JF: Are we serious na mapambano na ufisadi?

Binti Maria

Senior Member
Jun 26, 2007
158
33
Hii haijakaa sawa, haiwezekani JF sasa hivi ndio inaongoza kupambana na ufisadi nchini halafu tunaruhusa watu wanajiita Fisadi humu tunawaruhusu, jamani tuonyeshe mfano. Pamoja na uhuru tulio nao lazima kuna vitu tuvikatae ambavyo vina contradict our own principles. Sisi tumeshaamua kwamba tuna vita na ufisadi, sasa iweje tena turuhusu watu humu wajisifu kwa ufisadi kwa kujiita majina ya ajabuajabu: Fisadi, fisi, etc.

Nashauri kwamba hawa ndugu washauriwe na ikibidi washurutishwe kubadilisha majina yao, vinginevyo uanachama wao utenguliwe mara moja.

Moderators: sijui hii kama ni mahala pake hapa. Mnaweza kuipeleka panapohusika kama hapa siko.

Ndimi Binti.
 
I think It is a good inquiry, thus can sit on a political forum for a while before being moved to mapendekezo/maoni or another appropriate forum. Thanks for your suggestion and have a good day!
 
Mojawapo ya haki za msingi za binadamu ni haki ya kuweza kusema kile kinachoweza kuwaudhi watu. Jamii yenye kutaka kusikia kile inachokubaliana nacho tu inajiweka katika hatari ya kuwa na mawazo yaliyoelemea upande mmoja.

JF kama forum ni chombo huru na kisicho na itikadi au mlengo wa aina fulani ya kisiasa japo kuwa wanachama wake wengi wamejivika majukumu ya kupambana na ufisadi.

Badala ya kutaka kusababisha hawa ndugu wabadili majina (kitu ambacho hakitabdili walivyo) ni jukumu letu kupangua hoja zao na kuzionesha jinsi zilivyo dhaifu na kama ni za kifisadi kweli kama majina yao yalivyo.

Mimi nashauri as long as kwamba majina hayo siyo matusi ya wazi au yenye lengo la kinyume na sheria naamini wanastahili kujiita wanavyopenda.

Vinginevyo, wengine wenye majina ya wanakijiji tunaweza kujikuta tunalazimishwa kubadili majina yetu kwa sababu wanakijiji wengine huko ni wapenzi wa CCM na wamewakumbatia mafisadi!

Tuwashinde kwa hoja na si kwa majina!
 
Binti Maria,

Ni JF pekee ambapo people dare to talk openly, wanaweza pia kutumia majina wanayotaka ili mradi hayavurugi mapambano yetu na dhuluma mbalimbali TZ.

Tanzania tuna culture ya kuchukua maneno mapya na kuyafanya majina, mifano ya Osama, Taliban. faruja nk. watu wanatumia ili mradi na wenyewe wanajua yanayotokea duniani.
 
Binti Maria,

Ninakusikia loud and clear, lakini mkuu dawa ni mawe tu na kumkoma nyani, tena hao ndio wazuri maana ni kuwapa salam za kuwapelekea wazazi wao, toka majuzi nimekuwa ninam-forwardia mtoto mmoja wa Meghji, guess what?

Ujumbe wote umefika kama ulivyo bila sensa, it is the best we can do so far, isipokuwa the worst we can do ni kuacha kumkoma nyani hapa maana sasa imefikia time kwamba wakuu hawalali bila kupitisha macho hapa,

Majina yasikusumbue mkuu, dawa yao ni mawe and trust me mkuu it is working!
 
Binti Maria,

Ni JF pekee ambapo people dare to talk openly, wanaweza pia kutumia majina wanayotaka ili mradi hayavurugi mapambano yetu na dhuluma mbalimbali TZ.

Tanzania tuna culture ya kuchukua maneno mapya na kuyafanya majina, mifano ya Osama, Taliban. faruja nk. watu wanatumia ili mradi na wenyewe wanajua yanayotokea duniani.

usishangae likaanzishwa tawi la CCM linaitwa "Ufisadini" Maana nasikia kuna mahali panaitwa Faluja!
 
Kuna majina ni matusi kabisa yakitafsiriwa kwa kiswahili au kwa lugha zetu za asili.

Kuna wachagga wanaitwa "Mboro" kwao ni jina kiswahili ni matusi.

"Kirigini" ni jina la mtu lakini huko iringa lina maana ya Ukeni.

"Afwililwe" ni neno lenye maana kafiwa kinyakyusa kiswahili Toba!

"Namtombe mai?" ni kumsalimia mama yako mzazi kwa Kimachame Kiswahili Uwiiii!

Wengine wanaitwa "Mobitelinaoyuatoking" pengine kwa Kibritish ni matusi who knows!

Waache wajiite watakavyo.
Hakuna mdomo uwezao nena kuliko ukubwa wa mawazo yake wala hakuna mkono uwezao kuandika makuu kuliko wazo kuu akilini mwake.

Kuwapo wengi wa watu walio kinyume chetu hapa JF kunatukumbusha kusimama kidete na kutetea mawazo yetu bila aibu wala kuteteleka.
 
Kuwapo wengi wa watu walio kinyume chetu hapa JF kunatukumbusha kusimama kidete na kutetea mawazo yetu bila aibu wala kuteteleka.

Salute mkuu, maneno mazito sana I hope yamefika yanapotakiwa!
 
Hii haijakaa sawa, haiwezekani JF sasa hivi ndio inaongoza kupambana na ufisadi nchini halafu tunaruhusa watu wanajiita Fisadi humu tunawaruhusu, jamani tuonyeshe mfano. Pamoja na uhuru tulio nao lazima kuna vitu tuvikatae ambavyo vina contradict our own principles. Sisi tumeshaamua kwamba tuna vita na ufisadi, sasa iweje tena turuhusu watu humu wajisifu kwa ufisadi kwa kujiita majina ya ajabuajabu: Fisadi, fisi, etc.

Nashauri kwamba hawa ndugu washauriwe na ikibidi washurutishwe kubadilisha majina yao, vinginevyo uanachama wao utenguliwe mara moja.

Moderators: sijui hii kama ni mahala pake hapa. Mnaweza kuipeleka panapohusika kama hapa siko.

Ndimi Binti.

Sasa yametukuta maana HASARA et al wameshashatupa HASARA. Lakini mambano yanaendelea
 
Hii haijakaa sawa, haiwezekani JF sasa hivi ndio inaongoza kupambana na ufisadi nchini halafu tunaruhusa watu wanajiita Fisadi humu tunawaruhusu, jamani tuonyeshe mfano. Pamoja na uhuru tulio nao lazima kuna vitu tuvikatae ambavyo vina contradict our own principles. Sisi tumeshaamua kwamba tuna vita na ufisadi, sasa iweje tena turuhusu watu humu wajisifu kwa ufisadi kwa kujiita majina ya ajabuajabu: Fisadi, fisi, etc.

Nashauri kwamba hawa ndugu washauriwe na ikibidi washurutishwe kubadilisha majina yao, vinginevyo uanachama wao utenguliwe mara moja.

Moderators: sijui hii kama ni mahala pake hapa. Mnaweza kuipeleka panapohusika kama hapa siko.

Ndimi Binti.

Dada:

Wamakonde tuko wengi hapa. Mmakonde akienda gerezani na kufurahia pilau basi akipata mtoto jina Pilau. Hivyo tusameane.

Pamoja na hayo JF inabadili watu. Nilikuja hapa kusikiliza zilipendwa lakini nimebadilika na kuanza kuwa Born again Tanzanian (mzalendo).

Tuwe kama Bwana Yesu aliyeweza kuwabadilisha walevi kilabuni au wakusanya kodi.

Wako Bin
 
Hapa napo sijui mahali pake ama la!!! anyway nisameheni kama niweka pasipo!

Kwa kuwa wakati ni mali, na kwa kuwa tunataka kwa kiasi fulani tuwe effective!!! nashauri yafuatayo...

1. Iundwe timu ya moderators(inaweza kuwa iliyopo ipewe meno au nyingine, napenda kuwa na waandishi wa habari humo ndani), ambayo itapitia Thread na kuzipitisha ikiwezekana kuweka vichwa vya habari sawa sawa kwa mawasiliano na Mtoa hoja kabla hazijatufikia... kwa nini nasema hili, mara nyingi nimewahi ona issue moja inafunguliwa Thread kama tano hivi!!!.

2.Thread chache watu wataweka mawazo yao pamoja na baada ya muda, tutajifunza na pia tutaweka mambo sawa kwa urahisi zaidi, tutakuwa tuna-conclude issues kwa muda mfupi zaidi... kumbukeni tunahitajika kutumia muda vizuri ili tujenge nchi yetu... blabla zikiwa nyingi tutakuwa hatuitendie haki nchi yetu na watu wake.

3. Kuna wakati kufikisha ujumbe sio lazima kutukana hivyo sometimes... mwenye hoja anaambiwa aweka vichwa vya habari kidogo vyenye utanzania, kiswahili chenye isilahi...

4. Kumbukeni hiko ni chombo kikubwa sana kwa hiyo lazima tuji-shape kidogo,,, uhuru usio kuwa na mipaka it is simply a mess....

5. Tunahitaji Blog, kwa ajili ya kuwasiliana na moderators... na pia yeyekutoa matangazo mbalimbali... ya kwake hayatakiwi yaje kwenye thread... we need them to be available everytime.
 
Kasheshe: hoja yako ni nzuri sana. Lakini najua itapambana na upinzani mkubwa sana hasa kwa wazushi wa mambo, watasema wanaonewa pale watakapokuta mada zao zimehaririwa
 
Unafki mkubwa wa kutaka ku-censor majina huo. Kama hupendi jina langu, jitie kidole mdomoni utapike.
 
fiSADIST
Banned

Thanks for this, well done. Atarudi, najua, au kesharudi, lakini ninaamini amejifunza.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom