JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,717
2,000
Dube ni nani? Kuna wanaosema kifo chake kilipangwa

..jina kamili ni Dumisani Dube.

..Ni mkimbizi tuko Afrika Kusini aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Landcruise ambayo iligonga gari la Waziri Mkuu Sokoine na kusababisha kifo chake.

..inasemekana Dumisani Dube alikuwa akiendesha gari kwa kasi na alishindwa kutii maelekezo ya waongoza msafara wa Waziri Mkuu.

..inasemekana alipokaribia msafara wa Waziri Mkuu Dumisani Dube alijaribu kuukwepa msafara lakini gari lake " LILISEREREKA" na kugongana na gari lililokuwa limempakia Waziri Mkuu Sokoine.

..taarifa za wakati huo zinasema kutokana na impact Waziri Mkuu Sokoine alirushwa toka kiti cha nyuma na kwenda kujibamiza kwenye viti vya mbele au dash board, they were not very clear.

..msiba wa Edward Sokoine na msiba wa Raisi Samora Machel wa Msumbiji uliwagusa sana waTz. Ni misiba ambayo ilifuatana ktk kipindi kifupi.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,302
2,000
Rapper Jadakiss, katika wimbo wake "Kiss of Death" aliimba "controversy sells, but it ain't like death".

Akimaanisha, migogoro inasaidia kuuza rekodi, lakini kifo ndicho kinaweza kumpaisha mtu juu kabisa.

Kwa sababu mtu anapofariki, ndipo rekodi ya maisha yake inafungwa.

Tukirudi nyumbani, Waswahili walisema, hujafa hujaumbika. Ukiwa hai, kila siku unaendelea kuumbika. Unaweza kukosea kimoja rekodi yako yote ikaharibika.

I get the nostalgia angle. I get the "don't soeak ill if the dead angle". I reject all that.

If you go that route you will start to say Idi Amin was an angel.

I get the sympathy. Sokoine dies in action. Sometime ago. When there was virtually no press. In an enigmatic accident. Most of the kids here were not even alive.

Mimi nimepanga zike foleni za kulazimishwa kununua unga wa muhogo ili kuoata sukari ofisi ya CCM. Duka la Kaya. Unanunua kwa kusainiwa kitabuni. Those were some hard times.

Mnafukuzana na gari la ugawaji. Mjumbe wa nyumba kumi anakuwa kama demigod wa mtaa. Ujinga mtupu.

Sokoine ni mmoja kati ya watu waliotukwamisha kwa siasa mbovu za Ujamaa, kamatakamata, kuendesha nchi ki imla, ukali usio na mkakati, na ujinga mwingi uliojikita katika kukimbizana na walanguzi na wahujumi uchumi katika nchi qmbayo haina uchumi wa maana.

Sijawahi kumuona kama mtu mwenye mawazo ya kimapinduzi ya kuitoa Tanzania kwenye umasikini.

Alikuwa ni mmoja kati ya watu waliotuzungusha katika lindi la umasikini kwa kufukuza ndoto zisizotekelezeka za Ujamaa unaokinzana na Kujitegemea.

Ni muhimu tujue historia, hivyo uzi huu ni muhimu.

Ila hii cult of personality ya kumtukuza Sokoine kama mwanamapinduzi fulani, siioni kama inachunguza mambo kwa undani.
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
16,477
2,000
[QUOTE="Kiranga,
Fikra za wajamaa zinapokwama kuwaletea maisha bora wananchi ndipo uonevu unaopewa jina la " vita ya kiuchumi" huibuka ujambazi wa kidola huhalalishwa rasmi dhidi ya wananchi waliopata Mali kihalali.

Hiyo vita ya Sokoine ya uhujumu uchumi ndiyo ililenga kujenga mfumo primitive ya kijamaa na siyo kupambana na uhujumu uchumi.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,302
2,000
Fikra za wajamaa zinapokwama kuwaletea maisha bora wananchi ndipo uonevu unaopewa jina la " vita ya kiuchumi" huibuka ujambazi wa kidola huhalalishwa rasmi dhidi ya wananchi waliopata Mali kihalali.

Hiyo vita ya Sokoine ya uhujumu uchumi ndiyo ililenga kujenga mfumo primitive ya kijamaa na siyo kupambana na uhujumu uchumi.
Ni kweli.

Wakubwa wa vyama vya Ushirika walikuwa wanaiba sana, na Nyerere hakuwafanya kitu, sanasana alikuwa anawabadilisha kazi tu, anawatoa hapa, anawapeleka pale.

Sokoine pia hakuwagusa.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,029
2,000
Mimi natatizika mpaka Kichwa kinaniuma Kwa nini Sokoine apewe sifa Sana wakati wake mambo yalienda harijojo??
Ukitaka kujua na kuondokewa na huko "kutatizwa" kwako kwa nini "Mambo yalikwenda harijojo," kama usemavyo; na bado Sokoine aliendelea/anaendelea "kupewa sifa sana yeye," ni lazima ujue sababu za hayo mambo kwenda harijojo, na juhudi zilizokuwa zinafanyika kurekebisha.

Wananchi walielezwa na walijua kwa nini mambo yalikwenda yalivyokwenda wakati huo, na walijua kwamba sio Sokoine wala serikali aliyokuwa akiiongoza iliyosababisha 'harijojo'.

Uchumi sehemu zote duniani wakati huo ulikwama, ukianzia kwenye matatizo yaliyotokana na vurugu za wakubwa wa Magharibi na Mashariki,.

Vita vya Israel na waarabu na bei za mafuta kupanda sana. Na kama hayo hayakutosha, nasi tukapata mgogoro wetu hapahapa kwenye ukanda wetu, wa vita na Uganda. Hili lilitudidimiza sana; lakini hatukuwa na njia ya kuiepuka vita hiyo. Ilikuwa ni lazima tuipigane.

Na licha ya yote hayo - fahamu uchumi wetu ulikuwa unategemea nini - mazao yetu makuu yaliyokuwa yanatuingizia pesa za kigeni yalikuwa Kahawa, katani, pamba, Chai.

Bei za mazao yote haya wakati huo ilishuka sana. Brazil alichukua soko lote la kahawa, na mkonge, ukapata mshindani wa nguvu kweli kweli, 'synthetic fibres', nylon. Kamba za mkonge hazikuwa na wanunuzi tena, na magunia ya nylon ndio kila nchi iliyategemea. Mkonge ukafa kifo cha kibudu!

Chakula pia ikawa shida, kwa sababu ya ukame, kwa hiyo ikabidi kuangukia "yanga" wakati fulani. Lakini hakuna mTanzania aliyekufa kwa njaa. Pasingekuwa na juhudi nzuri na mipango mizuri iliyotumika, pengine historia yetu hadi sasa ingekuwa inaonyesha aibu ya waTanzania kufaa kwa sababu ya kukosa chakula. Hili pia inabidi ulielewe wakati unapojaribu kuelewa kwa nini waTanzania walienzi uongozi wao wakati huo.

Ukisikiliza kwa makini sauti za wanaolaumu, utadhani kuwa ni Tanzania pekee iliyokumbwa na matatizo ya kiuchumi wakati huo. Kenya walikula "Yanga", pamoja na kwamba wao ndio hutumiwa kama mfano wa mafanikio katika eneo hili letu kila tunapolinganishwa. Lakini unafuu waliokuwa nao Kenya pia unaelezeka sababu zake.

Sasa, kama kweli uliuliza swali kwa nia ya kutaka kujua, nadhani unaweza kuanzia hapo, na kuendelea kujijengea uelewa mwenyewe kwa kuchambua mbivu na mbichi kila unapokutana na mijadala ya aina hii.

Nitashukuru kupata 'feed back'.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,029
2,000
Kiranga,
So hard to resist the temptation to respond to all this.
Who said 'Ujamaa' was meant to bring about instant glory? Have never even seen an instantaneous development unleashed by capitalism anywhere!

It has taken the Chines decades, why was it expected to be different here?
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,302
2,000
So hard to resist the temptation to respond to all this.

Who said 'Ujamaa' was meant to bring about instant glory? Have never even seen an instantaneous development unleashed by capitalism anywhere!

It has taken the Chines decades, why was it expected to be different here?
Who said anything about instant glory?

And who said Tanzanians did not have glory in the midst of their abject poverty?

Indeed. What is glory?
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,717
2,000
Mimi natatizika mpaka Kichwa kinaniuma Kwa nini Sokoine apewe sifa Sana wakati wake mambo yalienda harijojo??

..ni sababu ya PROPAGANDA za wakati ule, na the fact kuwa amefariki.

..na amefariki kabla wananchi hawajapata nafasi ya kuchambua mitizamo yake na matokeo ya utendaji wake.

..na kwa mila zetu waTz ni mwiko kumkosoa marehemu.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,029
2,000
Who said anything about instant glory?

And who said Tanzanians did not have glory in the midst of their abject poverty?

Indeed. What is glory?
Well, I have no idea about all of the above! I guess we need to consult a dictionary, and may be we can find out about "having glory in the midst of abject poverty."
 

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,830
2,000
Na alifia kwa mabepari,ile policy ni ngumu sana kuiishi
Nimeona ameshuka kutoka kwenye Mercedes Benz made in Germany baba wa Capitalism.

Usiamini communist hata siku moja, Stalin na Mao waliuwa watu zaidi milioni 100 kueneza communism, Mwalimu Nyerere alikuwa anatibiwa London na siyo Soviet Union au China!
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,302
2,000
..hivi ni nani aliweka marufuku ya magari madogo kutembea jumapili baada ya saa 8 mchana?
Hahaa. Sikumbuki vizuri mazee. Inawezekana Sokoine.

Sokoine alikuwa anasifiwa eti Waziri Mkuu mwenye suti tatu, anarudia hizo hizo kila siku.

Hilo nalo tuliona jambo la kusifia.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,302
2,000
Well, I have no idea about all of the above! I guess we need to consult a dictionary, and may be we can find out about "having glory in the midst of abject poverty."
And therein lies the problem.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom