JF EXCLUSIVE: Sababu ya Kuachishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

Ndiyo yale yale ya kuwataka madaktari warudi kazini na kutoa huduma kwa wagonjwa huku wanajua kabisa CT Scan haifanyi kazi, X Ray machines zinasuasua na hata gloves zinapatikana kwa mbinde. Serikali inataka "optimal performance" lakini haitoi "Optimal cooperation"! Wanataka wavune wasichopanda!!!

Mhando hakutakiwa kusubiri hadi apigwe mkwara; alitakiwa ajiuzulu kazi na kugoma kama walivyofanya madaktari. Utaweza vipi kumkamua ng'ombe maziwa wakati halishwi?

Tukisema sera yao ya nishati ni mbovu watu wanasema "ooh siyo sera ni watu!"!

kwa kifupi sikumbiki exact figure ila huwezi kuzalisha umeme kwa mfano shilingi 10 per unit kisha uuze kwa shilingi 6 .... hasa hasa zanzibar na kale katarriff chao ka muungano!

it is about time watanzania waambiwe ukweli watu wote walipie umeme kadri wanavyotumia fair and square bila kujali zanzibar au siasa nyingine za kuogopa serikali kudondoka
 
Kiongozi wa nchi dhaifu, so wateule wake dhaifu pia. Na huyu mjeshi wa meremeta, na muuzaadini yetu anafanya nn tanesco..? hivi hakuna mainjinia wanaofaa kuongoza bodi..? Kama dhaifu anampenda sana mpeleke ktk bodi za wanyamapori akatoe mbinu za kuwalinda akina joji- faru ( hope sio kuiba twiga zaidi..!!)

mkuu, lissu aliposema bungeni wakasema chadema hao ... ndio mambo ya kupeana vyeo hayo bila qualifications + akili ndogo kuongoza akili kubwa ....... chadema mara nyingi wanatoa changamoto nzuri kwa serikali, wakizifanyia kazi zitasaidia sana nchi yetu, wote tunajenga nyumba moja ya TANZANIA tuachane na siasa
 
Ndio maana ikawa kila siku tunasisitiza, kazi na maamuzi ya kitaalamu yafanywe na wataalamu na sio wanasiasa. Kumfukuza Mhando hakutapelekea mabwawa kujaa mali wala kupatikana mafuta ikiwa hakuan pesa, hasa ikitiliwa maanani kuwa shirika/serikali imekuwa mdaiwa sugu wa makampuni ya mafuta.

Kwa kumfukuza kazi Mhando, Wizara isidhani itasalimika kulaumiwa na wapinzani na wananchi kwani wanaelewa juu ya ukosefu wa nia safi kwa upande wa serikali juu ya kutatua tatizo la umeme. Kinyume chake, katika kikakao hiki cha kuliko vikao nyengine vyovyote, wapinzani watawalimeni kisawasawa kwani ahadi zimekuwa nyingi na Watanzania wameshachoshwa nanyi.

Kitu pekee ambacho serikali ingefanya, kama imebakiwa na akali ya uungwana, tahayuri na huruma kwa Watanzania, ni kujiuzulu kwa mpigo!

hapa mkuu kwa serikali hii ishajipanga na muongoza mjadala bungeni .... UCHUNGUZI WA TUME UNAENDELEA ... kwa hiyo issue itazimwa kiaina na spika au muongoza mjadala ili bajeti ipite .... kwa kifupi siasa ndio zinaua TANESCO na issue ya umeme tanzania! ... ufisadi upo, kama ulivyo sehemu nyingine lakini asilimia kubwa ya ufisadi wa tanesco una mkono wa wanasiasa na serikali kwa ujumla
 
Nasikia majuzi umeme ulikafika Bungeni wakati Prof. Tibaijuka anahitimisha hotuba yake ya budget ya wizara ya ardhi. Ndio hujuma hii?

yaani ule ukumbi wa bunge mpya hauna standby generator..... au washachakachua hela ya mafuta!
 
Aliyesimamishwa si Mkurugenzi Pekee, Na huyo mwengine yeye amemkosea nani ikiwa Muhando Kamkosea Katibu wake Mkuu??
 
Ndiyo yale yale ya kuwataka madaktari warudi kazini na kutoa huduma kwa wagonjwa huku wanajua kabisa CT Scan haifanyi kazi, X Ray machines zinasuasua na hata gloves zinapatikana kwa mbinde. Serikali inataka "optimal performance" lakini haitoi "Optimal cooperation"! Wanataka wavune wasichopanda!!!

Mhando hakutakiwa kusubiri hadi apigwe mkwara; alitakiwa ajiuzulu kazi na kugoma kama walivyofanya madaktari. Utaweza vipi kumkamua ng'ombe maziwa wakati halishwi?

Tukisema sera yao ya nishati ni mbovu watu wanasema "ooh siyo sera ni watu!"!
MM ukiona orodha kamili ya wadaiwa sugu wa TANESCO waliolimbikiza madeni tena makubwa ya bili za umeme utashangaa utakapoona wanaoongoza ni serikali yenyewe kupitia mashirika yake ya umma kama vile mamlaka za maji nchini zinazopokea ruzuku kutoka serikalini. Mbali ya hilo, serikali ndiyo inayoingia mikataba na makampuni ya kinyonyaji ya umeme na kuikabidhi TANESCO itekeleze bila kujali faida na hasara za mikataba kwa shirika hilo nyeti. Katika mazingira kama hayo, hata akija Malaika kutoka Mbinguni hawezi kuendesha TANESCO kwa ufanisi. Kwa hiyo, naungana na wewe kwa asilimia mia moja kwamba Eng. Mhando hakutakiwa asubiri asimamishwe kazi na wakubwa zake kama tayari kulikwa na dalili za kutofautiana kimtazamao na kimaamuzi na wakubwa zake. Hiyo ndiyo Tanzania yetu.
 
Wanajf wenzangu,

Kwanza asanteni kwa jf kutupatia hii exclusive, maana its a long time kupata kitu kama hii!.

Nimesoma maoni tofauti juu ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, wengi wakitoa maoni kuwa amefanywa ni "mbuzi tuu wa kafara" katika "preemptive move" ili bajeti ya Nishati na Madini ipite!.

Mimi najikita kwenye facts only za kilichotokea, nini kilipaswa kufanyika na matokeo yake ndio haya ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuwajibishwa!.

Kabla ya kuusoma uzi huu, nakuomba sana, kwanza tembelea hii jf exclusive na uzisome hizo attachment kwa makini, ndipo uje unisome!.

Baada ya kusoma memo ya Katibu Mkuu Nishati kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco na majibu yake, nawaombeni sana tuwe wakweli kwa kukubali facts!. "Mhando hajaonewa!", amepatiwa alichostahili kwa msingi mmoja tuu ufuatao wa "kukiuka taratibu"!.

1. Serikali inafanya kila kitu kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni!. Mhando aliambiwa kwa maandishi, kabla ya kuruhusu mgao wowote wa umeme , ki "utaratibu" kwanza ni lazima apate kibali cha maandishi toka kwa Katibu Mkuu wake!.
2. Hii inamaanisha Mhando kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, hana mamlaka ya kuidhinisha mgao wa umeme, no matter what!.
3. Mhando alipoona hali ya umeme ni ngumu, na kuna ulazima wa kuanza kwa mgao wa dharura, "kiutaratibu" alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu wake na kumjulisha situation ilivyo na nia ya kuanzisha mgao huo wa dharura.
4. Katibu Mkuu angemjulisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye nae angemjulisha mwenye (dhamana) nchi atoe idhini mgao huo wa dharura uanze!.
5. Katibu Mkuu Kiongozi angetoa majibu hayo kwa Katibu Mkuu Nishati ambaye naye angetoa idhini kwa Mkurugenzi Mkuu Tanesco kuanzisha mgao!. Huu ndio utaratibu ambao haukufuatwa!.
6. Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuidhinisha mgao ambao sio mamlaka yake, huu ni ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea hivyo alistahili adhabu ila siyo kali kiasi cha kusimamishwa!.
7. Kitendo cha kuidhinisha mgao huo bila kufuata taratibu na ikatokea ni kipindi cha kikao cha bunge la bajeti, kinatafsirika kama ni "hujuma" dhidi ya serikali!. Hiki kinastahili adhabu kali kama hiyo aliyoipata na uchunguzi kuhusu authenticity ya mgao huo kama kweli ni wa dharura na ulikuwa hauepukiki unafuatia!. Ikidhibitika huo ulikuwa ni mgao shinikizo ili wabunge waijue hali halisi ya Tanesco!, the next step ni Mhando kupandishwa kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka!.
8. Ukiyasoma majibu ya Mhando kwa Katibu Mkuu wake, utagundua Mhando hakujibu alichoulizwa na badala yake analeta maelezo marefu ya kimepanda, kimeshuka!. Mhando ameulizwa maswali mawili tuu 1. Kwa nini ameidhinisha mgao bila kibali cha maandishi cha serikali 2. Kwa kwa kufanya hivyo kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu?. Alipoaswa kutoa sababu za udharura wa mgao huo lakini maelezo yake hayakuonyesha udharura wowote!.
9. Japo hili halikuelezwa, lakini pia kuna uwezekano kuwa Mhando aliidhinisha mgao huo bila kuiarifu bodi yake!. Kitendo cha mgao wa dharura wakati wa kikao cha bunge la bajeti, bodi ya Tanesco haijui!, Waziri wa Nishati hajui!, Mkuu wa nchi hajui!, its a sensetive issue! na hatua hizo ndio impact ya sensetivity ya issue yenyewe.

Japo kusimamishwa kwa Mhando kumefanywa na Bodi ya Tanesco, ila amini msiamini ni kwa maelekezo kutoka Juu!. Huu sasa ni uthibitisho wa zile kauli za "dhaifu" na "kushindwa kufanya maamuzi magumu", zinajibiwa kwa vitendo ili ku proove si "dhaifu"!.

10. Kwa kuzingatia hayo, Mhando hakuonewa hata kidogo bali hiyo ni stahili yake!. Japo lazima nikiri kuna udhaifu mkubwa serikalini katika kufikia maamuzi ambayo yako based kwenye kufuata taratibu tuu ambazo sio sheria wala kanuni kwa mtu kufanya kosa moja dogo tuu likayafuta mema na mazuri yote Mhando aliyo ifanyia Tanesco!.

Pasco
 
attachment.php

attachment.php

attachment.php
 
Pasco bwana! Nakumbuka wakati uleee ukiendesha kipindi cha mada motomoto ama kitu kama hicho. Nakumbuka mdahalo wa wagombea Urais 1995 uliofanyika pale jengo la utamaduni wa Korea. Ulikuwa macjachari.

Mhando anasema alipiga simu kwa kuwa mgawo ulikuwa wa dharura! Hapa naona kuna hatari, kumbe TANESCO haina meno! Kumbe DG wa TANESCO ni ceremonial!
 
Last edited by a moderator:
Kama Mkurugenzi na Katibu Mkuu wanashindwa hata kupigiana simu wakajulishana juu ya mgao wa umeme basi uhusiano kat ya Wizara na Tanesco una matatizo makubwa kuliko inavyoonekana. Yaani Katibu Mkuu naye anausikia mgao kwenye vyombo vya habari!!!!

Jamaa yangu nadhani huu sasa ni uvivu wa kusoma taarifa ambao anao Maswi kakuambukiza na wewe! Taarifa zote umewekewa ziko hapo! mawasiliano yapo tena yote, kimaandishi, kwa simu na ana kwa ana! huu nao ni udhaifu wa maswi,'LIKE FATHER LIKE SON"
 
Wanajf wenzangu,
Kwanza asanteni kwa jf kutupatia hii exclusive, maana its a long time kupata kitu kama hii!.

Baada ya kusoma majibizano ya Mhando na Katibu Mkuu wake, nawaombeni tuwe wakweli kwa kukubali facts!. Mhando hajaonewa!, amepatiwa alichostahili kwa msingi mmoja tuu ufuatao.

1. Serikali inafanya kila kitu kwa mujibu wa taratibu, sheria na kanuni!.
2. Mhando aliambiwa kwa maandishi, kabla ya kuruhusu mgao wowote, ni lazima kwanza apate kibali cha maandishi toka kwa Katibu Mkuu.
3. Hii inamaanisha Mhando kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, hana mamlaka ya kuidhinisha mgao wa umeme, no matter what!.
4. Alipoona hali ni ngumu, alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu na kumjulisha situation ilivyo na nia ya kuanzisha mgao wa dharura.
5. Katibu Mkuu akamjulisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye nae angemjulisha mwenye (dhamana) nchi atoe idhini mgao uanze!.
6. Katibu Mkuu Kiongozi angetoa majibu hayo kwa Katibu Mkuu Nishati ambaye naye angetoa idhini kwa Mkurugenzi Mkuu Tanesco kuanzisha mgao!.
7. Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuidhinisha mgao ambao sio mamlaka yake, huu ni ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea hivyo alistahili adhabu ila siyo kali kiasi cha kusimamishwa!.
8. Kitendo cha kuidhinisha mgao kipindi cha kikao cha bunge bila kufuata taratibu za mgao, kinatafsirika kama ni "hujuma" dhidi ya serikali!. Hiki kinastahili adhabu kali kama hiyo aliyoipata na uchunguzi kuhusu authenticity ya mgao huo kama kweli ni wa dharura na ulikuwa hauepukiki unafuatia!. Ikidhibitika huo ulikuwa ni mgao shinikizo ili wabunge waijue hali halisi ya Tanesco!, the next step ni Mhando kupandishwa kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka!.
9. Ukiyasoma majibu ya Mhando kwa Katibu Mkuu wake, utagundua Mhando hakujibu alichoulizwa na badala yake analeta maelezo marefu ya kimepanda, kimeshuka!. Mhando ameulizwa maswali mawili tuu 1. Kwa nini ameidhinisha mgao bila kibali cha maandishi cha serikali 2. Kwa kwa kufanya hivyo kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu?. Alipoaswa kutoa sababu za udharura wa mgao huo lakini maelezo yake hayakuonyesha udharura wowote!.
10. Japo hili halikuelezwa, lakini kuna uwezekano pia kuwa Mhando aliidhinisha mgao huo bila kuiarifu bodi yake!. Kitendo cha mgao wa dharura wakati wa kikao cha bunge la bajeti, bodi ya Tanesco haijui!, Waziri wa Nishati hajui!, Mkuu wa nchi hajui!, its a sensetive issue!. Japo kusimamishwa kwa Mhando kumefanywa na Bodi ya Tanesco, ila amini msiamini ni kwa maelekezo kutoka Juu!. Huu sasa ni uthibitisho wa zile kauli za "dhaifu" na "kushindwa kufanya maamuzi magumu", zinajibiwa kwa vitendo ili ku proove si "dhaifu"!.

Mhando hakuonewa bali hiyo ni stahili yake!.

Pasco

PASCO UMEJITAHIDI KUJIELZA Lakini siamini kama ulimaanisha Mhando angelingoja grid ianguke ili Maswi asimlime! Umeambiwa ule mgao ulikuwa wa dharura, na dharura haijawahi kufuata taratibu hata wakati moja! Mbinu za kukabiliana na dharura huwapo palepale site! Mhando katika maelezo yake kasema Aliwajulisha wanene wake wote kwa simu juu ya kilichotokea. Ulitaka aseme nini zaidi katika mazingira ya dharura?
 
Aisee! huu ni mdundiko wa kisiasa ngoja tuone wanavyoucheza, maana wanakanyagana wao kwa wao!
 
Leo kwa mara ya kwanza nimetambua kwamba , utetezi mwngi humu ni wa majungu na kutotambua facts za kila kinacho zungumzwa,nadhani sitaamini chohocte kinacho jadiliwa humu. Kwa mimi niliye fanya kazi na Mhando naweza sema, ni mhujumu mkubwa wa nchi hii na hafai na kama atatolewa ni jambo kubwa sana katika kuendeleza nchi hii katika masuala ya nishati ya umeme. Huyu mtu asikilizi mtu, wala hana muda wa kufanya kazi zaidi ya kusafiri na kukwepa wageni na wawekezaji wanao kuja kwa nia nzuri ya kuwekeza.KUna project nyingi zilikuja kwa ajili ya kuokoa hilo shirika lakini hakua na muda zaidi ya kukwepa nakukimbia officini huku shirika halina pesa. Kitendo chake cha kufanya mamamuzi bila kumshirikisha Katibu mkuu ni kutokana na yeye kutamba kwamba kapewa rungu na raisi ,kwa hiyo hakuna mtu naweza mgusa, baada ya raisi kumuamini huyu jamaa. Hakuna bifu ni kubweteka kwa huyu Mhando na ni janga la taifa kama atarudishwa hapo.
 
Mmmh ! Mambo haya , mkuki kwa nguruwe ........ ! Ipo kazi matokeo ya kutaka cheo kwa wudi na uvumbi ndio haya hapa
 
Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake na mbibu kuliko mbichi maana mwisho wa mbivu huoza. Kila jambo kwa nchii hii limeoza, tutaona na kusikia mengi.
 
Wanabodi,

Nimesoma maoni tofauti juu ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, wengi wakitoa maoni kuwa amefanywa ni "mbuzi tuu wa kafara" katika "preemptive move" ili bajeti ya Nishati na Madini ipite!.

Mimi najikita kwenye facts only za kilichotokea, nini kilipaswa kufanyika na matokeo yake ndio haya ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuwajibishwa!.

Kabla ya kuusoma uzi huu, nakuomba sana, kwanza tembelea hii jf exclusive na uzisome hizo attachment kwa makini, ndipo uje unisome!.

Baada ya kusoma memo ya Katibu Mkuu Nishati kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco na majibu yake, nawaombeni sana tuwe wakweli kwa kukubali facts!. "Mhando hajaonewa!", amepatiwa alichostahili kwa msingi mmoja tuu ufuatao wa "kukiuka taratibu"!.

1. Serikali inafanya kila kitu kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni!. Mhando aliambiwa kwa maandishi, kabla ya kuruhusu mgao wowote wa umeme , ki "utaratibu" kwanza ni lazima apate kibali cha maandishi toka kwa Katibu Mkuu wake!.
2. Hii inamaanisha Mhando kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, hana mamlaka ya kuidhinisha mgao wa umeme, no matter what!.
3. Mhando alipoona hali ya umeme ni ngumu, na kuna ulazima wa kuanza kwa mgao wa dharura, "kiutaratibu" alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu wake na kumjulisha situation ilivyo na nia ya kuanzisha mgao huo wa dharura.
4. Katibu Mkuu angemjulisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye nae angemjulisha mwenye (dhamana) nchi atoe idhini mgao huo wa dharura uanze!.
5. Katibu Mkuu Kiongozi angetoa majibu hayo kwa Katibu Mkuu Nishati ambaye naye angetoa idhini kwa Mkurugenzi Mkuu Tanesco kuanzisha mgao!. Huu ndio utaratibu ambao haukufuatwa!.
6. Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuidhinisha mgao ambao sio mamlaka yake, huu ni ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea hivyo alistahili adhabu ila siyo kali kiasi cha kusimamishwa!.
7. Kitendo cha kuidhinisha mgao huo bila kufuata taratibu na ikatokea ni kipindi cha kikao cha bunge la bajeti, kinatafsirika kama ni "hujuma" dhidi ya serikali!. Hiki kinastahili adhabu kali kama hiyo aliyoipata na uchunguzi kuhusu authenticity ya mgao huo kama kweli ni wa dharura na ulikuwa hauepukiki unafuatia!. Ikidhibitika huo ulikuwa ni mgao shinikizo ili wabunge waijue hali halisi ya Tanesco!, the next step ni Mhando kupandishwa kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka!.
8. Ukiyasoma majibu ya Mhando kwa Katibu Mkuu wake, utagundua Mhando hakujibu alichoulizwa na badala yake analeta maelezo marefu ya kimepanda, kimeshuka!. Mhando ameulizwa maswali mawili tuu 1. Kwa nini ameidhinisha mgao bila kibali cha maandishi cha serikali 2. Kwa kwa kufanya hivyo kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu?. Alipoaswa kutoa sababu za udharura wa mgao huo lakini maelezo yake hayakuonyesha udharura wowote!.
9. Japo hili halikuelezwa, lakini pia kuna uwezekano kuwa Mhando aliidhinisha mgao huo bila kuiarifu bodi yake!. Kitendo cha mgao wa dharura wakati wa kikao cha bunge la bajeti, bodi ya Tanesco haijui!, Waziri wa Nishati hajui!, Mkuu wa nchi hajui!, its a sensetive issue! na hatua hizo ndio impact ya sensetivity ya issue yenyewe.

Japo kusimamishwa kwa Mhando kumefanywa na Bodi ya Tanesco, ila amini msiamini ni kwa maelekezo kutoka Juu!. Huu sasa ni uthibitisho wa zile kauli za "dhaifu" na "kushindwa kufanya maamuzi magumu", zinajibiwa kwa vitendo ili ku proove si "dhaifu"!.

10. Kwa kuzingatia hayo, Mhando hakuonewa hata kidogo bali hiyo ni stahili yake!. Japo lazima nikiri kuna udhaifu mkubwa serikalini katika kufikia maamuzi ambayo yako based kwenye kufuata taratibu tuu ambazo sio sheria wala kanuni kwa mtu kufanya kosa moja dogo tuu likayafuta mema na mazuri yote Mhando aliyo ifanyia Tanesco!.

Pasco

Pasco maelezo yako yamekazania sana " mgao wakati wa kikao cha bunge" kana kwamba kikao cha bunge hakitakiwi kukatiwa umeme ila wananchi ndiyo waumie. Haya ni mawazo ya kitwana sana.
 
Mimi naona mnajikita kwenye barua ya KM wakati sababu za kusimamishwa kazi zimebainishwa wazi

Vilevile hakuna any technical director ambaye amesimamishwa naye kazi director wa transmission, distribution and generation are all intact hivyo tatizo sio technical failures no other engineer has been touched!

Wakurugenzi waliosimamishwa ni wenye taaluma ya uhasibu na mkuu wa manunuzi.....

Tuangalie kwa umakini sana hizi tender za manunuzi na perfomance yake, PPRA iliweka wazi kati ya procuring entities zilizofanya vibaya sana TANESCO imo na iko below 30% that's alarming

PPRA walisema wazi kuwa wamepeleka hizo procuring entities TAKUKURU na watendaji wake wakuu wanahojiwa

Nimalizie kwa kusema manunuzi ya TANESCO ni ya 2 kwa ukubwa ukianza na TANROADS
 
Pasco bwana! Nakumbuka wakati uleee ukiendesha kipindi cha mada motomoto ama kitu kama hicho. Nakumbuka mdahalo wa wagombea Urais 1995 uliofanyika pale jengo la utamaduni wa Korea. Ulikuwa macjachari.

Mhando anasema alipiga simu kwa kuwa mgawo ulikuwa wa dharura! Hapa naona kuna hatari, kumbe TANESCO haina meno! Kumbe DG wa TANESCO ni ceremonial!
Mkuu Kimbunga, mimi ni Pasco wa jf tuu. Kufuatia issue ya mgao kuwa ni very sensetive kiuchumi na kiusalama, iliamuliwa atakaye idhinisha mgao ni mkuu wa nchi tuu and no one else. Tena kibali cha kuanza kwa mgao lazima kitolewe kwa maandishi!. Huo ndio utaratibu!. Mhando alipaswa kumuandikia Katibu Mkuu wake ili nae amuarifu Katibu Mkuu Kiongozi amuarifu mwenye nchi kibali kitolewe!.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom