JF Exclusive: Dr. Ulimboka kwa maneno yake mwenyewe * Dakika chache baada ya mateso *

Tukio lililomsibu dokta linasikitisha na ni vigumu kushawishi watu kuwa pale katika viwanja vya leaders,

ambavyo ni hatua chache toka makao makuu ya usalama, kituo cha polisi Oysterbay, kituo cha salendar na

makao makuu ya Ultimate security, kuwa mtu anaweza kutekwa kirahisi vile bila kuwa na mpango kabambe

unoshirikisha wadau wa usalama. Maeneo ya kupumzika pale Leaders yako mita 70 toka geti kuu la

kuingilia. Pia pale getini pana mlinzi, Je ilikuwa ni ngumu kwa wasamalia wema kuweza kuwadhibiti

watekaji hao
 
Kwakweli awa jamaa kwa mwendo mzima walikuwa wanategemea angefariki Alafu angekuja kupatika badae kabisa, but Mungu mkubwa watu waliyo muokoa wamesaidia kutupatia ushaidi wa kutisha kuwamaliza Serekali, chamsingi ni sisi watanzania tuseme TUMECHOSWA NA UNYANYASAJI. Atuna la zaidi ya Kufanya Maamuzi magumu kwa sasa.
 
Cjackia maneno toka kwa dokta mkuu matokeo yake nimesikia simulizi toka kwako.

Hujasikiliza hadi mwisho. Huu ni mwanzo wa ukombozi Tanzania. Dr Ulimboka hata akifa leo, ujasiri wake na taaluma yake vitaenziwa vizazi na vizazi.
 
Mwanzoni nilidhani kwamba kazi ya "AKILI" inahitaji watu wenye akili nyingi sana; kinyume chake, ni waoga kama MBWA KOKO na vilaza wasiyojua wafanyalo! Ebo, sipati picha...ati kwa kumtesa na kutaka kumuua Dkt. Ulimboka walidhani watawatisha MADAKTARI waache mgomo na warejee kazini, siyo?!

Angalia sasa...kitendo cha kijinga na cha kiwendawazimu kimesababisha madaktari na wauguzi kutumia SIKU NZIMA ya JUMATANO kumhudumia DKT. ULIMBOKA na hata kumpa HESHIMA ya mpiganaji (anayefia kazi yake) huu ni ujinga nambari wahedi kwa kada ya AKILI na KANZU-KOFIA wanaoacha kufanyakazi ya kutumia akili (nyingi kama lilivyo jina la AKILI) badala yake wanafanyakazi kwa kutumia "MITULINGA" kama enzi zile za watu wa darasa la pili na wale wachakachuaji wenye vyeti vya "wizi" na majambazi wa elimu...!

Sikutegemea kama Tanzania tunakwenda kama enzi za kupotea kwa akina Kassim Hanga (aliyepotea enzi za Karume Baba)...au kama alivyouwawa Robert Ouko; au mauwaji ya Dkt Nicas Mahinda (aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda)...hivi, kwa mwendo huu AKILI mbona wanakuwa kama....!

Kwa bahati mbaya sana; DKT. ULIMBOKA ni mzima, na angalau ameweza kuzungumza na baadhi ya vyombo vya habari (pamoja na TBC) jinsi alivyochukuliwa na hata alivyofanywa! Nadhani hapa ndipo tunapoweza kupata "picha" ya nini ni wazimu na kipi ni wendawazimu! Kama ikiwa bahati nzuri...basi waliyefanya unyama ule watajulikana (walidhani DKT. ULIMBOKA) amekufa...!

Masikini; ati wanawatisha madaktari kwa kumtesa na kutaka kumuua KIONGOZI wao...!? Sidhani, kama mwanzo basi NGOMA bado mbichi...muda utazungumza.
 
Mora ampe nguvu na namwombea dokta apone mapema.

Kama waasisi wa hili tukio ni sehemu ya utawala

basi leo hii 27/06/2012 unabii wa J. Mnyika umedhiirika

kweli UDHAIFU ni mkubwa. Sirikali yenye baraza la mawaziri

na vyombo mbalimbali vya kushughulika na kero za raia wake leo

inatetemeshwa na raia mmoja, tena asiyekuwa hata na bisibisi

bali hekima na kipawa cha kutetea haki.

UDHAIFU umedhiirika
 
Wabongo bwana kila kitu siasa! huyu jamaa kachukuwa kipigo pointers zote zinaenda kwenye siasa. je kama anadaiwa au kachukuwa mke au girlfriend wa mtu au wale ambao ndugu zao walikufa kwenye mgomo wa kwanza wakaamua kuchukuwa sheria mikononi kwani tunakimbilia kutoa hukumu kabla polisi na sheria kufanya kazi yake. hii nchi ina kazi kweli kweli. Hivi ni watu wangapi walikufa wakati wa migomi ya madaktari? Nauliza tu!

sheria mkononi wanatakiwa kuchukua dhidi ya serikali na sio madaktari. maana si wangeleta madaktari wa kichina kama walivyoahidi? Ni wajibu wa serikali kutoa huduma ya afya na si wa madaktari. ndio maana serikali ilsema italeta madaktari wa kichina.
 
