JF EXCLUSIVE: Sababu ya Kuachishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF EXCLUSIVE: Sababu ya Kuachishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Jul 14, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco, Robert Mboma amekataa kuhudhuria mkutano wa waandishi wa habari unaotarajia kumsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, William Mhando.

  Uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhando unatokana na bifu linalosemekana kuwapo kati ya Mhando na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi; lakini katibu mkuu huyo ametumia udhaifu wa serikali na tanesco kumwadhibu Mhando.

  Inasemekana sababu inayotolewa na Katibu Mkuu ni kwamba Mhando alimdharau kwa kutompa taarifa kabla ya Tanesco kutangaza mgawo wa umeme wa hivi karibuni. Kwa mantiki hiyo, akamlima Mhando barua akisema anahujumu shirika. Hata hivyo, wananchi na watumishi wa Tanesco wanajua kuwa anayehujumu Tanesco ni serikali, ambayo inalinyima shirika hilo pesa ilizoahidi kwa ajili ya miradi ya uzalishaji na usambazaji wa umeme, na kulizuia shirika hilo kuuza umeme kwa faida, kwa sababu za kisiasa.

  Inasemekana hatua dhidi ya Mhando inatokana na woga wa waziri na katibu mkuu juu ya mjadala mkali unaotarajiwa kuibuka bungeni wakati wa kujadili bajeti ya wizara yao. Mhando anatolewa kafara kisiasa, lakini taarifa zinasema naye amejibu barua ya katibu mkuu kueleza jinsi asivyohujumu shirika hilo. Habari zaidi baadaye.

  source east africa radio breaking news

  Breaking news:mkurugenzi mtendaji wa tanesco william mhando asimamishwa kazi
  [​IMG]

  Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi WILLIAM MHANDO (pichani) ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa dhidi ya Menejimenti ya TANESCO.

  Taarifa hiyo imetolewa na mwenyekiti wa bodi hiyo Jenerali Mstaafu ROBERT MBOMA ambapo katika taarifa yake amesema maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha dharura kilichofanyika jana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.


  Taarifa zinasema katika kikao hicho, Bodi iliona tuhuma hizo ni nzito hivyo ni vyema zikafanyiwa uchunguzi huru na wa kina mara moja
  KWA HABBARI KAMILI BOFYA HAPA

   

  Attached Files:

 2. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,100
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280  .........
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Ndiyo yale yale ya kuwataka madaktari warudi kazini na kutoa huduma kwa wagonjwa huku wanajua kabisa CT Scan haifanyi kazi, X Ray machines zinasuasua na hata gloves zinapatikana kwa mbinde. Serikali inataka "optimal performance" lakini haitoi "Optimal cooperation"! Wanataka wavune wasichopanda!!!

  Mhando hakutakiwa kusubiri hadi apigwe mkwara; alitakiwa ajiuzulu kazi na kugoma kama walivyofanya madaktari. Utaweza vipi kumkamua ng'ombe maziwa wakati halishwi?

  Tukisema sera yao ya nishati ni mbovu watu wanasema "ooh siyo sera ni watu!"!
   
 4. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kiongozi wa nchi dhaifu, so wateule wake dhaifu pia. Na huyu mjeshi wa meremeta, na muuzaadini yetu anafanya nn tanesco..? hivi hakuna mainjinia wanaofaa kuongoza bodi..? Kama dhaifu anampenda sana mpeleke ktk bodi za wanyamapori akatoe mbinu za kuwalinda akina joji- faru ( hope sio kuiba twiga zaidi..!!)
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red umeniwahi. Ni lini watendaji wataishi dhana ya kujiuzulu pale wanapogeuzwa 'waimba mapambio? Mabwawa ya maji 'yalishakataa' kujaa maji sasa wanafanya nini hawa watu ofisini huku wakijua hakuna umeme utakaozalishwa? Na sasa mfumo wa 'kukataa' umehamia kwenye upatikanaji wa gesi, wakina symbion kila kukicha hawana gesi - kisa? gesi 'imekataa?
   
 6. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  yesu wangu,kumbe watu wanahangaika na umeme kumbe ni jitu moja kwa sababu zake binafsi ndilo linalosababisha,...mnh,.....:wacko:
   
 7. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Duh inavyoonekana wanataka kujifanya wamechukua hatua ili wapate cha kujieleza wakati wa budget yao ikifika. Naona kama mnamtoa kafara tu mhando
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Serikali yetu ipo hivi......
  1. Kwenye kila tatizo la nchi hii kuna mtu/watu wa/ananufaika nalo
  2. Mtu akishupalia kitu kwa nguvu ana maslahi au kanyimwa ulaji

  Kwa kifupi ni hatupo "Real" kabisa, huyo katibu mkuu kaandika hadi povu limemtoka ila ukija kuambiwa mengine yake utachoka kabisa !

  Haya Mzee Mboma naye kwanini akimbie waandishi wa habari??

  Hamna hata mwenye maana hapo kwenye mtiririko mzima wa kisa ni kama vita ya kiroho yaani inapiganwa kwenye ulimwengu mwingine, sisi tunaona vitimbi tu ambavyo haviingii kwenye akili ya mtu mzima....

  Mambo haya ndio yamekuwa yakitufanya watu wengine tubaki na misemo tu kuwa "Nchi hii bado sana"
   
 9. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  I love jamii forums... Yaani humu ndani utafikiri ni usalama wa taifa yaani mpaka barua iliyotumwa ikulu imefika humu ndani. Nice work ppooooo
   
 10. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #10
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,100
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280


  ...............
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Baada ya kupitia madai ya Katibu na majibu ya Mhandisi Mhando nimegundua kuna mambo makuu mawili:

  1.Siasa
  2.Matumizi mabovu ya madaraka!


  Hayo yote nimeyaona yakitawala mezani kwa Katibu mkuu, anajaribu kutumia mamlaka aliyonayo kutawala kisiasa mambo ya kitaalamu yasiyohitaji siasa!

  Anajaribu kutokeza akiitaka shikamoo/kunyeyekewa kitwana kwa mambo aliyopewa taarifa ya zaidi ya mamra moja (simu, barua na mdomo)

  Sijui hapa Katibu anasimamia kuwa kosa la Mhando ni kuwa alichukua hatua kabila ya kujibiwa kwa maandishi au nini?

  Bajeti haikwepwi kwa staili hiyo, walifanikiwa kwa Jah Hero lakini kwa hapa wamechemka kabisa!
   
 12. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana nawe,lakini tatizo ni mfumo mzima ndio mbovu, kuna kunyenyekeana sana na kutukuzana.....nafikiri huyu Mhando alipaswa ajiuzulu mapema sana kwani serikali haimpi ushirikiano ihali anabaki kunyenyekea na kutukuza.
  Ona sasa ametolewa sandakarawe ili bajeti ipite.
   
 13. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nakushukuru sana mleta thread,,kwenye inshu nzima naona ni suala la kujisafisha/kujihami na mjadala wa bajeti yao tu.
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kama Mkurugenzi na Katibu Mkuu wanashindwa hata kupigiana simu wakajulishana juu ya mgao wa umeme basi uhusiano kat ya Wizara na Tanesco una matatizo makubwa kuliko inavyoonekana. Yaani Katibu Mkuu naye anausikia mgao kwenye vyombo vya habari!!!!
   
 15. D

  Doreen22 JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 475
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  So, ina maana wanaonea dagaa?!, wanawakwepa kambale!
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Naona ni WIVU wa Mhando kuwa na GENERETA wakati Katibu Mkuu hanalo; Sasa Anamsimamisha na baadaye

  Atamwambia asiiwashe hiyo GENERETA auone utamu wa GIZA
   
 17. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu wala usishangae, kuna wizara nyingine Katibu mkuu aelewani na Waziri hata waziri akitoa amri jambo fulani kufanyika Katibu mkuu anapuuzia tu au anafanya atakavyo! Kisa cha kutuniana misuri: "wote wanateuliwa na RAIS!" Bila ya kurekebisha suala hili la uteuzi wa viongozi wakuu Serikalini, uendeshaji wa utawala utakuwa mgumu sana.
   
 18. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ndio maana ikawa kila siku tunasisitiza, kazi na maamuzi ya kitaalamu yafanywe na wataalamu na sio wanasiasa. Kumfukuza Mhando hakutapelekea mabwawa kujaa mali wala kupatikana mafuta ikiwa hakuan pesa, hasa ikitiliwa maanani kuwa shirika/serikali imekuwa mdaiwa sugu wa makampuni ya mafuta.

  Kwa kumfukuza kazi Mhando, Wizara isidhani itasalimika kulaumiwa na wapinzani na wananchi kwani wanaelewa juu ya ukosefu wa nia safi kwa upande wa serikali juu ya kutatua tatizo la umeme. Kinyume chake, katika kikakao hiki cha kuliko vikao nyengine vyovyote, wapinzani watawalimeni kisawasawa kwani ahadi zimekuwa nyingi na Watanzania wameshachoshwa nanyi.

  Kitu pekee ambacho serikali ingefanya, kama imebakiwa na akali ya uungwana, tahayuri na huruma kwa Watanzania, ni kujiuzulu kwa mpigo!
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi Mkurugenzi anareport kwa nani? Nilidhani taarifa kati ya TANESCO na Wizara zinapitia kwenye bodi!
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nasikia majuzi umeme ulikafika Bungeni wakati Prof. Tibaijuka anahitimisha hotuba yake ya budget ya wizara ya ardhi. Ndio hujuma hii?
   
Loading...