Jezi za Waarabu zilivyosifiwa kwa kuchafuka

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,663
Kwa hakika siku zinaenda leo jezi kuwa na wadhamini wengi zinaitwa siyo za mpira, bahasha za khaki ni hatari sana

===

Sare ya Yanga na uchafu wa jezi ya Al Ahly​

MONDAY APRIL 11 2016​

sare pic

Summary

Mbele ya mboni za macho yangu ni kama vile Yanga wameshinda. Wamewezaje kucheza na timu ambayo ina wadhamini 16 wakati wao wanahangaika na mdhamini mmoja tu Bia ya Kilimanjaro, ambaye tena wamechangia na watani zao Simba?

USIIKASHFU sana sare ya Yanga dhidi ya Al Ahly. Wangefanya nini zaidi? Walichopata ndicho walichokistahili. Tena inawezekana hawakustahili hata hiyo sare kama tutafuata misingi halisi ya soka. Walistahili kufungwa.

Mbele ya mboni za macho yangu ni kama vile Yanga wameshinda. Wamewezaje kucheza na timu ambayo ina wadhamini 16 wakati wao wanahangaika na mdhamini mmoja tu Bia ya Kilimanjaro, ambaye tena wamechangia na watani zao Simba?

Tuache vichekesho. Jezi ya Al Alhy imejaa matangazo mengi kama uchafu. Jezi yao imechafuka kwa matangazo. Wale wote wanatoa pesa nene. Pesa ambazo zinasababisha watengeneze timu ya kisasa zaidi miaka nenda rudi. Wale wachezaji uliowaona juzi wameandaliwa tangu wakiwa na miaka sita kuja kucheza Al Alhy. Niambie ni mchezaji gani aliandaliwa kisasa kuja kucheza Yanga. Walijiandaa wenyewe.

Mkataba wao na kampuni ya Vodafone ambayo umeiona kifuani katika jezi yao umeipatia klabu hiyo kiasi cha dola 22 milioni. Lakini Oktoba mwaka jana wameingia mkataba na kampuni ya Sela Trading Company ya Saudi Arabia ambao watalipwa dola 30 milioni.

Wana mkataba mnono na kampuni ya simu ya Huawei kama ulifanikiwa kuiona logo yao katika jezi ya Al Ahly. Barani Ulaya kampuni hiyo ya simu imefanikiwa kuingia mkataba na klabu za Paris-Saint Germain, AC Milan, Arsenal, Borussia Dortmund, Ajax, Atletico Madrid na Galatasaray. Unashindana vipi na timu ya namna hii?

Matokeo ya pesa zote hizo ndio yanapelekea jeuri ya kumuajiri kocha Martin Jol, ambaye ni miongoni mwa makocha bora barani Ulaya. Yule sio kocha wa bei rahisi. Amewahi kufundisha Tottenham, Fulham na Ajax. Sio kocha wa bei rahisi.

Wachezaji ambao wapo Al Ahly ni mkusanyiko wa watu waliokuwa wana ndoto za kuichezea timu hiyo kubwa Afrika kutoka katika idadi ya watu milioni 92 ambayo ndio idadi ya watu wa Misri. Kama una huduma bora, katika idadi hiyo ya watu lazima uwe na timu ambayo itatengeneza kikosi bora.

Mwisho wa siku tofauti hii unakuja kuiona uwanjani wakati wanapocheza na timu kama Yanga. Unapokuwa umejiandaa kisayansi hauitaji kwenda Pemba kuweka kambi. Unahitaji kuingia uwanjani na kucheza.

Na kabla hata ya kucheza jaribu tu kutazama jinsi jamaa walivyokuja na kundi kubwa la watu wanaoifanyia kazi klabu. Wana madaktari zaidi ya watatu, wakati sisi anasafiri daktari mmoja tu. Wana jopo la waandishi wao, wana benchi kubwa la ufundi na kila mtu ana shughuli zake.

Wakati wachezaji wakipasha misuli moto, Al Ahly walikuwa wamesimamiwa na watu wanne wa mazoezi ya viungo. Kocha wao Jol na msaidizi wake walikuwa wanapiga stori. Kule Yanga mazoezi yao ya viungo yalikuwa yanasimamiwa na kocha Juma Mwambusi. Mwambusi ana utaalamu na masuala ya viungo au ni kocha? Jiulize.

Naambiwa wachezaji wa Yanga hawajalipwa mishahara ya Mwezi Machi mpaka sasa, lakini hapo hapo naambiwa kuwa Al Ahly wamegoma kumuuza winga wao, Ramadan Sobhi aliyevaa jezi namba 27 ambaye alikuwa anatakiwa na Arsenal. Wanataka ashiriki michuano ya klabu bingwa ya dunia Desemba mwaka huu. unazilinganishaje timu mbili za namna hii.

Na ndio narudia kusema usiikashifu sare ya Yanga. Wale wachezaji wa Yanga kwa kiwango walichocheza dhidi ya Al Ahly wanapaswa kupongezwa sana. Kuna pengo kubwa sana la hali na mali baina yao na wachezaji wa Al Ahly.

Lolote linaweza kutokea uwanjani kama ambavyo Yanga walikaribia kuitoa Al Ahly misimu miwili iliyopita kule Cairo. Lakini wakati ule Wamisri walikuwa wanavuna matunda ya machafuko ya kisiasa nchini mwao.

Hata hivyo, wakati timu zote mbili zinapokuwa katika maandalizi sahihi, ni ngumu sana kwa Yanga kuitoa Al Ahly. Na hili halitokani na makosa ya wachezaji wa Yanga uwanjani wala makocha. Linatokana na mfumo mzima wa klabu yao. Maandalizi yao ni ya dakika 90 za mechi ya leo, sio kuwekeza katika mfumo sahihi wa soka la vijana pamoja na kutengeneza timu yenye uchumi imara.

Wanaofanya yote haya ni watu wachache ambao wanajua timu kubwa kama Simba na Yanga zikijitegemea basi watapoteza umaarufu wao na umuhimu wao klabuni. Ndio maana kila siku wanaziacha zilipo ingawa wanajua kuwa wangeweza kutumia idadi kubwa ya mashabiki waliopo kuzifanya ziwe tajiri walau nusu ya Al Ahly.

Mtaji mkubwa wa utajiri na umaarufu wa Al Ahly pamoja na Zamalek ni ukichaa mkubwa wa soka walionao Wamisri pamoja na idadi yao kubwa ya watu. Hayo mambo mawili yote yanapatikana Tanzania lakini hayajatumika. Jiulize, Yanga inakuaje na mdhamini mmoja mpaka leo? Kwanini hasa? Kwanini jezi yao haijachafuka kama ya Al Ahly?

Chanzo: Mwanaspoti
 
Kisikiza redioni na ukisoma magazeti wote sasa wanaungana na lopolopo la dunia kwamba jezi zisizochafuka ndizo nzuri kimpira, bahasha za khaki zinawafanya waonekane majinga kabisa.
 
Kisikiza redioni na ukisoma magazeti wote sasa wanaungana na lopolopo la dunia kwamba jezi zisizochafuka ndizo nzuri kimpira, bahasha za khaki zinawafanya waonekane majinga kabisa.
mwandishi wa hiyo makala bila shaka ni edo kumwembe....... sijawahi kumsikia akiongea masuala ya kipuuzi puuzi huyo jamaa!

tumpe heshima yake, atleast ame-maintain misimamo yake!
 
Mtaji mkubwa wa utajiri na umaarufu wa Al Ahly pamoja na Zamalek ni ukichaa mkubwa wa soka walionao Wamisri pamoja na idadi yao kubwa ya watu. Hayo mambo mawili yote yanapatikana Tanzania lakini hayajatumika. Jiulize, Yanga inakuaje na mdhamini mmoja mpaka leo? Kwanini hasa? Kwanini jezi yao haijachafuka kama ya Al Ahly?
Jezi ya Yanga ina sportpesa main sponsor,ina gsm foam,taifa gas na maji ya afya,hao wote wanailipa Yanga,jezi ya mikia imejaa matangazo ya mo tu na main sponsor sportpesa na itakayotoka kwenye ligi inaweza kuongezewa vunja bei
 
Simba kaingia mkataba na Vunja bei mauzo ya jezi,vipi huko kwenu mtani mna mkataba wa jezi kama Simba na Vunja bei?

Sent from my SM-T285 using JamiiForums mobile app
 
Jezi ya Yanga ina sportpesa main sponsor,ina gsm foam,taifa gas na maji ya afya,hao wote wanailipa Yanga,jezi ya mikia imejaa matangazo ya mo tu na main sponsor sportpesa na itakayotoka kwenye ligi inaweza kuongezewa vunja bei
Yeees.......
 
Back
Top Bottom