Mwanakijiji
Tupe update kila inapobidi inasikitisha sana

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Jamani mimi mbona nimefungua na kusikia sauti ya ulimboka,nafikiri tatizo ni Michina mnayotumia.
 
Aisee....ni hatari.mmm vp hawa jamaa watakimbilia kutrace simu ya dr SM ili kukubaini kumbe umetumia chip unregistered....chenga ya mwili
 
Steve Biko! Shocking!

Steve Biko anayechochea umauti wa watz wenzake tena mafukara ..shocking!
inapotokea fisi kula swala ni sawa, ila akitokea mbabe kuliko fisi akataka kufanya vilevile inakua kosa. senti.
 
Asante mkijiji inatia uchungu sana. Hivi nyie mnaosema hakuna kitu sikiliza toka mwanzo hadi mwisho sio mnasikiliza mwanzoni halafu mnaanza kulaumu. Dr Ulimboka sauti yake inasikika anasema alivyopigwa nakupelekwa kwenye nyumba nzuri ila haitambui ni sehemu gani kwa vile alifungwa kitambaa cheusi usoni. Jamani tumshukuru mkjj kwa video yake hii.

Ila serikali imechoka na leo wametoa tamko Bungeni kuwa kesho litakalokuwa na liwe. Hili neno lina maana nyingi na wanaposema hivyo ujue kwamba 2015 kuachia ngazi kwa ccmafisi itakuwa ngoma yaani tutmwaga damu kama yaliyotokea kenya. Kama mgomo tu wa Madakatari ndio hivi. Itkuwaje kwa chama cha ccmafisi kuondolewa madarakani.

Hivyo Watanganyika wote tujiandae kwa kuwaondoa kwa kura na wakikataa kwa njia ya kura basi tutamwaga damu. Ila hatutakubali tena kutawaliwa na ccmafisi. Akina sijui nchemba wanasema wao na wanauchumi makini wa BOT ilikuwaje pesa zikaibiwa BOT.

Hivi hizi pesa za EPA, MEREMETA,TANGOLD, RADA, Ritchmond zingedhibitiwa na kulipwa madaktari, walimu hivi leo hii madakatari wangegoma. Matokeo yake wezi walimbiwa rudisheni. Akina Mramba, Yona, Mngoja, Chenge, Rostam, Lowassa wanadunda mitaani na tunawaabudu halafu useme kuwa serikali ya ccmafisi ni wasikivu. Yana mwisho na mwisho wao 2015.
 
Steve Biko anayechochea umauti wa watz wenzake tena mafukara ..shocking!
inapotokea fisi kula swala ni sawa, ila akitokea mbabe kuliko fisi akataka kufanya vilevile inakua kosa. senti.

Ni vigumu kuamini Tanzania tuna watu wanye ujasiri wa kutetea kilichotokea!
 
Ni vigumu kuamini Tanzania tuna watu wanye ujasiri wa kutetea kilichotokea!
ikibidi mtu mmoja hata asiye na hatia aonje mauti ili kulinusuru taifa, we call it JUSTIFIED. kila serikali duniani inafanyaga kaa hujui.
 
hakuna sauti ya dr ulimboka hata kidogo, sasa MK tusubirie hicho kipande cha pili mpaka lini? okey ngoja tuwe na subira

mbona jamani sauti ya dr imesikika mwishoni kabisa? mimi nimeisikia na inasikika sauti ya kike mwishoni kabisa nadhani ni yule mama kijo bisimba
 
Hamna lolote zaidi ya majungu, Ulimboka kaoneshwa live anaongea kweny TBC na kakaa ingawa kavimba sana uso kwa kichapo lakini alikuwa anaongea mwenyewe, sasa leo tena hili ya kuletewa sauti za watu wengine kusema Ulimboka kama si unafik ni nini.
 
Steve Biko anayechochea umauti wa watz wenzake tena mafukara ..shocking!
inapotokea fisi kula swala ni sawa, ila akitokea mbabe kuliko fisi akataka kufanya vilevile inakua kosa. senti.

Kwahiyo ni sawa JK na serikali yake kuendelea kula bata (e.g. kutibiwa nje, kuchota fedha za walala hoi) wakati watanzania waliowengi wanaendelea kuteseka including madaktari?
 
Kwahiyo ni sawa JK na serikali yake kuendelea kula bata (e.g. kutibiwa nje, kuchota fedha za walala hoi) wakati watanzania waliowengi wanaendelea kuteseka including madaktari?
kwa hiyo ni sawa madaktari kuwakomoa mafukara wanaotegemea solely hospitali za serikali kisa JK na serikali yake wanakula bata pamoja na uchafu wake?
 
Back
Top Bottom