JF Exclusive: UVCCM Yajibu vikali Magazeti ya Raia Mwema na Mwanahalisi - Yasema Yamezua habari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF Exclusive: UVCCM Yajibu vikali Magazeti ya Raia Mwema na Mwanahalisi - Yasema Yamezua habari!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 24, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,379
  Trophy Points: 280
  Magazeti ya Raia Mwema na Mwanahalisi yalitoka na makala siku ya Jumatano ambazozilikuwa zinahusiana na kikao cha Umoja wa Vijana wa CCM Mwishoni mwa Juma lililopita. Makala hizo inaonekana zimegusa mishipa mibaya ya uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM na hivyo kumlazimisha Katibu Mkuu wa Umoja huo Bw. Shigela kutoa tamko kali lenye kufafanua baadhi ya madai ya magazeti hayo:

  Jisomee:
   

  Attached Files:

 2. m

  matawi JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Barua ya kihuni, ilitakiwa ikanushe kwa kila hoja kama ilivyoandikwa gazetini. Pili kama si kweli mbona hawaendi mahakamani ili wapewe haki yao?
   
 3. k

  kayumba JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Watanzania wana uwezo wa kuchambua, ipi pumba na upi mchele!

  Ole wenu mnaodhania watanzania ni mbumbumbu!
   
 4. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I support UVCCM
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  wanatapatapa kama mataputapu
   
 6. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mbona hawakukanusha lile bifu la Makamba na Shy - Rose?
   
 7. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pole yao UVCCM kwani hawakujua wanayoyasema humo ndani yatatoka kama walisemana kama kawaida yao hadi mambo binafsi. Basi wangejibu kwa msingi wa hoja na si kijumlajumla kama hivi. UVCCM K'njaro nao wamekuja na lao wanapinga Baraza kuu kweli ccm sasa maji shingoni kila mtu nalake
   
 8. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  wafikili hapa dunia kuna siri, hii watatafutana mpaka.Mwisho wake hakuna la maana litafanyika
   
 9. n

  nndondo JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  foolish young man what is he saying here? poor them kwa hiyo kama magazeti yamedanganya ya wenzao wa kilimanjaro je? pia wamedanya? shigela achague bega je ni wa kikwete ama lowassa? huku wataka na huku wataka utapasuka msamba mtoto mmeshaambiwa wenzenu hawawataki na watawatoa kabla ya 2012 mnatia aibu kuwageuza vijana safi wa CCM mandondocha kwa vishilingi mbili vya kubadili chupi mnavyopewa na mafisadi maana kama ni maisha yenu pia ya shida kama ya wengine
   
 10. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa katika barua yao sioni majibu badala ya kujikanyaga kwa viongozi wa ccm ikiwemo taasisi zao zote kazi namba moja ni kumlinda Mwenyekiti wao JK kwa njia yoyote awe sahihi au la kwa maana nyingine naweza kusema KUJIPENDEKEZA na sio masilahi ya walala hoi.Hiki ndicho kilichoifanya CCM kufikia na kuifikisha nchi hapa ilipo.HAWASOMI ALAMA ZA NYAKATI. kichekesho katika headed paper yao"KAULI YETU NI KULINDA NA KUJENGA UJAMAA"Hii ni kweli au wanakabiliwa na uhaba wa karatasi na hivyo wameamua kutumia za zamani? Hii inaonesha ni kwa kiasi gani wasivyo makini.TUSUBURI MENGI .
  Na kwa haya yafuaatayo watatujibu nini.Kufukuzwa kwa Sitta ulezi wa UVCCM na hili la Kilimanjaro.

  Daniel Mjema, Moshi
  MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Vunjo na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Aloyce Kimaro ameushambulia Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) akisema umepoteza mvuto huku akiufananisha na bua lililokauka linaloweza kusukumwa na upepo.

  Kimaro alisema hayo jana mjini hapa na kusisitizakuwa ameamua kujitokeza hadharani kutoa maoni yake akiwa mwanachama wa CCM. Alisema umoja huo unastahili kubeba lawama kutokana na vijana wengi kuamua kukiunga mkono chama cha upinzani cha Chadema.

  “UVCCM hauna nguvu tena, hivi wanataka viongozi wa CCM wawaogope kwa lipi? Hawana ushawishi tena kama wana nguvu waende UDSM (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) kama kuna vijana watawasilikiza,” alisema Kimaro.
  Kimaro alihoji UVCCM kilikuwa wapi muda wote wakati Serikali ya CCM ikihusishwa na ufisadi na kuongeza kuwa walipaswa kujitokeza wakati huo na kujibu mapigo, ikiwamo kuwataja wale wanaokipaka matope.

  “Leo baada ya mambo kuharibika ndiyo wanajitokeza, hivi jamii itawaaminije kama hawatumiwi na mafisadi? Tungewaona wako makini kama wangekuja na mkakati wa kuiimarisha CCM kabla ya 2015 na siyo kupayukapayuka tu,” alisisitiza.

  Kimaro alisema kitendo cha kumshambulia Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ni cha utovu wa nidhamu kwa sababu heshima ya Sitta mbele ya jamii ya Watanzania ni mara dufu ya heshima ya umoja huo.

  Mbunge huyo wa zamani ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu, alisema Sitta alipokuwa Spika wa Bunge alionyesha uzalendo wa dhati kwa nchi yake kwa kuongoza mijadala iliyokuwa na maslahi ya nchi... “Kupayuka payuka leo na kuwashumbulia viongozi wa kitaifa wa CCM na hata kuwapa ultimatum (ukomo) wa kuchukua hatua ni sawa na kumtisha mtu mzima kwa picha ya nyau (paka).”

  Kimaro alimtaka Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malissa na kundi lake kuacha kujifurahisha kwa kutoa matamko ambayo jamii haiyasikilizi na badala yake waweke mikakati ya kuurudishia heshima umoja huo.

  “UVCCM sasa hivi inamwakilisha kijana gani hapa nchini? Vijana wote wamekimbilia Chadema huku umoja huo ukitazama, halafu leo wanajifanya kumtafuta mchawi… waache usanii waje na mikakati,” alisitiza Kimaro.
   
 11. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Tulijua tu watakanusha kuwa hawajakanusha!
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sasa mbona maazimio ya kikao chao chenyewe mbona hajayataja popote huyu ndugu Shighela?? Ndio tuelewe kilichopotoshwa kipi na ukweli wa mambo ndio upi hasa basic on certain authentic documents za kutoka kwenye vikao vyao???
   
 13. K

  Kalila JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza umoja wenyewe umejaa wazee cdm inabidi muimarishe bavicha ili kuwapiga bao la kisigino huo umoja wa watoto wa vigogo
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Sioni cha maana walichojibu,labda utuwekee na hizo makala ili tuweze kujua ni nini hasa wanajibu/pinga.Ni one issue kama wanasema mwandishi kapachika maneno ambayo hawakuyazungumza(habari mpya),na its also another issue kama ni kweli walizungumza mambo flani kuhusu JK na wengineo ila wanapingana na utafsiri uliofanywa na magazeti hayo.

  So ni vyema kama tukipata walichosema kwenye kikao kilichopita vebartim.
   
 15. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hizi episodes za CCM sasa zinaanza kufanana na za Jerry Springer!
   
 16. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kwa kifupi ccm haina vijana! Hao ni marobot ya mafisadi. Once someone say something, mafisadi wana switch on halafu maneno yanawatoka hao watoto kama kaseti na hawana control maana they work after remote control. Poor them. Acha walumbane wakati cdm wanakijenga chama! Adui yako mwombee njaa. Sasa njaa ndio inawamaliza!
   
 17. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Wasubirie tu ndio kwanza mwanzo huu maana wanafanya watu hawana akili...Hiyo barua inaonesha wanajikosha na kutaka kuonekana hawana makosa......
   
 18. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mkuu MMKJJ, Nakushuru kwa taarifa nzuri, pia nikupongeze kwa kazi nzuri iliyotukuka, maana zikuzote umekuwa ukitumia jembe lako vyema, labda kama husinge weka hii barua pia wangejitokeza kukushutumu tena kama kawaida yao, labda safari hii tena wangetoa tamko la kupinga kuwa wao hawajapinga habari za magazeti husika! yanii ili mradi kuonyesha kuwa wewe ni muongo! lakini hata hivyo nasubiri waje wapinge kuwa hii habari yako ni ya uongo! la sivyo wanyamaze hadi milele na wakiri kuwa habari zako zote uwa ni za ukweli siku zote, au watasema hii ndiyo ya ukweli peke yake lakini zilizobaki zote ni za kuchochea uongo!? watakuwa wanafanya maigizo.

  CCM ya leo ina bahati mbaya kubwa sana, pamoja na kukosa viongozi waadilifu lakini pia haina tank la vijana wenye uwezo kiakili, maadili, na uweledi; kwa hivyo hawana hata sehemu ya kuchota viongozi wajao, hivyo ni lazima waondoke madarakani; mimi binafsi namfahamu sana Shigella na mwenzake Malisa, katika vijana wasio na lolote katika vichwa vyao naweza kusema ni hao wawili, Shigela yupo CCM siku nyingi anaipenda lakini bahati mbaya Mungu hakumjalia uwezo katika thinking, Malisa alijiunga CCM 2003/2004 haijui hata katiba ya CCM ni kwa vile Kijana wa Kikwete alikuwa anahitaji mtu zoba ambaye atakuwa kibaraka wake ndani ya umoja huo ndio maana walilazimisha Malisa kuwa M/kiti.

  Wakati Kikwete alipoona huyo Malisa hata pata hiyo nafasi walitafuta ujanja wa kuweka Mzanzibar ambaye walijua kuwa lazima watamtoa na baadae arudi kibaraka wao; Wakati ule Kikwete aliwaadaa wa Zanzibar kuwa safari hii nafasi hiyo ni yao, pia alitumia udanganyifu wa kuwa hilo ndilo suluhisho la kuepuka vurugu, lakini baadae wakamuanzishia Masauni zengwe na kumtoa sasa kama Kikwete alikuwa hawaadai wa Zanzibar mbona walipo mtafutia Masauni sababu ya kumng'oa hawaku muweka Mzanzibari kukaimu? wakamrudisha yule yule ambaye wakatika wa uchaguzi waliambiwa kuwa wakirusiwa kugombea Uwenyekiti kutazua vurugu?

  Hiyo UVCCM ni mali ya Kijana wa Kikwete ndio mwenyekiti na ndio Katibu, ila wanapoona sasa wanabaki kombo wanachanganyikiwa na kulalama kama chura. CCM kukosa vijana walionauwezo itawagharimu sana maana iwapo ikitokea kushindwa uchaguzi hawata weza kusimama tena Milele watajiunga na wenzao KANU ya Kenya.
   
 19. only83

  only83 JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
   
 20. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Hii ni taarifa kwa vyombo vya habari na siyo kwa umma..

  Mie ni bora hata magazeti wasiijibu kupitia gazetini...

  wamjibu huyo huyo jamaa...

  anyway "hagusiki"
   
Loading...