JF EXCLUSIVE: Sababu ya Kuachishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

Pasco
Mhando amesimamishwa kwa lipi maana barua zinaonyesha ni utovu wa nidhamu kwa katibu mkuu ili hali Radio na TV zinasema kwa sabavu ya ubadhilifu sasa lipi ni lipi

Pasco na ufahamu wako naomba nikuulize hizo barua kati ya Katibu Mkuu Maswi na MD wa Tanesco zimetolewa kama sehemu (attachment) ya barua ya kumsimamisha Mhando?
 
Leo kwa mara ya kwanza nimetambua kwamba , utetezi mwngi humu ni wa majungu na kutotambua facts za kila kinacho zungumzwa,nadhani sitaamini chohocte kinacho jadiliwa humu. Kwa mimi niliye fanya kazi na Mhando naweza sema, ni mhujumu mkubwa wa nchi hii na hafai na kama atatolewa ni jambo kubwa sana katika kuendeleza nchi hii katika masuala ya nishati ya umeme. Huyu mtu asikilizi mtu, wala hana muda wa kufanya kazi zaidi ya kusafiri na kukwepa wageni na wawekezaji wanao kuja kwa nia nzuri ya kuwekeza.KUna project nyingi zilikuja kwa ajili ya kuokoa hilo shirika lakini hakua na muda zaidi ya kukwepa nakukimbia officini huku shirika halina pesa. Kitendo chake cha kufanya mamamuzi bila kumshirikisha Katibu mkuu ni kutokana na yeye kutamba kwamba kapewa rungu na raisi ,kwa hiyo hakuna mtu naweza mgusa, baada ya raisi kumuamini huyu jamaa. Hakuna bifu ni kubweteka kwa huyu Mhando na ni janga la taifa kama atarudishwa hapo.

Mkuu pole sana, unategemea kwa maelezo yako ndiyo umetoa facts ambazo zitatushawishi kuamini kuwa Muhando anahujumu shirika. weka facts za maana siyo kuilaumu JF kwani wanaotoa mada ni members kama wewe wenye maoni na mawazo huu.

Kama umesoma maelezo ya mwanakijiji utagundua tatizo lipo wapi na hatakama ni tatizo ni Mr. Muhando bado serekali ya CCM na sera zake juu ya nishati ni hovyo tangu awamu ya tatu ya uongozi jambo ambalo viongozi hawataki kukubali, wanataka kuvuna wasichopanda huwezi kumfukuza mtu kwa maelezo eti hukumtaarifu juu ya mgao kipi ni cha dharura hapo kusolve tatizo au kutoa taarifa.
 
Wanajf wenzangu,
Kwanza asanteni kwa jf kutupatia hii exclusive, maana its a long time kupata kitu kama hii!.

Baada ya kusoma majibizano ya Mhando na Katibu Mkuu wake, nawaombeni tuwe wakweli kwa kukubali facts!. Mhando hajaonewa!, amepatiwa alichostahili kwa msingi mmoja tuu ufuatao.

1. Serikali inafanya kila kitu kwa mujibu wa taratibu, sheria na kanuni!.
2. Mhando aliambiwa kwa maandishi, kabla ya kuruhusu mgao wowote, ni lazima kwanza apate kibali cha maandishi toka kwa Katibu Mkuu.
3. Hii inamaanisha Mhando kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, hana mamlaka ya kuidhinisha mgao wa umeme, no matter what!.
4. Alipoona hali ni ngumu, alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu na kumjulisha situation ilivyo na nia ya kuanzisha mgao wa dharura.
5. Katibu Mkuu akamjulisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye nae angemjulisha mwenye (dhamana) nchi atoe idhini mgao uanze!.
6. Katibu Mkuu Kiongozi angetoa majibu hayo kwa Katibu Mkuu Nishati ambaye naye angetoa idhini kwa Mkurugenzi Mkuu Tanesco kuanzisha mgao!.
7. Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuidhinisha mgao ambao sio mamlaka yake, huu ni ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea hivyo alistahili adhabu ila siyo kali kiasi cha kusimamishwa!.
8. Kitendo cha kuidhinisha mgao kipindi cha kikao cha bunge bila kufuata taratibu za mgao, kinatafsirika kama ni "hujuma" dhidi ya serikali!. Hiki kinastahili adhabu kali kama hiyo aliyoipata na uchunguzi kuhusu authenticity ya mgao huo kama kweli ni wa dharura na ulikuwa hauepukiki unafuatia!. Ikidhibitika huo ulikuwa ni mgao shinikizo ili wabunge waijue hali halisi ya Tanesco!, the next step ni Mhando kupandishwa kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka!.
9. Ukiyasoma majibu ya Mhando kwa Katibu Mkuu wake, utagundua Mhando hakujibu alichoulizwa na badala yake analeta maelezo marefu ya kimepanda, kimeshuka!. Mhando ameulizwa maswali mawili tuu 1. Kwa nini ameidhinisha mgao bila kibali cha maandishi cha serikali 2. Kwa kwa kufanya hivyo kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu?. Alipoaswa kutoa sababu za udharura wa mgao huo lakini maelezo yake hayakuonyesha udharura wowote!.
10. Japo hili halikuelezwa, lakini kuna uwezekano pia kuwa Mhando aliidhinisha mgao huo bila kuiarifu bodi yake!. Kitendo cha mgao wa dharura wakati wa kikao cha bunge la bajeti, bodi ya Tanesco haijui!, Waziri wa Nishati hajui!, Mkuu wa nchi hajui!, its a sensetive issue!. Japo kusimamishwa kwa Mhando kumefanywa na Bodi ya Tanesco, ila amini msiamini ni kwa maelekezo kutoka Juu!. Huu sasa ni uthibitisho wa zile kauli za "dhaifu" na "kushindwa kufanya maamuzi magumu", zinajibiwa kwa vitendo ili ku proove si "dhaifu"!.

Mhando hakuonewa bali hiyo ni stahili yake!.

Pasco

Matransifoma ya umeme hayana muda wa kusubiri barua na maamuzi ya katibu mkuu yakiwa overloaded yanazima au yanapasuka .politic doesent work here
 
Huu mwaka mpaka uishe tutashuhudia mengi ya kushangaza,kila kukicha linakuja jipya kutusahaulisha yaliyopo! This country bwana..back to the topic..Tanesco ina matatizo ambayo haihitaji Masters kuyatambua! Thanks God Mungu anawaangaza! Unaweza kudanganya watu kwa wakati fulani lakini sio siku zote! Yangu macho na masikio...
 
Pasco na ufahamu wako naomba nikuulize hizo barua kati ya Katibu Mkuu Maswi na MD wa Tanesco zimetolewa kama sehemu (attachment) ya barua ya kumsimamisha Mhando?
Mo-Town na wengine, naingia miusa ya saa 3:30 nikitoka saa 5:00 nitawajibu kwa ufasaha ila Mhado hiyo ni stahiki yake!.
 
PASCO UMEJITAHIDI KUJIELZA Lakini siamini kama ulimaanisha Mhando angelingoja grid ianguke ili Maswi asimlime! Umeambiwa ule mgao ulikuwa wa dharura, na dharura haijawahi kufuata taratibu hata wakati moja! Mbinu za kukabiliana na dharura huwapo palepale site! Mhando katika maelezo yake kasema Aliwajulisha wanene wake wote kwa simu juu ya kilichotokea. Ulitaka aseme nini zaidi katika mazingira ya dharura?

Hivi dharura huko TANESCO hazina alert????? Definition ya dharura mimi naona kama ni hali inayohitaji sensors kuweza kujua au wao dharura ni nini kwa mfano???? Hawana indicators au sensors kweli??? kama ni mechanical collapse may be ........ if he was real he could go by the time wanakodi majenereta ya mafuta ambayo ilikuwa ni awkward case

Akufukuzaye hakuambii toka wakuu......kupewa jambo gumu kulifanya katika mazingira magumu ni bora kuacha kuliko kujaribu ilhali ukijua utashindwa.............
 
Pasco,umejitahidi sana kuitetea serikali na kutuamoinisha kuwa Mhando alistahili adhabu.

Nachokifahamu watendaji hawa wa Tanesco wanafanya kazi katika mazingira magumu sana,kwani katika mambo ya utaalamu siasa zinapoingia ni tatizo kunwa sana.

Naungana na wengi waliosema alipaswa kujihudhuru mapema sana.

Tatizo la viongozi hawa ni fadhila wanazopata katika nafasi zao Mf.Mhando anaenda kufanya check up na clinic nje ya nchi kila baada ya mda flani,bado anatunzwa kwa kununuliwa mahitaji makubwa na shirika hii ni hatari sana,watu wanaona hawezi kuachia nafasi zao.
 
Hivi bunge no Generator, no CCTV cameras du no any security systems. mtatuua CCM kwa uzembe huo sehemu nyeti ile. Estate manager wa Bunge naye ajiuzulu.
 
TANESCO na serikali yake wajue kuwa kusimamishwa kazi kwa DG huyo hakuwezi kumaliza tatizo la umeme nchini.
 
2. Mhando aliambiwa kwa maandishi, kabla ya kuruhusu mgao wowote, ni lazima kwanza apate kibali cha maandishi toka kwa Katibu Mkuu. Nini mamlaka ya CEO wa shirika la umma? kuanzisha mgao ni operations issue sio strategic ambayo ingebidi apate kibali kwa bodi na wizara. Mfano angeamua kuingia ubia au kuchukua mkopo mkubwa sana. Lakini kina cha maji kimepungua ghafla wewe unasubiri? Yaani nchi imevamiwa ghafla na ndege ya adui kikosi cha anga kinasubiri Amiri Jeshi Mkuu atoe amri ya kutungua? Kuna maamuzi ambayo mkuu wa zamu anapaswa kuchukua na kutoa maelezo baadaye.3. Hii inamaanisha Mhando kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, hana mamlaka ya kuidhinisha mgao wa umeme, no matter what!. Silly CEO wa nn?
4. Alipoona hali ni ngumu, alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu na kumjulisha situation ilivyo na nia ya kuanzisha mgao wa dharura. Sio lazima ilikuwa dharura simu ingetosha. Siku hizi kuna teknolojia sio kila kitu mpaka maandishi ndio maana hata barua tumeipata JF5. Katibu Mkuu akamjulisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye nae angemjulisha mwenye (dhamana) nchi atoe idhini mgao uanze!. Red tapes
6. Katibu Mkuu Kiongozi angetoa majibu hayo kwa Katibu Mkuu Nishati ambaye naye angetoa idhini kwa Mkurugenzi Mkuu Tanesco kuanzisha mgao!. Red tapes
7. Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuidhinisha mgao ambao sio mamlaka yake, huu ni ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea hivyo alistahili adhabu ila siyo kali kiasi cha kusimamishwa! Ni dharura.
8. Kitendo cha kuidhinisha mgao kipindi cha kikao cha bunge bila kufuata taratibu za mgao, kinatafsirika kama ni "hujuma" dhidi ya serikali!. Hiki kinastahili adhabu kali kama hiyo aliyoipata na uchunguzi kuhusu authenticity ya mgao huo kama kweli ni wa dharura na ulikuwa hauepukiki unafuatia!. Ikidhibitika huo ulikuwa ni mgao shinikizo ili wabunge waijue hali halisi ya Tanesco!, the next step ni Mhando kupandishwa kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka!. Bungeni ile ni hitalafu mbona vipaza sauti vilikuwa vinafanya kazi? Au vinatumia Maji? Kwa nini hawana back up system?
9. Ukiyasoma majibu ya Mhando kwa Katibu Mkuu wake, utagundua Mhando hakujibu alichoulizwa na badala yake analeta maelezo marefu ya kimepanda, kimeshuka!. Mhando ameulizwa maswali mawili tuu 1. Kwa nini ameidhinisha mgao bila kibali cha maandishi cha serikali 2. Kwa kwa kufanya hivyo kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu?. Alipoaswa kutoa sababu za udharura wa mgao huo lakini maelezo yake hayakuonyesha udharura wowote!. Ulitaka maji yaishe Mtera na mashine ziharibike ndio iwe dharura?10. Japo hili halikuelezwa, lakini kuna uwezekano pia kuwa Mhando aliidhinisha mgao huo bila kuiarifu bodi yake!. Kitendo cha mgao wa dharura wakati wa kikao cha bunge la bajeti, bodi ya Tanesco haijui!, Waziri wa Nishati hajui!, Mkuu wa nchi hajui!, its a sensetive issue!. Japo kusimamishwa kwa Mhando kumefanywa na Bodi ya Tanesco, ila amini msiamini ni kwa maelekezo kutoka Juu!. Huu sasa ni uthibitisho wa zile kauli za "dhaifu" na "kushindwa kufanya maamuzi magumu", zinajibiwa kwa vitendo ili ku proove si "dhaifu"!. Hatuihitaji bodi kama ni hivyo

Nakushauri Next time jaribu kuwa integrative zaidi katika kuchanganua mambo. Fahamu kuwa nje ya darasa the line btn operational na strategic issue si tu inategemea issue husika bali pia ni nyembamba sana kuliko maelezo.

