Jezi za Taifa Stars zimeangalia maslahi ya Yanga

Tangia wazindue jezi walizoziita ni za Taifa huku zikifanana na jezi za ombaomba (Yanga) naacha rasmi kuishabikia nchi yangu. Hivo nimeanza maombi ya kuiombea mabaya, ifungwe,ifungwe ifungwe kabisa
 
Shirima unawaza vibaya sana.

So kimsingi unamaana Simba kwako kama timu ni bora kuliko Taifa, mapenzi yako kwa uSimba ni makubwa kiasi cha kuombea mabaya kwa Taifa.

Anyways hupangiwi mkuu, goodluck kwenye maombi yako
 
Mbegu ya utengano iliyopandwa katika Taifa inaota kwa kasi sana.

Kama si Yanga na Simba basi CCM na Chadema. Kama si Ukristo na Uisilamu basi Uzanzibari na Utanganyika. Kama si Uchaga na usukuma basi ni mwanaume wa Dar na wa Mkoani.

Wakuu tusipoangalia kuna bomu kubwa sana linatunyemelea.

Hii ni kitu kidogo sana mkuu, hukupaswa hata kupeleka mawazo yako kwenye uYanga na uSimba.
Tukishaanza hizo bifu basi tegemea tutasonga zaidi ya hapo. Bado bifu la Ufupi na Urefu,
Watu weupe vs Weusi,
Wanene vs Wembamba,
Masikini Vs Matajiri,
Waliosoma vs Wasiosoma,
etc
 
Tukishaanza hizo bifu basi tegemea tutasonga zaidi ya hapo. Bado bifu la Ufupi na Urefu,
Watu weupe vs Weusi,
Wanene vs Wembamba,
Masikini Vs Matajiri,
Waliosoma vs Wasiosoma,
etc
Shida sana mkuu. Watu wanachukulia mchezo mchezo hawajui nini kinakuja mbele yaani
 
Siyo lazima uvae......
Au katafute jezi za simba, liverpool na Manchester zina rangi nyekundu
 
Sijawahi kupenda rangi ya blue katika jezi zetu za taifa. Kwanza mimi ni mnazi ya Simba (Mimi ni Kilomoni Jr.) ila ahuweni tutumie rangi hizi mbili (kijani na njano) au kama tunatumia blue basi iwe kwenye soksi ama bukta na iwe blue ya kukoza kama ile ya Brazil.

Fulana zikiwa kijani zitaleta muonekano mzuri sana na iwe kijani ya kukoza sana na bukta ndizo ziwe za blue.

Mwisho: kwa aina ya wachezaji wetu hata ukiwapa jezi za dhahabu ni sawa na kipini cha dhahabu juu ya pua ya nguruwe.

Wapeni tu hayo hayo majezi mabaya yanayoendana na uchezaji wao wa hovyo...
Utakuwa mkenya wewe...na tunasema " upumbavu ni sawa na kipaji cha ufupi ama urefu".
 
Haya majezi kuna rushwa.. haiwezekani timu ya taifa iwe na jezi mbaya kuliko za Yanga. Yanga ni Addidas halafu taifa sijui mdudu gani huyu UHLsport.
 
Hebu nipatie na mimi jezi ya Yanga nataka niitundike nyumbani ili siku nikitaka kugombana na mtu naingalia kwanza jezi ya Yanga ili inipandishe hasira😃😃😃
Hahahaaa. Nakuletea baadae japo nawaza tu isije kuwa kinyume chake kwamba ukiiangalia hiyo jezi unajikuta hautamani hata kumkasirisha. 😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom