JF Exclusive: OC CID Kawe... (inahusiana na Dr. Ulimboka)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
''mm sijahusika kabisa na kutekwa kwa Ulimboka. Jamani msinidhuru. Tena cku hyo mm ckuwepo'.. David Mapunda

OC CID Kawe (Mkuu wa Upelelezi) David Mapunda amepata ajali ya gari akiwa amesimama nje ya gari lake (gari lilitokea na kumgonga). Amevunjika pelvis na licha ya jitihada za kukwepa kupelekwa Muhimbili alijikuta anaishia mikononi mwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI). Vyanzo vya ndani vya Intelligensia iliyokuhubu vinadokeza kuwa Afande huyo wa polisi amejikuta aki"sema" mengi kuhusiana na "kutokuhusika kwake" na tukio la utekaji nyara, kuteswa na jaribio la mauaji ya Dk Ulimboka.

Kwa mujibu wa "Nzi" ambaye amekuwa akiendesha uchunguzi "mbadala" wa kukusanya intelligensia ya suala hili:

Kumekuwa na doria za kila mara ndani na sehemu mbali mbali za wodi za MOI mpaka staff wamefikia kulalamika juu ya hilo japo maaskari hao wamekuwa wakijibu kwa jeuri kwamba wapo kazini.
Ndugu na jamaa wa afande huyo wamekuwa hawana amani kwa hofu kwamba ma-dr wanaweza kulipiza kile alichofanyiwa mwenzao Dr. Ulimboka. Kumekuwa na maoni mchanganyiko kutokana na kuweweseka kwa afande huyo na kuropoka ovyo. Wapo wanaodai kwamba ''amri ya Ulimboka kukaa zaidi ya masaa matatu katika kituo cha polisi Bunju ni kutokana na order alizotoa afande huyo kwamba akae na asipatiwe matibabu ya haraka''.

Haijulikani kama ajali yake ni tukio lililokusudiwa kumnyamazisha daima au ni ajali ya kawaida.

Ni matumaini yangu madaktari watamtendea kwa kadiri ya uwezo wao wote kuokoa maisha yake.

ADDITION:

From "Nzi":

Mkuu MM tunaendelea kumonitor..:
OC CID KAWE APATA AJALI NA KUSEMA MENGI KHS DR.ULIMBOKA
Mkuu huyu jamaa alipata ajali jana baada ya kugongwa na gari akiwa amesimama nje ya gari. Amevunjika Pelvis. Alifikishwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili jana Mchana. Alifikishwa hapo baada ya kuzungukia hosp mbalimbali za jijini ikiwamo ''Lugalo referral hosp'',mmala na aga khan lakn akaambiwa kwamba kwa fracture kama hyo lazima afike muhimbili-MOI in particular. Baada ya kuona kwamba hawezi kuepuka kwenda muh2, ikabidi aende tu huko lakn akiwa hana amani. Baada ya kufika MOI wafantakazi wa Taasisi hyo walishangaa kundi kubwa la askari wakimwagwa hosp hapo ndio wakaanza kujiuliza ni nn kinaendelea?
Katika hali isiyo ya kawaida,afande huyo akaanza kujitetea huku akiwa na uchungu mkubwa kwamba ''mm sijahusika kabisa na kutekwa kwa Ulimboka. Jamani msinidhuru. Tena cku hyo mm ckuwepo''. Hali iliendelea kuwa hivyo hasa pale alipotakiwa kuchomwa sindano,alionyesha uoga na kuuliza ''Jamani mnanichoma sindano gani hyo,msiniue jamani?''. Wakati hayo yakiendelea,mama mzazi wa afande huyo aliwashangaza watu alipomfata Dr mmoja(jina linahifadhiwa) kwa kutambaa na kumuomba huyo Dr kwamba ''jamani mwanangu hakuhusika kabisa jamani. Naomba mumsaidie

ADDITION:
Mpango wa kumpeleka India uko njiani japo vyanzo vinadokeza kuwa tatizo alilompata linaweza kutibiwa hapa hapa nchini.... wakati huo huo...

Yupo askari mwingine wa polisi ambaye naye amepata tatizo la kudislocate mguu na amekuwa hospitali kwa wiki kama tatu lakini hakuna mtu ambaye ana wasiwasi kuwa anaweza kudhuruliwa; wanauliza kwanini Mapunda wanapata pressure kubwa?

July 25, 2012 (Magazetini)

Kigogo polisi atoboa siri kipigo cha Dk. Ulimboka

• Alazwa Muhimbili, awaomba madaktari wasimdhuru

na Betty Kangonga na Abdallah Khamis

MKUU wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Kawe (OC CID), David Mapunda, ametoa siri ya kutekwa, kupigwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari, Dk. Steven Ulimboka.

OC CID huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) alilazimika kutoboa siri ya kipigo cha Dk. Ulimboka ili aweze kupata matibabu ya majeraha ya ajali ya kugongwa na gari aliyoipata juzi.

Dk. Ulimboka alipookotwa na wasamaria wema katika msitu wa Pande na kufikishwa katika kituo cha polisi Bunju, kilicho chini ya kituo cha Kawe, OC CID huyo anadaiwa kutoa amri ya Dk. Ulimboka kukaa zaidi ya saa tatu ili asipate matibabu ya haraka.

Vyanzo vyetu vya habari vililiambia gazeti hili kuwa mara baada ya kugongwa na gari juzi, kigogo huyo wa polisi alijitahidi sana kukwepa kwenda Muhimbili lakini alijikuta akiishia mikononi mwa madaktari wa taasisi hiyo ya mifupa ya Moi, hivyo aliingiwa hofu ya kutotendewa haki ya matibabu.

