Jeuri Ya Mwekezaji Kuzuia Kamati Ya Bunge Inatokana Na Nini?

Mr EWA

JF-Expert Member
Mar 15, 2007
331
64
Wabunge wamechachama kwa kamati ya bunge kuzuiwa na mwekezaji kuingia katika Hoteli yake.

1.Nini kinampa kiburi mwekezaji kuwa na Jeuri kama hii?

2.Je kuna mapungufu kwenye mkataba aliowekeana na serikali yetu?

3. Ama ni viongozi wetu kuwa karibu na wawekezaji karibu kuliko kawaida?

4.Hayo waliyoyaona ni kidogo tu yako mengine mengi kama hayo?

5.Je yule bwana aliyesema serikali ameiweka mkononi enzi ya Nyerere alifanywaje?

6.Nini kifanyike ilikuweka heshima kwa nchi yetu?
 
Nimesikia bunge limeiomba serikali itoe tamko kuhusu sakata hilo,mimi binafsi nimesikitika sana na nikajiuliza ni kwa nini haya yanatokea hapa nchini kwetu,je nini kimetufikisha hapa?
 
Sorry Wakuu naomba hii iunganishwe na ile ya mwanakijiji kumbe jamvi lilishafunguliwa mapema.
 
Huyu mdosi ameonyesha jeuli sana, nilipokuwa nafanyakazi Ngara kwa wakimbizi kuna visa viwili vilitakea; Muitaliano mmoja wa kampuni iliyo kuwa inajenga barabara ya lami inayokwenda Bujumbula alikuwa anakiburi na kunyanyasa wafanyakazi, sikumoja alimfanyia kitu mbaya jamaa yetu mmoja, yule jamaa akaenda polisi huyo mdosi alipoitwa akafanya jeuli, FFU walimfuata walimleta kituoni kwa kwa mguu akiwa peku alipewa masaa 24 na mkuu wa wilaya awe ametoweka nchini aliondoka. Kulikuwa pia na Mjelumani mmoja naye alileta jeuli ya kunyanyasa watu na kutukana hata viongozi wkija viongozi wa serikali ofisini kwake ana wafukuza, naye alipewa 24hrs aondoke aliondoka. Aliyekuwa anawapa 24hrs ni mkuu wa wilaya tu, Sasa huyu kaonyesha dharau kubwa kwa bunge serikali na Watanzania kwa ujumla. Kwa kweli huyo jamaa wa hotel ya VIP ashikishwe adabu liwe funzo. Mnasemaje washikadau
 
Kuna kitu anachojivuniaa..huyoo au sababu mkuu wa kaya huwa anashinda huko wakati wa mapumziko anaona nae ni ni mbia wa madaraka yake???
 
ndio mtaji wa kubebana katika serikali yetu. wabunge wamepoteza mafuta bure mpaka serengeti wakarudi watupu
 
hii kali na nimeipenda. na wakome kufuatilia biashara za watu
 
Back
Top Bottom