Jeshi lilijua kuwa mabomu yangelipuka...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi lilijua kuwa mabomu yangelipuka...?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DKNY, Feb 18, 2011.

 1. D

  DKNY Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Habari za kuaminika ni kwamba, wanajeshi wa kambi ya Gongo la Mboto walitambua kuwa mabomu hayo yangelipuka hours before the action started, and wat they did ni kuhamisha familia na ndugu zao na kutoa taarifa kwa marafiki zao wachache (mmoja akiwa huyu aliyenipa taarifa hz, jina nalihifadhi)

  :mad:
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ninaposikia taarifa kama hii napata shida sana kutoamini kuwa huu sio ugaidi hasa wa ndani. Inakuwaje wanajeshi wote wahamishe familia zao na kuwa hakuna mwanajeshi aliyeathirika? Hapa iko namna. Ukweli utajulikana tu.

  Kwenye ugaidi watu hutishia kupewa kitu fulani na kutishia kulipua au kuua mateka wasipotimiziwa haja zao. Isije ikawa waheshimiwa wa dowans wametishia kuwa wasipolipwa watafanya kweli na hayo ndiyo maafa yake na kuwa wanasubiri kufanya zaidi.

  Hivi Watz tuko salama kweli kwa ugaidi huu?

  Ni mahali gani Tz ambako jeshi halina kikosi? Kwa D'Salaam tu ni karibu kila mahali. Fikiria Kimara, Kigamboni, Kunduchi, Boko, Kibaha, Bagamoyo, nk. Je, tutaaminije kuwa serikali yetu si mu-bia wa ugaidi huu kwa majibu na hoja nyepesi nyepesi wanazotupa?

  Serikali inaposhindwa kulinda raia wake hasa kuwatoa hofu kuwa japo si ya kuwa kuna vita bali kuwa vyombo vya ulinzi na usalama viko makini katika kulinda usalama wa wananchi. Leo hii mtanzania hana hofu ya mipaka ila ana hofu kuwa walinzi wake kikatiba watafanya uzembe ambao utasababisha vifo kwake na kwa familia yake na kuleta maafa mengine. Huu ni ugaidi. Viongozi wetu ni vema wajue hivyo na wawajibike
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Inawezekana sio ugaidi...Na inawezekana ni muendelezo tu wa kukosa uadilifu. Hakuna kitu cha hatari kama kukata tamaa na siasa kuharibu karibu miundombinu yote inayolitegemeza Taifa. Rushwa ndio imekuwa driving force ya kufanya siasa na biashara sasa kwanini rushwa isiwe biashara sehemu nyingine? Well, ukweli tutaujua tu with time!!!
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mimi naamini walijua kwa sababu kuna taarifa wataalamu wa amary (watunza silaha) walishaonya kuwa mabomu yale yalikwisha muda wake na kilichokuwa kinasubiriwa ni mchakato tu wa kuyaharibu.

  kupuuza huku kulitokana na kilio cha uhaba wa fedha kwani uteketezaji wa mabomu kama yale ni ghali na mara nyingine huitaji hata kukodi wataalamu kutoka nje. Hivyo basi serikali yetu imekwepa gharama ya kuyaharibu na sasa inalipa gharama kama fidia kwa uharibifu uliofanywa na mabomu haya ukitoa roho za watu ambazo kztu huwezi kuzirejesha!

  Hatari hii inaweza kuwepo kwa maghala mengine ya Ngerengere, Tabora ambayo nayo inawezekana kabisa mabomu yalipitwa na muda wake bado yanahifadhiwa kw1 kisingizio cha fedha!

  Mwisho wana JF kinachofanyika sasa ni kuaandaa lugha laini ambayo itawasilishwa kwa wanannchi ili kuiingia kifua serikali yetu ambayo IMESHINDWA KUWAJIBIKA IPASAVYO.
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kwa wale tulioangalia series ya 24hrs tunaweza kuamini unachokisema.
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  ninaamini kwa sababu wanajeshi nao wameshachoka ..maisha magumu , hakuna haja ya missing in action ...mabo ya kizamani
   
 7. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Na hicho ndicho ninachosema. Kwa vile taarifa za jeshi ni siri kubwa huwezi kujua kilichomo ndani. Utakachojua baadaye ni taarifa kama za Kagoda na Meremeta ni mambo ya kiusalama. Wizi unapohusishwa na usalama ni ugaidi.

  Leo tunazungumzia maafa ya watoto wetu kufeli mitihani kwa kiwango cha 88.5% ambao wamepata madaraja ya IV na O; hata kabla hatujatulia na tukiwa kwenye mgao usio na ukomo watz wanuawa si kwa majeshi kutoka nje ila kwa uzembe wa walinzi wao.

  Halafu tunapewa lugha nyepesi kabisa kwa mambo mazito kama hayo. Spika wa Bunge tukufu, anasema si dharura na hapo hapo anaahirisha bunge. Hii maana yake ni nini? Kwa nini Spika asite kuruhusu mjadala wa jambo zito kama hili? Anaufanyia mjadala huu kadablakadabla kama hoja ya Mh. Lema?

  Huu ni Ughaidi.
  Nitaendelea kuamini hivyo mpaka nitakapopata majibu ya msingi.
   
 8. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Cha msingi wakataze hao watoto, pili piga simu kwa mkuu wa majeshi umjuze hilo au namba maalumu zilizotolewa au mpigie mkuu wa operations wa jeshi la polisi Ndugu Chagonja simu namba 0754 489567 kama longolongo piga kwa Said Mwema 0787444433. Nimekupa namba za polisi maana ndiyo wenye kuandalia usalama wa raia.
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Feb 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,337
  Likes Received: 19,507
  Trophy Points: 280
  kama ni kweli basi tushapata pa kuanzia lakini allin all hakuna mtu atakayewajibiswa wala kuwajibika
   
 10. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bila kuipumzisha ccm hii nchi ya TZ haitapona. Uzembe na blabla za siasa kwenye kile kitu. Wataalamu wamegoma mgomo baridi sehemu nyingi kwa sababu kila kitu ni siasa.
  Serikali inatumia hela kwa kizembe na siasa za ccm.

  Tutaendelea kuteseka mpaka siku mfumo tunakapobadilika.....katiba ya wananchi.
   
 11. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #11
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,025
  Likes Received: 8,514
  Trophy Points: 280
  ahahahaaaaa,kadablakadabla haahaaaaa,YOU ARE NUTJOB
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yeah kila charles logan na Tony Almeda duh kweli aisee these things happen
   
 13. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #13
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  yes ,they before it happened thats why they left the scene earlier and left uninjui:rain:red
   
 14. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Mkataa pema pabaya panamwita, watanzania walikataa vyama vya upinzani wakang'ang'ania CCM kwa misingi ya udini na ujinga. malipo ndio hayo. na bado huo ni mwanzo.
   
 15. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hili mbona nisuala rahisi kulijua, tena wewe mwenywe unaweza fuatilia kujua kama walijua au la, unachotakiwa kufanya, anza uchunguzi, fuatilia hizo fammilia , lazima zina watoto na watoto hao ni rahisi kueleza siri bila kujua, kwa kuwauliza je siku ya tukio walikua wapi? ukisha pata jibu kua familia zaidi ya 10 za wanajeshi zili ondoka eneo hilo kabla ya tukio basi hapo nadhani utakua umeshapata chanzo cha tetesi kua jeshi lilijua.
   
 16. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Inaelekea tunaanza kupata mwanga kidogo.

  1. Palikuwa na ukaguzi siku moja kabla ya mlipuko na ukaguzi huo unafuatia ukaguzi wa ndani.Kwani ukaguzi mwingine ulifanyika wakati ukaguzi wa mwanzo ulionyesha kuwa mambo ni shwari?
  2. Hakuna askari aliyekufa
  3. Familia za askari zilihamishwa
  Inaweza kuna mapungufu ambayo yalionekana wakati wa ukaguzi wa mwanzo na watu wameamua kupoteza ushahidi kama inavyotokea ofisi kuungua wakati wa auditing.
  TUKUMBUKE-kuna bank ilifilisika hapa na wakati watu wanalalamika Governor BoT akasema hali ni swari ndani ya bank but within a week the bank was cllosed.Alijitetea baadae kuwa hakutaka watu wa panic!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  sidhani kama walijua.sehemu kebwa ya wakazi wa g-mboto ni ex army,hivyo ni vigumu wao kufanya setup ya namna hii.
  kilichotokea ni kwamba storage facility ya haya mabomu ni mbovu na ya zamani sana,imechakaa bila matengenezo.
  angalia TBC news ghala la mabomu lina kutu.bati limechoka.kipindi cha wiki ya milipuko kulikuwa na upepo mkali sana.hivyo inawezekana kabisa bati na mbao ziliangukia mabomu na kuanzisha moto huo ulioanza kufyatua makombora
   
 18. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jamani naomba nijuzwe, nimesoma news nyingi sana kuhusu mabomu, ila sijaona sehemu iliyotaja ni wanajeshi wangapi wamekufa na wangapi wamejeruhiwa.

  kama hamna mtu aliyekufa wala kujeruhiwa then hii itakuwa imeendaliwa.
   
 19. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aleluyah!

  Wasalam Waleikum wna JF!

  Nimekuwa nikitafakari sana mlipuku wa Gongo la mboto na bado sijapata jibu sahihi, naamini humu ndani wachambuzi waona mbali ni wengi hebu nisaidieni.

  Kule Mbagala Wanajeshi wanne walikufa, kwanini hapa G/Mboto hakuna aliyekuwa na milipuko hii imekuwa mikubwa kuliko ya Mbagala. Yaani namaanisha maghala 23 yamelipuka bila ya mwanajeshi yeyote kudhurika, je hapa hakuna hila kweli?
  Lakini pia tunaambiwa kuwa maghala yalikaguliliwa siku tatu kabla ya Tukio, nadiriki kusema hao wakaguzi ndo walienda kufanya jambo humo kwani ukifuatilia kwa kina utaona kuwa hata wanajeshi walio kwenye hiyo kambi wanahakika kuwa mabomu yalikuwa safi kabisa.
  Nawasilisha!
   
 20. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 876
  Trophy Points: 280
  Mh.... Ngoja nikapungze hasira ntarudi!!!
   
Loading...