Kabla ya kufikishwa Muhimbili, askari huyo alikwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Lugalo na Aghakan, lakini alijikuta anatakiwa kufika Kitengo cha Mifupa cha Moi, Muhimbili, ambako hadi sasa bado anaendelea na matibabu.

Kwa mujibu wa habari hizo kutokana na hofu ya kususiwa na madaktari, polisi huyo alilazimika kuwapigia magoti na kueleza mengi kuhusu kipigo cha Dk. Ulimboka na kwamba yeye hahusiki na sakata hilo.

Mtoa habari wetu alisema kuwa OC CID huyo mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo akiwa na maumivu makali, alisema hahusiki na kipigo cha Dk. Ulimboka na hata siku ya tukio hakuwepo.

Katika hali isiyo ya kawaida, kigogo huyo alijitetea huku akiwa na maumivu makali ya majereha aliyopata.

"Mimi sijahusika kabisa na kutekwa kwa Ulimboka. Jamani msinidhuru. Tena siku hiyo mimi sikuwepo,' alikaririwa OC CID akisema.

Habari zaidi zinasema kuwa askari huyo aliendelea kueleza mengi na hata alipotakiwa kuchomwa sindano, alionyesha woga na kuuliza anachomwa sindano gani.
Ili kuhakikisha anatibiwa vizuri, kumekuwa na doria za kila mara ndani na sehemu mbali mbali za wodi za MOI hali iliyowafanya madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo kulalamikia hali hiyo.

Mbali ya OC CID huyo kuingiwa na hofu ya kulipiziwa kisasi, hofu hiyo pia imewakumba ndugu zake kwani hawana amani na matibabu ya ndugu yao.

Tanzania Daima Jumatano ilipofika katika hospitali Muhimbili, ilishuhudia kuwapo kwa askari polisi wakilinda doria, huku OC CID akiwa amelazwa chumba cha peke yake akiendelea kutibiwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, mmoja wa madaktari wa Muhimbili ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema Mapunda alifikishwa hospitalini hapo juzi akiwa katika hali mbaya na mara baada ya kufikishwa aliomba msamaha kwamba hakuhusika kumteka Dk. Ulimboka.

"Ni kweli jamaa alipokelewa lakini tulishangaa kwani alikuwa akiongea kwa kuweweseka kwamba hajahusika na tukio la kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka na akawa anaomba tusimdhuru," alisema daktari huyo.

Kwa mujibu wa daktari huyo, kilichowashangaza zaidi ni ulinzi mkali wa polisi aliowekewa mgonjwa huyo huku kukiwa na watu wanaofuatilia kila anayeingia katika wodi namba D aliyolazwa.

Afisa Uhusiano wa Moi, Jumaa Almasi, alisema mgonjwa huyo alifikishwa hospitalini hapo wiki iliyopita akiwa amepata majeraha mwilini baada ya kugongwa na gari.

Kuhusu mgonjwa huyo kumtaja Dk. Ulimboka, Almasi, alisema hawezi kuzungumzia tukio hilo kwani hakuwepo wakati akifikishwa hospitalini hapo.

Kwa Upande wake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kupata ajali kwa OC-CID Mapunda na kuongeza kuwa ajali hiyo aliipata wakati akitekeleza majukumu yake.

Alisema hakuna uhusiano wowote wa tukio la kutekwa Ulimboka na ajali hiyo.
Tangu tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka serikali kupitia maafisa wake wa usalama wamekuwa wakihusishwa kwa namna moja au nyingine.

Kuhusishwa huko kwa serikali hususan jeshi la polisi kunafuatia matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na afisa upelelezi kutoka kituo cha Selanda Bridge katika eneo la Muhimbili, matamshi ya kutatanisha ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova pamoja na kukamatwa kwa mtu aliyedaiwa kuungama kanisani kuwa ndiye aliyemteka na kumtesa Dk. Ulimboka.

CHANZO: Tanzania Daima
 
ajali haina kinga hutokea sehemu yoyote kwa mtu yoyote, na wala isihusishwe na mambo ya ulimboka. Get well soon kamanda
 
Madr wamerekodi maelezo yake kama sehemu ya ushahidi, kwa nini aseme hivyo, kimantiki ina maana anawajua watekaji wa Dr Ulimboka au ulivyokuwa mpango mzima wa utekaji.
 
"For every Action there is an equal and opposite reaction" Newton 3rd law of Motion!! Aint sure if it can be applied here!!!
 
Hilo ni ni pigo tosha toka kwa Mungu, yeye wamtibu tu atakuwa amejifunza kitu.
 
Drs watamsaidia kwani maadili ya kazi zao yanataka hivyo.

Ila kumbuka hao ma Dr's wanakitu inaitwa "NAFSI". Hii kitu nafsi ikiota kutu huwa hakuna cha maadili wala Kiapo... Ni kama viongozi wetu waliokula kiapo cha "NITASEMA KWELI DAIMA UONGO KWANGU MWIKO" "SITAPOKEA WALA KUTOA RUSHWA"

Swali je?? Wanatekeleza... Usinijibu ila Jibu lako liunge kwa Dr's...
 
Si kuna dawa ya kumfanya mtu aongee ukweli (l know from movies msinishambulie); l wish madaktari wangetumia hii kitu!
 
Kama amevunjika pelvis anzeni maombi. Kuna uwezekano utumbo mpana, kibofu cha mkojo, mirija ya mkojo na mishipa ya damu na fahamu vimeathirika.
Polisi anzeni kuchangishana fedha kumpeleka kusikojulikana chini ya ulinzi mkali akatibiwe.
 
Back
Top Bottom