JF EXCLUSIVE: Sababu ya Kuachishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

Kama Mkurugenzi na Katibu Mkuu wanashindwa hata kupigiana simu wakajulishana juu ya mgao wa umeme basi uhusiano kat ya Wizara na Tanesco una matatizo makubwa kuliko inavyoonekana. Yaani Katibu Mkuu naye anausikia mgao kwenye vyombo vya habari!!!!

Ni Kwamba, Mhando huwa anatamba kwamba yeye kapewa mamlaka na raisi katika maamuzi ya Tanesco na hatakiwi kuingiliwa na Wizara.
 
Inasemekana hatua dhidi ya Mhando inatokana na woga wa waziri na katibu mkuu juu ya mjadala mkali unaotarajiwa kuibuka bungeni wakati wa kujadili bajeti ya wizara yao. Mhando anatolewa kafara kisiasa, lakini taarifa zinasema naye amejibu barua ya katibu mkuu kueleza jinsi asivyohujumu shirika hilo. Habari zaidi baadaye.


usifunike ukweli juu ya ubadhirifu na wizi wa kutisha unaonendelea tanesco na uteuzi wa Mhando kuwa kibosile pale uligubikwa na ufisadi na wala siyo stahiki yake watumishi wengi ndani ya tanesco wanapenda aje mgeni na badala ya mtu wa ndani ambaye ameshikwa na baadhi ya makundi................tuongolee tuhuma badala ya kuleta mkanganyiko usio na mwelekeo........
 
Mkuu wala usishangae, kuna wizara nyingine Katibu mkuu aelewani na Waziri hata waziri akitoa amri jambo fulani kufanyika Katibu mkuu anapuuzia tu au anafanya atakavyo! Kisa cha kutuniana misuri: "wote wanateuliwa na RAIS!" Bila ya kurekebisha suala hili la uteuzi wa viongozi wakuu Serikalini, uendeshaji wa utawala utakuwa mgumu sana.
Kama ndoa ya mitala vile, mke mdogo anamdharau mkubwa na mkubwa akimdharau mdogo maana wote wanaamini kuwa wanapendwa na bwana aliye waowa.
 
Nasikia majuzi umeme ulikafika Bungeni wakati Prof. Tibaijuka anahitimisha hotuba yake ya budget ya wizara ya ardhi. Ndio hujuma hii?

Aibu bungeni hamna stand by generator. Ideally the generator should be wired to automatically switch on power failure.
 
PASCO UMEJITAHIDI KUJIELZA Lakini siamini kama ulimaanisha Mhando angelingoja grid ianguke ili Maswi asimlime! Umeambiwa ule mgao ulikuwa wa dharura, na dharura haijawahi kufuata taratibu hata wakati moja! Mbinu za kukabiliana na dharura huwapo palepale site! Mhando katika maelezo yake kasema Aliwajulisha wanene wake wote kwa simu juu ya kilichotokea. Ulitaka aseme nini zaidi katika mazingira ya dharura?
Mkuu Hodogo, kama utaratibu unasema mgawo utaidhinishwa kwa kibali cha maandishi, maandishi ndio yanatakiwa na sii vinginevyo!.

Unaajiriwa taasisi sensetive za umma, kuna maeneo ya mamlaka yako na kuna maeneo ni mamlaka ya mkuu wa nchi. Iliamuliwa mgao ni mamlaka ya mkuu wa nchi!.

Sasa hivi tunayo serikali mtandao, mawaziri wote wana BB na I pads zinalipiwa na serikali 24/7!. Baada ya kuwarifu kwa simu, short sms zikifuatiwa na e-mails kwenye BBM zingefuatia kupata kibali!. Tanesco ni moja ya taasisi zibazongoza kwa mtandao makini humu nchini, very efficient,safe and secure!. Jamaa anajibu BBM hata akiwa kwenye....
Swali ni Mkuregenzi wa Tanesco kapata wapi mamlaka ya kuidhinisha mgao?!.

Mfano rais wa nchi ndio Editor in Chief wa Radio Tanzania, TBC na Magazeti ya serikali. Likitokea jambo lolote la dharura kulazimisha mitambo ya kurusha matangazo kuzimwa, lazima aarifiwe popote alipo na atoe ridhaa!. Vivyo hivyo ikitokea dharura yoyote kupelekea Daily News lisichapishwe huarifiwa kutoa ridhaa.

NB. Ridhaa hiyo haihusu jambo lolote la dharura ambalo ni technical kama hitilafu na umeme kuzima nchi nzima, hapa huarifiwa tuu kuwa kumetokea hivi na vile!. Mgao ni process inaotokana na alerts kama ambavyo Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco alivyoidhinisha internally ndivyo angepata udhini hiyo within the system.
 
Wanajf wenzangu,
Kwanza asanteni kwa jf kutupatia hii exclusive, maana its a long time kupata kitu kama hii!.

Baada ya kusoma majibizano ya Mhando na Katibu Mkuu wake, nawaombeni tuwe wakweli kwa kukubali facts!. Mhando hajaonewa!, amepatiwa alichostahili kwa msingi mmoja tuu ufuatao.

1. Serikali inafanya kila kitu kwa mujibu wa taratibu, sheria na kanuni!

Sijui ndugu yangu umepata wapi huu uthabiti wa kusema serikali inafanya "kila kitu" kwa "mujibu wa taratibu, sheria na kanuni". Ingekuwa hivyo tusingefika hapa!!! Kama hujasoma ripoti ya CAG na ripoti nyingine serikali (watumishi wake) hawafanyi kila kitu kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu.

2. Mhando aliambiwa kwa maandishi, kabla ya kuruhusu mgao wowote, ni lazima kwanza apate kibali cha maandishi toka kwa Katibu Mkuu.

Kanuni au sheria inasemaje kuhusu mgao unaotokea kwa bahati mbaya? Kwa mfano, umeme unapokatika kwa ghafla kabla ya kuandika barua Mkurugenzi anatakiwa afanye nini au kanuni zina presume kuwa kila mgao utakuwa unajulikana KABLA na mkurugenzi?


3. Hii inamaanisha Mhando kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, hana mamlaka ya kuidhinisha mgao wa umeme, no matter what!.

No matter what? kanuni gani au sheria gani inasema hivyo? Kama tukikubali - for the sake of argument point yako ya 1 - tunaweza kuuliza ni sheria gani au kanuni gaini inayosema "no matter what" mkurugenzi lazima apate kibali kwanza kabla ya kuidhinisha?

4. Alipoona hali ni ngumu, alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu na kumjulisha situation ilivyo na nia ya kuanzisha mgao wa dharura.

"Hali ngumu"? kwamba umeme umeshakatika na mgao umeanza au hali ngumu alipoona hakuna maji Mtera au mabwawa mengine? au alipoona hali ngumu kuwa serikali haijatoa udhamini wa mkopo wa hela za kununulia mafuta?


5. Katibu Mkuu akamjulisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye nae angemjulisha mwenye (dhamana) nchi atoe idhini mgao uanze!.

Sijui kama umesahau kuwa serikali hii hii ilitangaza kusitisha kutoa udhamini kwa makampuni ya umma baada ya utaratibu huo kutumiwa vibaya hasa kwenye mfano wa .... Richmond na ATCL? Hiyo serikali haijui kuwa inahitaji kutoa dhamana hiyo kwa sababu jambo hilo siyo mara ya kwanza kuzungumzwa na mawaziri kulizungumzia hili. Kweli unafikiria serikali ilikuwa haijui kuwa ipo haja ya kutoa dhamana ya mkopo hadi Mhando aiambie rasmi baada ya Waziri (Ngeleja at the time) kulizungumzia hili hili?


6. Katibu Mkuu Kiongozi angetoa majibu hayo kwa Katibu Mkuu Nishati ambaye naye angetoa idhini kwa Mkurugenzi Mkuu Tanesco kuanzisha mgao!.

Kama hakuna umeme na mgao umejianzisha; huo mlolongo wa ukiritimba unaweza vipi kuzuia mgao; sema kwa mfano agizo linakuna na kusema "usianzishe mgao" Mhando anatakiwa kufanya nini wakati hana umeme wa kuzuia mgao kutokea?

7. Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuidhinisha mgao ambao sio mamlaka yake, huu ni ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea hivyo alistahili adhabu ila siyo kali kiasi cha kusimamishwa!.

Hivi ni wapi panasema sheria na kanuni inasema Mkurugenzi hawezi kuanzisha mgao kitu ambacho siyo "mamlaka yake". Katibu Mkuu ndio ametoa agizo hilo kwenye barua. Ukisoma majibu ya Mhando kasema wazi kuwa "mgao wa tarehe 10 Julai" ulitokea bila "kukusudiwa". Na kaelezea ilikuwa kuwaje mgao huo ukatokea.

Lakini cha kushangaza ni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara kasema tu kuwa asianzishe mgao bila kibali kutoka kwake; kwenye barua yake hapo juu (nikiassume kuwa ni ya kweli) Katibu Mkuu hasemi ni kipengele gani kinampa yeye prerogative ya kuruhusu kuwepo kwa mgao! Hakuna sheria wala kanuni aliyoinukuuu isipokuwa barua yake! Well, TUNAJUAJE kuwa Katibu Mkuu ana madaraka ya kuamuru Tanesco isianzishe mgao wa umeme bila ruhusa yake.

Kwa vile unaamini serikali "inafanya kila kitu" kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu - ni sheria, kanuni au taratibu ipi ambayo inampa madaraka katibu mkuu kuzuia kuanza kwa mgao au kusitishwa kwa mgao?


8. Kitendo cha kuidhinisha mgao kipindi cha kikao cha bunge bila kufuata taratibu za mgao, kinatafsirika kama ni "hujuma" dhidi ya serikali!. Hiki kinastahili adhabu kali kama hiyo aliyoipata na uchunguzi kuhusu authenticity ya mgao huo kama kweli ni wa dharura na ulikuwa hauepukiki unafuatia!. Ikidhibitika huo ulikuwa ni mgao shinikizo ili wabunge waijue hali halisi ya Tanesco!, the next step ni Mhando kupandishwa kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka!.


Kama hili lingekuwa kweli, kwanini Wakurugenzi wa TBC1 na wao hawachukuliwi hatua za kuhujumu serikali pale wanapokata matangazo Bungeni kwa "matatizo ya kiufundi"? kwanini hiyo isionekane pia kuwa ni hujuma? Lakini inaweza vipi kuwa hujuma kama ni ajali au jambo lililo nje ya uwezo wa mtu? Hoja ya hujuma haiingii akilini. Kwanini tusiseme serikali kwa sera yake mbovu ya nishati inalihujumu taifa na kujihujumu wenyewe. Kwani ni Mhando aliyeanda kuwaleta Richmond, Dowans au Symbion?

9. Ukiyasoma majibu ya Mhando kwa Katibu Mkuu wake, utagundua Mhando hakujibu alichoulizwa na badala yake analeta maelezo marefu ya kimepanda, kimeshuka!. Mhando ameulizwa maswali mawili tuu 1. Kwa nini ameidhinisha mgao bila kibali cha maandishi cha serikali 2. Kwa kwa kufanya hivyo kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu?. Alipoaswa kutoa sababu za udharura wa mgao huo lakini maelezo yake hayakuonyesha udharura wowote!.

Sijui kama ndugu yangu umesoma maelezo ya Mhando. Amesema hivi katika barua yake akijibu hoja ya udharura wa mgao uliotokea:

Julai 2012 (kuanzia majira ya saa 1 jioni) ulitokea kwa dharura na bila kukusudiwa. Kilichotokea ni kwamba kuanzia tarehe 8 na 9 kina cha maji katika bwawa la Kidatu kilishuka kwa kasi kubwa na hivyo kuhatarisha usalama wa miundo mbinu ya kufulia umeme katika kituo cha kidatu. Utakumbuka mara moja tarehe 10 Julai 2012 yapata saa 1 usiku nilikupigia simu kukuarifu juu ya hali hii na hata athari zake kwamba, hali hii ingepelekea kuwepo kwa mgao wa dharura wa MW 95. Taarifa hii nilimpa pia Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika.

Umesema hajajibu suala la udharura; ina maana -

- unakataa kuwa kina cha maji Kidatu hakikupungua kwa kasi sana kati ya Julai 8 na 9 mwaka huu?
- Kwamba kupungua huko hakukuwa tishio kwa miundombinu ya ufuaji umeme Kidatu?

Kama unakataa hilo ni wazi utakuwa unajua kama kina kilikuwa cha kiasi gani kule kwa siku hizi mbili ambazo zilitangulia mgao wa Julai 10. Lakini zaidi tumeambiwa kuwa hakupuuzuia wajibu wake; utaona kuwa alitoa taarifa kwa Katibu na kwa Mwenyekiti wa bodi ASAP baada ya umeme kukatika. Ulitaka aandike barua usiku ule kumpa taarifa Katibu Mkuu ili imfike muda gani ili kuwahi asionekane amechelewa?
10. Japo hili halikuelezwa, lakini kuna uwezekano pia kuwa Mhando aliidhinisha mgao huo bila kuiarifu bodi yake!.


Mbona imeshajibiwa hapo juu; soma kidogo kaka - kaandika alimuambia Mwenyekiti wa bodi Gen. Mboma. Unless una maana kama aliitisha kikao cha bodi usiku uleule wa mgao!
Kitendo cha mgao wa dharura wakati wa kikao cha bunge la bajeti, bodi ya Tanesco haijui!, Waziri wa Nishati hajui!, Mkuu wa nchi hajui!, its a sensetive issue!. Japo kusimamishwa kwa Mhando kumefanywa na Bodi ya Tanesco, ila amini msiamini ni kwa maelekezo kutoka Juu!. Huu sasa ni uthibitisho wa zile kauli za "dhaifu" na "kushindwa kufanya maamuzi magumu", zinajibiwa kwa vitendo ili ku proove si "dhaifu"!.

Haya hata hayahitaji kujibiwa kwa kweli. Serikali isingekuwa dhaifu kusingekuwa na mgao!!! wala hizi barua zisingeandikwa.
 
wamemsimamisha ili uchunguzi upitishwe,but mi nawaambia watamrudisha jamaa tusubiri tu.
 
Pasco napata tabu kidogo kukuelimisha kuhusu hili jambo.
Taabu ninayopata kwanza naona inawezekana unashindwa kutofautisha mambo ya kiufundi na kisiasa.
Nitakupa mfano.
Gari inapochomoka matairi haiwezi kutembea hata kama tajiri mwenye gari hajatoa kibali kwa dereva cha gari isitembee.
Atakachofanya dereva cha kwanza ni 'kupaki' gari then maelezo mengine yanafuatia.

Ukisoma barua ya Katibu mkuu alichohofia yeye ni kuwa 'Serikali itashambuliwa bungeni' basi. Ingawa taarifa za mgao alikuwa nazo tena mapema(kumbuka alipigiwa simu).
Katibu mkuu hajasema lolote kuhusu utatuzi wa ki'technical wala ufumbuzi wowote wa kukabiliana na uhaba unaoikabili tanesco ambao naamini ndio ingekuwa suluhisho la mgawo huo wa dhalula. sio kusema tu SITISHA mgao na hali hujafanya jitihada zozote za kiufundi.

Tatizo siasa zinaingizwa kila sehemu hata zisipostahili.
Kama ningekuwa rais wa nchi hii kwanza ningepiga chini katibu wa wizara then mambo mengine ndio yangeendelea.
 
It's funny how Katibu Mkuu anasema rudisha umeme 'mara moja' kana kwamba umeme huo upo tele na unafuliwa kwa ziada. Je, kama kina cha Mtera hakitoshelezi?!

..Ndiyo matatizo ya kuwa na uelewa DHAIFU katika mambo ya uzalishaji umeme, alichoona yeye ni kuhujumiwa kwa Serikali.
 
PASCO UMEJITAHIDI KUJIELZA Lakini siamini kama ulimaanisha Mhando angelingoja grid ianguke ili Maswi asimlime! Umeambiwa ule mgao ulikuwa wa dharura, na dharura haijawahi kufuata taratibu hata wakati moja! Mbinu za kukabiliana na dharura huwapo palepale site! Mhando katika maelezo yake kasema Aliwajulisha wanene wake wote kwa simu juu ya kilichotokea. Ulitaka aseme nini zaidi katika mazingira ya dharura?

mkuu ungemuuliza PASCO engineer wa umeme? unajuaje huo mgao umeweza kusaidia kuzuia madhara makubwa zaidi kwenye grid ya taifa.... tungoje uchunguzi, tena wa kitaalam maana kama ni wa kisiasa tutakua kwenye matatizo makubwa zaidi
 
What goes around comes around. Mhando alifanya mtima nyongo wa kumwondoa FO mahili ili amuweke mtu wake watafune vizuri hela ya Tanesco.

Uliza wafanyakazi husika...ukweli ni kwamba sababu kubwa ya mgawo wa umeme huwa inatengenezwa kwa lengo la kuzinufaisha kampuni binafsi zinazouzia umeme Tanesco.
 
Hapo kwenye red umeniwahi. Ni lini watendaji wataishi dhana ya kujiuzulu pale wanapogeuzwa 'waimba mapambio? Mabwawa ya maji 'yalishakataa' kujaa maji sasa wanafanya nini hawa watu ofisini huku wakijua hakuna umeme utakaozalishwa? Na sasa mfumo wa 'kukataa' umehamia kwenye upatikanaji wa gesi, wakina symbion kila kukicha hawana gesi - kisa? gesi 'imekataa?

Watu wanaendekeza njaa na heshima za muda mfupi. Viposho na visafari vinafanya watu wauze utu wao!
 
MM ukiona orodha kamili ya wadaiwa sugu wa TANESCO waliolimbikiza madeni tena makubwa ya bili za umeme utashangaa utakapoona wanaoongoza ni serikali yenyewe kupitia mashirika yake ya umma kama vile mamlaka za maji nchini zinazopokea ruzuku kutoka serikalini. Mbali ya hilo, serikali ndiyo inayoingia mikataba na makampuni ya kinyonyaji ya umeme na kuikabidhi TANESCO itekeleze bila kujali faida na hasara za mikataba kwa shirika hilo nyeti. Katika mazingira kama hayo, hata akija Malaika kutoka Mbinguni hawezi kuendesha TANESCO kwa ufanisi. Kwa hiyo, naungana na wewe kwa asilimia mia moja kwamba Eng. Mhando hakutakiwa asubiri asimamishwe kazi na wakubwa zake kama tayari kulikwa na dalili za kutofautiana kimtazamao na kimaamuzi na wakubwa zake. Hiyo ndiyo Tanzania yetu.

Njaa baba njaa, tatizo Mhando nae inaonekana kwa uzoefu wake pale alikuwa nae ana issue zaki. Ila ukiangalia bodi ya Tanesco haikumtaka kabisa huyu Mhando, kwa hiyo ilipotokea hii sababu, wakaunganisha mambo na hao watu wengine baada ya kupata backup ya katibu mkuu, wakaamua kuwatoa kafara.... kwa uhakika nakuambia hapo lengo si kutatua tatizo la umeme, ni kupitisha budget na kupalilia njia safi ya ufisadi, kulinda msalahi yao....
 
As long as tanesco iko chini ya Serikali DG wake siku zote anatakiwa kwa mujibu wa sheria kuwajibika kwa Katibu mkuu na waziri wa Nishati, hivyo ndio jinsi ilivyo, hao ndio mabosi wake pamoja na Bodi yake. Ukweli hili shirika haliko huru, period. Sasa kwa mantiki hiyo ni wazi kuwa DG alitakiwa kuwaandikia mabosi wake kuhusu ili swala na sio eti kupiga simu or otherwise, huo ni uzembe na alijua wazi kwa hilo. Unapoandika barua unacover your tracks hata ukija ulizwa baadae unaweza sema mbona barua nimekuandikia mkuu. Pili huu ni utata yaani maana kwa haya maelezo ina maana mgao ni mpaka ridhaa itolewe? sasa kwa mantiki hiyo ni kuwa wanaweza kuuzuia, jee hapo inakuwaje iwapo mitambo imefail? ni wazi hii imekaa kisiasa zaidi ya technical.

Ushauri mkuu hapa ni kuwa hii Tanesco inabidi imegwe kiutendaji na kuunda mashirika mbadala.

Yaani mosi kuwe ni shirika tofauti la ufuaji umeme (generation kama yalivyo Pan African, symbion etc) na hili lipewe dhamana ya mabwawa na miundo mbinu yote ya uzalishaji ambayo ipo chini ya Tanesco sasa.

Pili kuwe na shirika kuu la usambazaji yaani transmission na hili lipewe jukumu la kusimamia national grid.

Tatu kuwe na retail na hii ndio sekta yenye matatizo sana maana hii ndio inayodili na wateja moja kwa moja. Hii sekta ni wajibu ifunguliwe na kuruhusu makampuni binafsi yashindane na tanesco. Hapa haya makampuni yawe na uhuru wa kununua umeme toka kwa wazalishaji (ona moja hapo juu) na kutuuzia sisi wateja.

Bila kufanya haya mabadiliko Tanesco itaendelea kututesa na kutuhujumu kwa madili feki na kuingiliwa kisiasa kila siku hata aje nani.
 
yesu wangu,kumbe watu wanahangaika na umeme kumbe ni jitu moja kwa sababu zake binafsi ndilo linalosababisha,...mnh,.....:wacko:

think out of the box mamaa kuna kitu hapo na hilo ili liishe lazima ukubali kuchukiwa na kila mtu hadi na yule aliyekuweka hapo..
 
Serikali ya visa, visasi, kuviziana na ubabe.
Serikali ndiye mdaiwa namba moja wa Tanesco lakini haifanyi juhudi yoyote kulipa madeni yake.
Serikali imeshindwa kuwekeza katika sekta ya umeme na imeshindwa kuiwezesha Tanesco kuwa na miradi endelevu ya umeme pamoja na miundombinu yake.
Serikali imeendelea kuirundikia Tanesco mikataba ya kinyonyaji hivyo kuifanya ilemewe na mzigo wa madeni.
Eliakim Chacha Maswi naye kumbe ni wa hovyo sana hana tofauti na maccm mengine.
 
Njaa baba njaa, tatizo Mhando nae inaonekana kwa uzoefu wake pale alikuwa nae ana issue zaki. Ila ukiangalia bodi ya Tanesco haikumtaka kabisa huyu Mhando, kwa hiyo ilipotokea hii sababu, wakaunganisha mambo na hao watu wengine baada ya kupata backup ya katibu mkuu, wakaamua kuwatoa kafara.... kwa uhakika nakuambia hapo lengo si kutatua tatizo la umeme, ni kupitisha budget na kupalilia njia safi ya ufisadi, kulinda msalahi yao....

kudos ndugu mkuu ni kweli kabisa ndivyo ilivyo soon tu utasikia wanapandisha bei ya umeme..
 
Nini kilifanya kina cha maji kupungua ghafla tarehe 8 na 9 julai.
Ni kwa nini Mhando kasimamishwa kwa tuhuma za ubadhirifu na sio kudharau mamlaka?
 
Back
Top Bottom