JF Businesss Ideas Competition

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,401
1,312
Wana JF

Nimekua nikipitia jukwaa hili la businesss and economy na kukutana na mawazo mazuri sana ya biashara kutoka kwa members wengi

Naomba nitoe wazo la kuanzishwa kwa mashindano ya mawazo mazuri ya biashara kwa members wa JF

Mashindano haya yanaweza kuratibiwa kwa ushirikiano na UDEC (University of Dar es salaam Entrepreneurship Center)

Mashindano haya ya mawazo ya biashara yatakuwa ni challenge kwa wote wenye mawazo mazuri na chachu ya kuwawezesha ili mawazo hayo yaweze kutekelezeka na kufanikiwa

Mashindano haya basi yanaweza kuwa katika madaraja mbali mbali kutokana na kiasi cha mtaji wa kuanzisha biashara, yaani kunaweza kuwa na daraja la kwanza ambalo ni biashara mpaka Tsh. 25m, daraja la pili mpaka Tsh. 15m na daraja la tatu mpaka Tsh. 5m, pia kunaweza kuwa na washindi maalum (special category) kama vile kilimo na ufugaji, mazingira na utalii

Mashindano haya yanaweza kupata udhamini kutoka makampuni na wafadhili kama airtel, TPSF, TBL, SIDO, UNIDO, TCCIA, TIB, NMB na wengine wengi

Mashindano haya pia yatatoa fursa za kutoa elimu ya ujasiriamali kwa washiriki, mentorship, networking, market opportunities, financial assistance opportunities na kuwawezesha washiriki kuwa marafiki wa mabenki na taaasisi za kifedha kwa kuwafanya kuwa wanakopesheka

the competition is suggested to be 80% online

nawakilisha
 
Kuna NBPC na sido ndio waendeshaji kama sikosei.
Wazo lako sio baya ingawa mashindano mengi hulalamikiwa kuwa na longolongo kama hilo la NBPC.
 
Wana JF

Nimekua nikipitia jukwaa hili la businesss and economy na kukutana na mawazo mazuri sana ya biashara kutoka kwa members wengi

Naomba nitoe wazo la kuanzishwa kwa mashindano ya mawazo mazuri ya biashara kwa members wa JF

Mashindano haya yanaweza kuratibiwa kwa ushirikiano na UDEC (University of Dar es salaam Entrepreneurship Center)

Mashindano haya ya mawazo ya biashara yatakuwa ni challenge kwa wote wenye mawazo mazuri na chachu ya kuwawezesha ili mawazo hayo yaweze kutekelezeka na kufanikiwa

Mashindano haya basi yanaweza kuwa katika madaraja mbali mbali kutokana na kiasi cha mtaji wa kuanzisha biashara, yaani kunaweza kuwa na daraja la kwanza ambalo ni biashara mpaka Tsh. 25m, daraja la pili mpaka Tsh. 15m na daraja la tatu mpaka Tsh. 5m, pia kunaweza kuwa na washindi maalum (special category) kama vile kilimo na ufugaji, mazingira na utalii

Mashindano haya yanaweza kupata udhamini kutoka makampuni na wafadhili kama airtel, TPSF, TBL, SIDO, UNIDO, TCCIA, TIB, NMB na wengine wengi

Mashindano haya pia yatatoa fursa za kutoa elimu ya ujasiriamali kwa washiriki, mentorship, networking, market opportunities, financial assistance opportunities na kuwawezesha washiriki kuwa marafiki wa mabenki na taaasisi za kifedha kwa kuwafanya kuwa wanakopesheka

the competition is suggested to be 80% online

nawakilisha
Muhimu hakimiliki za watoa mawazo zilindwe..!!
 
Mkuu Bongo sheria za hakimiliki ziko katika vitabu tu.Ningumu kuzi Police kama ugumu wa TBL kuuza Juice.

LAT: hapa JF kuna mawazo mazuri lukuki.tuanze na Thread yenye mkusanyiko wa IDEAs za members.
this is how it can work.
member anapokutana na IDEA posting nzuri ktk JF ,anaikopi na kuweka ktk hiyo Thread of IDEAs.then zikiwa nyingi kutakuwa na Volunteer Editors wanazikunya into a single PDF file .
Nina Amini baaday miezi 6 tu ,hiyo Thread itakuwa a popular destination of Wajasiriamali wa Tanzania
 
UK na Marekani kumewahi kuwa na TV show za watu ku-pitch business ideas zao to potential investors. Idea ikiwa nzuri basi unajipatia partner, mwekezaji au mzunuzi wa shares. You may be onto something here...
 
Bongo unauza idea unapondwa..ukimpa kisogo mtu anaifanyia kazi na huna pa kupigania ubunifu wako... hakia unaipata AHERA..
 
wazo zuri. kuna mtu humu ndani alikuja na idea similar to that, watu wakamjibu ovyo ovyo naona thread ikaishia
 
I ain't no fool, idea is all that matters...people like fallen Jobs kept apples to the sky bse of his unique ideas! Beside we don't have patent/copyright laws in place in tz!
 
Inawezekana ila MBWEHA ni wengi! walengwa tutakula kwa macho, wenye hela wanatumia mawazo yetu! Try! ila mimi nina bad experience kwenye hii idea!
 
My JF Family, niliwahi kuhudhuria International Trade Fair 2008.niliona kampuni inayouza mitambo ya kutengeza Cement.kuna mtambo unaanzia Dola Elfu 40.ipo inayozidi hapo.Founder wa hii kampuni ni Mtu wa INDIA.yeye alianza na mtambo wa kutengeneza 200KG/Day. akawa anauzia majirani zake,baada ya miaka kadhaa akafungua kiwanda cha kutengeneza viwanda vya cement.siku hiyo nilikutana na Mjukuu wake huyo mzee.
Sikuhishia hapo nikafanya tafiti online nikagundua China wanakuletea mtambo na mafundi wawili onsite for 1yr.na bei za wachina kama tujuavyo ni za kujipimia tu.

Wazo langu:JE Saccos ikishasimama wima,tufikirie jinsi ya kuweza ktk uzalishaji wa Cement.hiki kiwanda kitakuwa cha wazawa 100%.viwanda vya cement vilivyopo sasa karibuni vyote ni vya wageni.
Cement inatumika na kila mtanzania na itazidi kutumika kwa miaka mingi ijayo.Tafakari Chukua HAtua :)
 
I ain't no fool, idea is all that matters...people like fallen Jobs kept apples to the sky bse of his unique ideas! Beside we don't have patent/copyright laws in place in tz!

I couldn't agree more with you. What we need is for the organizers to encourage people to come up with ideas, business plans, proposals etc
 
Nmeipenda hiyo idea na mda mrefu nilikuwa naitafuta xna!so ndugu,vp kuhusu usalama wa ideas zetu?kwani huo ni mtaji usiokuwa na interest rate!
 
Mi nilikuwa na idea ya kuanzisha biashara, ila katika harakati za kutafuta mfadhili kuna watu wakaidakia juju. Mpaka leo wanaendelea nayo
 
My JF Family, niliwahi kuhudhuria International Trade Fair 2008.niliona kampuni inayouza mitambo ya kutengeza Cement.kuna mtambo unaanzia Dola Elfu 40.ipo inayozidi hapo.Founder wa hii kampuni ni Mtu wa INDIA.yeye alianza na mtambo wa kutengeneza 200KG/Day. akawa anauzia majirani zake,baada ya miaka kadhaa akafungua kiwanda cha kutengeneza viwanda vya cement.siku hiyo nilikutana na Mjukuu wake huyo mzee.
Sikuhishia hapo nikafanya tafiti online nikagundua China wanakuletea mtambo na mafundi wawili onsite for 1yr.na bei za wachina kama tujuavyo ni za kujipimia tu.

Wazo langu:JE Saccos ikishasimama wima,tufikirie jinsi ya kuweza ktk uzalishaji wa Cement.hiki kiwanda kitakuwa cha wazawa 100%.viwanda vya cement vilivyopo sasa karibuni vyote ni vya wageni.
Cement inatumika na kila mtanzania na itazidi kutumika kwa miaka mingi ijayo.Tafakari Chukua HAtua :)

Hapo red mkuu, je hakuna mitambo ya bei ya CHINI zaidi ya hapo? Biashara hii ni siku nyingi sana coz kuna mtu mmoja mikoani alikuwa akihitaji sana kulifanya, in fact sijui kafikia wapi,
Je mfano unaweza kujua raw materials za cemen?
 
Wazo ni zuri mkuu, ila kumbuka kuwa wizi wa ideas umeshamiri sana siku hizi.. unaweza kupewa zawadi ya idea bora lakini wenzako wakakupiku kwenye utekelezaji wake, ukaishia kuwa na zawadi tu..!
 
Back
Top Bottom