JF Exclusive: Hotuba ya Nyerere 1995

Nyerere Baba yetu,tunakukumbuka kwa mawazo yako, the guy has ability to see future, has subconcious mindset.Anyway,kizuri hakikai, kibaya tunacho mpaka leo
 
MwanaFalsafa1, shukrani nyingi kwa ku-upload hizi hotuba za baba yetu wa taifa hayati mwl JK Nyerere. Nimetumia siku nzima kuzisikiliza kwa makini sana na kurudia rudia mara nyingi. Huyu mtu alikuwa kiongozi mzuri tuliyekuwa tumepewa, na maneno yake yanagusa hisia, akili na moyo. Maneno yake yamesheheni hekima na utambuzi uliopeuka. Kama tungeweza kumsikiliza na kumwelewa kisha tukatenda kama alivyotuusia, ni hakika tusingekuwa hapa tulipo sasa. Nitakapo kaa sawa nitazitafuta hotuba zake zote (DVDs) nizinunue ili niendelee kujifunza kutoka kwa mwalimu huyu wa Tanzania. Ijapokuwa amekufa bado angali akinena.
 
Ni kweli mkuu. Tatizo wakati huo watu walikua wanaona asha pitwa na wakati na mawazo yake yame pitwa na wakati wakampuuzia. Uliona alivyo mgeukia Mramba na kumfokea "Basil, kwa nini hamkuanyi kodi?" Yani this speech was visionary.
 
Ni kwenye hotuba hii mwl alizungumzia ubinafsishaji wa washirika ya umma. Alikemea ubinafsishaji wa mashirika hata yale yaliyokuwa bado yalikuwa yanaendeshwa kwa faida na kuonya kwamba tukienda hivyo, tutabinafsisha hadi magereza!
 
Ni kweli mkuu. Tatizo wakati huo watu walikua wanaona asha pitwa na wakati na mawazo yake yame pitwa na wakati wakampuuzia. Uliona alivyo mgeukia Mramba na kumfokea "Basil, kwa nini hamkuanyi kodi?" Yani this speech was visionary.

Mimi nimeona kuwa kemeo lile lilikuwa zaidi ya uelekeo wa Mramba peke yake, bali lile lilikuwa kemeo ama wosia kwa kila mtanzania aliyepo madarakani, asiyekuwepo na atakayekuja kuwa madarakani. Huo ulikuwa wosia mkubwa sana kuuelekeza kwa Mramba peke yake kwani kuna Ngereja, Mkulo, Kikwete, Luhanjo, Balali, Mkapa..nk. Sasa hivi kuna dalili za ki=Mramba kwa kila mwananchi Tz, na mfano mdogo ni uongozi wa jiji la Dar es Salaam uliopekelea kuzalisha neno "masaburi"... huio ni wosia ama kemeo kwa kila mwananchi wa Tz na hata nje ya Tz. Mseven wa Uganda anapaswa kusikiliza hotuba hizo, Kagame, Raila na hadi Somalia. Huo ni wosia wa Africa nzima.

Mimi sijuwi kama hawa viongozi wetu wanazo hizi hotuba na kama huwa wanazisikiliza.. Je wakizisikiliza huwa wanaelewa jukumu lao kama alivyousia Mwalimu? Haya madudu anayofanya Mh Kikwete yanaonesha uwezo mkubwa wa 1.kushindwa kuelewa 2.kupuuzia mambo muhimu 3.tatizo kubwa la ubinafsi na ufisadi
 
Mwalimu alikuwa na uchungu wa dhati wa nchi hii.
Aliiona tanzania kama kaya yake na watanzania kama watoto wake.
R.I.P MWALIMU MKUU WA WATANZANIA NA DUNIA!
 
Nyerere ndiye aliyesababisha haya matatizo yote ya UFISADI,RUSHWA ndani ya TZ. "Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" Nyerere kaileta CCM, Kailea CCM, na Kaiacha CCM. Matatizo haya yote yanatokana na Nyerere.
 
Nyerere Baba yetu,tunakukumbuka kwa mawazo yako, the guy has ability to see future, has subconcious mindset.Anyway,kizuri hakikai, kibaya tunacho mpaka leo

Ndiyo, kwa sababu alijua kabisa vile alivyoiweka CCM madarakani, ndivyo itakavyokua. Nyerere ndiye aliyeleta huu UFISADI.
 
Anatetea haki za Raia na kukosoa mfumo uliopo, kama vile unaokataza haki za mgombea binafsi katika mfumo wa demokrasia za vyama vingi, haki ambazo hata yeye alipokuwa na mamlaka ya nchi hakuzitoa.

Alikuwa mwanasiasa mnafiki sana.
 
Ukisikiliza hotuba amekubali kosa la kuminya vyama vya upinzani. Amekiri yote hayo. Sasa kwa vile Nyerere alikosea basi na wao wengine kuendeleza hayo makosa ni sahihi?
 
Ukisikiliza hotuba amekubali kosa la kuminya vyama vya upinzani. Amekiri yote hayo. Sasa kwa vile Nyerere alikosea basi na wao wengine kuendeleza hayo makosa ni sahihi?
Kama anakubali yeye alivurunda basi anapoteza haki ya kuwa mkufunzi, lecturer, mkosoaji wa mambo ambayo yeye yalimshinda, anafundisha ambayo hakuweza kuya practice. Siasa hizo ni unafik.

Anawaambia wafanyakazi kwamba bado anaamini katika Azimio la Arusha, lakini analaumu msingi wa Azimio wa Kujitegemea umevunjwa kwa sababu tunadhani tumepata mjomba, mfadhili, nje. Wakati wa utawala wake, hakukuwa na nchi Afrika iliyokuwa inapokea misaada ya Wajomba wa Scandinavia kama Taifa la Nyerere. Sasa anamkosoa nani kama yeye yalimshinda haya ya kujitegemea? Hakuwa mkweli hata kidogo.
 
Asante sn bwn kwa kuwezesha kupata hotuba hii, naomba km una hotuba nyingine in any way may be written, recorded(MP3 and / MP4) please help me to have them. Tuwasiliane through andrewwama@yahoo.com. asante sn
 
tunaotumia simu tumeikosa. tunaomba aliye na mashine aifungue na kuitandaza hapa jamvini ili wote tuifaidi. mia
 
Moderator Invisible na Maxmello najaribu kuona uzito wa hotuba hizi katika kutafakari directions ya mambo katika nchi yetu, pamoja na critical view of his idiologies bado ana opinions ambazo zinahold a lot of water for making decission about how we move forward. mfano Htuba yake ya mwaka 1991 alipokuwa akiongea na wajumbe wa NEC ina vission ya ajabu sana jinsi Tanzania Vis a Vis Global direction in terms of social policital and economic context.

Nawasilisha.
 
Ila ziwekwe kwa kuonyesha ilitolewa wapi, mwaka gani !!!!na hata zipewa title!!!!
 
Back
Top Bottom