Tanesco si shirika au kama kampuni ya bia kiwango cha public interest kwa Tanesco ni kikubwa kuliko maelezo. Na kwa maana hiyo sina uhakika kama unafahamu kuwa umeme ni strategic issue kwa nchi. Vile kwa darasani ni rahisi kusema kuwa kina cha maji kimepungua ghafla na sio ktk real life never...kina cha maji kinakuwa monitored na kupungua kwake haliwezi kuwa swala la dharura.
 
Tanesco inaendeshwa kisiasa zaidi badala ya kitaalamu, viongozi wa tanesco hawana uhuru wa kufanya kazi, hakika hali itakuwa mbaya zaidi siku zijazo kama hali itaendelea kuwa hivyo. Umeme kukatika bungeni ndiyo imemuondoka Mhando....!!!!?
 
Mhando hakutakiwa kusubiri hadi apigwe mkwara; alitakiwa ajiuzulu kazi na kugoma kama walivyofanya madaktari. Utaweza vipi kumkamua ng'ombe maziwa wakati halishwi?

Tukisema sera yao ya nishati ni mbovu watu wanasema "ooh siyo sera ni watu!"!
Mkuu MM,
Msamiati wa kujiuzulu kwa watumishi wengi serikalini haupo kwenye dictionary yao. Wapo radhi wafukuzwe na wadhalilishwe kuliko kuchukua hatua wao wenyewe.
 
Wanajf wenzangu,
Kwanza asanteni kwa jf kutupatia hii exclusive, maana its a long time kupata kitu kama hii!.

Baada ya kusoma majibizano ya Mhando na Katibu Mkuu wake, nawaombeni tuwe wakweli kwa kukubali facts!. Mhando hajaonewa!, amepatiwa alichostahili kwa msingi mmoja tuu ufuatao.

1. Serikali inafanya kila kitu kwa mujibu wa taratibu, sheria na kanuni!.
2. Mhando aliambiwa kwa maandishi, kabla ya kuruhusu mgao wowote, ni lazima kwanza apate kibali cha maandishi toka kwa Katibu Mkuu.
3. Hii inamaanisha Mhando kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, hana mamlaka ya kuidhinisha mgao wa umeme, no matter what!.
4. Alipoona hali ni ngumu, alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu na kumjulisha situation ilivyo na nia ya kuanzisha mgao wa dharura.
5. Katibu Mkuu akamjulisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye nae angemjulisha mwenye (dhamana) nchi atoe idhini mgao uanze!.
6. Katibu Mkuu Kiongozi angetoa majibu hayo kwa Katibu Mkuu Nishati ambaye naye angetoa idhini kwa Mkurugenzi Mkuu Tanesco kuanzisha mgao!.
7. Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuidhinisha mgao ambao sio mamlaka yake, huu ni ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea hivyo alistahili adhabu ila siyo kali kiasi cha kusimamishwa!.
8. Kitendo cha kuidhinisha mgao kipindi cha kikao cha bunge bila kufuata taratibu za mgao, kinatafsirika kama ni "hujuma" dhidi ya serikali!. Hiki kinastahili adhabu kali kama hiyo aliyoipata na uchunguzi kuhusu authenticity ya mgao huo kama kweli ni wa dharura na ulikuwa hauepukiki unafuatia!. Ikidhibitika huo ulikuwa ni mgao shinikizo ili wabunge waijue hali halisi ya Tanesco!, the next step ni Mhando kupandishwa kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka!
9. Ukiyasoma majibu ya Mhando kwa Katibu Mkuu wake, utagundua Mhando hakujibu alichoulizwa na badala yake analeta maelezo marefu ya kimepanda, kimeshuka!. Mhando ameulizwa maswali mawili tuu 1. Kwa nini ameidhinisha mgao bila kibali cha maandishi cha serikali 2. Kwa kwa kufanya hivyo kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu?. Alipoaswa kutoa sababu za udharura wa mgao huo lakini maelezo yake hayakuonyesha udharura wowote!.
10. Japo hili halikuelezwa, lakini kuna uwezekano pia kuwa Mhando aliidhinisha mgao huo bila kuiarifu bodi yake!. Kitendo cha mgao wa dharura wakati wa kikao cha bunge la bajeti, bodi ya Tanesco haijui!, Waziri wa Nishati hajui!, Mkuu wa nchi hajui!, its a sensetive issue!. Japo kusimamishwa kwa Mhando kumefanywa na Bodi ya Tanesco, ila amini msiamini ni kwa maelekezo kutoka Juu!. Huu sasa ni uthibitisho wa zile kauli za "dhaifu" na "kushindwa kufanya maamuzi magumu", zinajibiwa kwa vitendo ili ku proove si "dhaifu"!.

Mhando hakuonewa bali hiyo ni stahili yake!.

Pasco
Hapo kwenye no.8 na wewe unaona kuwa mgao haustahili katika kipindi cha bunge tu na wakati mwingine mgawo ni sawa tu? Hilo bunge linafanya nini cha maana sana katika uchumi hadi ionekane katika kipindi cha mkutano wao ndo mgao usiwepo? Mi nafurahi sana mgao uwepo wakati huu wa bunge ili nao waonje ladha ya mgao. Japokuwa wana majenereta lakini ndo kipindi muhimu kwani serikali itawajibika kwa kuahidi mwaka jana kuwa mgao utakuwa historia wakati bado ni tatizo. Hii inaonekana ni ukosefu wa mipango thabiti na sikubaliani na wote wanaodhani eti mgao ni sahihi kutokuwepo wakati wa bunge
 
Pasco bwana! Nakumbuka wakati uleee ukiendesha kipindi cha mada motomoto ama kitu kama hicho. Nakumbuka mdahalo wa wagombea Urais 1995 uliofanyika pale jengo la utamaduni wa Korea. Ulikuwa macjachari.

Mhando anasema alipiga simu kwa kuwa mgawo ulikuwa wa dharura! Hapa naona kuna hatari, kumbe TANESCO haina meno! Kumbe DG wa TANESCO ni ceremonial!

Kimbunga nikukumbushe tu bwana Pasco ndio chanzo cha jina KITI MOTO ambalo ni jina maarufu sana hapa Tanzania kwa sasa. Ninachotaka kusema ni kuwa hali ya mambo ndivyo sivyo. Hakuna matarajio ya mabadiliko makubwa katika chombo hiki cha Tanesco, kwakuwa kwa sasa Nishati ni chanzo kikubwa cha migogoro duniani na madili yake hayana tofauti kubwa na madawa ya kulevya, ila tu hii nishati ni halali. Vyanzo vingi vikubwa vya vita kwasasa Afrika ni nishati iwe kuni, mafuta, umeme n.k. hata wabadilishe wakurugenzi mara milioni, kama hakuna nia ya dhati ya kuboresha mfumo wa nishati, basi hakuna kitakachotokea. Na nia ya dhati ni serikali kuacha uvivu wa kuwaweka wawekezaji katika chombo hiki muhimu, mnaona uvivu wa kufikiri unavyowagharimu? Mbaya zaidi ninashawishika kusema udhaifu na uvivu huu unawafaidisha wachache walioko madarakani ndio maana hata maamuzi yao yako kibinafsi zaidi kuliko kiuzalendo na kiutaalamu. Ninatishwa na hali ilivyo kwenye chombo hiki haiwezi kuwa shwari leo wala kesho, mpaka mabadiliko ya kisiasa ya ndani au ya nje ya serikali (au ya kichama) yatokee na mapinduzi hayo yaje na nia ya dhati ya kubadili hali
 
Mkuu M.M Mwanakijiji et all..

Jana nilisikia kuhusu hili na nimeonelea ni vyema nikachangia machache baada ya kusoma Barua za SIRI. This is wehre I like JF

1.Hivi ni sheria gani ambao inamtaka mkurugenzi yeyote kuiharifu serikali kama kuna mgao wa dhararula? Dharula siku zote unaipredict vipi? Kama katibu alivyoelezwa kwa simu kwanini hakumuarifu KMK na rais pia kuhusiana na dharula? Je walisemaje? Au yeye kama katibu anaogopa maamuzi ambayo yatafuata?

2.Nahitaji kusoma Sheria ya TANESCO vyema ili kujua nafasi ya Bodi ipo wapi? Je kuna Gap lipi kati ya Bodi na wizara? .Kimsingi naamini katika kuyaachia Mashirika yawe huru katika kujiendesha na hapa MD alitakiwa kuileza Bodi then Bodi ingemweleza Rais kuhusiana na tatizo hili. Wizara iwepo kutengeneza sera na kusimamia utekelezaji wa sera za serikali na hii itasaidia separation of duty. Inapotekea wizara kuingilia utendaji wa mashirika inavuruga na ndiyo maana miradi mingi hainde mbele coz hawa ma-PS wanashadadia sana hizi agency ili wapige dili. Hili ni la kulibadilisha mara moja

3.Hivi kwanini Waziri anaweza kumsimamisha mtu kazi siku ya Jumamosi? Kwanini asingesubiri mpaka Jumatatu na hapa kwa mapendekezo yangu alitakiwa ashauriane na bodi kwanza then bodi ingemsimamisha kazi huyu MD.

TANESCO itaenda mbele kama serikali itafanya yafuatayo

1.Kwanza itengeneze sera mpya ya umeme ambayo itakuja na mkakati wa muda mrefu wa jinsi ya kutafuta njia mbadala za umeme na ikiwezekana tutatumiaje Gesi kufufua Umeme.Huu mpango uwepo na usimamiwe na wizara

2.TANESCO wachukue mradi na kutengeneza Financial framework na mkakati wa kitaalam wa jinsi watakaifanikisha sera ya serikali

3.Serikali waipe pesa TANESCO kwa kuanzia ili miradi ifanikiwe

4.Tujiandae mapema na issue ya gas
 
Siasa vs Utaalamu. Hivi kama kuna mgao wa umeme watumiaji hawana haki ya kupewa taarifa ya kabla? Nimeona katibu mkuu alitaka apewe yeye taarifa, ndio najiuliza vipi kuhusu watumiaji?
 
Kama nikafara au kafiri mim kwangu powa tuu.

Haiwezekan kila mwaka kwetu migao haiishi! Tuanzie hapa hatakama mhando kaonewa kwanin mgao bwana? Kama aliona anahujumiwa na katibu kwanin asing'atuke? Mjinga huyu tena sana tu...

Tunahitaji umeme si migao ya kipuuzi huku wao wakirindimisha migenerator kwa gharama za kodi zetu.
 
  • Duh hii ni zaidi ya hatari kuna baadhi ya idara/sekta siasa ingetolewa mambo mengine ni ya kitaalamu ss huyo katibu mkuu hata ngetaarifiwa mapema angetatua hilo tatizo wakati wao wenyewe ndo wanaoongoza kwa kulikopa shirika hilo???
 
Ndiyo yale yale ya kuwataka madaktari warudi kazini na kutoa huduma kwa wagonjwa huku wanajua kabisa CT Scan haifanyi kazi, X Ray machines zinasuasua na hata gloves zinapatikana kwa mbinde. Serikali inataka "optimal performance" lakini haitoi "Optimal cooperation"! Wanataka wavune wasichopanda!!!

Mhando hakutakiwa kusubiri hadi apigwe mkwara; alitakiwa ajiuzulu kazi na kugoma kama walivyofanya madaktari. Utaweza vipi kumkamua ng'ombe maziwa wakati halishwi?

Tukisema sera yao ya nishati ni mbovu watu wanasema "ooh siyo sera ni watu!"!


Umesema sawa, mhando lazima alipaswa kukaa pembeni mapema.

Ukisoma barua yake anaonekana ni mtu mwenye nidhamu ya uoga sana, anajinyenyekesha kupita kiasi na labda ndio maana watu wana-mtembelea hadi kichwani


kuna sehemu anasema yeye na menejimenti wanafanya kila kitu kuhakikisha huo mgao wa dharura unaondoka mara moja, aaah kumbe vipo vitu wangeweza kufanya kuzui mgao? kumbe ni uzembe tu? au ni uoga hadi anato ahadi zilizo nje ya uwezo wake?
 
Back
Top Bottom