JF EXCLUSIVE: Sababu ya Kuachishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

Wanajf wenzangu,
Kwanza asanteni kwa jf kutupatia hii exclusive, maana its a long time kupata kitu kama hii!.

Baada ya kusoma majibizano ya Mhando na Katibu Mkuu wake, nawaombeni tuwe wakweli kwa kukubali facts!. Mhando hajaonewa!, amepatiwa alichostahili kwa msingi mmoja tuu ufuatao.

1. Serikali inafanya kila kitu kwa mujibu wa taratibu, sheria na kanuni!.
2. Mhando aliambiwa kwa maandishi, kabla ya kuruhusu mgao wowote, ni lazima kwanza apate kibali cha maandishi toka kwa Katibu Mkuu.
3. Hii inamaanisha Mhando kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, hana mamlaka ya kuidhinisha mgao wa umeme, no matter what!.
4. Alipoona hali ni ngumu, alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu na kumjulisha situation ilivyo na nia ya kuanzisha mgao wa dharura.
5. Katibu Mkuu akamjulisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye nae angemjulisha mwenye (dhamana) nchi atoe idhini mgao uanze!.
6. Katibu Mkuu Kiongozi angetoa majibu hayo kwa Katibu Mkuu Nishati ambaye naye angetoa idhini kwa Mkurugenzi Mkuu Tanesco kuanzisha mgao!

mkuu Pasco
labda mimi naweza nisijue haya madaraka lakini kwa haraka sioni kosa la Mhando kuwa kitendo cha kuzima mitambo baada ya kuona kuna hatari ya kulipuka maji yanapo pungua kumbuka kuwa hii issue siyo ya kisiasa ni practical issue jaribu kufikiri kama mitanbo ingelipuka pindi Mhando anasubiri hicho kibali hali ingekuaje sasa ??

kosa ni la serikali ambayo haikutaka kutekeleza ahadi ya kudhamini mkopo wa bilioni 408 kama shirika lilivyo pia katibu mkuu kuidhinisha mgawo sioni logic yake kwani yeye siyo fundi hususani matatizo ya kiufundi yanapo jitokeza
 
Pasco
Mhando amesimamishwa kwa lipi maana barua zinaonyesha ni utovu wa nidhamu kwa katibu mkuu ili hali Radio na TV zinasema kwa sabavu ya ubadhilifu sasa lipi ni lipi
 
Acha Mungu akupe baraka zake muda apendao. Achana na hizi ajira zakuonyesha kadi ya chama kwanza!
 
2. Mhando aliambiwa kwa maandishi, kabla ya kuruhusu mgao wowote, ni lazima kwanza apate kibali cha maandishi toka kwa Katibu Mkuu. Nini mamlaka ya CEO wa shirika la umma? kuanzisha mgao ni operations issue sio strategic ambayo ingebidi apate kibali kwa bodi na wizara. Mfano angeamua kuingia ubia au kuchukua mkopo mkubwa sana. Lakini kina cha maji kimepungua ghafla wewe unasubiri? Yaani nchi imevamiwa ghafla na ndege ya adui kikosi cha anga kinasubiri Amiri Jeshi Mkuu atoe amri ya kutungua? Kuna maamuzi ambayo mkuu wa zamu anapaswa kuchukua na kutoa maelezo baadaye.3. Hii inamaanisha Mhando kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, hana mamlaka ya kuidhinisha mgao wa umeme, no matter what!. Silly CEO wa nn?
4. Alipoona hali ni ngumu, alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu na kumjulisha situation ilivyo na nia ya kuanzisha mgao wa dharura. Sio lazima ilikuwa dharura simu ingetosha. Siku hizi kuna teknolojia sio kila kitu mpaka maandishi ndio maana hata barua tumeipata JF5. Katibu Mkuu akamjulisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye nae angemjulisha mwenye (dhamana) nchi atoe idhini mgao uanze!. Red tapes
6. Katibu Mkuu Kiongozi angetoa majibu hayo kwa Katibu Mkuu Nishati ambaye naye angetoa idhini kwa Mkurugenzi Mkuu Tanesco kuanzisha mgao!. Red tapes
7. Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuidhinisha mgao ambao sio mamlaka yake, huu ni ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea hivyo alistahili adhabu ila siyo kali kiasi cha kusimamishwa! Ni dharura.
8. Kitendo cha kuidhinisha mgao kipindi cha kikao cha bunge bila kufuata taratibu za mgao, kinatafsirika kama ni "hujuma" dhidi ya serikali!. Hiki kinastahili adhabu kali kama hiyo aliyoipata na uchunguzi kuhusu authenticity ya mgao huo kama kweli ni wa dharura na ulikuwa hauepukiki unafuatia!. Ikidhibitika huo ulikuwa ni mgao shinikizo ili wabunge waijue hali halisi ya Tanesco!, the next step ni Mhando kupandishwa kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka!. Bungeni ile ni hitalafu mbona vipaza sauti vilikuwa vinafanya kazi? Au vinatumia Maji? Kwa nini hawana back up system?
9. Ukiyasoma majibu ya Mhando kwa Katibu Mkuu wake, utagundua Mhando hakujibu alichoulizwa na badala yake analeta maelezo marefu ya kimepanda, kimeshuka!. Mhando ameulizwa maswali mawili tuu 1. Kwa nini ameidhinisha mgao bila kibali cha maandishi cha serikali 2. Kwa kwa kufanya hivyo kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu?. Alipoaswa kutoa sababu za udharura wa mgao huo lakini maelezo yake hayakuonyesha udharura wowote!. Ulitaka maji yaishe Mtera na mashine ziharibike ndio iwe dharura?10. Japo hili halikuelezwa, lakini kuna uwezekano pia kuwa Mhando aliidhinisha mgao huo bila kuiarifu bodi yake!. Kitendo cha mgao wa dharura wakati wa kikao cha bunge la bajeti, bodi ya Tanesco haijui!, Waziri wa Nishati hajui!, Mkuu wa nchi hajui!, its a sensetive issue!. Japo kusimamishwa kwa Mhando kumefanywa na Bodi ya Tanesco, ila amini msiamini ni kwa maelekezo kutoka Juu!. Huu sasa ni uthibitisho wa zile kauli za "dhaifu" na "kushindwa kufanya maamuzi magumu", zinajibiwa kwa vitendo ili ku proove si "dhaifu"!. Hatuihitaji bodi kama ni hivyo
 
katika wale waliosimamishwa kazi tanesco yupo mmoja, Lusekelo Kasange, ninamfahamu ki-binafsi kabisa na ninaweza kuthibitisha kwa 100% kwamba sio fisadi hata kidogo!

kwamba wale watu wamesimamishwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha, na mmoja wa watuhumiwa ni Lusekelo Kasanga inanifanya niamini kwamba sababu ni hizo alizosema mtoa hoja, kwamba inawezekana na sababu za kisiasa bse ukiniamnbia Lusekelo fisadi, HAPANA ninafahamiana nae miaka mingi, najua maisha yake, najua tabia yake, najua misimamo, kwa sie tunaomjua tunajua kwamba sio fisadi!
 
Nini kilifanya kina cha maji kupungua ghafla tarehe 8 na 9 julai.
Ni kwa nini Mhando kasimamishwa kwa tuhuma za ubadhirifu na sio kudharau mamlaka?
Maelezo ya Mhando ni kuwa mafuta yalichelewa kufika kwenye mitambo ya Sio Mbio na Do One hivyo hawakuzalisha umeme matokeo yake matumizi yakaongezeka Kidatu
 
mkuu ungemuuliza PASCO engineer wa umeme? unajuaje huo mgao umeweza kusaidia kuzuia madhara makubwa zaidi kwenye grid ya taifa.... tungoje uchunguzi, tena wa kitaalam maana kama ni wa kisiasa tutakua kwenye matatizo makubwa zaidi
.
Pasco namfahamu, ni mwana JF wa siku nyingi, na toka nimepata kumfahamu katika mada zake nyingi ni mtu wa kutaka kuibua mijadala kwa maana kuwaona watu waki-debate. Kwa namna yoyote alichokifanya Mhando cha kuepusha umeme usikatike nchi nzima ni cha kizalendo na cha kuonesha ukomavu wa kiuongozi, yaani kuchukua maamuzi magumu, fupa linalowashinda viongozi wa Tanzania. Madhara yangekuwa makubwa zaidi kuliko yeye kupoteza kibarua, Hilo hata halihitaji tume. Fikiria mahospitali mangapi yangeathirika, viwanda n.k. Alifika mahali(Mhando) akasema LIWALO NA LIWE, wachache wakose, wengi wapate! Ripoti kila siku zinamfikia Katibu mkuu zikionesha tulipo na maangalizo kibao juu ya hali ya mabwawa! Urasimu! Jambo liko wazi Toa pesa, kama vipi Muulizeni Lowasa ile issue ya Mvua za wale waasia!
 
Pasco napata tabu kidogo kukuelimisha kuhusu hili jambo.
Taabu ninayopata kwanza naona inawezekana unashindwa kutofautisha mambo ya kiufundi na kisiasa.
Nitakupa mfano.
Gari inapochomoka matairi haiwezi kutembea hata kama tajiri mwenye gari hajatoa kibali kwa dereva cha gari isitembee.
Atakachofanya dereva cha kwanza ni 'kupaki' gari then maelezo mengine yanafuatia.

Ukisoma barua ya Katibu mkuu alichohofia yeye ni kuwa 'Serikali itashambuliwa bungeni' basi. Ingawa taarifa za mgao alikuwa nazo tena mapema(kumbuka alipigiwa simu).
Katibu mkuu hajasema lolote kuhusu utatuzi wa ki'technical wala ufumbuzi wowote wa kukabiliana na uhaba unaoikabili tanesco ambao naamini ndio ingekuwa suluhisho la mgawo huo wa dhalula. sio kusema tu SITISHA mgao na hali hujafanya jitihada zozote za kiufundi.

Tatizo siasa zinaingizwa kila sehemu hata zisipostahili.
Kama ningekuwa rais wa nchi hii kwanza ningepiga chini katibu wa wizara then mambo mengine ndio yangeendelea.

Thahks kwa ku simplify hii kwa Pasco.
Kitu kingine kama tatizo lilikuwa tu kwa umeme bungeni kipindi cha bugdet.. hivi office za bunge hazina standby genereta ambayo ina automatic change over switch, na hata backup UPS kuweza kuepukana na swala la even slightest power failure ni aibu kama ndo ukumbi upo upo tu. Kwa kifupi mimi naona huyu bwana katolewa kafara tu... inawezekana ana makosa yake ila kwa hili imetafutwa sababu ya ku msideline mambo yaende.
 
Wanabodi,

Nimesoma maoni tofauti juu ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, wengi wakitoa maoni kuwa amefanywa ni "mbuzi tuu wa kafara" katika "preemptive move" ili bajeti ya Nishati na Madini ipite!.

Mimi najikita kwenye facts only za kilichotokea, nini kilipaswa kufanyika na matokeo yake ndio haya ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuwajibishwa!.

Kabla ya kuusoma uzi huu, nakuomba sana, kwanza tembelea hii jf exclusive na uzisome hizo attachment kwa makini, ndipo uje unisome!.

Baada ya kusoma memo ya Katibu Mkuu Nishati kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco na majibu yake, nawaombeni sana tuwe wakweli kwa kukubali facts!. "Mhando hajaonewa!", amepatiwa alichostahili kwa msingi mmoja tuu ufuatao wa "kukiuka taratibu"!.

1. Serikali inafanya kila kitu kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni!. Mhando aliambiwa kwa maandishi, kabla ya kuruhusu mgao wowote wa umeme , ki "utaratibu" kwanza ni lazima apate kibali cha maandishi toka kwa Katibu Mkuu wake!.
2. Hii inamaanisha Mhando kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, hana mamlaka ya kuidhinisha mgao wa umeme, no matter what!.
3. Mhando alipoona hali ya umeme ni ngumu, na kuna ulazima wa kuanza kwa mgao wa dharura, "kiutaratibu" alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu wake na kumjulisha situation ilivyo na nia ya kuanzisha mgao huo wa dharura.
4. Katibu Mkuu angemjulisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye nae angemjulisha mwenye (dhamana) nchi atoe idhini mgao huo wa dharura uanze!.
5. Katibu Mkuu Kiongozi angetoa majibu hayo kwa Katibu Mkuu Nishati ambaye naye angetoa idhini kwa Mkurugenzi Mkuu Tanesco kuanzisha mgao!. Huu ndio utaratibu ambao haukufuatwa!.
6. Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuidhinisha mgao ambao sio mamlaka yake, huu ni ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea hivyo alistahili adhabu ila siyo kali kiasi cha kusimamishwa!.
7. Kitendo cha kuidhinisha mgao huo bila kufuata taratibu na ikatokea ni kipindi cha kikao cha bunge la bajeti, kinatafsirika kama ni "hujuma" dhidi ya serikali!. Hiki kinastahili adhabu kali kama hiyo aliyoipata na uchunguzi kuhusu authenticity ya mgao huo kama kweli ni wa dharura na ulikuwa hauepukiki unafuatia!. Ikidhibitika huo ulikuwa ni mgao shinikizo ili wabunge waijue hali halisi ya Tanesco!, the next step ni Mhando kupandishwa kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka!.
8. Ukiyasoma majibu ya Mhando kwa Katibu Mkuu wake, utagundua Mhando hakujibu alichoulizwa na badala yake analeta maelezo marefu ya kimepanda, kimeshuka!. Mhando ameulizwa maswali mawili tuu 1. Kwa nini ameidhinisha mgao bila kibali cha maandishi cha serikali 2. Kwa kwa kufanya hivyo kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu?. Alipoaswa kutoa sababu za udharura wa mgao huo lakini maelezo yake hayakuonyesha udharura wowote!.
9. Japo hili halikuelezwa, lakini pia kuna uwezekano kuwa Mhando aliidhinisha mgao huo bila kuiarifu bodi yake!. Kitendo cha mgao wa dharura wakati wa kikao cha bunge la bajeti, bodi ya Tanesco haijui!, Waziri wa Nishati hajui!, Mkuu wa nchi hajui!, its a sensetive issue! na hatua hizo ndio impact ya sensetivity ya issue yenyewe.

Japo kusimamishwa kwa Mhando kumefanywa na Bodi ya Tanesco, ila amini msiamini ni kwa maelekezo kutoka Juu!. Huu sasa ni uthibitisho wa zile kauli za "dhaifu" na "kushindwa kufanya maamuzi magumu", zinajibiwa kwa vitendo ili ku proove si "dhaifu"!.

10. Kwa kuzingatia hayo, Mhando hakuonewa hata kidogo bali hiyo ni stahili yake!. Japo lazima nikiri kuna udhaifu mkubwa serikalini katika kufikia maamuzi ambayo yako based kwenye kufuata taratibu tuu ambazo sio sheria wala kanuni kwa mtu kufanya kosa moja dogo tuu likayafuta mema na mazuri yote Mhando aliyo ifanyia Tanesco!.
Pasco
Pasco Mayala, umeandika kwa kirefu na nimesoma katikati ya mistari hoja yako. Kimsingi, nakubaliana na wewe kwamba Bw. Mhando alifanya kosa kwa maana kwamba alifanya jambo kinyume na maagizo ya mamlaka iliyo juu yake. Sina uhakika sana na udharura wa mgawo lakini inawezekana Bw. Mhando hakuwa na jinsi ya kuanza mgawo kwa kufuata utaratibu kutokana na hali halisi iliyokuwepo. Jambo ninalojiuliza mpaka sasa sijapata jibu ni je, umeme unapokuwa kidogo kwa maana ya kutotosheleza mahitaji ya nchi nzima kwa wakati moja kuna muujiza gani wa kukwepa mgawo unaoweza kufanywa na Katibu Mkuu wa Nishati na Madini na Katibu Mkuu Kiongozi!!!?? Jambo hili linaweza kueleweka tu endapo tutakubaliana kuwa hitaji la mgawo halitakuwa la ghafla kwa maana kwamba linaweza kubashiriwa na kutafutiwa mkakati wa kulikwepa mapema. Katika mazingira ya namna hiyo, ni halali kwa TANESCO kumwandikia Katibu Mkuu Nishati na Madini na kumwomba kibali cha kuanza mgawo kwa baadaye. Inaweza ikatokea wakati mwingine mitambo inaharibika ghafla na kusababisha uhaba mkubwa wa umeme. Katika hali kama hiyo, TANESCO wanatakiwa kufanya nini kama siyo kuanza mgawo tu!!

Kwa upande mwingine, nakubaliana na wewe kuhusu namna serikali inavyoshughulikia masuala ya nidhamu kwa watumishi wake waandamizi kama wakuu wa
mashirika bila kujali rekodi zao za kutukuka zilizopita. Inawezekana lengo la serikali ni kuonyesha mbele ya umma kuwa sasa ipo seriou lakini serikali hii hii inalegalega kuchukua hatua stahili kwa masuala mazito na yanayohujumu nchi kwa kiasi kikubwa kama ya rada, EPA, n.k. Substandard hii ndiyo hii ndiyo inayolalamikiwa nawananchi wengi wa kila rika.

Mwisho, watumishi wa serikali na hasa wakuu wa idara na mashirika ya umma wanaofanya kazi kwa maelekezo ya serikali ifike mahali nao wajenge tabia ya kujiuzulu kwa hiari wanapoona mazingira ya kutekeleza wajibu wao ipasavyo yanakuwa magumu badala ya kusubiri kusimamishwa. Kwa namna hali ilivyo, ni jambo lililo wazi kwamba Bw. Mhando amekuwa katika hali ngumu ya kiutendaji kutokana na maagizo ya wakubwa yasiyotekelezeka lakini ameendelea kung'ang'ania tu mpaka imefikia hatua ya kusimamishwa.
 
Nasikia majuzi umeme ulikafika Bungeni wakati Prof. Tibaijuka anahitimisha hotuba yake ya budget ya wizara ya ardhi. Ndio hujuma hii?

yaani kitendo cha kukatika umeme bungeni ilikuwa ni aibu kubwa sana,Mhando alitakiwa kulijua hilo hata ikiwezekana kujaza maji kwa ndoo ilimradi umeme upatikane. tatizo hilo ndio linaonekana dharau na kuihujumu serikali.
 
What goes around comes around. Mhando alifanya mtima nyongo wa kumwondoa FO mahili ili amuweke mtu wake watafune vizuri hela ya Tanesco.

Uliza wafanyakazi husika...ukweli ni kwamba sababu kubwa ya mgawo wa umeme huwa inatengenezwa kwa lengo la kuzinufaisha kampuni binafsi zinazouzia umeme Tanesco.

Mo town nimeona mchangiaji mwingine ame toa hint kama hii ya uongozi mbovu wa huyu bwana, kunyanyasa HR Director na kumwondoa, na hii ya FO, una weza iweka wazi zaidi?
 
yaani kitendo cha kukatika umeme bungeni ilikuwa ni aibu kubwa sana,Mhando alitakiwa kulijua hilo hata ikiwezekana kujaza maji kwa ndoo ilimradi umeme upatikane. tatizo hilo ndio linaonekana dharau na kuihujumu serikali.

Mwanza, kama sababu ni hii watakuwa wamemuonea tena sana.... kwa sehemu muhimu kama bunge lazima uwe na proper power backup plan.. what if transformer tu iliyo karibu na hapo ingeungua.... kama ni hivyo anayehusika na maswala ya majengo na umeme pale bungeni ndio haswa wa kufukuzwa... na sio mkurugenzi wa Tanesco.
 

mkuu Pasco
labda mimi naweza nisijue haya madaraka lakini kwa haraka sioni kosa la Mhando kuwa kitendo cha kuzima mitambo baada ya kuona kuna hatari ya kulipuka maji yanapo pungua kumbuka kuwa hii issue siyo ya kisiasa ni practical issue jaribu kufikiri kama mitanbo ingelipuka pindi Mhando anasubiri hicho kibali hali ingekuaje sasa ??

kosa ni la serikali ambayo haikutaka kutekeleza ahadi ya kudhamini mkopo wa bilioni 408 kama shirika lilivyo pia katibu mkuu kuidhinisha mgawo sioni logic yake kwani yeye siyo fundi hususani matatizo ya kiufundi yanapo jitokeza

Double chriss Hapo kuna siasa zaidi kuliko kanuni za utendaji. Kushindwa kuidhamini Tanesco kupata mkopo ni hujuma, ili ionekane Tanesco imeshindwa kujiendesha hivyo iuzwe! Waigawane, kama walivyoanza maandalizi katika serikali ya awamu ya tatu! Kumfukuza Mhando, haitaongeza maji Mtera au kidatu! Ni lazima serikali itoe fedha, kwa kifupi serikali itimize wajibu wake kwa shirika na liachwe lifanye kazi kibiashara sio kisiasa!
 
katika wale waliosimamishwa kazi tanesco yupo mmoja, Lusekelo Kasange, ninamfahamu ki-binafsi kabisa na ninaweza kuthibitisha kwa 100% kwamba sio fisadi hata kidogo!

kwamba wale watu wamesimamishwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha, na mmoja wa watuhumiwa ni Lusekelo Kasanga inanifanya niamini kwamba sababu ni hizo alizosema mtoa hoja, kwamba inawezekana na sababu za kisiasa bse ukiniamnbia Lusekelo fisadi, HAPANA ninafahamiana nae miaka mingi, najua maisha yake, najua tabia yake, najua misimamo, kwa sie tunaomjua tunajua kwamba sio fisadi!

Mkuu binadamu huwezi kumuamini 100% na ukamtolea viapo sio malaika.
 
Sijui ndugu yangu umepata wapi huu uthabiti wa kusema serikali inafanya "kila kitu" kwa "mujibu wa taratibu, sheria na kanuni". Ingekuwa hivyo tusingefika hapa!!! Kama hujasoma ripoti ya CAG na ripoti nyingine serikali (watumishi wake) hawafanyi kila kitu kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, ni ukweli ulio wazi kuwa serikali inapaswa kutimiza majukumu yake kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, sasa kama sheria hizo, taratibu na kanuni zipo lakini hazifuatwi, hilo ni jingine. Huu ni mjadala wa "is" na "ought to be"!.
Kanuni au sheria inasemaje kuhusu mgao unaotokea kwa bahati mbaya? Kwa mfano, umeme unapokatika kwa ghafla kabla ya kuandika barua Mkurugenzi anatakiwa afanye nini au kanuni zina presume kuwa kila mgao utakuwa unajulikana KABLA na mkurugenzi?
Hakuna mgao wa bahati mbaya, umeme unapokatika ghafla hiyo ni dharura, mgao sio dharura bali ni delibarate move kuzima mitambo ya umeme kwa makusudi ili kupunguza matumizi ya maji kufuatia kupungua kwa kina cha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme.
No matter what? kanuni gani au sheria gani inasema hivyo? Kama tukikubali - for the sake of argument point yako ya 1 - tunaweza kuuliza ni sheria gani au kanuni gaini inayosema "no matter what" mkurugenzi lazima apate kibali kwanza kabla ya kuidhinisha?
Kuna barua ya awali ya Katibu Mkuu ambayo iliambatanishwa na ile memo, ambayo hapa jf haikuletwa, ikieleza "expressly" not "impliedly" kua kabla Tanesco haijaanzisha mgao wa umeme, lazima kwanza wapate kibali cha maandishi toka serikali kuridhia mgao huo!. Pia nakuomba utofautishe, sheria, taratibu na kanuni, sheria zinatungwa na bunge, kanuni zinawekwa kimaandishi, 'taratibu' no norms, sio lazima ziwe kimaandishi!, barua tuu ya Katibu Mkuu kumuelekeza DG wa Tanesco hawezi kuanzisha mgao wa umeme, bila kibali chake cha maandishi, inatosha kuwa ni taratibu!.
"Hali ngumu"? kwamba umeme umeshakatika na mgao umeanza au hali ngumu alipoona hakuna maji Mtera au mabwawa mengine? au alipoona hali ngumu kuwa serikali haijatoa udhamini wa mkopo wa hela za kununulia mafuta?
Kama nilivyokuambia, hakuna mgao wa dharura, umeme ukikatika ghafla hiyo ni hitilafu, mgao ni delibarate move na sio hitilafu.
Sijui kama umesahau kuwa serikali hii hii ilitangaza kusitisha kutoa udhamini kwa makampuni ya umma baada ya utaratibu huo kutumiwa vibaya hasa kwenye mfano wa .... Richmond na ATCL? Hiyo serikali haijui kuwa inahitaji kutoa dhamana hiyo kwa sababu jambo hilo siyo mara ya kwanza kuzungumzwa na mawaziri kulizungumzia hili. Kweli unafikiria serikali ilikuwa haijui kuwa ipo haja ya kutoa dhamana ya mkopo hadi Mhando aiambie rasmi baada ya Waziri (Ngeleja at the time) kulizungumzia hili hili?
Hili nalijua sana, na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, Mhe. ZZK, amelipigia kelele sana akiliita "Eyes On, Hands Off", mtangulizi wake Dr. Rashid alikuwa akitoa maonyo serikalini kwa maandishi kuwa nchi itaingia gizani!. Wajibu wa Mhando ilikuwa ni kutoa alert kwa maandishi kuwa kutokana na hali hii na hii, hiki kitafuatia!, na sio kuamua kuzima umeme bila taarifa ya maandishi!.
Kama hakuna umeme na mgao umejianzisha; huo mlolongo wa ukiritimba unaweza vipi kuzuia mgao; sema kwa mfano agizo linakuna na kusema "usianzishe mgao" Mhando anatakiwa kufanya nini wakati hana umeme wa kuzuia mgao kutokea?
Tunarudi kule kule, hakuna dharura ya mgao wa umeme, kiwango cha maji katika mabwawa kiko quatified na sio gues work, hivyo projections za kiwango hiki cha maji, kitaweza kuwasha mitambo kwa siku ngapi kipo, alichopaswa kufanya ni kutuma hiyo alert kwa wenye mamlaka kuwa kiwango cha maji kilichopo, kinaweza kuendesha mitambo kwa siku 7!, bila mgawo, nchini itaingia gizani jumla, wenye maamuzi ndio waamue zima mitambo ukoa umeme au acha tuutumie umeme uliopoi kwa hizo siku 7, halafu nchi iingie kwenye giza tororo!. Kuhusu issue ya mgao, mwisho wa mamlaka ya Mkurugenzi wa Tasco ni kushauri tuu mwenye mali na sio kumuamulia!.
Hivi ni wapi panasema sheria na kanuni inasema Mkurugenzi hawezi kuanzisha mgao kitu ambacho siyo "mamlaka yake". Katibu Mkuu ndio ametoa agizo hilo kwenye barua. Ukisoma majibu ya Mhando kasema wazi kuwa "mgao wa tarehe 10 Julai" ulitokea bila "kukusudiwa". Na kaelezea ilikuwa kuwaje mgao huo ukatokea.

Lakini cha kushangaza ni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara kasema tu kuwa asianzishe mgao bila kibali kutoka kwake; kwenye barua yake hapo juu (nikiassume kuwa ni ya kweli) Katibu Mkuu hasemi ni kipengele gani kinampa yeye prerogative ya kuruhusu kuwepo kwa mgao! Hakuna sheria wala kanuni aliyoinukuuu isipokuwa barua yake! Well, TUNAJUAJE kuwa Katibu Mkuu ana madaraka ya kuamuru Tanesco isianzishe mgao wa umeme bila ruhusa yake.

Kwa vile unaamini serikali "inafanya kila kitu" kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu - ni sheria, kanuni au taratibu ipi ambayo inampa madaraka katibu mkuu kuzuia kuanza kwa mgao au kusitishwa kwa mgao?
Mkuu Mwanakijiji, sio kila kitu lazima kiwekwe wazi, bali kwa kukusaidia tuu, mwenye kutoa kibali mgao uanze, sio huyo Katibu Mkuu, sio Waziri, sio Katibu Mkuu Kiongozi, bali ni "mwenyewe"!, kama ambavyo Bodi ya Tanesco ilivyomsimamisha Mhando, mnaoamini ni bodi, aminini hivyo!, aliyemsimamisha ni "yeye"!.
Kama hili lingekuwa kweli, kwanini Wakurugenzi wa TBC1 na wao hawachukuliwi hatua za kuhujumu serikali pale wanapokata matangazo Bungeni kwa "matatizo ya kiufundi"? kwanini hiyo isionekane pia kuwa ni hujuma? Lakini inaweza vipi kuwa hujuma kama ni ajali au jambo lililo nje ya uwezo wa mtu? Hoja ya hujuma haiingii akilini. Kwanini tusiseme serikali kwa sera yake mbovu ya nishati inalihujumu taifa na kujihujumu wenyewe. Kwani ni Mhando aliyeanda kuwaleta Richmond, Dowans au Symbion?
Naomba tofautisha kukatika umeme kwa hitilafu na kukatwa umeme kwa mgao!. Vivyo hivyo kukatika kwa matangazo kunakosababishwa na hitilafu na kuzimwa kwa mitambo ya matangazo kwa sababu zozote zile!.
Sijui kama ndugu yangu umesoma maelezo ya Mhando. Amesema hivi katika barua yake akijibu hoja ya udharura wa mgao uliotokea:

Julai 2012 (kuanzia majira ya saa 1 jioni) ulitokea kwa dharura na bila kukusudiwa. Kilichotokea ni kwamba kuanzia tarehe 8 na 9 kina cha maji katika bwawa la Kidatu kilishuka kwa kasi kubwa na hivyo kuhatarisha usalama wa miundo mbinu ya kufulia umeme katika kituo cha kidatu. Utakumbuka mara moja tarehe 10 Julai 2012 yapata saa 1 usiku nilikupigia simu kukuarifu juu ya hali hii na hata athari zake kwamba, hali hii ingepelekea kuwepo kwa mgao wa dharura wa MW 95. Taarifa hii nilimpa pia Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika.

Umesema hajajibu suala la udharura; ina maana -

- unakataa kuwa kina cha maji Kidatu hakikupungua kwa kasi sana kati ya Julai 8 na 9 mwaka huu?
- Kwamba kupungua huko hakukuwa tishio kwa miundombinu ya ufuaji umeme Kidatu?

Kama unakataa hilo ni wazi utakuwa unajua kama kina kilikuwa cha kiasi gani kule kwa siku hizi mbili ambazo zilitangulia mgao wa Julai 10. Lakini zaidi tumeambiwa kuwa hakupuuzuia wajibu wake; utaona kuwa alitoa taarifa kwa Katibu na kwa Mwenyekiti wa bodi ASAP baada ya umeme kukatika. Ulitaka aandike barua usiku ule kumpa taarifa Katibu Mkuu ili imfike muda gani ili kuwahi asionekane amechelewa?
Hapa ndipo penye kosa kuu la Mhando "Kilichotokea ni kwamba kuanzia tarehe 8 na 9 kina cha maji katika bwawa la Kidatu kilishuka kwa kasi kubwa na hivyo kuhatarisha usalama wa miundo mbinu ya kufulia umeme katika kituo cha kidatu"
Baada tuu ya Mhando kulijua hili hiyo hiyo tarehe 8, na 9, alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu kumuarifu na kueleza nini kingefuatia!. Nimebahatika kusafiri na hawa wazee wetu toka wa Top mpaka buttom na najua huwa wanakuwa buzy na nini wakati wa usiku!, Masikini Mhando alijua kupiga simu kungetosha!, kiutaratibu kaambia ataeleza kwa maandishi, yeye hiyo hali ameiona tangu tarehe 8, alikuwa anasubiri nini asitume maandishi, na kuja kuwapigia simu usiku wakati wenyewe wako kwenye ... zao!, ulitegemea nini?.

Haya hata hayahitaji kujibiwa kwa kweli. Serikali isingekuwa dhaifu kusingekuwa na mgao!!! wala hizi barua zisingeandikwa.
Hii sasa ndio counter measure ya serikali tulio iita "dhaifu", imeanza to "hit them hard!" kuonyesha kinyume cha udhaifu, sasa tunaanza kupiga kelele nyingine kuwa kuwa mapigo are "too hard", or the "blows are too big!" or "too harsh!".
 
Duh!!!hii nayo kali
Ila bwana Mhando analizungumziaje suala la watumishi kuanzisha vitanesco vyao ndani ya shirika????kama kuna system fake za LUKU na zinauza token halali tokea zamani na uongozi wapo lazima kuna ka mtindio ka kiuongozi. I heard for the first time in 2004 kuwa kuna token za deal zinatokea TANESCO na mpaka juzi nimesikia amekamatwa mtu ana unit elfu kumi kwenye mita wakati kwenye system halali anaonekana amenunua unit 2000 tu kwa mwaka mzima. Mhando anaposema hakuna pesa na hakusanyi ipasavyo mi binafsi namwona ni another useless gamba as usual....vituo vilivyoko dsm vinatumia umeme bure na yeye anapretend kutojua...shame!!!! Kumlamba miguu Maswi hakuleti tija simamia haki na tekeleza wajibu wako...kama hupati ushirikiano sepa/resign kwa ukiondoka TANESCO utakufa????unaleta za akina PM kuwa he has done his very best wakati amefail na kuresign hataki!!!!!magamba mna shida nyie!!!
Mmmmmh
 
Mkuu binadamu huwezi kumuamini 100% na ukamtolea viapo sio malaika.

Ritz Umesoma hizo barua?

Sababu ni Mgao, huyo aliyewasimamisha anasema sasa ni kipindi cha bunge na kuruhusu mgao ni kutaka wao wawashiwe moto, soma barua ya huyo katibu, Imebandikwa hapa.

ninapata hisia kuwa sababu sio ubadhirifu wa fedha, nina uhakika mmoja wao sio badhirifu KABISA!
 
katika wale waliosimamishwa kazi tanesco yupo mmoja, Lusekelo Kasange, ninamfahamu ki-binafsi kabisa na ninaweza kuthibitisha kwa 100% kwamba sio fisadi hata kidogo!

kwamba wale watu wamesimamishwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha, na mmoja wa watuhumiwa ni Lusekelo Kasanga inanifanya niamini kwamba sababu ni hizo alizosema mtoa hoja, kwamba inawezekana na sababu za kisiasa bse ukiniamnbia Lusekelo fisadi, HAPANA ninafahamiana nae miaka mingi, najua maisha yake, najua tabia yake, najua misimamo, kwa sie tunaomjua tunajua kwamba sio fisadi!

kaka usimsemee mtu usije umbuka nani asiejua rushwa ya tanesco katika nchi hii, inawezekana asiwe fisadi ila kama ufisadi umetokea katika kitengo chake either awe anajua au hajui hiyo haimsadii asisimamishwe kupisha uchunguzi
 

mkuu Pasco
labda mimi naweza nisijue haya madaraka lakini kwa haraka sioni kosa la Mhando kuwa kitendo cha kuzima mitambo baada ya kuona kuna hatari ya kulipuka maji yanapo pungua kumbuka kuwa hii issue siyo ya kisiasa ni practical issue jaribu kufikiri kama mitanbo ingelipuka pindi Mhando anasubiri hicho kibali hali ingekuaje sasa ??

kosa ni la serikali ambayo haikutaka kutekeleza ahadi ya kudhamini mkopo wa bilioni 408 kama shirika lilivyo pia katibu mkuu kuidhinisha mgawo sioni logic yake kwani yeye siyo fundi hususani matatizo ya kiufundi yanapo jitokeza


Pasco kama watu wanafanya kazi zao vizuri kupungua kina cha maji kamwe si dharura...isipokuwa kwa muktadha wa business as usual period

WanaJF Wenzangu yuko sahihi...serikali haifanyi kazi anyhow ni lazima kuwe na taratibu. Haiwezekani kwa mamlaka ya juu kuwa uninformed na kinachoendelea kwa ngazi za chini. Sina shaka KM Maswi ameonyesha leadership sahihi kabisa na sio swala la kubebana...
 
Kazi ipo! lakini je hii hali ya watendaji kusimamishwa kila kukicha mpaka sasa imeleta mabadiliko kiutendaji? Mi naona kama kufurahisha kijiwe tu ilihali uozo unabaki palepale!
 
Back
Top Bottom