JF Exclusive: Makubaliano ya SFO na BAE Sytems yaliyoiweka Nje Serikali ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF Exclusive: Makubaliano ya SFO na BAE Sytems yaliyoiweka Nje Serikali ya Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 29, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  bae-sfoagreemend.png
  Kuna nyaraka za aina mbili; ya kwanza ni makubaliano ya BAES na SFO kuhusiana na sakata la Rada la Tanzania. Tutaona kuwa serikali ya Tanzania haikuwa sehemu ya kesi yenyewe wala haikutoa hata hoja za kisheria.

  Nyaraka ya pili ni jaribio la taasisi za harakati kuzuia makubaliano hayo (CAAT na Corner House). Kinachoshangaza ni kuwa muda wote tangu makubaliano hayo yaingiwe Serikali ya Tanzania haikujaribu hata mara moja - as far as I know kujaribu kuzuia makubaliano hayo. AG wetu hakutoa hoja yoyote au hata kujiunga na wanaharakati hawa. Naamini serikali ingefanya hivyo ingejionesha kweli inajali kwani makubaliano haya (ukisoma pingamizi la wanaharakati) yameipendelea sana BAES.

  Inasikitisha vyombo vingi vya habari havijaripoti sakata zima hasa siku za karibuni kwa usahihi na hii inawezekana ni kutokana na watu kutokuchukua muda kujifunza juu ya sakata zima na badala yake wanakuwa wanatoa ripoti tu hata zisizokuwa sahihi. Natumaini nyaraka hizi zitawasaidia waandishi na wengine kuweza kuzungumzia sakata la rada na fedha za hisani toka BAES kwa usahihi zaidi.
   

  Attached Files:

 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Asante MMKJJ kwa hayo: Lakini pamoja na yote mimi nina tatizo na Membe anapodai kuwa BAE iliibia serikali ya Tanzannia hela zake na hivyo ni haki ya serikali kuzidai na kuzipata. Namuuliza hivi: Hivi ni lini BAE wailkuja na kuvunja mabenki yetu, BoT au Hazina na kuiba hizo hela?

  Akiweza kujibu hilo swali hapo ndiyo nitakubaliana naye.
   
 3. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante sana Mzee Mwanakijiji,
  Umetoa changamoto kwa waandishi kuandika "kwa usahihi zaidi" kuhusu sakata la rada hasa baada ya kupata na kusoma nyaraka hizo.

  Kwani umeshawasahau waandishi wetu wanapendelea kuandika kuhusu nini? Wengi wao ni "press secretaries" wa ruling party Mzee. Tusaidie kuandika hilo kwa faida ya watanzania wa vijijini wanaopotoshwa kila kukicha ili watawala wabovu waendelee kubaki madarakani. Heshima sana kwako Mkuu.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hata mimi hilo ndilo linalonitatiza katika sakata hili. Wenyewe tuliwaruhusu watuibie halafu tukakaa kimya tu, pasipo hata kuwawajibisha wale walioruhusu wizi huo. Mr Membe, tujibu swali hilo kwanza maana nimekusikiliza katika taarifa zako mbali mbali kuhusu suala hili, hilo hulikwepa, na huligusii kabisa.
   
 5. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Akina membe wanachachamaa nchi yetu kupangiwa namna huyo fedha itakyoletwa (Kwa kutumia NGO ZAO) na namna zitakavyotumikwa kwa namna NGO hizo zitakavyoona inafaa.. Iweje akina membe wasikubaliane ili hali wao i hakuifungili kes hiyo BAE... kama ni uchunguzi, ulifanywa na SFO .. hakukuwa na makubaliano kwamba ushahi wao pia utumike Tanzania na SFO si mali ya Tanzania.. mali ya Tanzania ni PCCB.. wao walisema kila kitu safi.. sasa iweje tena leo wakane kauli zao na kusema kuna wizi wakati tuliambiwa na PCCB kwamba mambo ya Rada ni usafi mtupu? Pia kuhusu fedhwa hizo kurudi serikalini Tanzania.. sikubaliani kwa sababu tu kwamba wale waliotufikisha hapa akiwe yule aliyesema tule nyasi bado wana hisa serikalini... ni wabunge...chenge yuko ndani ya chama, Lowasa na wengineo kibao...na hata hao wabunge waliokuja kuzifuatilia utaona kwamba kwamba aslimia 95 kati yao ni chama twawala..ya nini tuwaamini wakati walituambia mambo yakuwa safi mpaka mwanamume mwingine na serikali yake SFO NA uk KUJA kutupigania na kutuonesha kwamba kulikuwa kuna dalili ya kila aina mlungula ulitembezwa hadi kwa policy makers. Chenge na wengineo....

  Wawape wenzao na wao wale maana tayari wamekura zao sasa ni zamu yetu kupitia mashirikia ya NGO YA WAGENI nasi tule kiaina hata kama mlo hautakuwa kamili basi na sisi tutaonja walu kidogo...
   
 6. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Nadhani BAE na SFO walikubaliana kuyamaliza kiutuzima kwa style hiyo ili kulinda maslahi ya UK. Otherwise

  • BAE ambayo ndio muajiri mkubwa uk, kampuni kubwa na expoter mkubwa angefutiwa licence yake ya biashara EU
  • Naamin SFO wangeanika uchafu wote hadharani basi chenge Vithlani , some officers wa BAE and Co leo hiii wangekuwa segerea ya UK. kwamakosa ya kuomba kupokea na kutoa rushwa
  • Kama BAE ingekuwa ni kampuni ya Tanzania , china au nchi nyingine na Chenge angekuwa raia wa UK basi angekuwa yuko rumande siku nyingi
  SFO wamejaribu kuilinda BAE kwa maslahi na interestza UK. sasa sijui sisi Tanzania tunawalinda hao individual waliohusika na hiyo rushwa kwa maslahi ya nani ?
  Inashangza kwa kuwa SFO wamefunga kesi ndio kigezo hicho hicho DPP wetu na TAKUKURU wametumia kulimaliza hilo suala.


  sijui NGO yetu ya mzeee wa vijisenti inaendeleaje? Na hivi inaitwaje
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Namshangaa Membe, anajishaua tu, wezi wa hizo pesa zetu anawajua, Ina maana hajui Chenge et al ndio wezi wetu, lakini hawataki kuwabana warudishe hivyo vijisenti walivyoficha nje ya nchi. Shame!!!!
   
 8. M

  Marytina JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  100 Thanks to Mwanakijiji
   
 9. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Naifikiria hii serikali yetu bila majibu.
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Asante kwa documents, ngoja tuzipitie
   
 11. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  MImi mwenyewe nashangaa sana hata kiasi kimekuwa kinanukuriwa vibaya, wengine $20m mara $30M laikini mimi navyojua ni £30M au TZS 75B (hii ni faini) .

  Du kweli wakina chenge vidume kweli sasa naona mifupa ya albino imeaanza kuwasaidi. rada ilinunuliwa $39M na court Inataka GO Tanzania ipewe £30M (less court expenses) ambazo ni sawa na $ $48 kwa sasa. Hii maana yake kuwa rada tungekuwa tumepewa bure. Na membe angekuja bungeni kujisifia kuwa tumepata faida hivyo haka kamchezo ka rushwa huwa kanalipa wakati mwingine.

  Hii ni sawa na hela za EPa ambazo walikuwa wanasema kuwa si za Tanzania lakini ziliporudishwa na mafisadi zikaenda kwenye TIB du! kweli Tanzania ni nchi pekee ambayo rushwa inailipa serikali yake vizuri kuliko hata migodi
   
 12. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulitaka aseme nini?
   
 13. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mawazo hay ni kujenga kweli? Hivi Membe angekaa kimya tungemuelewaje?
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Thread kama hii huwezi kumuona hapa Faiza Foxy, Rits & co, hapo ndio utagunduwa hii forum siku hizi ina magarasa mengi.
   
 15. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kaka kuna matamko huwa yanatolewa na viongozi (sorry watawala) wa nchi hii mpaka unatamani ujivike bomu ulipuke nae.

  Membe anazungumzia kuibiwa lakini hasemi BAE walibomoa BOT yetu wakaiba. Kama hawakubomoa basi its an inside job, kwa nini hawataki kumshugulikia huyo aliyewafungulia wezi ili waibe wakati wengine tumelala.

  Mahali pengine anasema serikali ndio ilitoa hela kwa hiyo inastahili kupokea chenji, sh<nzy taipu kabisa. Nini kilitokea hadi ukalipa mara mbili ya bei?? Je ni kweli wanachotaka kulipa BAE ni chenji na sio kisafisha jina???

  Halafu unaambiwa kati ya watu wanaotamani uraisi 2015 na Benard Membe yumo. Tujiulize bila unafiki hivi kweli Membe ni presidential material???
   
 16. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Membe ni Waziri wa Mambo ya Nje, hana nguvu za kisheria za kuwabana wezi. Suala hili ni la Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Utawala Bora, Waziri Mkuu, na Rais wa nchi.

  Mimi nadhani tumshukuru Membe hata kwa hili maana ni yeye peke yake ktk Serikali nzima ndio aliyekuwa akilisema wazi wazi suala la Rada. Kumbuka Rushwa hii imetokea Wizara ya Ulinzi, mbona hatuulizi humu ndani, Hussein Mwinyi anachukua hatua gani?????
   
 17. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  big up mwanakijiji!
   
 18. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Na kwa Membe kuongea pumba tumweleweje?
   
 19. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusikate tamaa. Tatizo ni pale jukwaa linapogeuzwa kuwa chombo cha kulalamika tu na sio cha kutoa maoni. Hebu tuangalie ni wapi watu walifanikiwa kwa kulalamika?
   
 20. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaongea pumba gani? Lini na wapi?
   
Loading...