bure, hazina copyright for personal use, ila ukiomba video yoyote unaweza usipewe bure sio kwa sababu ya copyright but duplicating cost ndio maana uki digitize anybody can access freely.
P

Hahahaa! Kaazi kweli kweli yaani!!

Nakupongeza kwa kuwa na moyo wa kuelewesha wengine, hata kama ni kama kumpigia gitaa mbuzi!
 
CalvinPower

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,552
2,000
Sawa, leta ukweli wewe kwenye hilo? Kwa nini mabasi hayo yaliitwa daladala? Nipo 110% right.
unadanganya mkuu, mabasi yaliitwa daladala kwasababu nauli ilikuwa sh 5.
na shilingi 5 ilipata jina la dla mda kabla ya usafiri huo kuwepo. ilikuwa inaitwa dala. kwasababu ya exchange rate ya dola kwa wakati huo , na noti ya sh 20 iliitwa paund.
kwahiyo chochote ulichokuwa unalipia kwa thamani ya sh 5 ulikuwa unaambiwa dala. na mabasi haya yalipoanza nauli iliwa sh 5. na yalikuwepo ya rahisi ila haya yalikuwa sh 5 na ikawa inaitwa dala dala.
 
CalvinPower

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,552
2,000
unadanganya mkuu, mabasi yaliitwa daladala kwasababu nauli ilikuwa sh 5.
na shilingi 5 ilipata jina la dla mda kabla ya usafiri huo kuwepo. ilikuwa inaitwa dala. kwasababu ya exchange rate ya dola kwa wakati huo , na noti ya sh 20 iliitwa paund. na shilingi 100 iliitwa soo ( soketi ) sijui kwanini na sijui kama ni wakati huo ama la maana mm nilikuwa siwezi kuishika nilikuwa denti.
kwahiyo chochote ulichokuwa unalipia kwa thamani ya sh 5 ulikuwa unaambiwa dala. na mabasi haya yalipoanza nauli iliwa sh 5. na yalikuwepo ya rahisi ila haya yalikuwa sh 5 na ikawa inaitwa dala dala.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,037
2,000
Hawana haki ya milele; usichanganye na trade marks!
"Trade mark" ya 'milele'; lakini "Brand" isiwe ya 'milele'?

Ile 'shape' ya chupa tu imelindwa 'milele', itakuwaje kilichomo ndani ya chupa kisiwe na haki ya kulindwa 'milele'.

Anyway, maana ya 'milele' inavyotumika hapa ni nini?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom