JF EXCLUSIVE: Sababu ya Kuachishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

Mambo ya Tia maji Tia maji hayo
We need to come out with a permanent solution for Tanesco
 
Wakuu wa Jamvi naona niisisimue thread hii maana nishati ndiyo kiini cha maendeleo ya nchi nnyingi duniani, wakati sisi tunahesabu Hidro Power Stations zetu kwa Videlu, Pale Ostrusund Sweden nilihesabu kwa upeo wa mcho yangu kwa kamji kadogo tu Hidro Powere stations 12. Mji wa Goternburg una kiwanda cha chuma kinatumia Megawarst 350 za umeme, msiniulize ni sawa na asilima ngapi ya umeme wa nchi yetu. Sweden ina watu Milioni 9.

Niwarudishe kwenye sakata letu la TANESCO ambapo sioni mwenye huruma hatammoja. Hebu fuatilieni vyanzo hivi vya habari:


Waandishi Wetu

Toleo la 250
18 Jul 2012



  • Yakutwa na zaidi ya Sh. bilioni moja, uchunguzi waendelea
  • Mpango wa kupandikiza mgawo ‘feki’ wa umeme wafichuliwa

SIKU chache baada ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO), William Mhando na wenzake: Robert Shemhilu, Lusekelo Kassanga na Haruna Mattambo, akaunti ya mmoja wa vigogo wa shirika hilo ngazi ya menejimenti iliyoko katika moja ya benki nchini imezuiwa na vyombo vya dola nchini, Raia Mwema, limeelezwa.

Akaunti ya kigogo huyo (jina la benki na la mwenye akaunti yanahifadhiwa ili kutoharibu uchunguzi unaoendelea) imekutwa na fedha zaidi ya shilingi bilioni moja na sasa inadaiwa kuzuiwa kwa baraka za mamlaka za juu.

Vyanzo kadhaa vya habari vimeeleza ya kuwa kigogo huyo amekutwa na mabilioni hayo ya fedha huku chanzo cha mapato hayo yasiyolingana na kipato chake kama mtumishi wa umma kikiwa ni utata.

Hata hivyo, wakati uchunguzi huo wa awali unaofanywa na vyombo vya dola nchini ukiwa unaendelea, kwa upande mwingine kumebainika kuwapo na kampeni kali za kuuokoa uongozi wa TANESCO unaochunguzwa kwa sasa, juhudi ambazo zimekuwa zikihusisha hata Kamati za Bunge.

Kamati za Bunge ambazo baadhi ya wajumbe wake wanahusishwa katika ‘kuokoa’ jahazi la uongozi wa TANESCO uliosimamishwa ni pamoja na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo sasa wanatajwa kuanza kumwandama Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi pamoja na Waziri Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, George Simbachawene, wanaotajwa kuwa na msimamo mkali dhidi ya kile kinachodaiwa kuwa ni uzembe na ubadhirifu ndani ya TANESCO.

Mgawo feki wa umeme

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, kwa muda mrefu sasa kumekuwa na njama za kuandaa na kufanikisha mgawo ‘feki’ wa umeme nchini kwa njia mbalimbali. Lengo la mgawo huo ni kuwanufaisha baadhi ya vigogo TANESCO kwa njia ya ununuzi wa mafuta ya kuendeshea mitambo.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa na vyanzo mbalimbali vya habari ndani ya Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO, umebaini kuwa baadhi ya mitambo ya kuzalisha umeme jijini Dar es Salaam, na hasa baadhi ya mitambo iliyopo eneo la Ubungo na Tegeta imekuwa ikizimwa ili kuhalalisha migao na mpango wa ununuzi mafuta unaowaingizia fedha vigogo. Orodha ya mitambo inayozalisha umeme kwa mafuta jijini Dar es Salaam ni pamoja na IPTL, Symbion na Aggreko.

Taarifa zilizopo zinazidi kubainisha kuwa, baada ya kuzima mitambo hiyo na kusababisha mgawo wa umeme (usio wa lazima-feki), wito wa kuzalisha umeme wa mafuta hujitokeza.

Ni katika wito huo ambao msingi wake ni kupandikiza mgawo feki wa umeme, wakati mwingine Serikali hutoa fedha za ununuzi wa mafuta lakini wakati mwingine fedha hizo huchotwa kutoka TANESCO, shirika ambalo kila mwezi hukusanya shilingi karibu ya bilioni 100 kutoka kwa wateja wake.

Katika ununuzi huo wa mafuta kwa ajili ya kuendesha mitambo ili kuongeza uzalishaji wa umeme, mambo kadhaa huzingatiwa ili kunufaisha wahusika.

Jambo la kwanza ni kupatikana kwa kile kinachoitwa “ten percent” kinachogawanywa kwa waliofanikisha mpango huo. Pili, ni kuendelea kufanya wizi katika kiwango cha mafuta kilichokwishakununuliwa kwa ajili ya kuwasha mitambo husika.

Mchezo huo mchafu unadaiwa kuripotiwa kwa baadhi ya viongozi wa TANESCO lakini hapakuwa na hatua zilizopata kuchukuliwa hadi pale suala hilo lilipofika katika uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini.

“Suala hili limekuwa likifanyika kwa muda mrefu sasa, umeme unakatwa na kuzalishwa kwa kiwango cha chini ili kuibua mahitaji ya kuzalisha umeme kwa njia ya mafuta ili TANESCO wanunue. Katika ununuzi huo kuna suala la 10% na wizi wa hayo hayo mafuta yanayonunuliwa lakini pia ni manufaa kwa kampuni za uzalishaji umeme huo kwa kuwa zinakuwa zikifanya biashara kwa kuuza umeme huo TANESCO.

“Ni suala lililowahi kuripotiwa lakini likapuuzwa na menejimenti, ila miezi takriban mitatu kupita baada ya kuripotiwa kuliwahi kufanyika kikao cha wafanyakazi wote kupitia TUICO, baada ya wafanyakazi kutia shinikizo kuhusu hujuma hizi Mkurugenzi wa TANESCO, Mhando naye ndipo akadai kupata taarifa hizo hapo kwa mara ya kwanza na aliahidi kuchukua hatua,” kilieleza chanzo kimoja cha habari.

Hujuma kwa mtambo wa Kinyerezi

Hujuma nyingine inayotajwa kufanyika ndani ya TANESCO ni kuahirishwa mara kwa mara kwa mchakato wa kuanzisha mtambo wa kuzalisha umeme eneo la Kinyerezi, jijini Dar es Salaam.

Mtambo huo ambao utazalisha umeme kwa kutumia gesi, unatajwa kuwa tishio dhidi ya mtandao wa wauzaji mafuta kwa TANESCO kwa ajili ya uzalishaji umeme kwa kutumia mafuta.

“Kutokana na tishio la mradi huu utakapokamilika kuwanyima ulaji, walikuwa wakiukwamisha. Ni mradi wa megawati 240. Huu (mradi wa Kinyerezi) utaua kabisa mpango wao wa ulaji kwa kuandaa mgawo feki na kuzalisha umeme kwa mafuta. Waziri Muhongo alipoingia alihakikisha mradi unasainiwa ili kuanza....lazima wampige vita na aliwaeleza katika moja ya vikao (waziri) kuchukizwa na tabia hiyo,”

Wabunge nao watajwa

Mbunge mmoja wa Viti Maalumu kutoka mikoani (kwa sasa hatutamtaja kwa kuwa hatukufanikiwa kumpata) anadaiwa kunufaika na uongozi wa TANESCO uliosimamishwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia,mbunge huyo anadaiwa kupewa zabuni ya kusambaza matairi kwa ajili ya magari ya TANESCO kupitia kampuni yake. Madai yanayoelekezwa kwa mbunge huyo ni kwamba, kampuni yake ilipewa zabuni baada ya zabuni hiyo ‘kuporwa’ kutoka kwa kampuni nyingine.

Lakini wakati mbunge huyo wa Viti Maalumu akihusishwa na madai hayo, mbunge mwingine na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, naye anadaiwa kuwa na maslahi na uongozi uliosimamishwa wa TANESCO.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekuwa katika mazungumzo yanayotajwa kwenda vizuri ili auziwe mtambo wa kufua umeme unaoitwa Kikuletwa, ulioko katika Jimbo la Hai, ili baada ya kununua aweze tena baadaye kuiuzia umeme TANESCO kama inavyofanyika kwa kampuni nyingine za uwekezaji nchini ambazo kwa muda sasa zimekuwa zikitajwa kuuza umeme kwa bei kubwa.

Raia Mwema
halikufanikiwa kumpata Mbowe kusikia maelezo yake, lakini mmoja wa viongozi wa kurugezi za chama hicho, John Mrema, amemweleza mwandishi wetu kuwa anayetaka kununua mtambo huo si Mbowe binafsi bali ni Halmashauri ya Wilaya ya Hai.

“Mbowe kama mbunge alikuwa akisaidia kufanikisha hilo. Mpango uliopo ni kununua mtambo huo wa siku nyingi ambao hautumiki ni kuukarabati na kisha kuanza kuzalisha umeme ambao sehemu itatumiwa na wananchi wa Hai na kiasi kingine cha umeme kitauzwa TANESCO,” alisema Mrema.

Suala la kusimamishwa kwa uongozi huo wa juu wa TANESCO limevuta hisia nyingi huku makundi ya watu wakipita huku na kule kujaribu kubatilisha uamuzi huo, mengine yakidai kwamba taratibu za kuusimamisha zimekiukwa, mengine yakivurumisha tuhuma nzito dhidi ya uongozi wa wizara na mengine yakitaka Bodi nzima ya TANESCO iondolewe kwa vile baadhi ya wajumbe wa Bodi hiyo wamekuwa wakifanya biashara ya mafuta na shirika hilo.

Raia Mwema
limefahamishwa kwamba timu ya uongozi wa wizara jana ilikuwa Dodoma ambako iliitwa kwenda kujieleza mbele ya Kamati za Bunge zinazohusiana na TANESCO.

Tarifa zaidi zilizopatikana tukienda mitamboni zilieleza kwamba pamoja na kukutana na kamati hizo, timu hiyo ya wizara imeomba kukutana kwanza na kamati ya CCM ambako mtoa habari wetu ametufahamisha kwamba patamwagwa kila kitu hadharani kuhusiana na nani wanahujumu TANESCO, nani wanaofadika nayo na kwa njia zipi.

Kusimamishwa kwa Injinia Mhando na wenzake kulikuja kiasi cha siku tatu tu baada yaRaia Mwema kuripoti taarifa za kuwako makundi ya wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini na wenzao ndani ya mashirika na taasisi tanzu za wizara hiyo, wanaohujumu jitihada za sasa za kuisuka upya wizara na taasisi na mashirika yake.

Jitihada hizo, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari serikalini, zimekuwa pia zikiwahusisha kwa karibu baadhi ya wenyeviti wa bodi za mashirika na taasisi hizo na watendaji wakuu wake ambao wanahisi ya kuwa, kwa mazingira mapya wizarani, ajira zao zinakaribia ukingoni kutokana na ama utendaji binafsi usiokidhi au kwa kushindwa kudhibiti uozo katika taasisi na mashirika yao.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mtandao wa makundi hayo ulioungana ulikuwa ukiendesha kampeni ya kuukataa uongozi wa wizara kwa madai kwamba umekuwa ukiendesha mambo kibabe.

Raia Mwema
limedokezwa pia kwamba nje ya wizara, taasisi na mashirika yake, mtandao huo unaungwa mkono na baadhi ya wabunge, wengine wakiwa katika kamati zinazohusiana na wizara hiyo, na kwamba mipango iliyokuwa inasukwa ili kupeleka ujumbe kwa mamlaka husika kuwa uongozi wa wizara haufai, uondolewe, ni pamoja na kukwamisha bajeti ya wizara itakayowasilishwa bungeni wiki ijayo.

Hoja nyingine zanazodaiwa kushadidiwa na mtandao huo kama sababu za ziada kutaka mabadiliko ya uongozi wizarani ni kuwa Waziri mpya, Profesa Sospeter Muhongo, si mwanasiasa, ubunge wake uliompa uwaziri umetokana na yeye kuteuliwa na hilo linawakera baadhi ya wabunge wa majimbo ambao wanaona si vyema wao kuachwa, mtu wa “kuja” akapewa nafasi hiyo kubwa tena katika wizara inayotajwa kuwa tajiri na yenye ulaji kama ya Nishati na Madini.

Ukiacha hilo, Raia Mwema limeambiwa pia ya kuwa madai mengine ni suala ambalo chimbuko lake ni ukabila. Waziri Profesa Muhongo anatoka Mkoa wa Mara ambako ndiko anakotoka pia Katibu Mkuu, Eliachim Maswi, ingawa inafahamika kwamba wanatoka katika maeneo mawili tofauti ya mkoa huo. Kwa mujibu wa madai ya wana mtandao huo, Profesa Muhongo na Maswi kwa kutoka katika Mkoa mmoja na sasa wanafanya kazi ofisi moja ni tatizo.

Alipoulizwa na Raia Mwema juu ya madai hayo, mwanzoni mwa wiki iliyopita, Maswi alisema hakuwa na namna ya kuzuia watu wasizungumze wanayoyataka. Alisema yawepo au yasiwepo, yeye na timu wanayoijenga wizarani wameamua kufanya kazi ili kuleta tija katika maeneo waliyokabidhiwa kuyasimamia.

“Rais Jakaya Kikwete aliyetuteua hakufanya hivyo ili tuje hapa tuchezecheze. Tumepewa majukumu ya kutekeleza. Hebu niambie, nyumbani kwako siku hizi umeme unakatika mara ngapi?

“Ukiona kuna mawazo kama hayo, ujue tunafanya kazi. Sisi hatutajali yanayosemwa, kipimo chetu ni kama umma unaridhika. Kama unaona baadhi ya kero zilizokuwapo, zilizokuwa ndani ya uwezo wetu, sasa zimepungua kwenye vitu kama umeme, na kama tumeanza kupata stahili yetu kwenye maeneo kama ya migodi ujue wizarani sasa kuna wachapakazi,” alisema Maswi.

Katibu Mkuu Maswi aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Kaimu Katibu Mkuu katikati ya Julai mwaka jana, kiasi cha mwaka mmoja uliopita, akichukua nafasi iliyokuwa imeachwa na David Jairo aliyekuwa ametuhumiwa na Bunge, pamoja na mambo mengine, kwa ubadhirifu.

Aidha, Profesa Muhongo, mmoja wa Watanzania wachache wataalamu wa jiolojia, amejiunga serikalini mwanzoni mwa Mei, mwaka huu, baada ya kuteuliwa na Rais Kikwete kwanza kama mbunge kupitia nafasi 10 za Rais kuteua wabunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ni Shirika la Umeme (TANESCO) ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Jenerali mstaafu na mkuu wa zamani wa Majeshi, Robert Mboma, Mtendaji wake Mkuu ni Mhandisi Godfrey Mhando.

Mengine ni EWURA ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Simon Sayore; huku Mtendaji Mkuu akiwa Haruna Masebu; Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Balozi Ami Mpungwe na Mtendaji Mkuu ni Dk. Dk Lutengano Mwakahesya; Wakala wa Madini (TMAA) ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Dk. Yamungu Kayandabila, Mtendaji Mkuu akiwa Mhandisi Paul Masanja.

Mengine ni STAMICO ambalo Mwenyekiti wa Bodi ni Ramadhani Omari Hatibu, Mtendaji Mkuu akiwa Grey Mwakalukwa; GST lililo chini ya Uenyekiti wa Bodi wa Profesa Idrissa Kikula na Mendaji Mkuu akiwa Profesa Abdul Mruma na TPDC ambalo Mwenyekiti wake ni Michael Mwanda na Mtendaji Mkuu ni Yona Kilagane.





Na declare interest kuwa mimi ni Mbunge na nimeamua kuanzisha hii therad ili tuwekane sawa hapa baada ya kukamilisha uchunguzi wangu.

Kuna Mbunge mmoja wa kike juzi aliniomba tupate naye chakula na tulipokaa alianza kunishawishi kwa kwa nguvu nyingi sana kuwa tuikatae kwa nguvu zote bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini itakapowasilishwa na tukiweza tumseme sana na kumkataa Katibu wa Wizara hiyo kuwa hafai. Aidha alikuwa ananisisitizia niwambie na wengine hivyo na kwamba tumpongeze MD William Mhando maana anafaa sana. Mwisho wa chakula alikataa nisilipe na akanilipia na pia kutaka kunipa fedha za mafuta kwa ajili ya gari langu kitu nilichomkatalia.

Jana na leo baada ya hili la kuwasimamisha watumishi wa TANESCO nikaona niingie ndani kutafiti undani wa kinachoendelea na nikaunganisha zile juhudi za Mbunge mwenzangu ambaye alikuwa na mwenzake (Mh. wa kike ambaye ni shoga yake ) ikanibidi kuanza upelelezi wangu ambao sasa matokeo yake nimeamua kuyamwaga hapa wazi baada ya kupata ukweli toka vyanzo vyangu vinavyoaminika toka ndani ya TANESCO na Taasisi zingine husika za umma .

I. Uwezo mdogo sana wa ndg. Mhando katika kuongoza Shirika
Huyu jamaa ameshindwa kuongoza TANESCO KABISA. He lacks managerial skills and his interpersonal communication is very weak and questionable. Toka ameingia amejenga makundi kwa misingi ya ukabila, urafiki na wizi. Ushahidi pia mnaweza kuuliza yale maoni ya watumishi wa TANESCO yaliyokusanywa na Katibu Mkuu wa Wizara. Nimefuatilia hata shule yake ni ya kuungaunga na hakika ilikuwa mbovu sana aliposoma huko Cuba.

Hakika habari za ndani kabisa zinasema uteuzi wake kuwa MD alichukuliwa toka namba tatu katika ranking wakati kulikuwa na mtu wa kwanza na wa pili walioachwa wenye uwezo kwenye vetting yao.


II. Kushiriki wizi ndani ya Shirika
Huyu ni mwizi moja kwa moja kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Bodi yake Rtd. General Robert Mboma na Makamu wake. Yaani huyu Mwenyekiti wa Bodi, Afande yeye anawauzia mafuta ya kuendesha mitambo TANESCO tena kwa bei ya juu Tshs. 2000/= kwa lita wakati sokoni ni 1500/=. Kwanini Mwenyekiti wa bodi huyu mzee mstaafu wa jeshi afanye biashara na chombo anachokisimamia akisababisha a conflict of interests and zero accountability?

TANESCO wanakusanya yapata Tsh. Billioni 100 kwa kila mwezi na hakuna ajuaye hizo fedha zinafanya kazi gani zaidi yake MD, Incarge wa idara ya fedha na Gererali Mboma. Kwa sasa TANESCO wameshindwa hata kulipa madeni anayodaiwa na wako mbioni kuuza mitambo yake.

Kimkakati, sasa wamemega fedha nyingi mno (nasema tena mno) na wanazisabaza kwa kuanzia kwa baadhi tu (si wote) ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge na wao bila kufikiri wameamua kichwa kichwa eti kwenda kuonana na Wizara kesho kusimamisha hatua zilizochukuliwa na Wizara juu ya huyu MD.

Na kwa kudhihirisha mahusiano yake na Generali , kama mwenyekiti wa Bodi amekataa kusaini barua ya kumsimamisha MD na watuhumiwa wengine kitu cha ajabu sana kwa sababu tu ya kulinda maslahi yake ya biashara anayofanya hapo TANESCO. Mzee huyu hatosheki na pensheni na marupurupu apewayo kama posho za vikao na kutembelea Shirika n.k kila mara.


III. Hujuma kwa Taifa kwa lugha za ‘ kiufundi’ .
Leo nimeambiwa na Injinia mmoja mwandamizi wa Tanesco ninayemwamini sana kuwa hakika ugomvi umeanza kwa sababu kama kawaida yao, MD na kundi lake walitaka kutangaza kuwepo na mgao (kwa kubumba) wa umeme kwa lugha za kiufundi ili waendelee kufaidi kutokana na biashara zao za majenereta na mafuta. Sasa Wizara kwa kutaka kupigania maslahi ya wananchi wakawakatalia na hapo ndipo huyu kilaza anaamua kukata umeme mwenyewe kwa kiburi cha mwenyekiti wake anayetengeneza mamilioni ya fedha za nje (USD) kwa kila mwezi kupitia mgao wa kubumba.

Kilichoniuma kuliko vyote ni kwamba huyu Mh. Mwenzangu mwanadada kwa nini alinifuata na kunilisha nami chakula kichafu kama zilivyo fedha chafu bila mimi kujua, nitamshughulikia kibinafsi . Nimepata ukweli kuwa huyu mwanamama ni Mpenzi wake huyo MD na watu kibao wanalijua hili na yeye anatumia nafasi yake ya ujumbe kwenye kamati husika ya Bunge kuendelea kumfanya huyu MD buzi lake la kudumu. Tanesco.

Na kwamba haikuwa tu kwangu bali kawatembelea wengi akiwa na fuko la fedha akijaribu kugawa kwa usiri sana na kushawishi eti tukatae bajeti ya Wizara na pia wamfukuze Katibu Mkuu wa Wizara (eti wanasema anajifanya kuleta ulokole wa kisabato, kitu ambacho ni kweli huyu jamaa ni wa SDA lakini kosa lake sasa nalifahamu kuwa ni kwamba amekuta ameingia katika anga za TANESCO- mradi wa watu wachache na sio wa umma.


Hitimisho:
1. Wabunge tuweni macho (Independent Committee iundwe kama ya Mwakyembe ) tuone nani anasema ukweli na awajibishwe. Suala laBajetu hatuhitaji kufundishwa sisi tunawasubiri wao waiwasilishe tutaipima na kuuliza maswali yanayopaswa.

2. Mamlaka husika, vunja hiyo Bodi ya TANESCO kabisa sasa hivi na wawekwe watu wasiohusika na mahusiano ya kimaslahi na watumishi wa TANESCO na wawe wenye uwezo wa kuisimamia vyema. Why always taking retired people? Tanzania ni kubwa sana na ina wasomi kibao na wenye uwezo wa kuongoza Bodi kibao!!

MD na Mh. mpenzi wako na shoga wako na hii Kamati ya Bunge inayosimamia Wizara ya Nishati kuweni macho na kila mnachotaka kukifanya sasa maana media, wala kusambaza barua kwa Rais, PM na kwa Waziri mhusika haitawasaidia. Umma wa watanzania leo umesha wamulika kuwa ninyi ni wahujumu wa uchumi.

Sisi wabunge wenye akili na wananchi tutawaangukia ninyi na yeyote ambaye anataka kuwaunga mkono katika upuuzi wa kuihujumu TANESCO, kutumia mhusiano ya kimapenzi kujaribu kutuhadaa na zaidi ya yote kushindwa kuongoza shirika hili la TANESCO NA KUJITUNGIA MIGAO YA UMEME ILI MFAHIDI !
chanzo; https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...mhando-wa-tanesco-na-mh-mbunge-ni-hatari.html

Nishati na Madini yawagawa wabunge Send to a friend
Monday, 23 July 2012 20:59




digg

prof-muhongo.jpg
Waziri wa Nishati na Madini, Pofesa Sospeter Muhongo

KATIBU MKUU AZILIPUA KAMPUNI ZA MAFUTA, ASEMA HAKUNA MGAWO WA UMEME
Mwandishi Wetu
WAKATI baadhi ya wabunge wakitaka kuwachukulia hatua Waziri wa Nishati na Madini, Pofesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakimu Maswi kwa madai ya kuiuka sheria ya Ununuzi wa Umma, mtendaji mkuu huyo wa wizara ametupa kombora la ufisadi dhidi ya baadhi ya kampuni za mafuta nchini.Wanaowatuhumu akina Muhongo na Maswi wanadai kuwa, walikiuka sheria ya ununuzi wa umma kwa kuipa zabuni Kampuni ya Puma Energy ya kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL na kuziweka kando kampuni zilizokuwa zimechaguliwa kupitia mchakato halali wa zabuni ya Tanesco.

Suala hilo linahusishwa na kusimamishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, William Mhando kwamba alichukuliwa hatua baada ya kukataa kutii maelekezo ya Wizara.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonyesha kuwa kumekuwa na mgawanyiko miongoni mwa wabunge, ambao unaanzia kwenye Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo hadi sasa hawajaafiki uamuzi wa kuwachukulia hatua viongozi hao.

“Ni kama tumeshindwa kuelewana huko kwenye Kamati, lakini wabunge ndio tumekuwa tukilalamikia ufisadi Tanesco, sasa tunawashangaa wenzetu ambao wameanza kuiandama tena Serikali kwa kuchukua hatua,” alisema mmoja wa wabunge wa CCM.

Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa CCM alisema kuwa, Muhongo na Maswi walikiuka sheria.

“Tutakuwa tunakosea, tukiruhusu hawa watu wavunje sheria na halafu eti tuwaachie,” alsema mbunge huyo.

Nje ya Kamati hiyo, wabunge bila kujali itikadi zao nao wamegawanyika huku wengine wakitaka viongozi hao wachukuliwe hatua kuhusiana na suala hilo na wengine walisema: “Hakuna kosa walilofanya, waachwe waendelee na kazi.”

Chanzo cha mgawanyiko huo ni sababu zilizotolewa na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kwamba waliwapa Tanesco fedha za kununua mafuta mazito ili kuiepusha nchi na mgawo wa umeme, lakini wakaelekeza mafuta hayo yanunuliwe Kampuni ya Purma ambako bei ya lita moja ni Sh1,460.

Kwa kufanya hivyo uongozi wa Wizara unadaiwa kuokoa kiasi cha Sh3 bilioni ambazo zingetumika kama mafuta yangenunuliwa katika kampuni zilizokuwa zimeshinda zabuni kupitia mchakato wa Tanesco.

Ndani ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, baadhi ya wajumbe walinukuliwa wakisema kuwa hata kama Muhongo na Maswi walikuwa na nia njema ya kuokoa fedha za umma, lakini waondolee kwa kukiuka sheria.

Hata hivyo, hatua hiyo inapingwa na baadhi ya wajumbe wanaosema uamuzi waliofanya (Muhongo na Maswi) unapaswa kupongezwa, kwani ni mwanzo wa kumaliza ufisadi ulioota mizizi ndani ya Tanesco na Wizarani kwa ujumla.

Maswi afunguka
Maswi katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, aliwatupia kombora baadhi ya wamiliki wa kampuni za mafuta akisema zimekuwa zikifanya vitendo vya ufisadi na kutaka Watanzania wazalendo kuunga mkono juhudi za wizara yake za kupambana na hali hiyo.

Maswi alifafanua kwamba, baadhi ya kampuni (majina tunayo) zimekuwa zikinunua mafuta kwa bei rahisi kutoka Puma Energy na kisha kuiuzia IPTL kwa bei ya juu na kupata mabilioni ya shilingi.

Mtendaji mkuu huyo wa wizara alisema haiwezekani kwa akili ya kawaida Serikali iache kusimamia fedha za umma kwa kuhakikisha mafuta yananunuliwa kwa bei nafuu moja kwa moja toka Puma Energy badala ya kununua kwa mtu wa kati ambaye anaongeza bei ya mafuta hayo.

Akitoa mfano wa ufisadi unaofanywa na baadhi ya kampuni, Maswi alisema kuwa, Januari mwaka huu kampuni moja kati ya zilizopata zabuni ya kupeleka mafuta Tanesco, (jina tunalo) ilinunua mafuta kutoka kwa Puma Energy kwa bei ya Sh 1,068 kwa lita moja ya ujazo, kisha ikaenda kuuzia IPTL kwa Sh1,860.

“Kwa hiyo, haya mambo Watanzania wanapaswa kuyafahamu. Na ninyi waandishi msaidie kuandika mambo yenye maslahi kwa taifa. Mimi nitasimamia maslahi ya taifa, hatuwezi kuacha kununua mafuta kwa bei rahisi halafu tununue kwa bei ya juu. Shilingi moja tu kwa mfano, katika maisha ya Mtanzania ni kubwa. Si mnaona mkipandishiwa bei ya dizeli na petroli mnavyolalamika!” alisema.

Akizungumzia tuhuma za kukiuka sheria kwa kuipa zabuni PUMA Energy, Maswi alisema mchakato wote ulifanyika na kukamilika kabla hajateuliwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

“Ikumbukwe kuwa niliteuliwa kuja Wizara ya Nishati na Madini, tarehe 22 Julai, 2011 siku ya Ijumaa na nilianza kazi kama Kaimu Katibu Mkuu Julai 25, 2011 siku ya Jumatatu. Kabla ya kuanza kazi niliwaeleza wenzangu utendaji wangu na ninavyopenda twende kwa kufuata utaratibu,” alifafanua Maswi.
Alifafanua kwamba mwishoni mwa mwaka 2010/11 kulikuwa na mgawo mkubwa umeme nchini, na Serikali kulazimika kuingilia kati kuhakikisha mgawo huo unaondolewa na kuitaka IPTL kuwasha mitambo yake katika kiwango cha megawati 100.

“Aliyefanya hivyo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco na siyo Wizara. Ikumbukwe pia kipindi hicho IPTL ilikuwa inasimamiwa na Wakala wa Vizazi na Vifo (Rita) kwa kuwa kulikuwa na amri ya kufilisi (under liquidation process).” alisema Maswi


Aliongeza kwamba, Tanesco ilifanya hivyo kwa barua Kumb. Na. SMSC/MSC/IPTL ya Juni 10, 2011 ambapo kampuni hiyo ilitakiwa kuanza kufua umeme hadi Desemba 2011 na kuondoa mgawo wa umeme.

“Aidha, Tanesco walipeleka barua RITA wakitaka mafuta ya kuendesha mitambo yapatikane. Ieleweke kuwa ili kuendesha IPTL kwa siku moja tunahitaji MT500,” alifahamisha Maswi.

Mgawo wa umeme
Kuhusu mgawo wa umeme, Maswi alisema kumekuwa na upotoshaji wa makusudi kuhusu suala hilo.

Alifafanua kwamba, kwa jinsi Serikali na Tanesco walivyojipanga kuanzia sasa hadi Desemba, hakutakuwa na mgawo wowote wa umeme.

Maswi alisema uwezo wa juu wa ufuaji wa umeme (installed capacity) kwa sasa ni Megawati 1,375.74, ingawa, wastani wa uwezo halisi (available capacity) ni Megawati 873.

“Kwa upande mwingine, wastani wa mahitaji ya umeme kwa sasa ni kati ya Megawati 650 hadi 720,” alifafanua Maswi.

Alisema kutokana na hali halisi Serikali na Tanesco wamejipanga kuhakikisha hakuna mgawo wa umeme kuanzia sasa hadi Desemba.

Akitoa mchanganuo wa uzalishaji umeme, Maswi alisema nguvu za maji itazalisha megawati 120 hadi 151 (wastani wa megawati 132).

Mitambo ya gesi asili, itakuwa ikizalisha wastani wa Mewagawati 348 na mitambo ya mafuta itazalisha megawati 240.


chanzo: Nishati na Madini yawagawa wabunge
 
Kweli wapo wanaoendelea kufikiria tatizo ni "watu"; wanaamini "sera ni nzuri" ila "zimekosa watekelezaji". Tangu sera ya Nishati na Madini ya 1992 (chini ya JK) hadi leo hii kweli nchi imekosa watekelezaji? Kwanini hamtaki kusema ukweli kwamba sera ya nishati imeshindwa?

Nadhani siku hizi Mzee Mwanakijiji anaamini tatizo lilikuwa ni watu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom